Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Jinsi ya kutengeneza Fagi Ya Kumumunyuka Mdomoni

VIAMBAUPISHI

Maziwa mazito matamu (condensed milk) – 2 vibati

Sukari – 1 kikombe

Samli 1 ½ kikombe

Vanilla 2 kifuniko cha chupa yake

Hiliki ilosagwa – 2 vijiko vya chai

Sinia kubwa ya bati Paka samli

MAANDALIZI

Changanya maziwa, sukari na samli katika sufuria isiyogandisha chakula (non-stick) uweke katika moto.
Koroga huku ikipikika hadi ianze kugeuka rangi na kuanza kuachana. Usiache mkono kuroga isije kufanya madonge.
Tia hiliki na vanilla, endelea kuipika.
Itakapogeuka rangi vizuri mimina katika sinia na haraka uitandaze kwa mwiko huku ukiuchovya katika maji na kuendelea kuitandaza hadi ikae sawa kote.
Pitisha kisu kuikataka ili ikipoa iwe wepesi kuitoa vipande.

Kila inapozidi kupoa na kukaa ndipo fagi inakauka na kumumunyuka.

Jinsi ya kupika Mkate wa sinia

Mahitaji

Unga wa mchele (rice flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 3/4 ya kikombe cha chai)
Hamira (dried yeast 3/4 kijiko cha chakula)
Hiliki (cardamon powder 1/2 kijiko cha chai)
Ute wa yai 1(egg white)
Tui la nazi (coconut milk kikombe 1 na 1/2 cha chai)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Changanya unga wa mchele, hamira, hiliki na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastic kisha koroga vizuri. Ufunike na uwache katika sehemu ya joto mpaka uumuke.(ambayo inaweza kuchukua kama dakika 30-45. Ukisha umuka tia sukari na ute wa yai kisha ukoroge vizuri. Baada ya hapo washa oven katika moto wa 200°C kisha chukua chombo cha kuokea na ukipake mafuta na umimine mchanganyiko. Kisha utie katika oven na uoke kwa muda wa dakika 40. Hakikisha unaiva na kuwa rangi yabrown juu na chini. Na hapo mkate utakuwa tayari.

Hii ndiyo bongo sasa!!

Hii ndio Bongo

Ilikuwa Ijumaa mida ya saa 10 jioni, mzee mmoja aliingia na kibinti kizuri kwenye yard ya magari mapya.

MZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi….kabinti akazunguka yard yote mwisho akachagua Verrosa metallic .

BINTI: Mi naitaka hii

MZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima upate gari uloichagua mwenyewe. Mzee akatoa kitabu cha cheki na kuandika palepale na kumpa mwenye yard

MUUZAJI: Sasa Mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa Account yako ina pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee

MZEE: Hakuna tatizo (akampa namba). Haya twende zetu sweetie Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lako…

Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.

MUUZAJI: We Mzee kavu sana, akaunti yako haina hata senti tano.

MZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.

💦😆💦

Unayopaswa kujua Kuhusu Kipindi cha Majilio

Majilio (pia: Adventi ) ni kipindi cha liturujia ya
madhehebu mbalimbali ya Ukristo (kama vile
Kanisa Katoliki, ya Waorthodoksi , Waanglikana
na Walutheri ) kinatangulia sherehe ya Noeli na
kuanza mwaka wa liturujia. Kinaweza kudumu
kati ya siku 22 na 40.
Jina lake kwa Kilatini ni adventus maana yake
ujio (wa Yesu Kristo ), lakini jina la Kiswahili ni
sahihi zaidi kwa sababu linadokeza kuwa ujio
wa Yesu ni kwa ajili yetu na kuwa alikuja
zamani, anakuja kila siku na atakuja kwa
utukufu mwisho wa dunia.
Maana ya Majilio katika
maisha ya binadamu
Sisi binadamu hatuwezi kuishi daima katika
hali ileile bila ya matazamio. Hasa kijana
anatarajia mambo mapya tena mema. Hivyo
tunajitahidi kuyapata. Asiyetazamia chochote
amevunjika moyo, hana hamu ya kuishi. Lakini
matazamio ya kibinadamu yakimfikia mtu
hayamridhishi moja kwa moja. Kristo tu
anatimiza hamu zote kwa kumkomboa kutoka
unyonge. Majilio yanatukumbusha kila mwaka
matarajio ya kweli na hivyo yanaamsha hamu
ya kuishi kwa bidii ya kiroho.
MAJILIO: Katika Kanisa la Roma.
Katika mwaka wa liturujia ya Kanisa la Roma ,
sherehe ya Noeli inaandaliwa na kipindi cha
Majilio ambacho kina mambo mawili:
kinakumbusha Mwana wa Mungu alivyotujilia
mara ya kwanza, na papo hapo kinatuandaa
kumpokea atakapotujilia tena siku ya mwisho .
Kufuatana na hayo kina sehemu mbili: hadi
tarehe 16 Desemba kinahusu zaidi kurudi kwa
Bwana; siku nane za mwisho kinatuelekeza
moja kwa moja kuadhimisha kuzaliwa kwake.
Urefu wa Majilio unategemea siku
inayoangukia Noeli, kwa kuwa ni lazima yawe
na Jumapili nne. Hivyo basi yanaanza kwa
Masifu ya Jioni ya kwanza ya Jumapili
inayoangukia tarehe 30 Novemba au tarehe ya
jirani zaidi; yanakwisha kabla ya Masifu ya
Jioni ya kwanza ya Noeli.
Kwa jumla ni kipindi cha toba: rangi yenyewe
ni zambarau; haziruhusiwi sherehe za fahari;
ala za muziki na maua vinaweza kutumika
kwa kiasi tu. Masharti hayo yanalegezwa
katika Jumapili ya tatu kwa sababu ya furaha
ya kuona tunakaribia sherehe yenyewe.
Katika kipindi hicho tunaadhimisha tumaini la
Israeli lililotimizwa Yesu alipokuja katika
unyenyekevu wa umbile letu; pia tunangojea
arudi kwa utukufu. Kama alivyotekeleza ahadi
mara ya kwanza, atazitekeleza pia mara ya
pili, ingawa kwake miaka elfu ni kama siku
moja tu. Kati ya majilio hayo mawili, Bwana
anatujilia mfululizo kifumbo katika sakramenti
(hasa ekaristi ) na katika maisha ya kila siku
kwa njia ya matukio na watu (hasa maskini ).
Basi tunapaswa kuwa tayari daima kumpokea
ili siku ya mwisho tukamlaki, naye
atukaribishe kwenye uzima wa milele. Pia
tunapaswa kumuomba aje kutukomboa, yeye
aliye tumaini letu.
Katika safari ya Majilio watu watatu
wanatuongoza tukutane na Yesu:
1. Isaya
nabii wa tumaini, mwenye kipaji cha kutokeza
matazamio ya binadamu na kumhakikishia
atatimiziwa na Mwokozi
. 2. Yohane Mbatizaji ,
mwenye kuhimiza toba kwa kuwa tunapaswa
kupindua maisha yetu ili tukutane vema na
Kristo.
3. Maria , bikira aliyekuwa tayari
kumpokea Masiya kwa upendo na kushirikiana
naye katika kutimiza mpango wa wokovu .
Tukiwafuata hao watatu tunaweza kujipatia
maadili yale yanayotuandaa kumpokea
Mwokozi anapotujilia: ndiyo matunda maalumu
tunayotarajiwa kuyachuma wakati wa Majilio:
1. Kukesha katika imani, sala na kutambua
ishara za Bwana kutujilia katika nafasi yoyote
ya maisha na mwishoni mwa nyakati.
2.Kuongoka kwa kufuata njia nyofu.
3.Kushuhudia furaha inayoletwa na Yesu kwa
kuwa na upole na uvumilivu kwa wenzetu, kwa
tumaini la kuwa bidii zetu zinawahisha ufalme
wa Mungu wenye heri isiyo na mwisho.
4. Kutunza unyenyekevu kwa kufuata mifano ya
maskini wa Injili ambao ndio waliompokea
Mkombozi .
kwa mambo mengi mengine ya dini tembelea
https://ludovicktmedia.blogspot.com/

Kapresha kakiamua kuja kanakujaga tuu, cheki kilichompata huyu mme wa mtu mpenda michepuko

Kimchepuko chako kinakuandikia meseji kama hii…

…Samahani baby kama unavyojua nimeokoka ,nimetubu kanisani lakini nabii kaniambia niwaombe msamaha wote niliowakosea.

Nimemkosea sana mkeo kwa kumwibia mumewe na nimepanga kuja kumwomba msamaha kesho ntakuja na nabii na Mchumba wangu mpya nilie mpata kanisani.

Samahani kwa usumbufu uliojitokeza lakini hilo ni kwa ajili ya utukufu wa bwana!!!

Wako Manka wa Magorofani😅😅

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia limau au limao

Dawa nyingine nzuri kwa ajili ya chunusi usoni na mwilini ni limau. Limau linajitokeza kwenye vyakula vingi tunavyokula kila siku mathalani limau halikosekani pakiwepo supu au mapishi yoyote ya samaki.

Limau lina kiasi kingi cha vitamini C ambayo inaweza kutumika kama antibiotiki inayozuia kuongezeka na kukua kwa bakteria wanaosababisha chunusi.

Limau pia ina tindikali maalumu inayohamasisha chunusi kutoka katika ngozi.

Unachotakiwa kufanya ni kukata limau pande mbili au nne na upake majimaji yake moja kwa moja kwenye chunusi pole pole kwa dakika 10 hivi kasha jisafishe na maji safi.

Tindikali katika limau inaweza kuzidhuru seli zilizopo juu ya ngozi yako hivyo tumia dawa hii mara 1 au 2 tu kwa wiki na siyo kila siku.

Vitamini C iliyomo kwenye limau husaidia kukinga mwili dhidi ya magonjwa mengi sababu ndiyo vitamini inayosaidia kuongeza kinga ya mwili.

Kinga ni bora kuliko tiba!

Hivyo tumia vitamini C mara kwa mara au kunywa juisi ya limau kila siku ili kuweka mwili wako katika afya bora zaidi muda wote.

Safari ya kupata fadhila ya Unyenyekevu

Leo tunatafakari kuhusu safari ya kupata fadhila ya Unyenyekevu,

Fadhila ya Unyenyekevu ni tunda ya Upendo na Uvumilivu kwa hiyo ili kufikia Unyenyekevu yakupasa kuwa na Upendo wa kweli kwa Mungu na Wanadamu huku ukiwa mvumilivu, Mwisho wa yote hayo utapata fadhila ya Unyenyekevu

Mungu ni myenyekevu kwa kuwa anaupendo na Uvumilivu

Ni vigumu kuishi kitakatifu bila Unyenyekevu

Safari ya Kupata Fadhila ya Unyenyekevu

Leo tunatafakari kuhusu safari ya kupata fadhila ya unyenyekevu. Unyenyekevu ni moja ya sifa kuu ambazo zinatuwezesha kuishi maisha ya kiroho yaliyojaa amani na furaha. Hii safari inahitaji bidii na kujitoa kwa dhati katika kumfuata Mungu.

“Maana, ni nani aliyekudharau siku ya mambo madogo? Kwa maana hawa saba ni macho ya Bwana yanayopita huko na huko duniani mwote.” (Zekaria 4:10)
“Ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.” (1 Petro 5:5)
“Kwa maana kila ajiinuaye atashushwa, naye aishushaye nafsi yake atainuliwa.” (Luka 14:11)

Fadhila ya Unyenyekevu ni Tunda la Upendo na Uvumilivu

Fadhila ya unyenyekevu ni tunda la upendo na uvumilivu. Ili kufikia unyenyekevu, yakupasa kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu na wanadamu huku ukiwa mvumilivu. Huu upendo ni ule ambao haujifuni wala kujitafutia maslahi binafsi bali unajitoa kwa ajili ya wengine.

“Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wowote.” (1 Wakorintho 13:7-8)
“Naam, nyinyi wenyewe mwajua jinsi inavyotupasa kumfuata Bwana wetu Yesu Kristo, kwa kuwa yeye alikuwa mpole na mnyenyekevu moyoni.” (Mathayo 11:29)
“Na uvae upendo, ambao ni kifungo cha ukamilifu.” (Wakolosai 3:14)

Mungu ni Myenyekevu kwa Kuwa Anaupendo na Uvumilivu

Mungu ni mnyenyekevu kwa kuwa anaupendo na uvumilivu. Mungu, kwa huruma zake na neema zake nyingi, anajishusha kwa ajili yetu ili kutuokoa na kutubariki. Hii ni mfano bora wa unyenyekevu tunaopaswa kuiga.

“Acha moyo wangu uwe mnyenyekevu kwa kumcha jina lako.” (Zaburi 86:11)
“Bwana yupo karibu na wale waliovunjika moyo, na kuwaokoa waliopondeka roho.” (Zaburi 34:18)
“Basi jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua.” (Yakobo 4:10)

Ni Vigumu Kuishi Kitakatifu Bila Unyenyekevu

Ni vigumu kuishi kitakatifu bila unyenyekevu. Unyenyekevu hutufanya kuwa watiifu kwa Mungu na kutuwezesha kupokea baraka na neema zake. Bila unyenyekevu, ni rahisi kuanguka katika dhambi za kiburi na majivuno, ambazo zinatufanya tuwe mbali na Mungu.

“Basi ndugu zangu, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mnasihi kwamba nyote mseme mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mkaungane katika nia moja na shauri moja.” (1 Wakorintho 1:10)
“Wenye heri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao.” (Mathayo 5:3)
“Kwa maana yeye anayetaka kuokoa maisha yake atayapoteza, na yeye anayetayapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata.” (Mathayo 16:25)

Hitimisho

Safari ya kupata fadhila ya unyenyekevu inahitaji upendo wa kweli na uvumilivu. Mungu, kwa upendo na uvumilivu wake, anatufundisha kuwa wanyenyekevu. Kuishi kitakatifu bila unyenyekevu ni vigumu, lakini kwa kumtegemea Mungu na kufuata mfano wake, tunaweza kufikia unyenyekevu wa kweli.

“Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.” (Mathayo 5:14)
“Nimevipigania vile vitani vizuri, mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda.” (2 Timotheo 4:7)
“Wenye heri wanyenyekevu, maana watairithi nchi.” (Mathayo 5:5)

Elimu ya biashara

Jifunze kujikagua, jifunze kujiuliza je hapa ndipo napotakiwa kuwa? Usifurahie tu kwamba upo hapo kwa muda mrefu yamkini unaona panakufaa and you are settled lakini ukweli ni kwamba sio pako na haukutengenezwa kuwa hapo. Hata kama tai ataonekana kwenye banda la kuku lakini ukweli ni kwamba tai kaumbiwa kuwa angani tofauti na kuku aishie bandani. Jiulize hapo ulipo ni pako??

Na ndio maana kwenye maisha, mafanikio ya leo ni matokeo ya tulichojifunza kutoka kwa waliopita, baada ya wao kukosea mahali nasi tukaboresha, na kwa hakika vizazi vijavyo navyo vitaendelea kurekebisha pale tunapokosea sisi na hii yote ndiyo huleta ladha ya maisha. Ukipitia Changamoto mwenyewe na ukapambana kujikwamua mwenyewe, utapata somo litakalokufunza zaidi kuliko kusimuliwa changamoto walizopiti wengine.

Maisha ni Maamuzi, aliyekula Sahani mbili za wali mchana ili usiku asile tena, anaweza kuwa sawa na aliyeamua kutokula Mchana ili usiku ale sahani mbili za wali, japo hawa hawawezi kuwa sawa sawia na aliyeamua kula sahani moja ya wali mchana na moja ya wali usiku, Ijapokua mwisho wa siku wote wamekula sahani Mbili za wali kwa siku. Jumapili Njema kwenu nyote.

JIKUNG’UTE….JIPANGE…..ANZA……

Mapishi ya Biriani

Mahitaji

Mchele (rice 1/2 kilo)
Nyama (beef 1/2 kilo)
Vitunguu (onion 2)
Kitunguu swaum (garlic 1 kijiko cha chai)
Tangawizi (ginger 1 kijiko cha chai)
Maziwa mgando (yogurt 1 kikombe cha chai)
Hiliki nzima (cardamon 6)
Amdalasini nzima (cinamon stick 2)
Karafuu nzima (cloves 6)
Pilipili mtama nzima (black pepper 8)
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Binzari manjano (turmaric 1/2 kijiko cha chai)
Binzari nyembamba nzima (cumin 1/4 kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia nyama na uikaange kwa muda wa dakika 10. baada ya hapo tia tangawizi, kitunguu swaum, hiliki(4), amdalasini (1), karafuu (4), pilipili mtama (5), Curry powder, binzari manjano, binzari nyembamba na chumvi. Kisha koroga. Baada ya hapo tia yogurt na uipike mpaka ikauke kisha tia maji kidogo, funika na upunguze moto na uache ichemke kwa muda wa nusu saa.Baada ya hapo nyama itakuwa imeiva na mchuzi kubakia kidogo.Kwahiyo itatakiwa kuiipua.
Loweka mchele kwa dakika 10. kisha chemsha maji mengi kidogo katika sufuria kubwa. baada ya hapo tia hiliki (2) amdalamsini (1) karafuu(2) pilipili mtama (3) chumvi na mafuta kiasi. acha ichemke kidogo kisha tia mchele.Hakikisha maji yameufunika mchele kabisa na uuache uchemke kwa muda wa dakika 8 tu (kwani hautakiwi kuiva kabisa) kisha uipue na uchuje maji yote katika chujio. baada ya hapo chukua sufuria ya kuokea (baking pot kama unayoiona kweye picha) Kisha weka wali nusu na uusambaze sawia kisha weka mchuzi nyama na mchuzi wake pia utandaze na umalizie kwa kuweka leya ya wali uliobakia. Baada ya hapo ufunike na uweke kwenye oven kwenye moto wa 200°C kwa muda wa nusu saa.na baada ya hapo biriani litakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kutunza nyumba ya kuku ili kuzuia magonjwa

1. Nyumba ya kuku iwe safi na kavu muda wote kuzuia ueneaji na kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa

2. Nyumba ya kuku iwe na nafasi za kupitisha hewa ya kutosha ili kuepuka joto na unyevunyevu ambao unachangia uwepo wa magonjwa kwa kuku

3. Hakikisha unaondoa matandazo na takataka zote kwenye banda wakati wote hasa yenye unyevu.

4. Fagia banda na kuhakikisha ni safi wakati wote. Weka matandazo mapya mara kwa mara.
5. Weka sehemu za kutosha kuku kupumzikia.
6. Weka viota vya kutosha.
7. Weka maji sehemu ambayo ni rahisi kusafisha.
8. Hakikisha unaondoa wanyama kama panya na wadudu nyemelezi kwenye sehemu ya malisho ya kuku kwani wao hubeba vimelea vya magonjwa.

Jinsi vitunguu swaumu vinavyosaidia kuzuia wadudu shambani

Vitungu saumu vina manufaa sana katika kukabiliana na aina mbalimbali za wadudu waharibifu na baadhi ya magonjwa kutokana na kuwa na harufu kali inayosaidia kuwafukuza wadudu kama vidukari, bungo na hata panya.

Hatua za kufuata kutengeneza dawa ya kitunguu saumu

  1. Saga kitunguu saumu kimoja,
  2. Changanyakwenye lita moja ya maji
  3. Nyunyizia kwenye mazao.

Namna nyingine ya kutengeneza dawa

  1. Unaweza pia kusaga vitunguu saumu 3,
  2. kishachanganya na mafuta taa,
  3. acha ikae kwa siku tatu,
  4. kisha ongeza lita 10 za maji ya sabuni na unyunyizie.

Hii itaondoa aina nyingi sana ya wadudu wanaosababisha magonjwa.

Mapishi ya Pilau Ya Kuku Kwa Mchele Mpya

Mahitaji

Mchele – 1 kilo

Kuku – 1

Vitunguu – 3

Viazi/mbatata – 5

Jira/bizari ya pilau nzima – 3 vijiko vya supu

Mdalasini – 1 kijiti

Pilipili manga – 1 kijiko cha supu

Hiliki – 3 chembe

Karafuu – 5 chembe

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa – 3 vijiko vya supu

Tangawizi mbichi ilosagwa – 3 vijiko vya supu

Mafuta ya kupikia – ½ kikombe

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote..
Menya viazi, katakata vipande vya kiasi.
Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau.
Tia bizari zote isipokuwa hiliki.
Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo.
Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi.
Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.

Kanuni ya fedha ya matumizi na mipango ambayo itakusaidia ukiifuata

Jifunze kanuni za fedha
kama ilivyoainishwa hapo chini.
Fedha inatakiwa uwe na nidhamu nayo katika kutumia
Hii kanuni inatumika kwenye vyanzo vyako vyote vya fedha ili uwe na mafanikio yenye amani

Tuangalie hapa chini hizi kanuni👇👇👇

Fungu la kumi 10%
Akiba 30%
Matumizi 40%
Dharura 10%
Msaada 5%
Sadaka 5%

👆👆hii kanuni inafanya kazi katika kila hela unayopata kama faida

Mfano : mtu mwenye mshahara wa mil 1 unayoipata kila mwezi baada ya makato

Fungu la kumi 10% (Tithe) hii ni mali ya Mungu si yako!!

👉itakuwa ni sh laki 1 unatakiwa uitoe sehemu unayoabudia kila mwezi na kama unabiashara zako faida yake ndani yake toa fungu la kumi
Pia hata kama ni hela unapewa kama zawadi itolee fungu la kumi

👉faida ya hii

🌸inalinda kazi au Biashara unayoifanya zidi ya adui
🌸magonjwa,ajali , ( vitu vitakavyokufanya utumie hela bila mpangilio),etc yanakuwa mbali nawe

Akiba 30%

👉hii unaiweka kwa matumizi yako ya baadae kama kujenga,kusomesha,kulima, investment, etc
👉unatenga laki 3 kwa mtu anaepokea mil 1

Matumizi 40%

👉hii itatumika kwa matumizi ya kila siku ,chakula ,Maji, etc

👉hapa unatenga laki 4 kwa ajili ya matumizi kwa mtu wa mshahara wa mil 1
👉note : hapa ndio hela yako ya kustarehe inatoka
Angalia matumizi yasizidi hela uliyonayo
👉wengi wao hapa watu ndio inamfanya awe na vyanzo vingi vya hela ili aweze kufanya starehe awezavyo
👉pia hii ndio hela unayotoa kwa ajili ya mbegu (sadaka ya gharama) wanaoifahamu

Dharura 10%

👉hii fedha unaitunza kwa ajili ya vitu usivyotarajia kama msiba, ndugu kuumwa au kukwama etc
👉unatunza laki 1 kwa mtu wa mshahara wa mil 1

Msaada 5%

👉hii inawahusu watoto yatima, wajane na wasiojiweza kama vilema
👉unatoa elfu 50 kwa mtu wa mshahara wa mil 1
👉unaigawa kama unamagroup yote hayo

Sadaka 5%

👉hii unatoa elfu 50 kwa mtu wa mshahara wa mil 1
👉igawe mara NNE coz mwezi una jumapili 4 ambayo utapata ni elfu 12500 ivyo basi kila jumapili peleka sadaka elfu 12500

Note:
👉Kitu chochote kinachoitwa sadaka kiombee kabla hujakitoa kama siku 2 au 3 ndio uitoe
sadaka
👉nakama unahitaji kitu mfano Nguo peleka nguo kwa waitaji uone utakavyopata Nguo
Nyingi
👉chukua mfano Bakhresa na Mengi wanavyojitolea mbona hawaishiwi, siri yao iko kwenye nidhamu hii ya pesa!!

Jaribu na wewe anza hata na kidogo kidogo kuwa na nidhamu na fedha uone nayo itakavyokuheshimu

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About