SMS Nzuri: Meseji za Visa Vya Ijumaa

Usichokijua kuhusu sungura, panya na jamii yao

JE WAJUA?

Sungura, panya na Jamii zao huwa na mwendo wa kukimbia na kuruka muda wote na umri wao wa kuishi ni miaka 15. Kobe ni mnyama mwenda pole, asiye na papara wala pilika, muda mwingi hujificha na kupumzika ndani ya jumba lake akikwepa maadui. Umri wa kuishi kobe hufikia hadi miaka 300.
FUNZO: Mazoezi ni kiinimacho na uongo mtupu. Jipumzikie mwaya!!!
🏃🏾🏃🏿‍

Mkalimani alivyoharibu ibada ya leo

Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji kutoka Bulgaria, Mahubiri yameanza saa 1 asubuhi hali ikawa kama hivi:

MCHUNGAJI: My name is Pastor Livingstone
MKALIMANi: Kwa jina naitwa mchungaji Jiwe linaloishi
MCHUNGAJI: We thank God for All goals we set by our hands
MKALIMANI: Tunamshukuru Mungu kwa Magoli yote tuliyoweka kwa Mkono

Hivi navyoongea kanisa halina viti waumini wote tumekimbia nje naona Mkalimani amebaki na kiatu cha kushoto tu.
Sunday joke

Cheki huyu mzee alichomfanyia muuzaji wa pharmacy

Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?….Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka …majimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;

MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo

Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe

Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi

PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!

Ulevi noma! Angalia huyu mlevi alichomfanyia huyu jamaa usiku! Ungekua wewe ungefanyaje?

Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About