Namna pekee ya kuwa na Amani ni kuishi Mapenzi ya Mungu, Kwa njia hii Moyo wako hautafadhaika, hautayumbishwa na hautajuta kwa kuwa utakua upo katika njia ya Mungu na njia ya Mungu haina Majuto kwa kuwa ni njema.

Siri ya mafanikio katika maisha: Usiangalie watu

Waziri mkuu wa zamani wa uingereza Sir Wiston Churchill aliwahi kusema
“huwezi kufika mwisho wa safari yako kama utakuwa unasimama kila mahali kumtupia jiwe kila mbwa anaye kubwekea”

▪Kauli hii ina maana kwamba kama una picha kichwani ya kule unakokwenda au umekusudia kufikia na kutimiza lengo fulani katika maisha, tambua kwamba unapokuwa njiani kutimiza lengo lako lazima utakutana na watu
▪ _watakaokuvunja moyo_ ,
▪ _watakaokusema vibaya_ ,
▪ _watakaokukatisha tamaa._
▪ _watakaokuchukia kwa sababu ya bidii yako_.

▪Mara nyingi sana unaweza kushawishika kutaka kumjibu kila mtu anayekusema vibaya , kukuchukia au kukukatisha tamaa (hapo ndo unakuwa sawa na yule anayesimama kumtupia jiwe kila mbwa anayebweka).

▪Wakati mwingine utashawishika kutaka kuona kila mtu anakukubali na kukuunga mkono, kitu ambacho hakiwezekani.
▪mtu mmoja alisema “siri kubwa ya kufeli katika maisha ni kujaribu kumpendeza kila mtu”.

▪Tambua kwambwa huwezi kumpendeza kila mtu hata ufanye jambo zuri kiasi gani “hata ukichezea maji utaambiwa unatimua vumbi”, yaani ilimradi tu wakupinge.

▪Itazame hatima yako.

*MWAMBA*