SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Ijumaa
Angalia huyu secretary anavyomjibu bosi wake
Boss mmoja aliingia kazini kwake kasahau kufunga zipu ya suruali yake sasa secretary wake akamfuata na mazungumzo yakawa hivi:
SECRETARY: Boss leo umesahau kufunga geti nyumbani kwakoโฆ
Boss akabaki anashangaaโฆ Baadae wakati anakwenda chooni kujisaidia ile anataka kufungua zipu akaikuta iko wazi ndio akajua alichokuwa ameambiwa na Secretary wake.
Akarudi mpaka kwa secretary na mazungumzo yakaendelea:
BOSS: Bibie ulivyoona geti wazi je uliona benz langu lime paki auโฆ?
SECRETARY: Hapana Boss niliona kitoroli kidogo kimepaki kina matairi mawili
Chezea kufulia!
Huu Mwezi jinsi nilivyofulia yaani hata nikikuta mende wamesimama wawili najua wananisema
๐๐๐
Cheki huyu mzee alichomfanyia muuzaji wa pharmacy
Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?โฆ.Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka โฆmajimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;
MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo
Cheki jamaa alivyoumbuka baada ya kuhudhuria semina isiyomuhusu
Jamaa kavamia semina ya wasomi iliyokua inafanyika maeneo ya ubungo plaza bas wakaanza kujitambulisha
1. Naitwa Anna niko SUA mwaka3 nasoma agriculture
2. Naitwa Stella niko UDSM mwaka2 nasoma public relation
3. Naitwa Emmanuel niko UDOM mwaka3 nasoma computer science
bas jamaa nae akainuka kwa kusuasua huku akijishtukia akasema”Naitwa Elisha niko Tanesco mwaka wa 7 nasoma mita”
BREAKING NEWS: WAZIRI ANASWA KOFI
Mkazi wa Mbagala Kibondemaji, Waziri Salum (23) amejikuta akinaswa makofi baada ya kupishana kauli na jirani yake.
Mambo ya mke na mume haya, chezea mchepuko!?
Mume akamwambia mke wake:
“Funga macho yako tufanye maombi”
Akaanza kwa Kimombo:-
“โฆ Lord I pray for Grace, I pray for Mercy, I pray 4 Joy, I pray 4 Love, I pray 4 Hope, I pray 4 GLORY, I pray 4 Faith, I pray 4โฆ.”
Mke akadakia, “Unadhani mimi sina ee” akaanza:-
I pray 4 Felix, I pray 4 Temu, I pray 4 Rweyemamu, I pray 4 Masawe, I pray 4 Benson, I pray 4 Onyango, I pray 4 Swai, I pray kwa wote niliowasahau!!
Chezea mchepukoโฆ!!
Sifa 10 za mwanaume ambaye kila binti anayetaka aolewe angependa aolewe naye!!
1. Awe na pesa nyingi
2.Siyo lazima awe mzuri wa sura
3. Ajenge ukweni
4.Awe mpole
5.Asimuonee wivu mke wake
6.Awe mwenye upendo wa dhati
7.Asishike simu ya mke wake.
8.Akimkuta na mwanaume apite tu, akitaka kujua ni nani asubiri nyumbani
9.Awe anamskiliza mke wake kwa kika kitu.
10.Asipende mwanamke mwingine zaid yake
UKIMPATA MWANAUME MWENYE SIFA HIZO KAPIME DNA LAZIMA ATAKUWA NI BABA AKO.
๐๐๐๐๐๐๐๐
Cheki masifa yalivyomponza huyu, Sifa nyingine ni mbaya jamani
Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.
Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.
Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.
Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.
Wakaingia msituni kila mtu njia yake.
โฆ Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.
Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala niniโฆ alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.
Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, โVipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?โ
Mkenya akamjibu: โMkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!โ
Angalia nilichokifanya Jana kumkomoa x-wangu
Mwenzenu nilikatiwa umeme jana basi leo si nikaamua kwenda kununua luku ya 10,000. Kufika njiani nikatamani fursana nikaingia kijisupermarket mara sindo nakutana na ex wangu! Mshenzi yule kaniona mimi sijui alikua na mpango wa kununua vocha ya jero eti kabadili kanunua vocha ya buku tano ilimradi nione maisha yake safi tangu tuachane. Mambo ya kijinga spendi kudadeky nimetoa buku kumi nikanunua mipampers nami nijifanye nimeowa nina mtoto halafu huyoo nikashika njia yangu.
Sasa washkaji zangu tafadhalini mwenye mtoto au shida ya pampers naomba anunue kwangu maana leo nalala tena kiza ๐โโ




































































I’m so happy you’re here! ๐ฅณ









Recent Comments