Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mambo ya kuzingatia kuhusu ugonjwa wa Kaswende

Kaswende husababishwa na bakteria aitwaye Treponema pallidum , ambaye pia huitwa spirochetes kutokana na umbo lake la mzunguko. Viumbe hawa hujipenyeza kwenye ngozi laini inayotanda midomo au sehemu nyeti. Yafuatayo ni mambo Muhimu ambayo unapaswa kuyafahamu kuhusu Ugonjwa wa Kaswende.

Jinsi ugonjwa wa Kaswende unavyoonea

Ugonjwa huu huenezwa kwa kugusa moja kwa moja mchubuko wa kaswende (syphilitic sore) uliopo kwenye ngozi. Kaswende haiambukizi kwa kuchangia vyoo, vitasa vya milango, mabwawa ya kuogelea, kuchangia nguo au vyombo vya chakula.

Kwa njia ya Kujamiiana

Kaswende ni ugonjwa unaoambukiza haraka sana, mara nyingi huambikizwa kupitia ngono. Kwa sababu ugonjwa huu huenezwa kwa kugusa moja kwa moja mchubuko wa kaswende (syphilitic sore) uliopo kwenye ngozi, njia kuu ya kuenea ni kupitia ngono ya kawaida, ya kutumia midomo na ile ya kinyume na maumbile.

Kwa njia ya kugusana Miili

Mara chache ugonjwa huu huweza kuambukiza kwa kubusiana au kugusana miili. Pamoja na kuwa ugonjwa huambukiza kupitia michubuko, mara nyingi michubuko hatarishi haitambulikani. Mtu aliyeambukizwa huwa hajielewi na hivyo kumwambukiza mpenzi wake.

Kwa mtoto kipindi cha ujauzito

Mwanamke mwenye mimba na ugonjwa huu anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni kupitia placenta au wakati wa kuzaliwa.

Aina hii ya kaswende huitwa congenital syphilis, na inaweza kusababisha kujifungua mtoto mfu au mtoto akafa muda mfupi baada ya kuzaliwa. Watoto wengi hawaonyeshi dalili wanapozaliwa. Baadaye watoto huota vijipele, hupata matatizo ya meno, na kubonyea kwa mfupa wa pua – hali inayoitwa saddle nose, kuwa viziwi, kuwa na watoto wa jicho na kifafa.

Hatua za Kaswende

Ugonjwa wa kaswende hugawanywa katika hatua na kila hatua ikiwa na dalili tofauti, lakini wakati mwingine hakuna dalili zitakazojitokeza kwa miaka mingi.

Uambukizaji unatokea kwenye hatua ya kwanza, ya pili na mara chache mwanzoni mwa hatua ya latent phase.

Hatua Ya kwanza Ya Kaswende – Primary Syphilis

Kaswende huanza kama mchubuko mmoja (au zaidi ya mmoja) mgumu usio na maumivu unaojulikana kama chancre kwenye sehemu za siri, kwenye mdomo, au kwenye ngoz,i siku 10-90 (wastani wa miezi 3) baada ya maambukizi.

Mchubuko huu unaweza kubaki hapo bila kuleta usumbufu kwa kipindi kirefu na hata maiaka mingi. Mchubuko huu wa mviringo hutokea kwenye eneo la maambuikizi. Hata bila ya tiba yo yote, mchubuko huu unaweza ukapona wenyewe bila kuacha kovu katika wiki sita.

Hatua Ya Pili Ya Kaswende – Secondary Syphilis

Hatua ya pili inaweza ikadumu kwa mwezi mmoja hadi miezi sita ikianza kama wiki sita hadi miezi sita baada ya maambukizi.
Dalili
Katika hatua ya pili, vijipele huota mara nyingi vikianzia mgongoni na kuenea mwili mzima, pamoja na kwenye viganja vya mikono na kwenye nyayo. Vijipele hivi huwa vya mviringo vyenye rangi nyekundu au vyenye wekundu wa kahawia.
Michubuko inayofanana na chunjua hutokea kwenye sehemu za midomo na mkundu. Vile kutatokea maumivu ya misuli, homa, kukauka koo, kuvimba tezi, kupunyuka nywele, kukonda na uchovu wa mwili.

Latent Syphilis
Kama tiba ya kaswende ya hatua ya pili haitatolewa, ugonjwa utaendelea kwenye hatua iitwayo latent stage. Katika hatua hii inayoweza kudumu kwa miaka kadhaa, mwili utautunza ugonjwa bila kuonyesha dalili zo zote. Pamoja na kuwa hakuna dalili zo zote zitakazoonekana, ugonjwa huu unaweza kuendelea kwenye hatua ya mwisho.

Hatua Ya Tatu Ya Kaswende – Tertiary syphilis

Asilimia 15 ya watu ambao hawakupata tiba kwenye hatua ya pili ya kaswende watapata kaswende ya hatua ya tatu – tertiary syphilis. Hatua hii inatokea miaka 10 hadi 30 baada ya dalili za mwanzo za kaswende.
Dalili
Dalili za kaswende za hatua hii ni pamoja na kushindwa kumudu matumizi ya viungo vya mwili, ganzi, upofu, ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, madhara kwenye moyo na mishipa ya damu, madhara kwenye ini, mifupa na maungio ya mifupa. Kifo huweza kutokea kutokana na uharibifu wa viungo vya mwili.

Matibabu ya ugonjwa wa Kaswende

Ugonjwa wa kaswende unatibika. Kuwahi kumpa tiba mgonjwa wa kaswende ni muhimu kwani kuchelewa kunaweza kumletea madhara makubwa ya mwili au kifo. Kama ugonjwa haujazidi mwaka mmoja, mara nyingi dozi moja ya ya penicillin hutosha.

Kaswende iliyoendelea kwenye hatua nyingine, dozi nyingine zitahitajika.

Mapishi ya Mchemsho wa ndizi na nyama

Mahitaji

Ndizi mbichi 6
Nyama ya ng’ombe (nusu kilo)
Viazi mviringo 2
Kitunguu swaum
Tangawizi
Kitunguu maji
Nyanya 1 kubwa
Mafuta (vegetable oil)
Chumvi
Limao
Pilipili

Matayarisho

Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa

Mbinu 5 za kukunufaisha maishani

Mbinu 5 za kukufanikisha maishani Unaweza ukawa upo kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu na unashangaa kwa nini hufanikiwi katika maisha yako kama jinsi unavyotaka wewe. Hali hii inaweza ikawa inakuumiza pengine kila ukiangalia rafiki zako ama maisha ya wengine yanavyozidi kuwa mazuri, wakati wewe upo katika hali ngumu. Na pengine umekuwa ukijiuliza nini siri kubwa ya mafanikio yao ambayo wanaitumia ambayo wewe huna. Kutokana na hali hiyo umekuwa ukijilaumu kujilaumu na kujiuliza kwanini nyingi ambazo hazina majibu. Kitu usichokijua watu hawa huwa wanatumia mbinu fulani kufanikiwa. Kawaida, katika maisha kama ulivyomchezo wa miguu, au michezo mingine mara nyingi huwa zipo mbinu za kufanikisha kile tunachokifanya. Mbinu hizi huweza kutambulika kama sheria, kanuni, au siri lakini zote hulenga kukufanikisha kama unataka mafanikio ya kweli. Mbinu hizi zinapotumiwa kwa bahati mbaya au nzuri huwa hazifanyi ubaguzi zinamwendea yoyote na kuleta matunda unayoyataka. Hata kama ikitokea umezitumia mbinu hizi kwa bahati mbaya bila kujijua ni lazima utafanikiwa katika maisha yako. Mbinu hizi ndizo wanazozitumia wengi wenye mafanikio na kuwafanikisha, ingawa huwa sio kwao kuwa rahisi kukwambia mbinu hizo. Haijalishi unaishi kwa sasa maisha gani au upo kwenye matatizo mengi vipi, ukizitumia mbinu hizi, zitakufanikisha na kukupa maisha ya mafanikio unayoyataka. Acha kulalamika tena na kuishi bila amani. Sasa unaweza ukawa na mafanikio makubwa kama hao unaowaona wamefanikiwa, ikiwa utatumia mbinu hizi kukufanikisha. Unajua mbinu hizi ni mbinu zipi?

Hizo Ndizo Mbinu 5 Za Kukupa Maisha Ya Mafanikio:-
1. Kuwa na nidhamu binafsi.

Ili kupata mafanikio makubwa unayoyahitaji sio suala la kufanya kazi kwa bidii tu, zaidi unachohitaji nikuwa na nidhamu binafsi ambayo itakuongoza kwenye malengo yako. Watu wengi hawana nidhamu binafsi kitu ambacho kinapelekea wengi ndoto zao zinaishia kati. Ni muhimu kuelewa kuwa ni lazima kufanya mambo yale yanayoendana na ndoto zako, hata kama kuna wakati unajihisi umechoka unalazimika kujikaza kufanya jambo hata dogo ambalo litakufikisha kwenye malengo yako. Ukishindwa kuwa na nidhamu binasi katk maisha yako elewa kuwa utashindwa kufikia mipango na malengo iliyo jiwekea.

2. Jifunze kila mara kwa watu waliofanikiwa.

Hii itakusaidia kujua vitu vingi usivovijua kuliko kukaa na kung’anga’nia mbinu zilezile ambazo hazikusaidii. Yapo mambo mengi sana usiyoyajua ambayo yanakufanya ushindwe kufanikiwa. Ikiwa utakuwa na uwezo wa kujifunza kwa wale waliofnikiwa utakuwa upo kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa na kusonga mbele. Maisha yako yanazidi kuwa magumu siku hadi siku, kutokana na kukosa kujifunza kwa wengine kwa kujua hilo badili mwelekeo wako na kuwa mtu wa kujifinza mwisho wa siku mafanikio yatakuwa makubwa kwako.

3. Jifunze kutokana na makosa uliyofanya.

Inawezekana kuna mahali utakuwa umekosea kwa namna moja au nyingine,badala ya kulaumu na kuumia moyo sana jifunze kutokana na hayo makosa liyoafanya ili isije ikawa kwako rahisi kufanya makosa yaleyale kwa mara nyingine. Ikiwa utajifunza kutokana na makosa na kufanyia kazi kile ulichojifunza hapo utakuwa umechukua hatua moja muhimu ya kuweza kukusaidia kusonga mbele kuyafata mafanikio unayoyataka. Unataka mabadiliko makubwa katika maisha jifunze kutokana na makosa yako na acha sana kulaumu.

4. Jenga tabia ya kujisomea kila siku.

Hili ni jambo ambalo nimekuwa nikiliongelea sana kuhusu huu umuhimu wa kujisomea. Unapojisomea unapata vitu vingi sana tena ndani ya muda mfupi. Kupitia huko utaweza kujifunza mambo mazuri yatakayoweza kubadili maisha yako kwa sehemu kubwa na kuwa mtu, tofauti kabisa. Acha uvivu jifunze vitu vipya kila siku. Unaweza ukajifunza kupitia vitabu, ama mitandao mizuri inayoelimisha kama huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kupata maarifa bora na sahihi kabisa. Unapojifunza inakusaidia kukabiliana na changamoto nyingi, ambapo kwako ingekuwa ngumu kuzikabili.

5. Kuwa na mahusiano sahihi na watu waliofanikiwa.

Katika kutafuta mafanikio ni vizuri ukawa na mahusiano ama mtandao na watu sahihi ambao watakusaidia kukufikisha kwenye lengo ulilojiwekea. Haina haja kuwa na watu ambao hawakusaidii kutimiza malengo yako. Watu hawa watakukwamisha na kukurudisha nyuma katika maisha yako tu siku zote. Jenga tabia ya kuwa na watu sahihi ambao utajifunza kitu kwao, utashirikiana nao na kujifunza mambo mengi huko ya mafanikio na hatimaye utamudu kusonga mbele

Jinsi ya kujua kama una Mimba: Dalili za kwanza kabisa za Ujauzito

Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.

Zifutazo ndizo dalili za awali za mimba changa:

Kutokwa damu bila kutegemea.

“Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito.

Kuchoka

Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.

“Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi”

Chuchu kuwa nyeusi.

Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, “Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.”

Maumivu kwenye matiti

Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

Maumivu mwilini

Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

Kuwa na hasira

“Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,”

Kuongezeka kwa joto mwilini.

Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.

Kichefuchefu.

Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.

Mwili kuvimba

Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.

Kwenda haja ndogo mara kwa mara.

Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.

Tamaa ya vitu mbalimbali.

Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

Kuumwa kichwa

Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebish a na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

Kufunga choo

Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.

Jinsi ya kuongeza wingi wa mbegu za kiume

Ili kuongeza mbegu za kiume zingatia haya yafuatayo;

Kula lishe bora

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu.

Punguza matumizi ya sukari na vyakula vya ngano. Ongeza zaidi matunda, mboga za majani na mafuta yenye afya.

Acha kutumia kahawa, vinywaji na vyakula vyenye kaffeina.

Kama una tatizo la kuwa na mbegu chache ni vizuri ukaacha kutumia vinywaji au vyakula vyote vyenye kaffeina kwanza.

Matumizi ya kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu kina Selenium na pia kinaondoa sumu mwilini vitu hivi viwili ni mhimu kwa ajili ya kuongeza spidi ya mbegu.

Vile vile Kitunguu swaumu kina ‘Allicin’ ambayo huongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uume.

Kujitibu unaweza kuongeza kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika. Pia unaweza kutafuna punje 2 au 3 kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata hizo punje 3 vipande vidogo vido (chop) kisha unywe na maji.

Usile zaidi ya punje 3 kwa siku.

Matumizi ya Mayai

Mayai yanachukuliwa kama mbadala wa uhakika zaidi katika kuongeza uwingi wa mbegu pamoja na kuongeza spidi au kasi yake. Yana vitamini E nyingi na protini ya kutosha vitu viwili mhimu katika kuongeza mbegu. Tumia mayai ya kienyeji zaidi na sio ya kisasa.

Matumizi ya Spinach

Mboga hii ina Folic asidi ambayo ni mhimu katika kuongezeka kwa mbegu za kiume.

Kula ndizi

Ndizi zina Magnesiamu, Vitamini B1 na Vitamini C, vitu ambavyo ni mhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume. Vile vile Ndizi zina kimeng’enya kimoja adimu sana kijulikanacho kama ‘Bromeliad’ ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa.

Matumizi mbegu za maboga

Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki ambayo ni mhimu katika kuundwa au kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosterone.

Vile vile mbegu hizi zina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni vitamini mhimu katika kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na nguvu kwa ujumla.

Kula zaidi mboga za majani

Mboga za majani zinapunguza homoni ya ‘estrogen’ na hivyo kufanya homoni ya ‘testosterone’ ipatikane kwa wingi na kiurahisi zaidi na hivyo mbegu zako ziweze kuongezeka bila vipangamizi vyovyote. Homoni hii ndiyo inayohusika na kuzalishwa kwa mbegu

Kunywa maji mengi kila siku

Kutokunywa maji ya kutosha kila siku kuna uhusiano wa moja kwa moja na kupungua kwa uwingi wa mbegu. Mbegu zako zimetengenezwa kwa maji, zipo kwenye hali ya kimiminika.

Kunywa maji ya kutosha kunasaidia kutengenezwa kwa mbegu nyingi.

Kutegemea na uzito wako unaweza kuhitaji maji lita 2 mpaka 3 kila siku.

Tumia vyakula vyenye folic asidi kwa wingi

Vyakula hivi ni pamoja na tunda la parachichi na karoti, mbegu za maboga, ufuta, alizeti, maharage, chungwa, papai, bamia nk

Hii kazi kweli kweli, Ungekua wewe ungefanyaje?

UNATOKA SEBULENI UNAENDA ZAKO CHOONI UNAINGIA TU HIVI GHAFLA UNAKUTANA NA MZIGO MKUBWA WA MAVI JUU YA CHOO ALAFU UNAAMUA KURUDI ZAKO ILE UNATOKA TU UNAMUONA DEMU MZURI ULIYEMTONGOZA JANA ANAKUJA KUINGIA CHOO ULICHOTOKA WW NA KINA MZIGO WA MAVI JUU NA AMEKUONA WW NDIO UMETOKA MLE NDANI ..unaamua kurudi ili uka flash bahat mby maji hakuna.!!!

😁😁😁HAPO NDIO UTAJUA KWANINI SIKU HIZI HATUPENDI UJINGA😆😆😆😆

JE UNAFAHAMU NINI KUHUSU KUJAMBA?

Kwanini tunajamba? kwanini “ushuzi” unanuka?
Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu,lakini
inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo
la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda.Kila
mtu anajamba,hata Halle Berry nae hujamba.

1.Kujamba ni nini hasa?
Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa,ambayo
inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi.Baadhi ni hewa
tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa.Hewa ingine
husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu
kutoka kwenye damu,na baadhi ya gesi huzalishwa na
kemikali katika utumbo au bakteria.Kwa kawaida
“ushuzi” unakua na asilimia 59 ya gesi ya
nitrogen,asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni carbon
dioxide,asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.
Asilimia moja tu ya “ushuzi” inaweza kuwa hydrogen
sulfide na mercaptans,ambayo ndio ina sulfur ndani
yake,sulfur ndo hufanya “ushuzi” utoe harufu mbaya
Kujamba huambatana na sauti,hii ni kutokana na
“vibration” katika njia ya haja kubwa.Ukubwa wa mlio wa
kujamba hutegemea “presha” inayosukuma gesi itoke nje
na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.

2.Kwa nini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?
Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa
mtu,vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio husababisha
hili.Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama
maharage,kabichi,soda na mayai.

3.Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku
Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa
siku.Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi
cha miaka 6,anaweza kuzalisha nishati ya kutosha
kutengeneza bomu la atomiki.

4.Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde.
Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada
ya mtu kujamba,hiyo ni kwa sababu inachukua muda
mrefu kwa harufu kufikia pua.

5.Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya Yako
Madaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia
kujamba ni hatari kiafya.Baadhi ya wataalam wanafikiri
kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa
mmeng’enyo wa chakula,hivyo kujizuia kujamba
haitakuletea madhara.Wengine wanadhani kwamba
kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa
gesi,na pia inaweza sababisha bawasili (hemorrhoids).

6.Kwa Baadhi ya Tamaduni,Kujamba Sio Ishu
Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba
lifanywe kistaarabu,kuna baadhi ya tamaduni hawaoni
haya kujamba hadharani,na pia hufurahia tendo
hilo.Mfano kabila la Yanomami huko America ya
Kusini,kwao husalimiana kwa kujamba,na China
unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya
zamani,Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia
kujamba inaweza kuwa hatari kiafya,alipitisha sheria
kwamba ni ruhusa kujamba kwenye “banquets”.

7.Ushuzi Unawasha Moto
Kama ilivyoandikwa hapo juu,methane na hydrogen
inayozalishwa na ushuzi inaweza sababisha moto.

8.Mchwa Hujamba Kuliko Wanyama Aina Zote
Ni ngumu kuamini kuwa mchwa ndo anawajibika na
matatizo yetu ya “Global Warming”.Mchwa huongoza kwa
kujamba kwa wanyama,na hiyo huzalisha gesi ya
methane.

9.Ukiubana Ushuzi,Utakutoka Usingizini
Hata ujitahidi kuubana vipi,ushuzi utatoka mara
utapokua umepumzika,hasa ukiwa umelala.

10. Watu Hujamba Hata Baada ya Mauti Kuwafika
Maiti huendelea kutoa gesi hadi masaa matatu baada ya
mtu kufariki dunia,hii huambatana na milio ya
kujamba.Hali hii husababishwa na misuli kusinyaa.

UKIPATA NAFASI JAMBA MWANANGU

Angalia huyu dada alivyoumbuka, Duh! Alijua haoni!!!

Dem anatoka kuoga akiwa na kanga moja tu anaskia hodi,kufungua mlango akakuta ni jirani yake frank ambaye ni kipofu, akamkaribisha ndani akakaa, dem kavua ile kanga akabaki uchi akainama akaanza kujipaka mafuta akijua frank hamuoni na mazungumzo yakawa ni Haya..

DEM: VIPI FRANK MBONA UMEPOTEA YAANI HUONEKANI SIKU HIZI..?

FRANK: AH NILIENDA INDIA KUFANYIWA OPERESHENI YA MACHO SASA HIVI NAONA VIZURI KABISA!…

😂😂😂

🏃🏻🏃🏻🏃🏻🏃🏻🏃🏻

Baada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta

MUME: Fungua mlango!

MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.

MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.

MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!

MUME kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!

MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.

MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.

MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.

Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi

Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.

Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?

Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.

SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.

Siri ya mafanikio katika maisha Ni Kutoangalia Watu

Baada ya kusoma makala kuhusu hofu zinazotugharimu katika safari ya mafanikio, Leo nimekuandalia Makala hii ya Siri ya mafanikio.

Katika safari ya mafanikio, watu wanaweza kuwa kikwazo kikubwa kinachosababisha ugumu wa kuendelea mbele. Wanaweza kuleta upinzani, kukosa imani, au hata kuzua vikwazo visivyo na msingi. Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kuwa changamoto hizi zilizoletwa na watu ni sehemu ya mchakato wa kufikia mafanikio. Ingawa inaweza kuwa ngumu kukabiliana na watu wenye upinzani au wasioamini katika safari yetu ya kufikia malengo yetu, tunapaswa kuzingatia kuwa hakuna mafanikio ya kweli ambayo hayakuja na changamoto. Naam, inaweza kuwa rahisi kufanya kazi peke yetu na kuepuka kukabiliana na watu wasioamini au wenye upinzani, lakini hiyo haitatupeleka mbali sana.

Tunahitaji kushughulikia changamoto hizi na kuona jinsi tunaweza kuzishinda. Kukutana na watu ambao hawana imani na malengo yetu inaweza kuwa kama mtihani mkubwa kwetu. Wanaweza kutushawishi kuacha au kuanza kutilia shaka uwezo wetu. Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa imani yetu ndio itakayotuendesha mbele. Tunapaswa kujikumbusha kuwa mafanikio hayangeweza kupatikana ikiwa tungekuwa na imani ndogo ndani yetu wenyewe. Mbali na hilo, tunapaswa pia kutambua kuwa vikwazo visivyo na msingi vinaweza kuwepo katika safari yetu ya mafanikio. Watu wanaweza kuzua vikwazo hivi kwa sababu ya wivu, woga, au tu kutokuelewa malengo yetu. Ni muhimu kutambua kuwa hatuwezi kudhibiti tabia au mitazamo ya watu wengine, lakini tunaweza kujifunza kuweka mipaka na kuendelea kufuata malengo yetu licha ya vikwazo hivyo. Katika safari yetu ya mafanikio, tunapaswa kuwa na uvumilivu na subira.

Tunapaswa kutambua kuwa kila changamoto tunayokutana nayo inatupa fursa ya kukua na kujifunza. Tunapaswa kutumia changamoto hizi kama nguvu ya kuendelea mbele badala ya kutuacha tukata tamaa. Kwa kumalizia, ingawa watu wanaweza kuwa kikwazo katika safari yetu ya mafanikio, tunapaswa kuona changamoto hizi kama sehemu ya mchakato wa kufikia malengo yetu. Tunapaswa kuwa na imani thabiti ndani yetu wenyewe, kuweka mipaka na kuendelea kusonga mbele licha ya vikwazo vinavyoweza kuzuka. Kwa kufanya hivyo, tutapata mafanikio kamili na kuwa bora zaidi katika safari yetu ya kuelekea mafanikio.

Wakati mwingine, tunaweza kukutana na watu ambao hawana imani na uwezo wetu au wanajaribu kutuweka chini kwa sababu ya wivu au tamaa. Ni muhimu kujifunza kuweka mipaka na kuendelea kusonga mbele, kujiamini katika uwezo wetu na kuendelea kufanya kazi kwa bidii kuelekea malengo yetu.

Watu wanaweza pia kuwa vikwazo kwa kuwa na maoni tofauti au kutokuwa na uelewa kamili wa malengo yetu. Katika hali hizi, ni muhimu kuwa na uvumilivu na kuwasiliana kwa wazi ili kuelezea malengo yetu na kutafuta njia za kuwashawishi au kuwashirikisha katika safari yetu ya mafanikio.

Hakikisha pia kuwa unazungukwa na watu wenye mawazo chanya ambao wanakuunga mkono na kukusaidia kufikia malengo yako. Kuwa na timu ambayo inakusaidia na kukutia moyo ni muhimu sana katika safari ya mafanikio.

Kwa hiyo, tunapokabiliana na vikwazo kutoka kwa watu katika safari yetu ya mafanikio, ni muhimu kujifunza kutokana na hilo, kuweka mipaka, kuwasiliana kwa wazi, na kuwa na timu yenye msaada karibu nasi. Hatimaye, tunapaswa kuendelea kuamini katika uwezo wetu wenyewe na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu.

Waziri mkuu wa zamani wa uingereza Sir Wiston Churchill aliwahi kusema;

“huwezi kufika mwisho wa safari yako kama utakuwa unasimama kila mahali kumtupia jiwe kila mbwa anaye kubwekea”

Sir Wiston Churchill

Kauli hii ina maana kwamba kama una picha kichwani ya kule unakokwenda au umekusudia kufikia na kutimiza lengo fulani katika maisha hupaswi kusikiliza, kupambana au kushindana nakila mtu.

Unapokuwa njiani kutimiza lengo lako lazima utakutana na watu wa aina hizi;

  1. Watakaokurudisha nyuma kwa kukuharibia mipango na juhudi zako
  2. Watakaokuvunja moyo na kukukatisha tamaa
  3. Watakaokusema vibaya hata kwa mazuri yako na kukuzushia uongo
  4. Watakaokuchukia kwa sababu ya bidii yako

Unaweza kushawishika kutaka kumjibu kila mtu anayekusema vibaya, kukuchukia au kukukatisha tamaa (hapo ndo unakuwa sawa na yule anayesimama kumtupia jiwe kila mbwa anayebweka).

Unaweza ashawishika kutaka kuona kila mtu anakukubali na kukuunga mkono, kitu ambacho hakiwezekani.
Kuna Msemo usemao “siri kubwa ya kufeli katika maisha ni kujaribu kumpendeza kila mtu”.

Hapa duniani huwezi kumpendeza kila mtu hata ufanye jambo zuri kiasi gani “hata ukichezea maji utaambiwa unatimua vumbi”. Mara nyingi tunajitahidi kufanya mambo mema na kuwa na nia njema, lakini bado kuna watu ambao hawatafurahia jitihada zetu na watatupinga tu. Hii inaweza kuwa changamoto kubwa kwetu kihisia na kijamii, kwani tunatamani kukubalika na kupendwa na kila mtu.

Lakini kumbuka, haifai kuchukulia kila upinzani kibinafsi au kuathiri thamani yako. Watu wana mitazamo tofauti na uzoefu wao binafsi, na huenda hawana ufahamu kamili wa hali yako au malengo yako. Badala yake, ni muhimu kuwa na imani katika nia zako na kuendelea kufanya mambo mema bila kujali jinsi watu wengine watakavyokuona au kukupinga.

Njia bora ya kushughulikia upinzani ni kujielewa na kuweka mipaka. Jifunze kuamini kwamba wewe ni wa thamani na una uwezo mkubwa wa kuathiri mazingira yako. Wacha maadili yako yaongoze vitendo vyako na usiruhusu maneno au maoni ya wengine kukufanya ujisikie vibaya au kupoteza lengo lako.

Kumbuka pia kuwa hakuna mtu aliyeweza kufanya kila mtu awe radhi. Hata watu mashuhuri na viongozi wa kiroho hawakuepuka upinzani. Kina Mandela, Mahatma Gandhi, au Martin Luther King Jr., walikabiliana na upinzani mkubwa, lakini waliendelea kusimama imara kwa imani zao na kufanikisha mabadiliko makubwa.

Ili kufanya mabadiliko katika jamii au ulimwengu, ni muhimu kuwa tayari kukabiliana na upinzani. Upinzani unaweza kukusaidia kukua kibinafsi na kitaaluma, kurekebisha njia zako, na kukuza uvumilivu wako. Ni nafasi ya kujifunza na kujenga hoja zako kwa msingi thabiti.

Hivyo, jinsi unavyokabili upinzani ina athari kubwa kwa maendeleo yako na mtazamo wako kwa maisha. Usikate tamaa na usiruhusu upinzani ukuzuie kufuata ndoto zako na kufanya mambo makubwa. Jiamini, thamini uwezo wako, na endelea kusonga mbele bila kujali kile ambacho wengine wanaweza kusema au kufikiria. Hakuna kitu kikubwa kilichofanyika bila ya upinzani, kwa hiyo endelea na safari yako na uhakikishe kuwa unaamini kwamba una nguvu ya kufanya tofauti.

Wewe fwatilia Mipango yako huku ukitazame hatima yako. Soma hapa mbinu hizi za kukunufaisha maishani.

Lakini haimaanishi uwachukie watu na kuwatendea mabaya ili ufanikiwe mwenyewe. Chuki na Mapambano hayanufaishi bali yanakufanya kuwa dhaifu.

Vivyo hivyo, Sio watu wote ni kikwazo. Kuna watu wa aina nyingine ambao wanaweza kukusaidia kufanikiwa. Unapaswa kuwa makini na kutumia Busara yako kuweza kuwatambua watu unaokuwa nao katika safari ya Mafanikio.

BareFoot Sprayer: Pampu imara ya kunyunyiza dawa – Mabomba ya kupulizia dawa mepesi kubeba na yenye nguvu

BareFoot Sprayer ni Pump Imara na yenye Nguvu Maalumu kwa ajili ya kunyunyiza/kupuliza dawa mashambani, kwenye mifugo nakadhalika.

BareFoot Sprayer imetengenezwa kwa Muundo mzuri kwa kurahisisha ubebaji na upigaji wadawa.

BareFoot Sprayer ina dumu imara lisilopasuka kirahisi na linaloweza kudumu kwa muda mrefu.

Bidhaa hii inaletwa Kwako na Kampuni ya BareFoot International Limited. Wauzaji na wasambazaji wa bidhaa Bora za Kilimo Tanzania.

Mawasiliano

Simu:

+255 756 914 936

WhatsApp:

+255 756 914 936

Email:

info@bfi.co.tz

NB: Tunapatikana Mikoa Yote Tanzania

Matumizi ya tunda la shelisheli kama dawa ya ngozi

Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo 6, ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu wa kati mita 9 hadi 18 na huanza kuzaa matunda ukiwa na miaka 6 na kuendelea kwa miaka zaidi ya 50.

Lakini pia tunda la shelisheli ni zao kuu maeneo ya Pasifiki na lina kiwango kikubwa cha wanga na huweza kuliwa likiwa bichi au baada ya kupikwa.

Tunda hili lina faida mbalimbali zikiwemo za kiafya na za kiuchumi, lakini moja ya sifa kuu ya tunda hili ni kuwa na kiwango kizuri cha wanga.

Kutokana na kiwango kikubwa cha wanga kwenye shelisheli kunalifanya tunda hilo kutumika badala ya unga wa ngano kwenye baadhi ya nchi na hivyo hutengenezewa chapati.

Aidha, utomvu wake unaelezwa kutumika kama njia asili ya kupunguza matatizo ya kuhara na magonjwa ya ngozi.

Hivyo basi kwa kuzingatia na kujali afya yako unashauriwa kuweza kutumia tunda hili ili uweze kuifanya ngozi yako iwe nyororo lakini pia uweze kujitibu matatizo yote yatokanayo na kuhara.

Ushauri wangu kwa leo: Zingatia hili, hamasika, badilika

Tupo kwenye dunia ambayo tulikuta watu na tutawaacha watu.
Vyote tulivyovikuta vilianzishwa na binadamu wengine wenye mawazo mema na wenye mawazo mabaya pia. Vitu vingi tunavyovifanya tunaendeleza tulivyovikuta ni mara chache kukuta kitu kipya ambacho hakitegemei mazingira na asili ya tulivyovikuta.

Hivyo basi kwa vyovyote vile unahitaji mtu wa kukuongoza au kuku Coach ili ufanikiwe katika pande zote za maisha.

Nitakwenda kuzungumzia sehemu kuu tatu za muhimu sana ambazo unatakiwa uwe na watu wa kukuongoza ili uweze kukua na kupanda viwango kila wakati.

Ni vitu vya kawaida sana lakini leo nitakwenda kuzungumzia uone ilivyo muhimu sana wewe kua na vitu hivi maana bila vitu hivi mafanikio yatakua magumu sana kufikia. Safari yako itakua ngumu zaidi kama utakosea sehemu hizi tatu.

Nitaomba tuelewane kwamba hapa huendi kuiga au kuwa hawa watu utakua wewe na utatimiza lile kusudi la Mungu ndani yako.

Kwanza kabisa uko hivyo ulivyo kwa sababu ya mazingira uliyokulia na watu ulioishi nao tangu ukiwa mtoto hadi hapo ulipo.

Kuna tabia nyingi sana unazo kutokana na mazingira uliyokulia.

(Hapa ndipo nakutana na kitu ambacho nakipenda sana kujifunza kwa wengine napenda kujifunza kwenye mazingira mapya na kwa watu wapya kwa kua wameishi maisha ambayo mimi siyajui na wanafahamu vitu vingi ambavyo mimi sifahamu. Watu wana utajiri mwingi sana ndani yao ukiweza kukaa na mtu ambaye humjui kabisa unaweza kujifunza mambo mengi ya ajabu kwake. )

Hawa ndio watu wa Muhimu sana kwenye safari yako usiwakose ili uweze kusonga mbele.

Sifa zao kabla hujawachagua ni za muhimu sana pia ili wasije wakakupoteza badala ya kukufikisha kule unakotaka kwenda.

(a)Awe na mafanikio (Amefika Mbali) kwenye hiyo sehemu.

(b)Awe na Tabia njema zinazokubalika na jamii yake na dini yake. (mfano hapa ukikutana na mtu ambaye anakuelekeza kuhusu biashara na ni mlevi na mzinzi hizi tabia lazima atakuambukiza kwasababu atakua mtu wako wa karibu sana)

(c)Awe amekuzidi sana kwenye kile unachotaka akulelee (akuongoze).

Hizo ni sifa za muhimu tu za kuangalia zipo nyingine nyingi sana utajifunza mwenyewe.

1. Mlezi wako wa Kiroho

Huyu ni mtu wa muhimu sana na nimemweka wa kwanza.

Bila roho hakuna mwili.

Bila roho mwili wako unakua umekufa.

Unahitaji ukue kiroho na upande viwango kila wakati ili uweze kuvutia mafanikio ya nje.

Ukishindwa hapa hata ukiwa bilionaire inaweza kuwa kazi bure.

Hutaweza kuzifurahia hizo pesa.

Tafuta mtu wa kukulelea kiroho.

Mtu wa kukufundisha kumcha Mungu.

Kama huna katafute mtu wa kukulea kiroho sifa nimezitaja hapo juu.

Mtu huyu anatakiwa akufahamu vizuri na wewe umfahamu vizuri.

Yaani muwe na mahusiano ya karibu sana.

Mtu huyu awe anafuatilia maendeleo yako ya kiroho kwa karibu sana.

Haijalishi uko Dini gani lazima umpate mlezi wa roho yako.

Dini ndio inahusika kulisha roho zetu.
Ndio maana hatufundishwi biashara kule.

2. Mlezi wa Mahusiano/Uchumba/Ndoa

Hapa ni kwa muhimu sana.

Ukiwa vizuri kiroho mahusiano yakawa na tatizo hutafika mbali.

Ukiwa vizuri kiroho ndoa ikasumbua nayo ni tatizo.

Tafuta mtu wa kukulea kwa upande huu pia mtu aliefika mbele zaidi yako.

Aliefanikiwa zaidi yako.

Kama unatafuta mchumba tafuta mtu aliye kwenye ndoa na amefanikiwa.

Ukimtafuta single mwenzako atakupoteza😀.

Mtu huyu awe karibu yenu kabisa kulea mahusiano/ uchumba au ndoa yenu.

Hakuna aliyezaliwa anajua kila kitu tunajifunza hapa duniani kwa waliotutangulia na waliopo pia.

3. Mlezi wa Maono yako/Ndoto zako/Malengo yako/Biashara Yako/Pesa. (Coacher).

Mtu huyu ni wa muhimu pia katika maisha yako.

Unataka kumiliki utajiri wa dollar billion moja lazima utafute mtu wa kukulelea na kukuwezesha ufikie huko.

Huwezi kwenda mwenyewe.

Unahitaji mtu wa kukuongoza kwenye kila unachotaka kukifanya.

Wengi wanakata tamaa kwa kua hawana watu hawa wa kuwalelea.

Mtu huyu anatakiwa awe anakufuatilia hatua kwa hatua kwenye kile unachokifanya.

Awe anapata taarifa za maendeleo yako kila wakati ikiwezekana hata kila week.

Ukipata mafanikio yeyote ajue pia ukipata changamoto ajue.

Mtu huyu anatakiwa awe amekupita kwenye kile unachokitaka na hapa huendi kuwa Follower,anakwenda kukutengeneza wewe uwe kiongozi.

Uweze kusimama mwenyewe na hatimae uongoze wengine.

Kwa Tanzania wapo watu wanaofanya kazi hizi kwa malipo pia.

Lakini hapa unaweza kuanza na mtu ambaye una mahusiano nae ya karibu awe anakulelea.

Siku hizi teknolojia imekua rahisi sana unaweza kuwa na mawasiliano na mtu yeyote unayemtaka popote alipo duniani.

Unaweza kujifunza pia vitu vingi sana kupitia mitandao hii kama hapa facebook.

Unaweza kusoma vitabu na vitu vingi sana vile unavyovitaka.

Naomba nimalizie kwa kusema kwamba.
Kwa hiki ulichokipata leo ukikifanyia kazi.

Utakua mshindi uliyezaliwa kuwa.

Utafikia Hatma yako kwa kufuata haya, namaanisha wewe uliyesoma hapa.

I will see you at the top!

JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

Soma kidogo hapa.. Kuna watu wa aina NNE tunapoongelea pesa na muda.

1. WANA MUDA MWINGI ILA HAWANA PESA

Watu ambao hawana pesa ila wana muda wa bwerere. Hawajui thamani ya muda. Hawa ndo wale ambao hawajui cha kufanya. Anaamka mpaka analala usiku hana specific timetable. Unaweza kumkuta anaenda dukani ukamwambia nisindikize saluni na akakubali. Yupo yupo tu. Unaweza kuta ameingia Facebook hajui hata kwa mini. Basi tu kwa sababu ana bando. Akiperuzi akaona mahali wanaongelea mpira yumo. Akiscroll post za chini akakuta kuna mtu kapost kuhusu UKAWA yumo. Akikuta kuna mtu kapost mtu ana uvimbe mkuuubwa watu wameambiwa wacomment AMEN na yeye huyo anacomment AMEN. Akikuta watu wanaongelea TRUMP na yeye anaingia kucomment. Kundi hili ni kundi lenye watu wengi mno. Watu wa aina hii kufanikiwa ni bahati nasibu. Labda kwa bahati tu akutane na post nzuri kama hii na post zingine nzuri huenda ikamsaidia. Otherwise hawa ndo hawaelewi maisha yanaenda wapi maana hawana kitu fulani specific wanachofanya. Wakisikia tu kuna kitu kiko kama dili hivi wanaenda. Wakikuta kumbe kinahitaji bidii na kujituma wanaondoka. Wanataka maisha mazuri yaje tu yenyewe.

2. WANA PESA ILA HAWANA MUDA

Hili ni kundi la watu wenye shughuli fulani ya kiuchumi. Labda ameajiriwa au amejiajiri. Wako busy kweli kweli. Na ukweli pesa inaonekana. Hawa huwezi kumwambia njoo tuonane akaja hapo hapo. Huyu lazima apange kwanza ratiba zake. Maana yupo busy. Au lazima aombe ruhusa kazini maana hana uhuru na muda wake. Muda wake kamuuzia mtu (mwajiri). Au labda atoroke ndo anaweza kupata muda wa kufanya mambo yake binafsi. Au asubiri weekend ambapo kila ratiba itategemea siku hizo mbili, kama ni ibada, usafi, kutembelea wagonjwa au ndugu kwenda mahali kuona labda kiwanja kinauzwa au kuona ujenzi au mradi wake unaendeleaje nk. Mara nyingi watu wa kundi hili hushindwa kufanya vitu vingi vinavyohusu maendeleo yako binafsi mfano kujisomea, kuhudhuria semina zinazofundisha mambo yanayoweza kuwa na manufaa kwake nk. Sababu ana ratiba iliyobana. Ukiwa na sherehe ukamwomba mchango hashindwi kukuchangia angalau chochote kile lakini muda wa kuja kujumuika na wewe ni vigumu akaupata.
Hili ni kundi ambalo kuna watu wanaitwa MIDDLE CLASS people. Watu wa maisha ya kati. Mambo yako si mabaya sana lakini si kwamba ni mazuri. Wasomi wengi na watafutaji wengi wapo hapa. Afu ndo wanahisi wanajua kila kitu. Na wengi wao huishia kupata changamoto za kifedha na kiafya ukubwani au uzeeni kama stress na maradhi mbali mbali nk. Sababu ya kutokuwa na muda hata wa kuangalia wa kuinvest na kujifunza biashara au ujasiriamali mapema wala kujishughulisha na afya zao, mazoezi, kupumzika vizuri nk kwa kuwa walikuwa busy siku zote. Maisha ya watu hawa middle class mwishoni huja kuwa magumu kwa kuwa hata kuwa na muda na majirani tu ilikuwa ishu. Kwa kuwa wengi wana magari (mengi ni mkopo. Wengine gari la kazini) na kwa kuwa wanaweza kulipa kodi ya nyumba au hata kupata kakiwanja na kuanza kujenga huko Malamba Mawili basi wanaridhika. Hawawezi kuota kumiliki nyumba Masaki au kununua kiwanja Upanga. Kama upo kundi hili lazima uanze kutafuta mbinu mbali mbali za kuyakabili maisha vizuri siku za usoni. Waangalie wastaafu ambao walikuwa busy zamani. Saivi utasikia mgongo, miguu, macho nk vinasumbua. Hawa middle class people ndo ukimkuta social media wengi wao wako critical kwa kila kitu. Maana haoni kama ana shida yoyote.

3. HAWANA MUDA WALA HAWANA PESA

Ulishasikia mtu anaambiwa “busy for nothing”? Ni kitu kama hicho. Yani mtu unakuta labda ni kibarua tu mahali anatumwa kazi asubuhi mpaka jioni. Labda ameajiriwa kazi ya ulinzi, au gereji, au kwenye mradi wa ujenzi anabeba zege au kupaka rangi. Hashindi njaa ni kweli lakini ukweli hana hela. Wala hatamani kuendelea kuwa hivyo. Kuamka alfajiri kulala saa tano usiku. Hela anayopata inatosha kula kwa mama ntilie tu na nauli. Basi. Hawezi kuota hata gari. Hata ya mkopo. Maana hata hakopesheki. Huyu hata muda wa Facebook ni nadra akiingia ni kupitisha macho afu anatoka. Au hata simu ya Facebook hana.

4. WANA MUDA NA WANA PESA

Hapa ndo utakuta wale ambao hana tena shida ya pesa. Pesa iko. Hana tena shida ya muda. Akihitaji kwenda mahali haombi ruhusa wala kuaga mtu labda kumuaga mwenza wake tu. Anaweza kusikia kuna shamba linauzwa mahali na hahitaji kutafuta hela tena ili akalinunue bali anaanza michakato ya kisheria pale pale kununua kama amelipenda. Kuna siku nilienda Morocco Square hapo Kinondoni jirani na Airtel kuna Apartments zinajengwa nikaonana na watu wa NHC waliokuwa wanakagua ujenzi unaendeleaje. Nikawauliza hizo apartments zinauzwaje wakasema kuna za milioni 600 na za milioni 800. Na unatakiwa kulipa cash 10% (yaani aidha milioni 60 au 80 cash) halafu inayobakia unaweza kuimalizia ndani ya miezi 12. Na kuna watanzania kadhaa wamenunua tena kwa hela halali. Hawa wako kundi hili hapa. Hela ipo. Muda upo. Kuna watu walienda kutembea Marekani kibiashara walipokuwa njiani kurudi wakapita mahalinchi nyingine wakakuta kuna mnada wa nyumba kwenye nchi hiyo. Hawakujiuliza mara mbili wakanunua. Kuna wazee fulani wana mtoto wao alikuwa akisoma Canada. Alipograduate wakamuuliza unataka kuishi wapi akasema huku huku Canada wakamnunulia nyumba Canada. Ukisikia hivyo unaanza kuwaza ni mafisadi. Mawazo yako ninkuwa bila ufisadi watu hawanunui nyumba Canada. Kwa taarifa yako Hawa siyo waajiriwa serikalini wala popote ni wafanya biashara.. Kundi la watu kwenye pesa. Na muda. Wanaweza kuamua kesho wakaenda kutembea visiwa vya Comoros. Watu wanaoishi kundi hili wana discipline kubwa ya maisha. Na watu wengi wanatamani kufika kundi hili. Lakini HAWANA discipline ya kujifunza tabia zinazoweza kukufikisha huko.

Swali muhimu tu la kujiuliza tu ni kuwa je, wewe upo kundi lipi.

Una muda mwingi lakini huna hela? = FUKARA

Una hela nyingi lakini huna muda? = MIDDLE CLASS

Huna muda wala huna hela.. Vijisenti unavyopata vinaishia nauli kula kodi ya nyumba nk? = MASKINI

Au una muda mwingi na hela siyo shida tena? = TAJIRI

Maswali na Majibu kuhusu Kanisa Katoliki

Sala ya kanisa ni nini?

Sala ya kanisa ni sala maalumu wasaliyo Maklero, Watawa, na Walei kwa ajili ya Kanisa zima


Vyanzo vya sala za Kikristo

Vyanzo vya sala za kikristo ni;
1. Neno la Mungu
2. Litrujia ya kanisa
3. Fadhila za Kimungu
4. Matukio ya kila siku


Je, ni sahihi kusali sala kwa kurudia rudia mfano Novena?

Ndiyo, Hii ni kwa sababu sala nyingi za kurudia ni za Ahadi na zinasaliwa ili kutimiza ahadi ile. Mfano Novena husaliwa kwa siku 7 au 9 kwa nia ya kupata kile kilichoahidiwa au kinachodhamiriwa. Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli wafanye Ibada maalumu kwa kurudiarudia mfano wakati walipoangusha kuta za Yeriko walifanya Ibada maalumu kwa siku 7 (Saba).
“Waisraeli walipopita waliagizwa na Mungu kuzunguka Mji wa Yeriko 2Kisha BWANA akamwambia Yoshua,“Tazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na watu wake wa vita. 3Zunguka mji mara moja pamoja na watu wako wote wa vita. Fanya hivi kwa siku sita. 4Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo waume mbele ya sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo. 5Utakaposikia makuhani wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watakwea, kila mtu aingie ndani moja kwa moja kutokea pale alipo.’’ (Yoshua 6:2-5).
Naamani aliambiwa na Nabii Elisha aoge mara saba kwenye mto Yordani ili apone.
14Hivyo akashuka na kujizamisha ndani ya mto Yordani mara saba, kama vile huyo mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia, nayo nyama ya mwili wake ikapona na kutakasika kama ya mwili wa mvulana mdogo. (2 Wafalme 5:14)
Yesu alisali sala ya kurdia rudia kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.’’ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, “Je, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41‘‘Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.’’ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.’’ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Je ni makosa kurudia sala maneno yale yale kwa Mfano Rozari?

Hapana sio Makosa. Kwa Mfano Biblia inatuambia kuwa Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia.
“8Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema: ‘‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.’’ (Ufunuo 4:8).
Vile vile tunasoma katika kitabu cha Isaya kuwa malaika walikua wakimsifu na kumtukuza Mungu kwa sala/ maneno ya kurudiarudia. “Katika mwaka ule mfalme Uzia alipokufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza hekalu. 2Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa menngine mawili walifunika miguu yao na kwa mawili walikuwa wakiruka. 3Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni BWANA Mwenye Nguvu, Dunia yote imejaa utukufu wake.”
Kama Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia kwa nini sisi tukifanya hivyo tuwe tunakosea? Na sisi tunaweza kumuomba, kumsifu na kumtukuza Mungu kwa sala au maneno ya kurudiarudia kama walivyofanya malaika. Kwa hiyo sala za kurudia rudia sio makosa.
Tukiangalia Zaburi ya 136 inarudia maneno “kwa maana fadhili zake zadumu milele” mara 26 yaani kwenye mistari yake yote. (Zaburi 136:1-26)
Yesu pia allimuomba Mungu Baba kwa kurudia maneno yale yale kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.’’ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, “Je, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41‘‘Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.’’ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.’’ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Sala kwa Mkatoliki ni nini hasa? Tunaposema sala tunamaanisha nini hasa?

Sala ni kuongea na Mungu. Sala kwa Mkatoliki inajumuisha maombi, tafakari, ibada, taamuli, shukrani na sifa. Maana ya sala kwa Mkristo Mkatoliki sio kuomba tuu kama wanavyotafsiri watu wasio wakatoliki. Wengi wa wasio Wakatoliki wanaposema Sala wanamaanisha Maombi.
Kwa hiyo kwa Mkatoliki, Sala ni zaidi ya Maombi. Ndiyo maana kwa mkatoliki kuna sala za namna mbalimbali kama vile za Tafakari, za Maombi za Sifa na za kushukuru. Mfano sala ya Atukuzwe Baba sio maombi bali ni sala ya kumtukuza Mungu kwa maana hiyo sio Maombi, ndiyo maana husaliwa baada ya sala au matukio fulani kama ishara ya kumtukuza Mungu na kutambua ukuu wa Mungu

Yesu alifundisha tusali vipi?

Kisha Yesu akawapa wanafunzi Wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa.
2Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. 3Katika mji huo alikuwako mjane mmoja ambaye alikuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, ‘Tafadhali nipatie haki kati yangu na adui yangu.’ Wa Mjane Asiyekata Tamaa 4“Kwa muda mrefu yule hakimu alikataa. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, ‘Japokuwa simwogopi Mungu wala simjali mwanadamu, 5lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbuasumbua, nitahakikisha amepata haki yake ili asiendelee kunichosha kwa kunijia mara kwa mara!’ ” 6Bwana akasema, “Sikilizeni asemavyo huyu hakimu dhalimu. 7Je, Mungu hatawatendea haki wateule Wake wanaomlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasaidia? 8Ninawaambia, atawapatia haki upesi. Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?” (Luka 18:1-8)


Ni ipi sala kubwa ya Kanisa?

Sala kubwa ya Kanisa ni Misa Takatifu


Ni ipi sala bora kwa Bikira Maria? Kwa nini Tunasali kwa Bikira Maria?

Sala bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu

Kwa nini watu wengi wanaomba kwa Bikira Maria?

Watu wengi wanaomba kupitia Bikira Maria kwa sababu wanashuhudia sala zao kujibiwa kirahisi zaidi wanaposali kupitia Bikira Maria kwani Bikira Maria anatuombea kile tunacho mwomba. Bikira Maria anasimama Kama mwombezi wetu mbele ya Mungu hasa pale tunaposhindwa kusali Inavyotakiwa.

Bikira Maria anatuombea kwa jina na mamlaka ya nani?

Bikira Maria anatuombea kwa jina la Yesu Kristu na kwa mamlaka ya Yesu Kristu aliye mwanaye. Hakuna Sala yoyote inayotolewa kwa Bikira Maria moja kwa moja kwani Sala zote kwa Bikira Maria zinatolewa kwa kusema utuombee ikimaanisha kuwa utupelekee Maombi yetu kwa Mungu. Bikira Maria hatusaidii sisi moja kwa moja bali anatusaidia kwa kutuombea msaada kutoka kwa Mungu.

Je ni halali au ni sawa kwa Bikira Maria kutuombea kwa Jina la Yesu? Na Je tunajuaje kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu?

Ni halali na nisawa kabisa Bikira Maria kutuombea. Tunajua kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu kwa kuwa Yesu mwenyewe alituambia kuwa “asiyepingana na sisi yupo upande wetu”. Biblia iintuambia…
“Yohane akadakia na kusema “Umemwona Mtu mmoja akifukuza pepo kwa kutumia jina lako, nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa si mmoja wetu.” Lakini Yesu akawaambia, “Msimkataze kwani asiyepingana nanyi yupo upande wenu” (Luka 9:49-50).
Kwa hiyo Bikira Maria anapolitumia jina la Yesu bila kupingana na sisi wala Yesu ni ishara tosha kuwa ni mshirika wa Mungu (Yesu)

Je ni kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo?

Sio kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo/Kishetani
Sababu hizi zifuatazo zinadhihirisha kuwa Bikira Maria sio Malkia wa kipepo;
1) Kuomba kwa jina la Yesu: Angekua ni Malkia wa Kipepo asingeomba kwa Jina la Yesu. Kama ilivyoelezwa hapo juu. Biblia iintuambia linapotamkwa Jina la Yesu mapepo hukimbia. Sasa iweje yeye alitumie Jina hilo kutuombea Kama yeye ni pepo? (Luka 10:17)
2) Hafundishi uovu/dhambi: Mbali na kuomba kwa jina la Yesu, vilevile Yesu alituambia tuzichunguze roho na tutazitambua roho hizo kwa matendo yake. Kwa lengo hili tukichunguza kuhusu Bikira Maria tutaona kuwa Bikira Maria ni Mtakatifu aliye upande wa Mungu kwa sababu Mara zote alipowatokea watu amekuwa akifundisha na kuelekeza watu kuishi maisha ya utakatifu na kumfuata Mungu kweli kwa kutii amri zake na kufuata mafundisho ya mwanae ambayo ni yakuelekea katika utakatifu. Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalihusishwa na vitendo viovu au vya kuvunja Amri za Mungu.
3) Mafundisho yake yanaendana na Neno la Mungu (Biblia): Bikira Maria hajawaji hata mara moja kufundisha na kuelekeza vitu vilivyo nje ya Mafundisho ya neno la Mungu (Biblia). Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalikinzana na Mafundisho ya Neno la Mungu.
4) Anahubiri Wema, Unyenyekevu, Upole na Utii: mambo ambayo ni alama ya kudhihirisha Utakatifu.
5) Anasisitiza Upendo kwa Binadamu wenzetu na kwa Mungu: Anahubiri Upendo hasa kwa Maadui zetu na wale wanaoipinga Imani ya Kikristu na wanaomkataa Yesu Kristu. Anasisitiza mara zote Tumpende Mungu na kumtii.
6) Anahubiri Amani: Anahubiri Injili ya Amani na Mara zote anasisitiza tuombe amani ambapo amani ndio Ishara ya Utakatifu.
7) Hajitukuzi mbele ya Mungu bali anajinyenyekesha: Hajawahi kufundisha kwamba tumtukuze yeye au tumuheshimu yeye. Mara zote anahubiri tumheshimu Mungu pekee na kumtukuza Mungu. Amekua akijishusha kwa unyenyekevu huku akituelekeza tuige mfano wake wa unyenyekevu wa kumuelekea Mungu aliye Baba wa huruma na upendo.
8) Anaongeza imani kwa Mungu: Kwa sala na Ibada za Bikira Maria waumini wanapata kuongezewa Imani na Uchaji wao kwa Mungu. Wengi wanabadili maisha yao ya dhambi na kuelekea Maisha mema ya utakatifu ya Kumtumikia Mungu.
9) Sala Ibada yake inachanganyika na Ibada nyingine za Kikristu: Hakuna mgongano/ushindani wa Ibada kwa Bikira Maria na Ibada nyingine za Kikristu. Kama angekua ni pepo kamwe Ibada yake isingechanganyika na Ibada Takatifu.
10) Ibada kwa Bikira Maria Imedumu: Haikufifia wala kupotea bali ilizidi kuendelea vizazi hata vizazi. Hii inadhihirisha kwamba kuna Neema ya Mungu.
Kwa sababu hizi unaweza ukaona kwamba Bikira Maria anaushirika na Mungu na ni Mtakatifu.


Umwilisho maana yake ni nini?

Umwilisho ni ile hali ya Yesu kama Mungu kujifanya mtu kwa Bikira Maria mzaa. (Yoh 1:14)


Kanisa linafafanuaje fumbo la umwilisho?

Linatamka kuwa Yesu Kristo ni Mungu kweli na Mtu kweli. (Ebr 4:15)


Kanisa Katoliki ni nini?

Kanisa Katoliki ndio Jumuia ya Wakristu Wote pamoja na Maaskofu na Mapadri wanaoshiriki imani moja chini ya Baba Mtakatifu Mkuu wao


Ni nini Msingi wa Imani na Mafundisho ya Kanisa Katoliki?

Msingi wa Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki ni;
1. Biblia Takatifu
2. Mapokeo Matakatifu
3. Mamlaka ya Kanisa


Ni nani ameanzisha Kanisa Katoliki?

Yesu Kristo ameanzisha Kanisa Katoliki


Yesu aliweka makanisa mangapi? Yesu hakufanya makanisa mengi?

Hapana. Yesu alifanya Kanisa moja tuu.
Mungu ni Mmoja muumba na Baba wa wote, Mkombazi ni mmoja tuu, Yesu Kristo, Dini ni moja, Imani ni moja, Ubatizo ni mmoja, basi Kanisa ni moja kwa watu wote na nchi zote


Kwa kusudi gani Yesu alianzisha Kanisa?

Yesu alianzisha Kanisa kwa nia ya Kuutangaza na kuueneza Ufalme wa Mungu (Mt 28:19-20)


Kanisa linatimiza kusudi la Yesu Kristo kwa namna gani?

Kanisa linatimiza kusudi la Yesu Kristo kwa;
1. Kwa Ualimu wake yaani kuwafundisha watu
2. Kwa Ukuhani wake yaani kuwatakasa watu
3. Kwa Uchungaji wake yaani kuwaongoza watu.


Alama za kanisa la kweli ni zipi?

Alama za kanisa la kweli ni hizi;
1. Kanisa ni moja
2. Kanisa ni a Takatifu
3. Kanisa ni Katoliki
4. Kanisa ni la Kitume
5. Kanisa ni la Kimisionari


Kanisa ni Moja maana yake ni nini?

Kanisa ni moja maana yake ni la mahali popote na siku zote lina mafundisho yale yale, Sakramenti zile zile na mkubwa mmoja


Kanisa ni Takatifu maana yake ni nini?

Kanisa ni Takatifu maana yake:-
1. Limeanzishwa na Mungu mwenyewe aliye Mtakatifu
2. Kristo aliye Mtakatifu alijitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake ili kulitakasa
3. Roho Mtakatifu hulihuisha kwa upendo wake
4. Ndani yake wamo Bikira Maria na Watakatifu wengi wanaoliombea


Kanisa ni Katoliki maana yake ni nini?

Kanisa ni Katoliki maana yake ni la watu wote mahali pote na nyakati zote.


Kanisa ni la Kitume maana yake ni nini?

Kanisa ni la Kitume maana yake wakubwa wake yaani Baba Mtakatifu na Maaskofu nimahalifa wa Mitume


Kanisa ni la Kimisionari maana yake ni nini?

Kanisa ni la Kimisionari maana yake limetumwa kupeleka habari njema kwa mataifa yote. (Mt 28:19-20)


Yesu amemweka nani kuwa mkubwa wa Kanisa?

Yesu amemweka Mtume Petro kuwa Mkubwa wa Kanisa zima. (Mt 16:18-19). Halifa wa Mtume Petro ni Baba Mtakatifu.


Kanisa Katoliki laweza kudanganya katika mafundisho yake?

Hapana. Kanisa Katoliki haliwezi kudanganya katika mafundisho yake kwa sababu Roho Mtakatifu analilinda daima lisikosee na analiongoza. (Yoh 14:26).


Jimbo Katoliki ni nini?

Jimbo Katoliki ni Jumuiya ya Wakristo ambao katika Imani na Sakramenti wana ushirika na Askofu aliye halifa wa Mitume.


Tuwaonaje Wakristo ambao sio Wakatoliki?

Ingawa wamejitenga katika ushirika kamili wa Kanisa Katoliki, tunawatambua kuwa ndugu zetu kutokana na ubatizo wao.


Nje ya Kanisa Katoliki hakuna Wokovu maana yake ni nini?

Nje ya Kanisa Katoliki hakuna wokovu maana yake ni Mkatoliki akijiondoa katika kanisa au mtu akukataa kuingia wakati anajua Yesu ameanzisha limuokoe atapotea Motoni Milele.


Taifa la Mungu limeundwa kwa namna gani?

Taifa la Mungu limeundwa kwa Maklero yaani Maaskofu, Mapadri, Mashemasi, Watawa na Walei.


Maklero ni wakina nani?

Maklero ni watu wote wenye daraja Takatifu yaani Maaskofu, Mapadri na Mashemasi.


Watawa ni akina nani?

Watawa ni Waamini, Walei au Maklero waliowekwa wakfu kwa Mungu katika Kanisa kwa ajilli ya wokovu wao na wa dunia:-
1. Kwa kufunga rasmi nadhiri za Kitawa mbele ya Kanisa
2. Kwa kuishi masharti ya injili, utii, ufukara na useja mtakatifu.
3. Kwa kufuata mtindo wa maisha uliokubalika na Kanisa


Walei ni wakina nani?

Walei ni wote katika Kanisa wasio na Daraja Takatifu


Ushirika wa Watakatifu ni nini?

Ushirika wa Watakatifu ni:-
1. Umoja na ushirikiano kati ya Wakristo Duniani, Watakatifu Mbinguni, na marehemu toharani.
2. Ni muungano wa Waamini wote katika Ekaristi Takatifu.


Ni kwa nini Bikira Maria anaitwa Mama wa Mungu? Na kwa nini aheshimiwe?

Bikira Maria anaitwa Mama wa Mungu kwa sababu amemzaa Yesu na Yesu ni Mungu.
“Mwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Gabrieli aende Galilaya katika mji wa Nazareti, 27kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yosefu wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Maria. 28Naye malaika akaja kwake akamwambia: “Salamu, wewe uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!” 29Maria akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, “Salamu hii ni ya namna gani?” 30Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Maria, umepata upendeleo kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na utamwita jina lake Yesu. 32Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele na ufalme Wake hautakuwa na mwisho.” 34Maria akamwuliza huyo malaika, “Maadam mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?” 35Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, nazo nguvu Zake Yeye Aliye Juu zitakufunika kama kivuli, kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu. 36Tazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa. 37Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana. 38Maria akasema, “Tazama, mimi ni mtumisi wa Bwana na iwe kwangu kama ulivyosema.” Kisha malaika akaondoka akamwacha.”(Lk 1:26-38).
Yesu ni Mungu ndio maana Bikira Maria akaitwa Mama wa Mungu kwa sababu ndiye aliyemzaa Yesu. Yaani Bikira Maria ni Mama wa Mungu tuu kwa sababu ya kumleta Yesu Duniani kama mzazi wa kimwili.

Je, Bikira Maria kuitwa Mama wa Mungu maana yake ni kwamba yeye ndiye chanzo cha Yesu na Bila yeye Yesu asingekuwepo?

Hapana, haimaanishi kwamba Bikira Maria ni chanzo cha Yesu. Hii haimaanishi kwamba Bikira Maria ni Mama wa Yesu kabla ya Yesu kuja Duniani kwa maana Yesu Alikuawepo kabla ya kuzaliwa kwake.
“Baba yenu Abrahamu alishangilia kwamba angaliiona siku Yangu, naye akaiona na akafurahi.’’ 57Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza hata miaka hamsini, Wewe wasema umemwona Abrahamu?’’ 58Yesu akawaambia, ‘‘Amin, amin, nawaambia, kabla Abrahamu hajakuwako, ‘Mimi niko.’’’ (Yohane 8:56-58)
Inamaana kuwa Yesu alikuwepo kabla ya Mama yake. Kwa sababu hiyo Umama wa Bikira Maria ni wa Kimwili tuu na sio Umungu. Bikira Maria hajatangulia kuwepo kabla ya Yesu Bali Yesu ndiye alikuwepo kabla na ni Mungu wake pia. Yesu kama Mungu alimuumba Bikira Maria na kumfanya Mama yake wa kimwili.
“Usiogope, Maria, umepata upendeleo kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na utamwita jina lake Yesu. 32Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele na ufalme Wake hautakuwa na mwisho.” (Luka 1:31-33)
Bikira Maria alipewa nafasi ya kipekee na Mungu kuwa Mama yake na ingewezekana nafasi hii apewe mwanamke mwingine kama Bikira Maria Asingekuwepo au asingekuwa tayari kupokea heshima hii. Ndiyo maana Bikira Maria katika unyonge wake alitambua kuwa ni nafasi ya upendeleo wa Mungu aliyopewa na hivyo alimshukuru na kumtukuza Mungu kwa nafasi hii.
41Naye Elizabeti aliposikia salamu ya Maria, mtoto aliyekuwa tumboni mwake akaruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu, 42akapaza sauti kwa nguvu akasema, “Umebarikiwa wewe miongoni mwa wanawake, naye mtoto utakayemzaa amebarikiwa. 43Lakini ni kwa nini mimi nimepata upendeleo kiasi hiki, hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? 44Mara tu niliposikia sauti ya salamu yako, mtoto aliyeko tumboni mwangu aliruka kwa furaha. 45Amebarikiwa yeye aliye amini kwamba lile Bwana alilomwambia litatimizwa.” 46Naye Maria akasema: “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, 47nayo roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu, 48kwa kuwa ameangalia kwa fadhili unyonge wa mtumishi wake, hakika tangu sasa vizazi vyote vitaniita mbarikiwa, 49kwa maana, Yeye Mwenye Nguvu, amenitendea mambo ya ajabu, Mtakatifu ndilo Jjina Lake.” (Luka 1:41-49)

Je Bikira Maria anamwonaje Yesu? Bikira Maria Anamchukulia Yesu kama nani Kwake?

Bikira maria anamwita Yesu Mwanae wa kumzaa kwa kuwa Bikira Maria ndiye aliyemzaa Yesu Duniani na kumlea kama mtoto wake. Vilevile Bikira Maria anamwita Yesu Bwana na Mungu wake kwa kuwa ni Mungu wake pia. Kwa sababu hivyo Bikira Maria ni mdogo mbele ya (Yesu) Mungu kama kiumbe cha Mungu (Yesu).

Kwa nini Bikira Maria anapewa Heshima kubwa

Tunamuheshimu Bikira Maria kwa sababu ya nafasi yake ya kipekee ya upendeleo aliyopewa na Mungu ya Kuwa Mama wa Mungu. Tunapomuita Bikira Maria Mama wa Mungu tunaheshimu nafasi yake ya kipekee ya kuizalia Dunia Yesu aliye Mungu na Mkombozi wetu.

Je, Bikira Maria anastahili kuabudiwa? Je Tunamwabudu Maria?

Hapana, Bikira Maria hastahili kuabudiwa na wala hatumuabudu Maria. Kwa kuwa Bikira Maria ni kiumbe wa Mungu na ni Mdogo kuliko Mungu kwa hiyo hana Umungu wowote hivyo haabudiwi kama Mungu au pamoja na Mungu.

Kwa nini tunamuheshimu Bikira maria na kusali kwake?

Tunamuheshemu Bikira Maria na Kumuomba atuombee kwa Mungu mwanaye Yesu kwa sababu anayo nafasi ya kipekee mbele ya Mungu mwanaye Yesu kama Mama yake wa kumzaa Duniani na kama mlezi wake akiwa duniani tangu kuzaliwa mpaka kufa Msalabani wakiwa pamoja.
Yesu mwenyewe alimtii na kumsikiliza Mama yake ndio maana muujiza wa kwanza aliofanya aliambiwa na mama yake. Bikira Maria ndiye aliyemwomba Yesu Afanye muujiza wake wa kwanza.
1 Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. 2Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. 3Hata divai ilipowaishia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. 4 Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. 5Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia, fanyeni. 6 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kunawa, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. 7Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza mpaka juu. 8Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa sherehe. Wakapeleka. 9Naye mkuu wa sherehe alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa sherehe alimwita bwana arusi, 10akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; na watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa. 11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. Yohana 2:1-11


Ni kwa nini Bikira Maria anaitwa Mama wa Kanisa?

Bikira Maria anaitwa Mama wa Kanisa kwa sababu ni yeye aliyemzaa Yesu Kristo ambaye amelianzisha Kanisa.


Bikira Maria anafaida yeyote kwa Kanisa?

Ndiyo. Bikira Maria ni mwombezi Mkuu wa Kanisa.


Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria ni ipi?

Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria inafuata baada ya Heshima kwa Utatu Mtakatifu


Kwa nini wakatoliki wanaweka sanamu Kanisani?

Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22)
Hata Waisraeli kwenye hekalu lao walikua na sanamu kama tunavyosoma hapa;
“18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :18-22.)
Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe aliagiza Sanamu za Malaika zichongwe na kusema atakua hapo na kuongea na watu wake. Je sio vyema zaidi kuwa na sanamu na Picha ya Mwanae wa Pekee Yesu Kristo na kuongea na Mungu mbele yake kama alitaka ya malaika ambao sio Mungu?
Mfano mwingine ni pale Mungu alivyomwabia Musa achonge Sanamu ya Nyoka wa shaba.
“BWANA akamwambia Mose, “Tengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti, ye yote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.’’ 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu ye yote alipoumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.” (Hesabu 21:8-9).
Kwa Mfano huu Je tunaweza kusema kuwa sanamu ya nyoka ina nguvu ya uponyaji kuliko ya Yesu aliye Mungu? Kumbuka hapa watu walioona sanamu hii ya nyoka hawakukoponywa na nguvu ya sanamu ya shaba bali kwa nguvu ya neema ya Mungu kupitia Imani kwa Mungu. Kwa hiyo unaposali mbele ya picha au sanamu hautegemei nguvu ya sanamu bali unategemea neema ya Mungu kwa njia ya Imani yako kwa Mungu.
Kama vile Sanamu hii ya nyoka aliyoagiza Mungu iwekwe ilivyowekwa kwa nia ya uponyaji kwa yule aitazamaye vivyo hivyo Sanamu na Picha za Kanisani zinawekwa kwa nia maalumu na kwa neema maalumu. Ndiyo maana hazifanani. Na zinabarikiwa kwa kuombewa Baraka Ili zizae neema kwa wanaozitumia.

Sanamu au picha sio haramu bali maana ya hiyo sanamu au picha ndio inaiharamisha.

Kuna tofauti kati ya kuabudu na kuheshimu. Wakatoliki wanaweka sanamu kwa heshima na sio kwa kuabudu, ndio maana unaposali mbele ya picha ya Yesu hausali ee sanamu nisaidie bali unasema ee Yesu nisaidie.
Je tuseme tunamwabudu Raisi kwa kuheshimu picha yake kwa kuiinamia? Je tunaabudu bendera kwa kuheshimu na kupigia saluti? Je taratibu zabunge za kutoa heshima na taratibu za mahakama ni kuabudu?. Je kuapa mbele ya picha ya Raisi ni kumuabudu Raisi? Je kuapa na Biblia ni kuabudu Biblia? Je tunapobusu Biblia na kuitunza kwa heshima tunaiabudu? Tofauti ya Biblia na sanamu ni nini? Je, kwenye Biblia kinachoheshimiwa ni karatasi au maana ya yale maneno kwenye karatasi. Pengine usingeheshimu kama hujajua kuyasoma.
Kuna tofauti gani kati ya biblia yenye Maandishi na msalaba wa kuchonga wenye kuonyesha kile kinachosemwa na biblia? kama unaweza kuheshimu biblia yenye karatasi tena pale unapoweza kuzisoma na pengine ungeizarau kama ni ya lugha tofauti na hujui kilichoandikwa? Je Msalaba uliobeba maana ya kile kilichoandikwa kwenye Biblia unaona si kitu? Kama Kinachoheshimiwa kwenye Biblia sio karatasi bali maana maneno yaliyoandikwa vivyo hivyo kinachoheshimiwa kwenye picha au sanamu sio chuma yake au mti ukiochongwa bali ni maana ya hiyo sanamu.
Hii ndio maana nasema kuna tofauti ya kuabudu na kuheshimu.
Kumbuka kuwa picha au sanamu yoyote ya Kikatoliki lazima ibarikiwe kwanza ndio uweze Kusali mbele yake. Inapobarikiwa inaombewa uwepo wa yule anayewakilishwa na picha/sanamu hiyo uwe pale sanamu ilipo na anayesali pale sala yake Ifike kwa mlengwa anayeonekana kwa ishara ya sanamu/picha. Kwa Mfano askofu au padri anapobariki sanamu ya Yesu anaomba kuwa “Yesu awepo pale kwenye sanamu na Neema zake”, kwa hiyo yeyote anayesali mbele ya sanamu hiyo anaamini kuwa Yesu yuko pale na anasali Mbele yake. Kwa hiyo kinachopewa heshima sio ile sanamu bali ni yule anayeonekana kwa ishara ya ile sanamu au picha.

Tofauti ya Sanamu za Kikatoliki na za kipagani ni Kwamba,

Sanamu za Kipagani: Sanamu hizi huchukuliwa kama Mungu na huabudiwa na kutolewa Sadaka kama Mungu Mwenyewe.

Sanamu za Kikatoliki: Sanamu hizi huchukuliwa kama ishara ya kile inachokiwakilisha, haiabudiwi kamwe bali inaheshimiwa tuu.

Daima Tumia Sanamu na Picha zilizobarikiwa kwani zimenuiwa uwepo wa yule inayemuwakilisha na utaongea naye hapo. Sisi tunaamini kwamba kwenye Sanamu ya Yesu kuna uwepo wa Yesu. Kama vile Mungu anavyowaambia Waisraeli katika (Kutoka 25 :22) baada ya kuwaagiza wachonge sanamu za Makerubi (Malaika) 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :22)Sanamu au picha ni ishara wazi ya uwepo wa kile kisichoonekana.

Jifunze kupitia Sanduku la Agano na Msalaba wa Yesu

Kwenye Agano la kale: Ndani ya hekalu la Waisraeli walikua na Sanduku la agano, sanduku hilo lilikua na vibao vya Amri za Mungu ambavyo ni Ishara ya Agano lao na Mungu na ndani ya sanduku kulikuwepo pia Mfano wa Kiti ambacho kimezugukwa na sanamu za viumbe kama malaika nyuso zao zikielekea kiti hicho Kutoka 25:10-22. Waisraeli walikua wanasali kuelekea sanduku la Agano wanapokuwa Hekaluni na hata wakiwa majumbani mwao walisali kuelekea upande lilipo Hekalu. Waisraeli walisali kuelekea Sanduku la Agano wakiamini kwamba Mungu yupo kati ya sanduku lile. Lakini sanduku lile halikuwa Mungu. Waisraeli waliona fahari juu ya Sanduku lile na walilithamini na kuliheshimu kwa kuwa lilionyesha uwepo wa Mungu na popote lilipokuwa waliamini Mungu yupo.
Kwenye Agano jipya: Wakristu wanasali Mbele ya Msalaba wa Yesu ambao unaonyesha kazi ya wokovu alioufanya Yesu kwa wanadamu ya Kuwakomboa watu kwa kifo chake Msalabani. Na Msalaba huo ni Ishara ya Ukombozi wa Agano jipya na la Milele. Kama ilivyokuwa kwa Sanduku la Agano, Wakristu wanaheshimu msalaba ambao ni ishara ya wokovu wao na wanaamini kuwa Mungu yupo kati ya Msalaba huo lakini Msalaba huo sio Mungu. Wakristu wanaona fahari juu ya msalaba wa Yesu kwa kuwa ndio ishara ya wokovu wao.
FUNZO:Kupitia Mfano wa Sanduku la Agano na Msalaba tunajifunza kuwa Vyote havikuwa Mungu ila vinaheshimiwa kwa Imani kuwa Mungu yupo pale. Vilevile, vyote ni ishara ya wazi ya Agano la Mungu na Wanadamu.

Kwa nini tunasali mbele ya Picha/Sanamu na Hasa kufanya Ishara ya msalaba?

Tunasali mbela ya sanamu kwa sababu tunaamini sanamu inaakisi uwepo wa mhusika aliyechorwa au kuchongwa kwenye hiyo sanamu/picha. Ndio maana wakatoliki wanasali kwenye picha au sanamu iliyobarikiwa tuu kwa sababu Sanamu inapobarikiwa inaombewa uwepo wayule anayewakilishwa pale.
Tunafanya ishara ya msalaba kwenye sanamu kama sala ya utangulizi ambayo inathibitisha kuwa hatuabudu kile kilichoko pale bali kile tunachokifanya tunakifanya huku tukikiri Umungu na Heshima ya Utatu Mtakatifu (Mungu; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.). Vile vile tunamtukuza Mungu katika Utatu Mtakatifu kwa sababu ya yule anayewakilishwa na picha au sanamu.

Kwa nini watu wanabusu picha na sanamu?

Hii ni ishara ya Upendo kwa yule anayewakilishwa kwenye picha au sanamu husika. Hata katika maisha ya kawaida watu hubusu picha za wazazi na wapendwa wao. Maana ni ile ile.


Je, inafaa tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi?

Hapana, haifai tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi wasiozingatia jinsi Yesu alivyolitimiliza kwa maneno na matendo hata wakamshutumu kutenda kinyume:
“Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato” (Yoh 9:16).
Alipofafanua amri 10 za Mungu alikariri:
“Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa… lakini mimi nawaambieni…” (Math 5:21,27,31,33,38,43).
Alipouliziwa unajisi wa vyakula kadhaa, alisisitiza,
“’Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni?’ Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote” (Mk 7:18- 19).
“Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Kol 2:16-17).
Hakika, mwili ni mzito kuliko kivuli chake.
Vile vile katika Warumi 4:16. Tunasoma “Kwa sababu hiyo, jambo hili lategemea imani, hivyo kwamba ahadi hiyo yatokana na neema ya Mungu, na kwamba ni hakika kuwa ahadi hiyo ni kwa ajili ya wote:si kwa wale tu wanaoishika sheria, bali kwa wale waishio kwa Imani kama Abrahamu. Yeye ni Baba yetu sote.”
Wakristo wengine wanachanganywa na wale wasioyajua maandiko na kuwataka washike sheria na Torati,basi tukisema ni lazima kushika sheria tutakua tunakataa kua Abrahamu hakuwa mtu wa Mungu maana kwa Abrahamu hatukuwa na Sheria wala Torati na alipata kibali machoni Pa Mungu tuu kwa Imani. Kumbuka pia Abrahamu alitahiriwa baada ya Kuwa tayari mtu wa Mungu kwa Imani yake na sio kwamba Kutahiriwa ndio kulifanya mtu wa Mungu.
Tumekombolewa kwa Imani na sio kwa Sheria. Wagalatia 5:18 “Lakini Mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria”
Hatumtumikii Mungu ili tuwe watu wa Mungu bali tukishakua watu wa Mungu ndio tunamtumikia Mungu.


Je, ufunuo wa Mungu unaweza kufafanuliwa rasmi na kila mtu?

Hapana, ufunuo wa Mungu unaweza kufafanuliwa rasmi na umoja wa Maaskofu tu, kwa kuwa ndio waandamizi wa Mitume 12 wa Yesu.
“Au je, neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?” (1Kor 14:36).
“Hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu” (2Pet 1:20-21).
Tunahitaji unyenyekevu wa Mwafrika ambaye shemasi Filipo alimsikia “anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, ‘Je, yamekuelea haya unayosoma?’ Akasema, ”Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza?’ Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye” (Mdo 8:30-31).


Tupokeeje ufunuo wa Mungu?

Tupokee ufunuo wa Mungu kwa kusadiki mafundisho ya Kanisa lake, ili tuzidi kumjua na kuambatana naye bila ya kudanganyika. Yesu aliwaambia Mitume wake,
“Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma” (Lk 10:16).
“Sisi nasi twamsukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kwelikweli, litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini” (1Thes 2:13).


Tunaweza kusadiki vipi?

Tunaweza kusadiki kwa msaada wa Roho Mtakatifu tu, anayetuelekeza kwa Mungu, akituangazia Neno lake na kutuvuta tulikubali kwa moyo.
“Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu” (Yoh 7:17).
“Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu kweli, nanyi mnajua nyote” (1Yoh 2:20).
Kumbe, “Mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni” (1Kor 2:14).


Je, miujiza inaweza kutusaidia tusadiki?

Ndiyo, miujiza inaweza kutusaidia tusadiki, lakini inaweza kutudanganya pia.
“Wakati huo mtu akiwaambia, ‘Tazama, Kristo yupo hapa’, au, ‘Yuko kule’, msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu, wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule” (Math 24:23- 24).
“Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru” (2Kor 11:13-14).
Alipomshawishi Yesu alitumia hata maneno ya Biblia “akamwambia, ‘Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini, kwa maana imeandikwa: Atakuagizia malaika zake, na mikononi mwao watakuchukua, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe” (Math 4:6).


Kanisa linahusika vipi na imani?

Kanisa linahusika na imani kama mama wa waamini wote, kwa sababu imani yake inatangulia, inazaa, inategemeza na kulisha imani yetu: lenyewe ni “nguzo na msingi wa kweli” (1Tim 3:15).
Tukiondoa nguzo na msingi, nyumba ya ukweli haiwezi kusimama.
“Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa?… Basi imani, chanzo chake ni kusikia” (Rom 10:13-15,17).
Hivyo wokovu unategemea kupokea kwa imani maneno ya watu hai waliotumwa rasmi, sio Biblia peke yake. Mitume waliandika tu kwa kutegemeza mahubiri yao:
“Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uongo wowote utokao katika hiyo kweli” (1Yoh 2:21).
“Nitakuwa tayari kuwakumbusha hayo sikuzote, ijapokuwa mnayajua na kuthibitishwa katika kweli mliyo nayo” (2Pet 1:12).


Je, tukipata mafundisho ya Kanisa tunapaswa kuyasadiki?

Ndiyo, tukipata mafundisho ya Kanisa tunapaswa kuyasadiki kwa moyo mmoja tupate uzima wa milele, kwa kuwa Yesu aliwaambia Mitume,
“Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa” (Mk 16:16).


Tunapaswa kusadiki hasa nini?

Tunapaswa kusadiki hasa Utatu wa Mungu pekee, kwamba ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Milele yote Baba kwa jinsi alivyo ndani mwake anamzaa Mwana na kumvuvia Roho Mtakatifu, kama vile jua linavyotoa mwanga na joto lisitenganike navyo.
Mwana, ambaye “ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake” (Eb 1:3), alisema: “Nimekuja kutupa moto duniani” (Lk 12:49).
Naye Roho aliwashukia wafuasi wake “kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu” (Mdo 2:3-4).


Je, Mungu amegawanyika sehemu tatu?

Hapana, Mungu hagawanyiki hata kidogo, bali daima ni Umoja kamili.
“Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja” (Mk 12:29).
Tumuabudu yeye peke yake katika nafsi tatu, na Utatu wa nafsi katika Umoja wa hali yake, tusichanganye nafsi wala kugawa Umungu. Baba si Mwana wala Roho Mtakatifu. Mwana si Baba wala Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu si Baba wala Mwana. Lakini milele yote nafsi hizo tatu ni Mungu yuleyule pasipo tofauti ya kuzitenganisha: kila moja imo ndani ya nyingine.
“Mimi na Baba tu umoja” (Yoh 10:30).


Kwa nini Maria anastahili kuitwa “Mama wa Mungu”?

Maria anastahili kuitwa “Mama wa Mungu” kwa sababu Mwana wa milele wa Mungu, ambaye ni Mungu sawa na Baba, alifanyika mtu toka kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa: “Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?
” (Lk 1:42-43).

Je, Bikira Maria ni kama Bahasha au chombo cha kumleta Yesu tuu Duniani au anayo thamani zaidi?

Bikira Maria sio kama bahasha au chombo cha kumleta Yesu tuu duniani. Yesu ametokana na Bikira Maria katika ubinadamu wake. Mwili wa Yesu wa kiubinadamu ni sehemu au uzao wa Bikira Maria. Bikira Maria anayo uhusiano wa damu na Yesu Kristu. Ndiyo maana Mungu alimtakasa Bikira Maria Ili atakayezaliwa kutoka kwake awe na yeye mtakatifu.
Mungu alimtakasa Bikira Maria kabla ya Kuamua kuzaliwa kupitia yeye kwa kuwa Mungu ni Mtakatifu. Ubinadamu wa Yesu (MWILI – Nyama na Damu) asili yake ni Bikira Maria.


Kanisa maana yake nini?

Kanisa maana yake ni “kusanyiko”: ndani yake Roho Mtakatifu anaunganisha na Yesu na kati yao wale waliopokea Neno la Mungu na sakramenti zake.
“Bwana alilizidisha Kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa… Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja” (Mdo 2:47; 4:32).
Ndio tokeo la ombi la Yesu:
“Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako, hao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma” (Yoh 17:21).
Kumbe utitiri wa madhehebu yaliyotenganika unaleta picha ya “tawanyiko” ambayo inakwaza ulimwengu usisadiki.
“Kila mtu wa kwenu husema, ‘Mimi ni wa Paulo’, na, ‘Mimi ni wa Apolo’, na, ‘Mimi ni wa Kefa’, na, ‘Mimi ni wa Kristo’. Je, Kristo amegawanyika?” (1Kor 1:12-13).


Je, Kanisa ni kundi la binadamu tu?

Hapana, Kanisa si kundi la binadamu tu, tunaloweza kulianzisha kama vile chama, timu n.k.
Kanisa ni fumbo la Mwili wa Kristo unaohuishwa na Roho Mtakatifu. Kama Yesu linaonekana upande wa ubinadamu tu, kumbe linaunganisha utu na Umungu.
Baba “alivitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote” (Ef 1:22-23).


Je, tunaweza kuambatana na Yesu tukilikataa Kanisa?

Hapana, hatuwezi kuambatana na Yesu kwa kulikataa Kanisa, kwa kuwa hao wawili ni mwili mmoja, kama Bwanaarusi na Bibiarusi.
“Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, ‘Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe” (Math 19:4-6).
“Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa” (Ef 5:32).


Je, Kanisa ni muhimu kwa wote?

Ndiyo, Kanisa ni muhimu kwa wote kwa kuwa ndilo ishara na chombo cha umoja wa watu na Mungu na kati yao.
“Aliwapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba. Akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu. Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja” (Ef 2:16- 18).


Wokovu unapatikana wapi?

Wokovu unapatikana kwa Yesu tu, anayeishi katika Kanisa lake. Hata hivyo Roho Mtakatifu anaweza akaongoza mtu asiyewajua bila ya kosa lake aungane nao kiroho kwa kumlenga Mungu na kujitahidi kumtii kwa moyo wote.
“Tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa waaminio” (1Tim 4:10).
“Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye… Twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vilevile kama wao” (Mdo 10:34-35; 15:11).


Mtu akijua Kanisa ni la lazima kwa wokovu asiingie au ajitenge nalo, itakuwaje?

Mtu akijua Kanisa ni la lazima kwa wokovu asiingie au ajitenge nalo hawezi kuingia mbinguni.
“Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe” (1Tim 4:1-2).
“Watoto, ni wakati wa mwisho. Na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu” (1Yoh 2:18-19).


Je, anayejiunga na Kanisa na kudumu ndani yake ana hakika ya kuingia mbinguni?

Hapana, anayejiunga na Kanisa na kudumu ndani yake lakini haongozwi na Roho Mtakatifu kuishi kadiri ya ubatizo wake atahukumiwa na Mungu vikali zaidi kwa kuchezea neema kubwa hivi.
“Kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi” (Lk 12:48).


Sifa kuu za Kanisa ni zipi na zinapatikana wapi?

Sifa kuu za Kanisa ni kuwa moja, takatifu, katoliki na la Mitume. Sifa hizo zinalitambulisha kati ya madhehebu mengi Kanisa pekee lililoanzishwa na Yesu kumpitia Mtume aliyembadilishia jina aitwe Petro, yaani Mwamba wa Kanisa lake lisilokoma wala kupotoka kamwe:
“Wewe u Simoni, mwana wa Yohane; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro)” (Yoh 1:42).
Siku ya Pentekoste, “waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu” (Mdo 2:41).
Ndiye aliyekaribisha hata wasio Wayahudi: “Tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini” (Mdo 15:7).
Baada ya kuongoza Mitume wenzake na Kanisa lote, aliuawa msalabani huko Roma kama alivyotabiriwa:
“’Utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka’. Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu” (Yoh 21:18-19).


Kanisa kuwa moja maana yake nini?

Kanisa kuwa moja maana yake ni “mwili mmoja na Roho mmoja”: lina “Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja” (Ef 4:4-5).
Yesu alisema, “Na kondoo wengine ninao. Ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja” (Yoh 10:16).
Hakuna Kanisa lingine, isipokuwa matawi ambayo yamekatika kwa kiasi tofauti, na yana uhai kadiri yanavyounganika bado na shina. Hata leo Kanisa Katoliki peke yake lina waamini wengi kuliko jumla ya madhehebu mengine ya Kikristo.


Kanisa kuwa takatifu maana yake nini?

Kanisa kuwa takatifu maana yake ni kazi ya Mungu mtakatifu inayong’aa katika watakatifu wa mbinguni, hasa Bikira Maria.
“Ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu” (1Pet 2:9-10).
“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika Neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa” (Ef 5:25-27).
Hata hivyo hapa duniani linaundwa na wakosefu pia:
“Ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya wa kila namna. Hata lilipojaa, walilivuta pwani, wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa” (Math 13:47-48).


Kanisa kuwa katoliki maana yake nini?

Kanisa kuwa katoliki maana yake linaweza kuwatolea watu wote wa mahali pote na wa nyakati zote kweli zote za imani na vifaa vyote vya kufikia wokovu wa milele.
“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari” (Math 28:18- 20).


Kanisa kuwa la Mitume maana yake nini?

Kanisa kuwa la Mitume maana yake limejengwa juu ya Mitume 12 wa Yesu na kuongozwa na waandamizi wao.
“Ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo” (Ufu 21:14).
“Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Yesu Kristo mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho” (Ef 2:20-22).


Kanisa limepewa na Yesu muundo gani?

Kanisa limepewa na Yesu wahudumu wenye daraja takatifu wanaoitwa makleri; waamini wengine wanaitwa walei. Kutoka pande hizo mbili wanapatikana watawa waliowekwa wakfu kwa namna ya pekee kwa kushika mashauri ya Kiinjili.
Yesu “alipanda mlimani, akawaita aliowataka mwenyewe; wakamwendea. Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri” (Mk 3:13-14).
“Walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yohane, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo. Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake” (Mdo 1:13- 14).


Je, Yesu amejenga Kanisa lake imara juu ya mwamba?

Ndiyo, Yesu amejenga Kanisa lake imara juu ya Mtume Petro, alichunge lote kwa niaba yake. Papa kama Askofu wa Roma ndiye mwandamizi wa Petro na mkuu wa kundi zima la Maaskofu, waandamizi wa Mitume.
“Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda” (Math 16:18).
“Atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba” (Math 7:24-25).
Historia ya miaka elfu mbili sasa imedhihirisha ukweli wa maneno hayo.


Papa amejaliwa na Mungu mamlaka gani?

Papa amejaliwa na Mungu mamlaka kamili juu ya waamini wote awafungulie ufalme wa mbinguni, kama Yesu alivyomuambia Petro: “Nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Math 16:19).
“Nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako” (Lk 22:32).
“Lisha wanakondoo wangu… Chunga kondoo zangu… Lisha kondoo zangu” (Yoh 21:15-17).


Maaskofu wote wamerithi mamlaka gani?

Maaskofu wote wamerithi mamlaka ya Mitume kwa kufundisha, kutakasa na kuongoza Kanisa lote pamoja na Papa na chini yake.
Wale waliokabidhiwa jimbo fulani ni msingi wa umoja kwa waamini wao na kati yao na Kanisa lote duniani.
“Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe” (Mdo 20:28).


Maaskofu wanasaidiwa na nani?

Maaskofu wanasaidiwa kwanza na mapadri katika uchungaji, halafu na mashemasi katika utumishi.
“Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye: lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia” (1Pet 5:1-2).
“Paulo na Timotheo, watumwa wa Kristo Yesu, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walioko Filipi, pamoja na Maaskofu na mashemasi” (Fil 1:1).


Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lingekuwaje?

Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lisingekuwepo kwa sababu uhai wake unategemea kabisa ekaristi iliyokabidhiwa kwao.
“Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja” (1Kor 10:16-17).
Bila ya ekaristi tusingekuwa Kanisa, bali jumuia tu, kama madhehebu mengi yaliyojichagulia viongozi wasioshirikishwa hizo daraja takatifu kwa kuwekewa mikono na mwandamizi wa Mitume.
“Uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu” (2Tim 1:6).
“Nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru” (Tit 1:5).
“Usimwekee mtu mikono kwa haraka” (1Tim 5:22).


Walei wanaitwa na Mungu kufanya nini?

Walei wanaitwa na Mungu kuratibu malimwengu yote yafuate matakwa yake.
“Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima” (Rom 13:7).
“Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema” (Tit 3:1).
“Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu; kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu” (1Pet 2:15-16).


Watawa wanashika mashauri gani ya Kiinjili?

Watawa wanashika hasa mashauri ya useja mtakatifu, ufukara na utiifu ambayo msingi wake ni maisha na mafundisho ya Yesu kadiri ya Injili.
“Wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee” (Math 19:12).
“Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate” (Math 19:21).
“Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo” (Yoh 15:14).


Ushirika wa watakatifu maana yake nini?

Ushirika wa watakatifu maana yake sisi, kwa kushiriki mafumbo matakatifu tunaunda ndani ya Kristo mwili mmoja, ambamo waadilifu waliopo duniani, marehemu wa toharani na wenye heri wa mbinguni tunaunganishwa na upendo tufaidike na mema ya kila mmoja.
“Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana. Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia” (Rom 14:8-9).
“Kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho. Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake” (1Kor 12:26-27).
Dhambi yoyote kubwa inatutenga na ushirika huo kama Yesu alivyosema,
“Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa” (Yoh 15:1-2).
Lakini “Mungu aweza kuwapandikiza tena… Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake” (Rom 11:23,29).


Je, Kanisa linaweza kutuondolea dhambi yoyote?

Ndiyo, Kanisa linaweza kutuondolea dhambi yoyote katika ubatizo na kitubio kwa kutumia mamlaka ambayo Yesu mfufuka aliwashirikisha Mitume wake alipowavuvia akisema:
“Pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa” (Yoh 20:22-23).
“Mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu” (1Kor 6:11).


Ekaristi maana yake nini? Je ni kweli Yesu yupo katika Maumbo ya Mkate na Divai?

Ekaristi maana yake ni shukrani, iliyokuwa msimamo wa msingi wa Yesu kwa Baba maisha yake yote, hasa alipofikia wakati wa kutolewa awe kafara ya wokovu wetu.
23Maana mimi nilipokea kwa Bwana yale maagizo niliyowaachieni: Kwamba, usiku ule Bwana Yesu alipotolewa, alitwaa mkate, 24akamshukuru Mungu, akaumega, akasema: “Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka.” 25Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe cha divai, akasema: “Hiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.”
26Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja. 27Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana. (1Kor 11:23-27).

Yesu alituambia nini kuhusu Mwili wake na damu yake?

Yesu alituambia hivi;
“Baba zenu walikula mana jangwani, lakini wakafa. 50Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni, ambao mtu ye yote akiula, hatakufa. 51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.’’ 52Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?’’ 53Hivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu. 54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. 57Kama vile Baba aliye hai alivyonituma Mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu. 58Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.’’ (Yoh 6:49-58)

Damu na Mwili aliotupa Yesu ni nini? Ekaristi ni nini hasa?

Maana ya Damu na Mwili aliyoisemea Yesu tunaipata hapa;
“Walipokuwa wakila, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi Wake akisema, “Kuleni, huu ndio mwili Wangu.’’ 23Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa wanafunzi Wake, wote wakanywa kutoka humo. 24Akawaambia, “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. 25Amin nawaambia, sitakunywa tena uzao wa mzabibu mpaka siku ile nitakapokunywa mpya katika Ufalme wa Mungu.’’ 26Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda kwenye Mlima wa Mizeituni. (Marko 14:22-26).
Kwa hiyo Yesu alionyesha upi ni mwili wake na damu yake

Fundisho hili la mwili na damu ya Yesu (Ekaristi) lilikua Agizo tunalopaswa kulitii mpaka leo?

Ndiyo, Yesu alisema tufanye hivyo kwa ukumbusho wake
“Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, “Huu ni mwili Wangu unaotolewa kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.” (Luka 22: 19).
Kwa hiyo aliwaagiza Mitume wafanye hivyo pia.

Mitume walitii Fundisho la Ekaristi na waliliishi?

Ndiyo, Kila walipokutana Walishiriki Meza ya Bwana Kama tunavyosoma Kwenye vifungu vifuatavyo;.
46Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe, (Mdo 2:46).
7Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. (Mdo 20:7)

Je mkate na divai vilichukuliwa na Mitume kama nini hasa? walichukulia Ekaristi kama nini?

Mitume walichukua Mkate na divai kama mwili na damu ya Yesu Kristu na walishiriki kiaminifu na kwa usafi wa moyo.
16Je, kikombe cha Baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17(Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa wote twashiriki mkate mmoja) (1 Wakorinto 10:16)
27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. 31Lakini kama tungejipambanua wenyewe tusingehukumiwa. 32Tunapohukumiwa na Bwana, tunaadabishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu. (1Wakorinto 11:27-32)
21Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na cha mashetani pia. Hamwezi kuwa na sehemu katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. 22Je, tunataka kuamsha wivu wa Bwana? Je, sisi tuna nguvu kuliko Yeye? (1 Wakorinto 10:21-22)

Je ni lazima Kwa Mkristu kupokea Mwili na damu ya Yesu (Ekaristi)?

Yesu alisema hivi;
53Hivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu. 54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. (Yohana 6:53–56)

Je ni kwa nini madhehebu mengine hawakubali mafundisho haya ya Ekaristi Takatifu, Je ni mara ya kwanza watu kukataa?

Hii ni sababu ya ugumu wa mioyo na kutokuelewa maandiko ndio maana madhehebu mengine wanaukataa kwa dhati Mwili na Damu ya Yesu.
Hata wakati Yesu akiyasema maneno haya Wafuasi Wengi Walimwacha kama Biblia inavyosema;
60Wengi wa wafuasi Wake waliposikia jambo hili wakasema, “Mafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?’’ (Yohana 6:60).
Haishangazi hata leo weni hawaamini mafundisho haya japokua ndio msingi wa Imani ya Kikristo.

Mitume walifundisha nini kuhusu Mwili na Damu ya Kristu (Ekaristi)?

23Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule alipotolewa, alitwaa mkate, 24naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema “Huu ndio mwili Wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.” 25Vivi hivi baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu Yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho Wangu.” 26Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo. 27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. (1 Wakorinto 11:23-30)
Kwa hiyo Mitume waliwaasa Wakristu wa kwanza Kushiriki Mwili na Damu ya Yesu kila mara na kwa Uaminifu.

Je Yesu Yupo Mzima katika Ekaristi Takatifu? Na kwa nini Tunaabudu Ekaristi?

Ndiyo. Ekaristi Takatifu inamuwakilisha Yesu Mwenyewe aliye Mungu na aliyeamua Mwenyewe kuwepo katika Maumbo ya Mkate na Divai.
Ukisoma Yoh 6:51-57 inasema hivi;
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.’’ 52Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?’’ 53Hivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu. 54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. 57Kama vile Baba aliye hai alivyonituma Mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu. (Yoh 6:51-57)
Mstari wa 51 Yesu alisema wazi Mkate huo ni Mwili wake.
Thamani na Uwepo wa Yesu Mwenyewe unaonekana katika Mstari wa 53 na wa 56. Kumbuka hapa amesema “Mimi nitakaa ndani yake” Hakusema Mwili wangu utakaa ndani yake. Kwa maana nyingine ni kwamba Ekaristi ni Yesu Mzima na Sio Mwili tuu.
54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake.
Wale Wanaopinga fundisho la Ekaristi wanafikiri Yesu alivyosema Mimi ni Chakula Kutoka Mbinguni hakumaanisha Mwili bali Maneno na Imani Kwake lakini Tukisoma 51 Yesu alisema wazi kuwa Mwili wake ndio Mkate wenyewe.
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.’’
Mitume wa Yesu walielewa hivi fundisho hili ndio Maana walishiriki Meza ya Bwana kila walipokutana na waliheshimu kama Mwili na Damu ya Kristo.
7Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. (Mdo 20:7)
Ili kujua kuwa Mitume waliheshimu Mwili na Damu ya Yesu Biblia inatuambia hivi;
23Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule alipotolewa, alitwaa mkate, 24naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema “Huu ndio mwili Wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.” 25Vivi hivi baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu Yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho Wangu.” 26Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo. 27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. (1 Wakorinto 11:23-30)
Kwa hiyo Mitume walisisitiza kuhusu Mwili na Damu ya Kristu kuwa ni Mtakatifu.
Kwa hiyo basi kama tunavyosoma katika Yoh 6:51; na
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.’’
Yesu alisema Mimi ni Mkate wa Uzima ambao alimaanisha upo katika Mwili wake. Mwili tuu hauna uzima kama hauna Yesu ndani yake. Kwa sababu Mwili ni Mzima na Unaye Yesu ndani yake ndiyo maana unaweza kuleta uzima kwa Wengine.
Tunaelewa kwamba Yesu alijitoa Msalabani Mwili Wake na Damu yake na ndicho alichotupa ktk Ekaristi. Na Mwili wake huo Ulikua umembeba yeye aliye Mungu ndiyo maana tunaabudu Ekaristi alipo Yesu aliye Mungu.
Kwa kuwa Yesu ni Mungu Kama tunavyosoma katika Yoh 1:1-12
1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watu……..14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. (Yoh 1:1-12)
Kwa hiyo Neno huyo huyo Ndiye aliyetukomboa kwa kuutoa mwili wake sadaka Msalabani na ndiye Aliyetupa Mwili Wake na Damu yake ktk Ekaristi na anaabudiwa kwa kuwa yupo katika mwili huo.
“Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, “Huu ni mwili Wangu unaotolewa kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.” (Luka 22: 19).
Kwa namna hii alitupa mwili wake.
Alisema fanyeni kwa ukumbusho wangu na Sio wa mwili wangu.
Hivyo Ekaristi ni Yesu Mwenyewe aliye Mungu. Ndiyo sababu tunaabudu Ekaristi Takatifu.


Je, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na Kanisa?

Ndiyo, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na Kanisa kwa sababu kazi ya wokovu haimtegemei binadamu, bali Mungu.
“Hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu” (Eb 5:4-5),
Yesu alisisitiza alivyopewa na Baba uwezo wa kutuokoa. “Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake” (Yoh 3:35).
“Kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele” (Yoh 17:2)
.
Kisha kufufuka alitumia mamlaka hiyo kuwatuma wanafunzi kumi na mmoja waliobaki:
“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari” (Math 28:18-20).
Mpaka mwisho wa dunia uwezo huo wa Kimungu utatolewa tu kwa sakramenti ya daraja, inayounganisha mtu na Mitume kupitia mlolongo usiokatika wa kuwekewa mikono ili kushirikishwa mamlaka. Bila yake, kuna upungufu katika ufundishaji, utoaji wa sakramenti na uongozi.


Je, wenye daraja wanastahili heshima?

Ndiyo, wenye daraja wanastahili heshima kwa sababu ya mamlaka ya Kiroho waliyonayo kutoka kwa Kristo.
“Amin, amin, nawaambieni: Yeye ampokeaye mtu yeyote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenipeleka” (Yoh 13:20).
“Jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu” (Gal 4:14).
“Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii” (Tito 3:1).
Wenye daraja wanaotimiza kazi zao vizuri wanastahili heshima kwa uaminifu wao pia.
“Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu, hasa hao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha” (1Tim 5:17).


Kanisa linaheshimu marehemu kwa namna gani?

Kanisa linaheshimu marehemu kwa kuwafanyia mazishi huku likiwaombea kwa Mungu.
“Watu watauwa walimzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu” (Mdo 8:2).
Yeye kama mfiadini, aliyefikia upeo wa upendo kwa kutoa uhai wake, hakuhitaji kuombewa. Lakini wafu wengine walitolewa sala na sadaka tangu Israeli ilipoanza kusadiki ufufuo.
“Kama asingalitumaini kuwa wale waliokufa watafufuka, ingalikuwa kazi bure isiyo na maana kuwaombea wafu. Lakini kwa kuwa aliufikiri utukufu wa thawabu waliowekewa wale wafao katika utauwa, wazo lake lilikuwa takatifu na la kicho. Ndiyo sababu alifanya upatanisho kwa wafu ili wafunguliwe dhambi yao” (2Mak 12:44-46).
“Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?” (1Kor 15:29).


Je, Kanisa linahimiza waamini wapokee Ekaristi wakati gani?

Kanisa linahimiza waamini wapokee Komunyo Takatifu kila siku wanaposhiriki Misa


Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake

Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vinavyohusu kazi ya Mungu ya kuwakomboa mwanadamu kuanzia enzi za Mababu na manabii Wa Waisraeli, Enzi za Yesu na za Mitume wa Yesu.

Je, Biblia ilipatikanaje? Nini chanzo na asili ya Biblia.

Biblia iliundwa kwa kukusanya vitabu vya dini vya wakristo hapo awali na kuunda kitabu kimoja. Kwa maana hii, Biblia ni vitabu teule vya dini vilivyoonekana vinafaa kutumika kwa waumini Wakristo ili kusaidia Imani yao. Hivyo basi, kama Biblia ni vitabu teule tuu vipo vitabu vingine vya dini ambavyo havikuwekwa Kwenye Biblia.
Wakristo wa kwanza walichagua vitabu kadhaa na kuviweka pamoja na kisha kuvita Biblia. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu muhimu tuu vya dini mpaka kufikia Enzi za Mitume.

Je, Biblia ndicho kitabu pekee cha neno la Mungu?

Hapana, Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu isipokua Biblia ni kitabu kilichoidhinishwa rasmi kutumika Kama kitabu kikuu cha Wakristo. Hii ni kwa sababu Biblia imeundwa na vitabu muhimu tuu vilivyochaguliwa na wakristo wa kwanza vilivyoonekana vinafaa kwa kufundishia, Ibada na kukuza Imani. Kwa hiyo basi vipo vitabu vingine ambavyo haikuwekwa Kwenye Biblia ambavyo ni Maneno ya Mungu.
Hii ndiyo sababu kwa nini Wakatoliki wana vitabu vingi kuliko madhehebu Mengine. Yaani sababu ni kwamba madhehebu Mengine walivitoa vitabu vingine vilivyounda Biblia. Na Wakatoliki waliweka vitabu vingine vya dini Kwenye Biblia walivyoona vinafaa pia kutumika.

Je nje ya Biblia hakuna Neno la Mungu au Maandiko matakatifu?

Nje ya Biblia kuna Neno la Mungu na Maandiko Matakatifu. Hii Inamaanisha kuwa Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu. Zipo nyaraka na Vipo vitabu vingine vingi ambavyo viliandikwa na Manabii na Mitume ambavyo havikuwekwa kwenye Biblia lakini ni mafundisho ya Mungu. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vikuu vya Mungu.
Kumbuka kuwa sio nyaraka zote za Mitume ziliandikwa Kwenye Biblia. Vile vile manabii walikuwa ni wengi kuliko waliowekwa Kwenye Biblia.

Je Biblia ndiyo mafundisho ya Mungu pekee?

Hapana, Biblia sio mafundisho pekee ya Mungu. Hii ni kwa sababu sio mambo yote aliyofanya na kusema Mungu yaliandikwa na vilevile Mitume hawakua watu wa Mwisho kupokea Roho mtakatifu na kupokea neno la Mungu.

Biblia inatuthibitishia yenyewe kuwa haijakamilika na Si mambo yote yameandikwa Kwenye Biblia

Biblia inatuthibitishia kuwa haijakamilika tunaposoma (Yohane 21:25)
Biblia inatuambia hivi…”Kuna mambo Mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo Kama yangeandikwa yote, moja baada ya jingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.”…Kwa mstari huu Biblia inatuthibitishia kuwa haikuandikwa vitu vyote.

Je Biblia ni mwisho wa Maandiko ya Mungu?

Biblia sio mwisho wa Maandiko ya Kimungu.
Biblia ni sehemu ya maneno ya Mungu mpaka miaka ya Mitume
Hata sasa Mungu anafanya kazi na watu wake kupitia Roho Mtakatifu na kwa kwa sababu hii Biblia sio mwisho wa kazi ya Mungu ya kusema na watu wake.
Mungu yu hai na anafanya kazi na watu wake mpaka sasa kwa kutumia vinywa vya watu Kama aliyofanya hapo awali.
Hata maneno unayohubiriwa sasa yanaweza kuwa ni kutoka kwa Mungu kwa maana hata waandishi wa Biblia walitumiwa na Mungu Kama wahubiri wa sasa. Mungu ni yule yule, Roho Mtakatifu ni yuleyule na Neno ni lile lile.
Kwa hiyo Biblia ni maneno yaliyochaguliwa mpaka enzi za Mitume. Vitabu vilivyofwata Baada ya Mitume japokuwa viliandikwa kwa Roho Mtakatifu havikuwekwa Kwenye Biblia.

Sababu ya Kanisa katoliki kutumia mapokeo na Maandiko ya Watakatifu

Kanisa katoliki linatumia mapokeo na Makala za watakatifu kwa Imani kuwa Mungu yule yule aliyefanya kazi tangu zamani anafanya kazi na watu wake mpaka sasa na hivyo Maandiko ya watu wa Mungu yanafaa kutumika kama yalivyotumika ya watu wa kale.

Yesu alituambia nini kuhusu Neno la Mungu na Mwendelezo wa kazi ya Mungu ya kusema na watu?

Yesu alituambia hivi katika (Yohane 16:12-15)..”Ninayo mengi ya kuwaambieni Ila kwa sasa hamuwezi kuyastahimili. Lakini atakapokuja huyo Roho wa Ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote. Maana hatasema kwa Mamlaka yake mwenyewe bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja. Yeye atanitukuza Mimi kwa kuwa atawajulisheni Yale atakayoyapata kutoka kwangu “…
Sasa basi,kama Roho Mtakatifu ni yuleyule na kazi zake ni Zile Zile za tangu Mitume, kwa nini hatukubali kuwa Anafanya kazi mpaka sasa kupitia watu wa Mungu? Kwa nini tunakataa mafundisho yao? Kwa nini tunashindwa kuelewa kuwa Biblia haikuwa mwisho wa Neno la Mungu? Kwa nini tunakana Mapokeo ya Watakatifu? Kwa nini hatuwaamini watumishi wake wa sasa?
Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About