Tatizo la kukuta nywele kwenye chakula
Hapa ni shida
KUKUTA NYWELE KWENYE CHAKULA SIO TATIZO,TATIZO NI KUWAZA ITAKUWA IMETOKA SEHEMU GANI
๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Hapa ni shida
KUKUTA NYWELE KWENYE CHAKULA SIO TATIZO,TATIZO NI KUWAZA ITAKUWA IMETOKA SEHEMU GANI
๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
MWALIMU kaingia darasani na kusema. “Wanaojijua wajinga wasimame”.
MADENGE akasimama peke yake.
MWALIMU: Wewe ndio mjinga?
MADENGE: Hapana, ila nimeona umesimama peke yako nikaona usijisikie vibaya angalau tuwe wawili.
LEO NIMEPITA MTAA FULANI NIKAKIMBIZWA NA MBWA, NDIO NIKAJUA NINA KIPAJI KINAPOTEA TUโฆโฆโฆ
SIO CHA KUKIMBIA, NI KUPIGA KELELE๐๐๐๐๐๐
01.๐ Wale wanafunzi walioongoza Mashuleni, wanaenda kwenye Engineering na Medical school.
02.๐ Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.
03.๐ Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia Siasa na kuwaongoza wote hapo juu. Yaani wa kwanza na wa pili.
04.๐ Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu wote hawana raha.
05.๐ Wale waliopata Zero na waliokataa shule wanakuwa waganga wa kienyeji, wote hapo juu watamtafuta huyu, pale mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake. ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Alipelekwa Hospitali na baba yake, baada ya vipimo Doctor akawa anamuandikia dawa, baba yake akatoka nje kuongea na cm.
Mtoto akamwinamia Doctor na kusema kwa sauti ya chini:- “Doctor Kwenye dozi ya dawa niandikie na FANTA BARIDII, CHIPS na MISHIKAKI kutwa mara 2 kwa siku 30.
CHEKA KIDOGO
Wachungaji watatu walikutana kwa siri na kuelezana matatizo yao ili waweze kuombeana.
MCHUNGAJI WA KWANZA: mimi tatizo langu ni wizi, kila nikimaliza ibada lazima niibe pesa za sadaka.
WA PILI: Mimi tatizo langu ni wanawake yani nimeshalala na wana kwaya wote pamoja na mke wa ASKOF.
WA TATU akaanza kulia badala ya kuongea.WENZAKE:
We vp unatatizo gani mbona unalia???
AKAJIBU: jamani mimi tatizo langu ni “umbea” haya yote tuliyoongea lazima nikaseme!
๐๐๐๐๐๐๐ป๐๐
Muda pekee ambao unaweza kumzoea DINGI ni pale unapomfundisha kutumia SMARTPHONEโฆ.
Wanakuwaga wapole sana aisee unaweza hata kumuagiza maji ya kunywa akakuleteaโฆ.
๐๐๐๐๐๐๐
Bibi kapigwa mtama na Kibaka na kuporwa simu,
Kainuka na kuanza kumkimbiza kibaka,
Kibaka kuona Bibi hakati tamaa akatupa simu,
Bibi kaikota na kuendelea kumkimbiza kibaka,
Kibakaย “Bibi kama ni simu yako si tayari umechukua”,
Bibi kajibuย “Bado Mtama”
bibi ujinga hapendagi”๐ก๐ก๐ก๐ก๐ก
MUME: “Mke wangu nasikia John katembea na wake za watu wooote hapa mtaani kasoro mmoja tu!”
MKE: “Mmmh! basi huyo aliebaki atakuwa MAMA MBILINGE KISIKI, maana yule mama ndo ANAJIFANYAGA MGUMU sanaaa.!!”
Je, huyu mama angekuwa mkeo ungekuwa na swali lingine la kumuuliza?
Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa.
Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba.
Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- “Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3.”
SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGINE
Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..
Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallahโฆ!!
sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!!
Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu..
Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.
Nimefika hapa Polisi Station nimefarijika sana na Kustuka baada ya kumkuta Askari hapa Kaunta anasoma Biblia nikajisikia fahari kuona anasoma neno kituo cha Polisi. Nikamuukiza Afande ni Nani alimuua Goliathi? Akasema Muulize Afande Mwita mlango namba 2 ndo anausika na Kesi za Mauaji.๐๐
GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enheeโฆ
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng’ombe napeleka kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia Range Rover Sport na mama mkwe ntampa Range Rover Evoque
GIRL: Baby u are awesomeโฆ
BOY: Halagu mdogo wako wa kiume ntampa Prado Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo sijaanza kulaโฆ.
GIRL: Enheeโฆna sisi??
BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti
Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu, itatupeleka hadi Maldives
GIRL: Baby I love you
BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon Bahamasโฆ.halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ua electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani
GIRL: Ooh my sweetheartโฆhalafu tukitoka huko??
BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo
Umeenda kutembea ukweni kwako baada ya chakula chausiku unapewa chumba chakulala inapofika usiku unatakakutoka kwenda kujisaidi kwasababu taa zimezimwa unapamia vyombo vya chakula sebleni kipindi unajalibu kupapasa uviweke sawa mala taa inawashwa na mama mkwe anaona umeshika vyombo anakwambia, baba kama ukushiba ungesema
Mke mmoja alimpa mme wake redio aende nayo chooni ili asiboreke kwa vile huwa anakaa muda mrefu.
Basi alvyotoka akamuuliza,”ehe mme wangu ulienjoy?” Mme,”ah wajinga hawa!
Wameniwekea wimbo wa taifa,nimejisaidia huku nimesimama
Recent Comments