Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Jinsi ya kupika Pilau Ya Nafaka Na Nyama Ya Kusaga

Viambaupishi

Mchele 3 vikombe

Nyama ya kusaga 1 LB

Mchanganyiko wa Nafaka (upendavyo) 1 kikopo

(maharagwe, njegere, mbaazi, na kadhalika)

Vitunguu maji kata vipande vipande 3 vya kiasi

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi 2 vijiko vya supu

Mafuta ยฝ Kikombe

Mchanganyiko wa bizari (Garam Masala) 2 vijiko vya chai

Vipande vya supu (Maggi cubes) 3

Maji (inategemea mchele) 5

Chumvi Kiasi

Jinsi ya kuandaa na kupika

1) Osha mchele na roweka.

2) Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu mpaka viwe brown.

3) Tia Thomu na tangawizi, kaanga kidogo.

4) Weka nyama ya kusaga, chumvi na garam masala, endelea kukaanga mpaka nyama iwive.

5) Mwaga maji yaliomo katika kopo la nafaka na utie nafaka pekee humo.

6) Tia maji na vipande vya supu (Maggi cubes) huku unavivuruga, koroga kidogo.

7) Tia mchele, koroga kidogo.

8) Funika na pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukikorogoka kidogo. (kama unavyopika pilau ya kawaida)

9) *Epua uipike katika moto wa oven 350-400 Deg kwa muda wa dakika 15.

*Kama sufuria uliyotumia sio ya kupikia katika oven, mimina katika chombo chochote kinachotumika kwa oven kama bakuli la pyrex au treya za foil.

10) Pakua katika sahani na iko tayari kuliwa.

Mapishi ya Pilau Ya Samaki Wa Tuna Na Mboga

Mahitaji

Mchele – 2 Mugs

Mboga mchanganyiko za barafu (Frozen veg) – Mug

Tuna (samaki/jodari) – 2 kopo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi -2 vijiko vya supu

Garam masala – 1 kijiko cha supu

Nyanya – 2

Kitungu maji – 1

Mdalasini nzima – 2 vijiti

Karafuu – 6 chembe

Pilipili mbichi – 1

Chumvi – kiasi

Viazi – 3

Maji – 2 ยฝ Mugs

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Maandalizi

Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20
Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga.
Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive.
Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu.
Tia maji, yatakapochemka tia mchele.
Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ยฝ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.

Jinsi ya kupika vizuri Wali Wa Karoti Na Nyama

MAHITAJI YA WALI

Mchele – 3 Magi

Mafuta – 1/4 kikombe

Karoti unakata refu refu – 3

Vitunguu maji kata vikubwa vikubwa – 1 kikubwa

Pilipli manga – 1/2 kijicho chai

Hiliki – 1/2 kijiko chai

Karafuu ya unga – 1/4 kijiko cha chai

Mdalasini wa unga – 1/2 kijiko cha chai

Zaafarani (ukipenda) roweka katika maji – 1 kijiko cha chai

Zabibu kavu (ukipenda) – 1/4 kikombe

Chumvi kiasi

KUPIKA WALI

Kwenye sufuria tia mafuta na kaanga karoti kidogo.
Tia vitunguu kisha tia bizari zote.
Tia maji kiasi (kutegemea aina ya mchele) na chumvi
Tia mchele upike uwive.
Karibu na kuwvia tia zabibu ukipenda.
Funika endelea kuupika hadi uwive.

MAHITAJI KWA NYAMA

Nyama – 2 Ratili (LB)

Chumvi – Kiasi

Mafuta – 1/4 kikombe

Kitunguu (kata virefu virefu) – 1 Kikubwa

Pilipili mboga kubwa – 2 ukipenda moja nyekundu moja kijani unazikata vipande virefu virefu.

Figili mwitu (celery) kata vipande virefu virefu- Miche miwili.

KUPIKA NYAMA

Chemsha nyama hadi iwive
Ikaange kwa mafuta hadi iwe nyekundu
Weka vitunguu, pilipili mboga na figili mwitu
Kaanga kidogo tu kama dakika moja.
Tayari kuliwa na wali.

Mapishi ya Wali Wa Kukaanga Kwa Nyama Mbuzi Ilichomwa Ya Sosi Ya Ukwaju

Vipimo Vya Wali

Mchele Basmati – 4 vikombe

Vitunguu vya majani (Spring onions) – 5 miche

Pilipili mboga nyekundu (capsicum) – 1

Pilipili mboga manjano (capscimu) – 1

Nyanya kubwa – 1

Supu ya kidonge – 2

Siagi – 2 vijiko vya supu

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele kisha roweka kiasi masaa matatu takriban.
Katakata vitunguu majani, mapilipili boga, nyanya vipande kiasi.
Weka siagi katika sufuria ya kupikia, weka katika moto iyayuke.
Tia vitunguu majani, mapilipili boga, nyanya, kaanga kidogo tu.
Tia mchele kaanga kidogo, kisha tia maji kiasi ya kuivisha mchele.
Tia supu ya kidogo au supu yoyote, funika wali upikike moto. mdogodogo.

Vipimo Vya Nyama Mbuzi Na Sosi Ya Ukwaju

Nyama mbuzi mapande makubwa kiasi – 7/8 vipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Ukwaju mzito ulokamuliwa – 1 kikombe cha chai

Jiyra/cummin/bizari pilau – 1 kijiko cha chai

Nyanya kopo – 2 vijiko vya supu

Siki – 2 vijiko vya supu

Mafuta – ยฝ kikombe cha chai

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Changanya vitu vyote pamoja katika kibakuli kidogo.
Weka nyama katika bakuli kubwa kisha tia mchanganyiko wa sosi, ubakishe sosi kiasi pembeni.
Roweka kwa muda wa masaa 3 โ€“ 5
Panga nyama katika bakuli au treya ya kuchomea katika oven.
Pika (bake) kwa moto wa kiasi kwa muda wa saa takriban.
Karibu na kuiva, epua, zidisha kuichangaya na sosi ilobaki.
Rudisha katika jiko uendelee kuipika muda kidogo tu.
Epua ikiwa tayari, weka juu ya wali uliopakuwa kisha mwagia sosi ya nyanya pilipili (chilii tomato sauce) ukipenda.

UNYONYESHAJI BORA WA MAZIWA YA MAMA

โ€ข Maziwa ya mama pekee ndio chakula na kinywaji cha mtoto bora zaidi kwa watoto kwa miezi sita ya kwanza.
โ€ข Ni jambo la muhimu sana kunyonyesha watoto wachanga kwa muda wa miezi minne na uendelee kunyonyesha hadi mtoto atakapofikisha mwaka mmoja na kuendelea.

โ€ข Mtoto akifikisha miezi sita ndio wakati muafaka wa kumpa vyakula vya nyongeza vilivyotayarishwakatika hali ya usafi.

โ€ข Onana na mnasihi akushauri kuhusu muda na jinsi ya kumuanzishia mtoto wako vyakula vya nyongeza

โ€ข Vyakula vya ngogeza viwe ni vya mchanganyiko wa makundi yafuatayo ya chakula:- vyakula vya nafaka, venye asili ya nyama, mbogamboga na matunda, mafuta na sukari (kiasi). Lisha kila chakula kwa siku kadhaa kwa kufuatanisha kabla hujaaza chakula chengine kipya.

โ€ข Usimuachilie mtoto alale kama chupa ya maziwa ingali mdomoni, ili kuepukana na kuoza kwa meno na madhara ya.

โ€ข Watoto wanaopewa maziwa ya mama pekee hawaugui mara kwa mara, na wakiugua, makali ya ugonjwa hupungua na hupona mapema kwa sababu yale maziwa ya mwanzo ya njano yenye viini vingi vya kumkinga dhidi ya magonjwa.

Jinsi ya kupika vitumbua inavyotakiwa

Mahitaji

Unga wa mchele ( Vikombe 2 vikubwa)
Sukari (Nusu ya kikombe kikubwa)
Hamira ( Nusu ya kijiko cha chai)
Hiliki (Nusu ya kijiko cha chai)
Tui la nazi ( Kikombe kimoja kikubwa)
Unga wa ngano (Vijiko viwili vya chakula)
Mafuta ya kuchomea (Vegetable oil)

Matayarisho

Unachanga unga, sukari, hamira, hiliki, unga wa ngano na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastiki. Kisha unaukoroga mpaka mchanganyiko unakuwa kama uji mzito. Kava bakuli lililokuwa na mchanganyiko kisha hifadhi katika sehemu yenye joto kwa muda wa masaa matatu.

Jinsi ya kupika

Weka chuma cha kuchomea vitumbua katika moto wa wastani, kisha weka mafuta kwenye chuma cha kuchomea ( Kijiko kimoja cha chai) mafuta yakisha pata moto tia uji wako (upawa mmoja) katika kila shimo la chuma cha kuchomea. Acha mpaka kitumbua kikauke kisha geuza na tia mafuta. Acha upande wa pili wa kitumbua mpaka uwe rangi ya kahawia na hapo kitumbua kitakuwa kimeiva utakitoa. Rudia hatua hizo kwa vitumbua vyote vilivyobaki.

Kujifunza Misingi ya Upishi Bora kwa Afya Yako

Kujifunza misingi ya upishi bora kwa afya yako ni hatua muhimu katika kuboresha maisha yako na kuhakikisha una lishe bora. Upishi bora unaweza kuboresha afya yako kwa kiasi kikubwa na kukufanya ujisikie vizuri kimwili na kiakili. Kwa hivyo, katika makala haya, nitakupa vidokezo kadhaa juu ya jinsi ya kujifunza misingi hii na kufurahia chakula chenye afya.

Kwanza kabisa, unahitaji kuelewa umuhimu wa vyakula vyenye afya katika maisha yako. As AckySHINE, naomba usisahau kwamba chakula ni kama mafuta ya injini ya gari. Ikiwa unaingiza mafuta mabaya, gari lako haliwezi kuendesha vizuri. Vivyo hivyo, kula chakula kisicho na afya kunaweza kuathiri afya yako. Kwa hivyo, kufahamu vyakula vyenye afya ni muhimu sana.

๐Ÿฅฆ Chagua vyakula vyenye afya: Kula matunda na mboga mboga mbalimbali, kupunguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari, na kula protini zenye afya kama samaki, kuku, na maharage.

๐Ÿ“ Ongeza matunda kwenye lishe yako: Matunda ni chanzo kizuri cha vitamini, madini, na nyuzi ambazo zinasaidia kuimarisha mwili wako na kulinda dhidi ya magonjwa. Kwa mfano, kula tunda moja la parachichi kila siku linaweza kuboresha afya yako ya moyo.

๐Ÿฅ— Jumuisha mboga mboga katika milo yako: Mboga mboga zina virutubishi muhimu kama vile vitamini, madini, na nyuzi. Kula mboga mboga kama vile spinach, karoti, au matango kila siku kunaweza kuimarisha kinga yako na kukuweka katika hali nzuri ya afya.

๐Ÿฝ๏ธ Pima sehemu ya kula: Kula sehemu ndogo lakini za usawa ni muhimu sana. Kujaza sahani yako na vyakula vyenye afya kama protini, nafaka nzima, na mboga mboga, na kupunguza ulaji wa vyakula vinavyoongeza uzito kama vile vyakula vyenye mafuta mengi na sukari.

๐Ÿฅ› Unywaji wa maji: Kunywa maji mengi ni muhimu kwa afya ya mwili na akili. Inashauriwa kunywa angalau lita mbili za maji kwa siku ili kuhakikisha mwili wako unakuwa vizuri.

๐Ÿฝ๏ธ Pika chakula chako mwenyewe: Badala ya kununua chakula kilichotengenezwa tayari au chakula cha haraka, jaribu kupika chakula chako mwenyewe. Hii itakupa udhibiti zaidi juu ya viungo na utengenezaji wa chakula chako na kukusaidia kudumisha lishe bora.

๐Ÿฅฆ Jaribu mapishi mapya: Kujifunza misingi ya upishi haimaanishi unapaswa kuwa mpishi wa kitaalam. Jaribu mapishi mapya na ubunifu na ujifunze jinsi ya kutengeneza chakula kitamu na chenye afya. Kwa mfano, weka ndizi kwenye smoothie yako badala ya sukari ili kuongeza ladha na virutubishi.

๐Ÿ— Punguza ulaji wa chumvi na sukari: Chumvi na sukari nyingi katika lishe yako zinaweza kuwa hatari kwa afya yako. Kula kiasi kidogo cha chumvi na sukari inaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa kama vile shinikizo la damu na kisukari.

๐Ÿฝ๏ธ Panga milo yako: Kuweka ratiba ya milo yako na kuhakikisha unakula mara kwa mara ni muhimu sana. Kula milo kubwa mara kwa mara inaweza kusababisha ongezeko la uzito na matatizo mengine ya kiafya. Jaribu kula milo midogo mara kwa mara ili kuweka viwango vya nishati yako sawa.

๐Ÿฅ— Toa kipaumbele lishe: Unapopanga chakula chako, hakikisha unatoa kipaumbele lishe. Jumuisha chakula chenye afya kwenye orodha yako ya ununuzi na epuka kununua vyakula visivyo na afya. Kwa mfano, chagua mkate wa nafaka nzima badala ya mkate wa ngano iliyosafishwa.

๐Ÿ“ Tumia viungo vyenye afya: Kuna viungo vingi vyenye afya ambavyo unaweza kuingiza kwenye milo yako ili kuongeza ladha na virutubishi. Kwa mfano, unaweza kuongeza parachichi kwenye sandwich yako badala ya mayonnaise ili kupunguza ulaji wa mafuta.

๐Ÿฝ๏ธ Fanya chakula kiwe raha: Kujifunza misingi ya upishi bora haimaanishi kuwa chakula chako lazima kiwe kisicho na ladha. Emba ubunifu na utafute njia za kufanya chakula chako kiwe raha na kitamu. Kwa mfano, unaweza kutumia viungo mbalimbali na vyakula vya kipekee ili kubadilisha ladha ya sahani yako.

๐Ÿฅ— Punguza matumizi ya vyakula vya haraka: Vyakula vya haraka mara nyingi huwa na mafuta mengi, sukari, na chumvi nyingi. Kula vyakula vyenye afya zaidi kama vile saladi, sandwiches za nyumbani, au supu mboga. Hii itakusaidia kudumisha afya njema na kuepuka magonjwa.

๐Ÿ“ Kula kwa utaratibu: Epuka haraka haraka wakati wa kula na kula kwa utaratibu. Kupunguza kasi ya kula kunaweza kukusaidia kuhisi kamilifu haraka na kuzuia kula zaidi. Kwa mfano, chukua dakika 20 kuweka chakula kwenye sahani yako na kula taratibu.

Kujifunza misingi ya upishi bora kwa afya yako ni uwekezaji muhimu katika maisha yako. Kwa kufuata vidokezo hivi, unaweza kuboresha afya yako na kufurahia chakula chenye afya na kitamu. Kumbuka kula kwa usawa, kufurahia mlo wako, na kufanya chaguo sahihi kwa afya yako. Je, una mawazo yoyote au maoni? Nipendekeze kuongeza nini katika vidokezo hivi?

Mapishi ya Wali, mchicha wa nazi na nyama ya kukaanga

Mahitaji

Mchele (rice 1/2 kilo)
Mchicha uliokatwakatwa (spinach mafungu 2)
Nyama (beef 1/2 ya kilo)
Nyanya (tin tomato 1/2 ya tin)
Nyanya chungu ( garden egg 3)
Kitunguu swaum (garlic cloves 3)
Tangawizi (ginger)
Curry powder
Vitunguu (onion 2)
Limao (lemon 1)
Chumvi
Pilipili (scotch bonnet pepper )
Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai)

Matayarisho

Kaanga kitunguu kikishaiva tia nyanya na chumvi. kaanga mpaka nyanya ziive kisha tia nyanya chungu,curry powder na pilipili 1 nzima, baada ya hapo tia mchicha na uuchanganye vizuri kwa kuugeuzageuza. Mchicha ukishanywea tia tui la nazi na uache lichemke mpaka liive na hapo mchicha utakuwa tayari.
Safisha nyama kisha iweke kwenye sufuria na utie chumvi, tangawizi, limao na kitunguu swaum. Ichemshe mpaka itakapoiva na kuwa laini. Baada ya hapo weka sufuria jikoni na mafuta kidogo yakisha pata moto tia vitunguu na nyama na uvikaange pamoja, kisha tia curry powder na ukaange mpaka nyama na viunguu vya brown. na hapo nyama itakuwa imeiva. Malizia kwa kupika wali kwa kuchemsha maji kisha tia mafuta, chumvi na mchele na upike mpaka uive. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuseviwa.

Mapishi โ€“ Saladi ya Matunda

Matunda ni mojawapo wa kundi la vyakula, ni muhimu sana kwa afya bora. Matunda yakitengenezwa vizuri yanavutia sana na yanakuwa ni chakula kizuri sana.

Mahitaji

Embe iliyoiva kiasi
Nanasi
Tango
Tikiti maji
Zabibu
Papai

Matayarisho

1. Ondoa maganda kwenye embe, nanasi, tango, papai na tikiti maji kisha kata kata vipande vidogo vidogo vya mraba

2. Changanya vipande vya matunda kwenye bakuli safikisha weka na zabibu zilizotolewa kwenye kikonyo chake.

3. Weka kwenye friji yapate ubaridi kidogo

4. Saladi yako tayari kwa kuliwa

Waweza kula saladi hii kama mlo wa kati au kama mlo kamili wa usiku.

Jinsi ya kuandaa Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ngโ€™ombe

Mahitaji

Ndizi mbichi – Kisia

Nyama ngโ€™ombe – ยฝ kilo

Pilipili ya kusaga – 1 kijiko cha chai

Tangawizi ya kusaga – 2 vijiko vya supu

Thomu (garlic/saumu) – 1 kijiko cha supu

Bizari mchuzi – 1 kijiko cha chai

Nazi ya unga (ukipenda kuongezea) – 2 vijiko cha supu

Chumvi – Kiasi

Ndimu – 1 kamua

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Weka nyama ngโ€™ombe katika sufuria, tia tangawizi, thomu, pilipili mbichi, bizari, chumvi. Roweka kidogo ukipenda kisha ikaushe yenyewe kwa maji yake
Ongezea maji ya kiasi yasizidi mno, kisha funika na chemsha.
Menya ndizi, ukatekate.
Nyama ikikaribia kuiva, weka ndizi uendelee kupika mpaka viive vyote.
Tia nazi ya unga kidogo tu ukipenda. Koleza kwa bizari mchuzi, pilipili, na ndimu
Epua mimina katika chombo cha kupakulia zikiwa tayari.

Upishi na Mafuta ya Zeituni: Faida za Afya na Matumizi ya Mapishi

Upishi na Mafuta ya Zeituni: Faida za Afya na Matumizi ya Mapishi ๐Ÿฝ๏ธ

Karibu katika makala hii ambayo itakuletea ufahamu zaidi kuhusu upishi na mafuta ya zeituni, pamoja na faida zake za kiafya na jinsi ya kuyatumia katika mapishi mbalimbali. Kama AckySHINE, ningependa kukushirikisha maarifa haya ili uweze kuboresha afya yako na kufurahia ladha ya vyakula vyenye mafuta ya zeituni.

Mafuta ya zeituni yamekuwa yakitumika kwa muda mrefu katika nchi za Mediterranean kama sehemu muhimu ya lishe yenye afya. Hii ni kutokana na faida zake nyingi za kiafya ikiwemo kulinda moyo, kuimarisha afya ya ngozi, na kuongeza kinga ya mwili.

Hapa chini ni orodha ya faida kumi na tano za afya za mafuta ya zeituni:

  1. Mafuta ya zeituni husaidia kulinda moyo dhidi ya magonjwa ya moyo ๐Ÿซ€
  2. Yanaboresha afya ya ngozi na kuzuia kuzeeka mapema ๐ŸŒŸ
  3. Mafuta ya zeituni husaidia kupunguza viwango vya sukari mwilini, hivyo ni nzuri kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari ๐Ÿ‘จโ€โš•๏ธ
  4. Husaidia katika kupunguza uzito na kudhibiti hamu ya kula ๐Ÿฅ—
  5. Ina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa saratani ๐Ÿฆ€
  6. Mafuta ya zeituni huimarisha mfumo wa kinga na kulinda mwili dhidi ya maradhi ๐Ÿ›ก๏ธ
  7. Husaidia katika kuzuia ugonjwa wa kiharusi ๐Ÿง 
  8. Mafuta ya zeituni yana madini ya chuma na vitamini E ambavyo husaidia katika kuboresha afya ya damu ๐Ÿ’‰
  9. Husaidia katika kudhibiti shinikizo la damu na kuzuia magonjwa ya moyo ๐Ÿ’“
  10. Ina mali ya kupambana na uchochezi mwilini, hivyo inaweza kupunguza hatari ya magonjwa ya viungo ๐Ÿฆด
  11. Mafuta ya zeituni husaidia katika uponyaji wa vidonda vya tumbo ๐Ÿฉบ
  12. Yanaweza kusaidia katika kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa Alzheimer’s ๐Ÿง 
  13. Husaidia katika kudhibiti viwango vya cholesterol mwilini ๐Ÿฅš
  14. Mafuta ya zeituni yana mali ya antibakteria na antiviral, hivyo husaidia mwili kupambana na maambukizi ๐ŸŒก๏ธ
  15. Yanaweza kusaidia katika kupunguza maumivu ya viungo na kuimarisha afya ya mifupa na misuli ๐Ÿ’ช

Kutokana na faida hizi za kiafya, ni muhimu kuyatumia mafuta ya zeituni katika mapishi yako ili kuboresha ladha na afya ya chakula chako. Hapa chini ni mapendekezo yangu ya matumizi ya mafuta ya zeituni katika mapishi mbalimbali:

  1. Changanya mafuta ya zeituni na limau na tumia kama saladi dressing ๐Ÿฅ—
  2. Tumia mafuta ya zeituni kwenye sahani za pasta ili kuongeza ladha na afya ya chakula chako ๐Ÿ
  3. Pika mboga za majani kwa kutumia mafuta ya zeituni badala ya mafuta ya wanyama ๐Ÿฅฌ
  4. Tumia mafuta ya zeituni kwenye mchuzi wa supu ili kuongeza ladha na afya ya chakula chako ๐Ÿฒ
  5. Tumia mafuta ya zeituni kwenye pilau au wali ili kuongeza ladha na afya ya chakula chako ๐Ÿš
  6. Tumia mafuta ya zeituni kwenye sandwichi badala ya mayonnaise ๐Ÿฅช
  7. Tumia mafuta ya zeituni kwenye kuoka mikate au keki ili kuongeza ladha na afya ya chakula chako ๐Ÿฅ
  8. Tumia mafuta ya zeituni kwenye kuoka samaki ili kuongeza ladha na afya ya chakula chako ๐ŸŸ
  9. Tumia mafuta ya zeituni kwenye kuandaa vitafunwa kama karanga za zeituni zilizokaangwa ๐Ÿฅœ
  10. Changanya mafuta ya zeituni na vikolezo vingine kama vile thyme au basil kwa kuongeza ladha kwenye sahani yako ๐ŸŒฟ

Kwa ujumla, mafuta ya zeituni yanaweza kubadilisha na kuimarisha afya yako kwa njia nyingi. Kama AckySHINE, natoa ushauri kuwa unatumie mafuta ya zeituni katika mapishi yako ili kufurahia ladha nzuri na faida za kiafya.

Je, umewahi kutumia mafuta ya zeituni katika mapishi yako? Ni mapishi gani unayopenda kutumia mafuta ya zeituni? Ni faida zipi za kiafya umepata baada ya kuanza kutumia mafuta haya? Nipo hapa kusikiliza na kujadiliana nawe. ๐Ÿ˜Š๐ŸŒฑ

Mapishi ya Bokoboko La Kuku

Mahitaji

Ngano nzima (shayiri) – 3 Vikombe

Kuku – ยฝ (3 LB takriban)

Thomu na tangawizi iliyosagwa – 1 kijko cha supu

Pilipili manga ya unga – ยฝ kijiko cha chai

Jiyrah (cumin/bizari ya pilau) – ยฝ kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Kidonge cha supu – 1

Samli ya moto – ยฝ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Roweka ngano (shayiri) tokea usiku au muda wa masaa.
Katakata kuku mtie katika sufuria, tia maji kiasi viungo vyote. Mchemeshe awive na ibakie supu yake.
Toa kuku, toa mifupa na umchambue chambue vipande vidogo vidogo.
Chemisha ngano (shayiri) kwa kufunika sufuria hadi iwive na kukauka maji.
Tia supu ya kuku katika ngano (shayiri), na kuku uliyemechambua. Tia kidonge cha supu.
Tia samli nusu (bakisha nusu) kisha songa mchanganyiko uchanganye hadi ivurugike kuku na ngano (shayiri) vizuri.
Mimina katika sahani, mwagia samli imoto ilyobakia likiwa tayari.

Jinsi ya kutengeneza Pilau Ya Kuku

Mahitaji

Mchele wa basmati – 3 vikombe

Kuku – ยฝ

Viazi – 4

Vitunguu – 2

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa – 2 vijiko vya supu

Binzari ya pilau nzima – 1 Kijiko cha chakula

Binzari ya pilau – ยฝ kijiko cha chai

Pilipili manga nzima – ยฝ kijiko cha chai

Karafuu nzima – 8

Iliki nzima – 6

Mdalasini nzima – 5 vijiti

Pilipili mbichi iliyosagwa – 2

Chumvi – kiasi

Mafuta ya kupikia – ยผ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu na tangawizi.
Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi.
Tia thomu na tangawizi na binzari zote kaanga kidogo
Kisha tia viazi kanga kidogo kisha tia kisha tia vipande vyako vya kuku na supu acha ichemke kidogo kisha tia maji ukisie kutokana na mchele unaotumia.
Mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na punguza moto mpaka uive (huku ukiugeuzageuza)
Ukishakuwa tayari pakua kwenye sahani tayari kwa kula na salad na pilipili.

Mapishi ya wali wa hoho nyekundu

Mahitaji

Pilipili hoho (Red pepper 3)
Cougette 1
Kitunguu (onion 1)
Uyoga (mashroom 1 kikombe cha chai)
Carrot 1
Nyanya (fresh tomato 1)
Nyanya ya kopo iliyosagwa (tomato paste 3 vijiko vya chai)
Giligilani (fresh coriander)
Binzari manjano (Turmaric 1/2 ya kijiko cha chai)
Curry powder 1/2 ya kijiko cha chai
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Kata hoho kati na utoe moyo wake kisha ziweke pembeni, Kisha katakata cougette, kitunguu, uyoga, carrot, nyanya katika vipande vidogo vidogo, Weka sufuria jikoni na uanze kupika uyoga kwa muda wa dakika 5, kisha weka curry powder, turmaric na chumvi na kaanga kidogo kisha weka vegetable zilizobakia pamoja na nyanya ya kusaga pamoja na giligilani. Zikaange kwa muda wa dakika 5 kisha zitie kwenye hoho na kisha uzibake kwa muda wa dakika 20 na hapo zitakuwa tayari kuseviwa na wali.
Wali: angalia katika recipe zilizopita

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng’ombe Karoti Na Zabibu

Vipimo – Nyama

Nyama ngโ€™ombe ya mifupa ilokatwa vipande – 1 kilo

Tangawizi na thomu (somu/garlic) ilosagwa – 2 vijiko vya supu

Bizari mchanganyiko/garama masala – 1 kijiko cha chai

Chumvi – Kiasi

Vipimo – Wali

Mchele – 4 glass

Mbatata/viazi menya katakata – 3 kubwa

Vitunguu katakata – 5

Kitunguu thomu kilosagwa (garlic/somu) – 1 kijiko cha supu

Hiliki ya unga – 1 kijiko cha chai

Bizari nzima ya pilau/cumin – 1 mti

Samli au mafuta – 2 Vijiko vya supu

Karoti zilokatwakatwa nyembamba – 6-7

Zabibu – Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katika sufuria weka mafuta kijiko kimoja cha supu tia nyama na viungo vyake.
kaushe katika moto hadi ikaribie kukauka kisha tia maji kiasi cha kuivisha na kubakisha supu ya mchele.
Katika sufuria ya kupikia weka samli au mafuta ishike moto.
Tia mbatata/viazi kaanga, tia vitunguu kaanga kidogo.
Tia kitunguu thomu, hiliki, bizari ya pilau endelea kukaanga hadi viwe rangi ya brown kidogo.
Tia mchele kaanga kidogo, kisha mimina nyama na supu yake. Funika wali uwive.
Weka kikaangio katika moto, tia samli kijiko kimoja kisha tia karoti na zabibu, kaanga kwa sekunde chache tu kwa ajili ya kulainisha karoti na zabibu.
Utakapopakuwa wali, pambia juu karoti na zabibu.

Mchemsho wa samaki na viazi

Mahitaji

Samaki mbichi (1)
Viazi mbatata (3)
Nyanya (1)
Kitunguu maji
Limao
Kitunguu saumu
Tangawizi
Chumvi
Pilipili
Vegetable oil

Matayarisho

Safisha samaki kisha mmarinate na tangawizi, kitunguu swaum, chumvi na limao kwa muda wa masaa mawili. Baada ya hapo menya viazi na uvikate vipande vidogo kisha vioshe na viweke kwenye sufuria yenye maji kiasi kwa ajili ya kuvichemsha. Viinjike jikoni na uviache vichemke kwa dakika 7. Vikisha chemka tia samaki, katia kitunguu,pilipili, chumvi, limao, vegetable oil na nyanya na uache supu ichemke mpaka samaki na viazi vitakapoiva. baada ya hapo supu itakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kupika Visheti

Viamba upishi

Unga 2 Vikombe

Samli au shortening ya mboga 2 Vijiko vya supu

Maziwa ยพ Kikombe

Iliki Kiasi

Mafuta ya kukarangia Kiasi

Shira

Sukari 1 Kikombe

Maji ยพ Kikombe

Vanila ยฝ Kijiko cha chai

Zafarani (ukipenda) Kiasi

Jinsi ya kupika na kuandaa

Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine.
Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo.
Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi.
Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha.
Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta.
Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote.
Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.

Mapishi ya Wali, samaki wa nazi na kisamvu

Mahitaji

Mchele
Kisamvu kilichotwangwa
Samaki
Mbaazi
Nyanya chungu
Vitunguu
Nyanya ya kopo
Tangawizi
Kitunguu swaum
Vegetable oil
Curry powder
Tui la nazi (kopo 2)
Chumvi
Pilipili
Limao

Matayarisho

Safisha samaki kisha wamarineti na kitunguu swaum, tangawizi, pilipili, chumvi na limao kwa muda wa masaa 3.Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana na uwaweke pembeni kwa ajili ya kuungwa.Katakata vitunguu maji, saga tangawizi na kitunguu swaum. Baada ya hapo injika sufuria ya mchuzi jikoni na mafuta kiasi ya kupikia, mafuta yakisha pata moto, tia vitunguu maji na vikaange mpaka viwe vya rangi ya brown. kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.kaanga kidogo kisha tia nyanya ya kopo moja na ufunike. acha mpaka nyanya ziive. Kisha tia chumvi na curry powder na uache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia samaki na nyanya chungu nakisha kamulia nusu ya limao. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi kopo moja na uache ichemke mpaka mchuzi uive.

Baada ya hapo chemsha kisamvu pamoja na mbaazi Kikisha iva, kaanga kitu na nyanya pembeni mpaka ziive kisha tia kisamvu. geuza mchanganyiko mpaka uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi na chumvi na aacha ichemke mpaka tui liive kisha ipua.malizia kwa kupika wali ambapo utachemsha maji kisha tia mafuta,chumvi na mchele na uupike mpaka uive kisha sevu na mboga ulizopika na mlo wako utakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kupika Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe

Viamba upishi

Unga wa ngano 1 Kilo

Siagi ยผ kilo

Mayai 2

Kastadi (custard) 3 vijiko vya supu

Baking powder 1 kijiko cha chai

Maziwa 1 ยฝ gilasi

Mafuta Ya kukaangia kiasi katika karai

Maandalizi na upikaji

Weka unga katika bakuli kubwa kisha changanya na unga wa kastadi na baking powder.
Tia siagi uchanganye vizuri.
Tia mayai, kisha maziwa ya baridi uchanganye vizuri usiukande sana.
Fanya madonge kisha kata vipande vidogovidogo kisha ubonyeze kwa kidole uvikwaruze kwenye chujio lenye tundu itokee shepu (design) yake.

5- Tia mafuta katika karai yakipata moto, kaanga visheti hadi viive. Usiache hadi vikageuka rangi sana.

6- Eupua, weka katika sufuria au chombo kikubwa kusubiri shira.

Vipimo Vya Shira

Sukari ยฝ kilo

Hiliki ilosagwa 1 kijiko cha chai

โ€˜arki (rose flavor) 5 matone

Maji 1 gilasi

Namna Ya Kutyarisha

Changanya sukari na maji uipike hadi iwe nzito.
Ukiona mapovu yanatoka tia hilik na โ€˜arki .
Mwagia katika visheti uchanganye vizuri hadi vishike na sukari.

Mapishi ya Ugali Mchuzi Wa Samaki Nguru Wa Nazi Na Bamia Za Kukaanga

Vipimo Vya Ugali:

Unga wa mahindi/sembe – 4

Maji – 6 takriban

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chota unga kidogo katika kibakuli uchanganye na maji kidogo .
Weka maji mengineyo katika sufuria kwenye moto.
Changanya na mchanganyiko mdogo ufanya kama uji.
Kisha kidogo kidogo unaongeza sembe huku unakoroga na kuusonga ugali hadi uive.

Vipimo Vya Mchuzi Wa Samaki Wa Nazi

Samaki nguru – 5 vipande

Pilipili mbichi ilosagwa

Kitunguu maji kilosagwa – 1 kimoja

Nyanya ilosagwa – 2

Haldi/tumeric/bizari ya manjano – ยผ kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Ndimu – 2 kamua

Tui la nazi zito – 2 vikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Baada ya kumuosha samaki, weka katika sufuria.
Tia chumvi, ndimu, pilipili mbichi ilosagwa.
Tia vitunguu na nyanya zilosagwa
Mkaushe kwa hivyo viungo, akianza kukauka tia tui la nazi.
Acha kidogo tu katika moto tui liwive mchuzi ukiwa tayari.

Vipimo Vya Bamia

Bamia – ยฝ kilo takriban

Nyanya kopo – 1 kijiko cha chai

Methi/uwatu/fenugreek seeds ilosagwa – 1 kijiko cha chai

Dania/corriander ilosagwa – ยฝ kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Mafuta – 1 kikombe cha kahawa

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katakata bamia kwa urefu.
Weka mafuta katika karai, kisha tia bizari zote na nyanya kopo, kaanga kidogo.
Tia bamia endelea kukaanga, kisha acha katika moto mdogomdogo ufunike.
Kila baada ya muda funua karai ukaange bamia hadi ziwive zikiwa tayari.

Shopping Cart
20
    20
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About