SMS Nzuri: Meseji za Visa Vya Juma Hili

Jinsi mzunguko wa elimu ulivyo

01.๐Ÿ‘‰ Wale wanafunzi walioongoza
Mashuleni, wanaenda kwenye
Engineering na Medical school.

02.๐Ÿ‘‰ Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa
wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.

03.๐Ÿ‘‰ Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia
Siasa na kuwaongoza wote hapo juu.
Yaani wa kwanza na wa pili.

04.๐Ÿ‘‰ Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu
wote hawana raha.

05.๐Ÿ‘‰ Wale waliopata Zero na waliokataa
shule wanakuwa waganga wa kienyeji,
wote hapo juu watamtafuta huyu, pale
mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake.
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‰๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿƒ๐Ÿฟ๐Ÿƒ๐Ÿฟ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ

Baadhi ya misemo mikali ya leo

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi kufunika sufuria.

Misemo 17 ya kuchekesha

1) gari la kuvutwa halina overtake
2) kisigino hakikakai mbele
3) wimbo wa taifa haupgwi disko
4) feni haiwashwi beach
5) mshkaki hauchomwi kwa jiko la ges
6) mganga haagiz tembele
7) hata bibi alikuwa bint
8) mke wa mtu sumu,mume wamtu maziwa
9) kipara bila pesa ni kovu
10) mbwa hanenepi migiuu
11) picha ya rais haina bodyguard
12) mjini shule kijiji tuition
13) saa ya ukutani haivaliwi mkonon
14) heshima pesa shkamoo makelele
15) ulinz pesa bastora mzgo
16) kuku ni kuku jogoo mbwembwe
17) kusoma kuelewa kukesha mbwembwe

Mkalimani alivyoharibu ibada ya leo

Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji kutoka Bulgaria, Mahubiri yameanza saa 1 asubuhi hali ikawa kama hivi:

MCHUNGAJI: My name is Pastor Livingstone
MKALIMANi: Kwa jina naitwa mchungaji Jiwe linaloishi
MCHUNGAJI: We thank God for All goals we set by our hands
MKALIMANI: Tunamshukuru Mungu kwa Magoli yote tuliyoweka kwa Mkono

Hivi navyoongea kanisa halina viti waumini wote tumekimbia nje naona Mkalimani amebaki na kiatu cha kushoto tu.
Sunday joke

Vichekesho kumi bora vya leo vya kuvunja mbavu

1. Maswali haya je una majibi? JIBU KISHA NITUMIE MAJIBU![mtihani wa maarifa ya dunia]1. Kama hela haioti kwny miti, kwnn bank zina matawi?
2. Kwnn gundi haigandi kwenye chupa yake?
3. Kama tunatakiwa tusi-drive wkt tumekunywa, kwnn bar kuna parking?
4. Kama neno abbreviation linamaanisha ufupisho, kwnn lenyewe ni refu hvo?
5. Kama tunatakiwa kufanya sex ndani ya ndoa 2, kwnn tunabalehe kabla ya kufunga ndoa? Kazi kwakoโ€ฆ



2.Taxi Mwanamke aliingia kwnye tax akiwa hana nguo,km alivyozaliwa!Dereva akawa anamshangaa,mwanamke akamuuliza hujawahi kuona uchi au! Dereva akajibu.ninachoshangaa c uchi wako,najiuliza pesa ya kunilipa utakuwa umeiweka wapi?


3.Siri Baba: mwanangu, enhe shika hii 500Tsh usimuambie mama yako kuwa nimelala na housegirl. Mtoto: sitaki, tatizo we baba ni mbahiri sana mwenzio mama akilala na dereva ananipaga 1,000Tsh.


4.Tendo la ndoa TENDO LA NDOA LINAVYOOMBWA:

WAMASAI: Mama Yeyo nipe ile kitu namesa mwensake

WAHAYA: Mama Koku infacti njoo tuperform

WACHAGA: Mama Manka Fungua Kibubu nitupe shilingi

WAPEMBA: Mama Ali panua paja mti waja!

WAZARAMO(hamna tafsida)andaa k*#, m*$$ yaja


5.Short na Long Call Kama haja ndogo ni ”short call” Haja kubwa ni “long call” Basi kujamba iitwe “missed call”


6.Heshima Mtoto kaona nyeti ya baba yake, Akauliza “nini hii”? Baba,akajibu “ni Heshima”, kesho yake wakaja wageni, baba akamwambia mtoto, “toa heshima kwa wageni”, mtoto akatoa Nyeti yake, akaonesha, wageni wakashangaa! mtoto akasema “mnashangaa haka kadogo, baba anayo heshima kubwaaaโ€ฆโ€ฆ!


7.Kurudi shule Mtoto kamuuliza babake; ” Eti baba, Unataka kuanza tena shule? Baba akauliza: “kwa nini Umeuliza hivyo? Mtoto akamwambia: Jana uthiku, nilickia ukimnong’oneza mama” Eti, kama anapenda, Muende la pili..! ” Hivi Baba mimi niko la nne wewe na mama itakuwaje mwende la pili? Uthikubali hata kdogo”


8.Mchaga. Mchaga alipata ajali alipozinduka pale hospitali akauliza “nipo wapi hapa?” Nesi akajibu,”umepata ajali, hapa upo hospitali. Bahati mbaya umekatika mkono.” Mgonjwa: Na je saa yangu ipo wapi ya Rolex? Ipo mzee, nesi alijibu. Nesi: Mkeo na watoto wapo hapa kukufariji. Mgonjwa: Yeuwiโ€ฆ Wamefunga duka?


9. Kimombo na sms Jamaa katumiwa msg na dem wake,kutokana na urefu wa msg ikashindwa kufika yote mwishoni ikaandika’some text missing’jamaa kizungu hajui hivyo maneno ya mwisho hakuelewa maana yake lkn akahisi litakuwa neno la kimahaba,kusudi aonekane mjanja akajibu, “some text missing too dear”


10.Vibweka vya housegirl Mama mwenye nyumba “jamani nyie watoto wa nyumba hii, vijiti vya meno nimeleta juzi tu leo vimeisha?” Ndipo hoousgirl akadakia na kusema “mama mimi simo humo maana kila nikitumia nikimaliza tu navirudishiaga humo humo.”

Je, hii ni kweli kwa wale wasichana wasiojibu meseji WhatsApp!!!?

Ukiona hivyo ujue ndio hivi

Mwanaume mwenzangu ukiona unamtext msg msichana WhatsApp kaisoma hajajibu, umetuma ya pili kasoma hajajibu, ukatuma ya tatu hajajibu mmmmmh๐Ÿ˜จ๐Ÿ˜จ hapo ujue mwenzio kaangalia kwenye profile yako, kakagua picha weee mwishoni akajisemea tuย “Huyu.mkaka hapana kwa kweli”๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ

๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚

Angalia huyu house girl wa mzungu alichokifanya na anachokisema

House girl mmoja alipewa kazi na mzungu mara akavunja sahani.
Mzungu aliporejea,kazin akamuuliza ‘what happened to my plate?
House girl akajbu: ‘The dog wow wow friji paaa, mchuzi mwaaaa the vyombo pangalapangala the sahan ngelengenjeeโ€ฆโ€ฆthe pasuka paaaaaaaa
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚hadi saiz mzungu bado anasoma dictionary hajui lugha gani imetumika

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About