Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Mapishi ya Maini ya ng’ombe

Mahitaji

Maini (Cow liver) 1/4 kilo
Vitunguu (chopped onion) 2
Nyanya (chopped tomato) 1
Kitunguu swaum/tangawizi (ginger /garlic paste) 1 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia
Chumvi
Coriander
Curry powder 1 kijiko cha chai
Limao (lemon) 1/4
Pilipili (scotch bonnet ) 1

Matayarisho

Safisha maini na ukate vipande vidogovidogo na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo(visiwe vya brown) kisha tia ginger/ garlic paste,carry powder kaanga kidogo kisha tia nyanya. Kaanga nyanya mpaka zitoe mafuta kisha tia chumvi, pilipili na vimaji kidogo. Acha vichemke kidogo kisha tia maini na uyapike mpaka yaive. Malizia kwa kukamulia limao na kutia coriander kisha ipua na hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya Kujiandaa kwa Chakula cha Wiki Nzima cha Lishe Bora

Jinsi ya Kujiandaa kwa Chakula cha Wiki Nzima cha Lishe Bora 🥗

Hakuna jambo bora kuliko kujihusisha na maisha yenye afya na lishe bora. Kwa wengi wetu, changamoto kubwa ni jinsi ya kujiandaa kwa chakula chetu cha wiki nzima ili tuweze kula vyakula vyenye virutubisho muhimu. Kama AckySHINE, mtaalamu wa lishe, ninafuraha kukushirikisha njia kadhaa ambazo unaweza kutumia kuandaa chakula chako cha wiki nzima cha lishe bora! 🌱

Hapa kuna orodha yangu ya 15 ya hatua unazoweza kuchukua kufanikisha lengo hili:

  1. Tengeneza orodha ya ununuzi: Kupanga ni muhimu sana. Andika vyakula vyote unavyotaka kuwa nayo katika chakula chako cha wiki nzima. 📝

  2. Tafuta mapishi: Tafuta mapishi mbalimbali yanayokusisimua na yenye lishe bora. Kuna tovuti nyingi na programu za simu ambazo zinaweza kukusaidia kupata mapishi haya. 📱

  3. Nunua vyakula vyenye virutubisho muhimu: Nunua mboga mboga, matunda, nafaka na protini zenye lishe bora. Epuka vyakula vyenye sukari nyingi au mafuta mengi. 🥦🍓

  4. Panga ratiba yako: Jijengee ratiba ya kushughulikia maandalizi ya chakula cha wiki nzima. Hii itakusaidia kuwa na mpango mzuri wa wakati na kufanya kazi yako vizuri. ⏰

  5. Fanya maandalizi ya kabla: Jitahidi kuandaa sehemu ya chakula chako kabla ya wiki kuanza. Kwa mfano, unaweza kuosha na kukata mboga mboga, na kuandaa mlo wa asubuhi kwa kuyaweka kwenye kontena. 👩‍🍳

  6. Pika mlo wa kwanza: Anza kwa kupika mlo wako wa kwanza wa wiki. Unaweza kuwa na chakula cha kiamsha kinywa, chakula cha mchana na chakula cha jioni tayari katika kontena au sahani zilizogawanyika kwa siku zote za wiki. 🍳

  7. Tumia vyombo vya kuhifadhia: Vyombo vya plastiki au glasi vyenye sehemu tofauti vinaweza kukusaidia kuweka chakula chako salama na safi kwa muda mrefu. Hakikisha kuandika tarehe za kumaliza mlo wako kwenye vyombo hivyo. 🥣

  8. Fanya chakula kuwa kiburudisho: Hakikisha kuwa chakula chako cha wiki nzima kinakufurahisha. Jaribu mapishi mapya na ubunifu ili uweze kula vyakula tofauti kila siku. 🍽️

  9. Tumia vifaa vya kuongeza lishe: Kwa kuongeza lishe, unaweza kutumia viungo kama vile mbegu za chia, karanga, na tasty na vinywaji vya afya kama vile smoothies au matunda ya kuchoma. 🌰🥤

  10. Hakikisha unakula kwa wingi: Ni muhimu kuhakikisha unapata mlo wa kutosha kwa siku nzima. Tenga sehemu yako ya kila mlo na kuzingatia uwiano sahihi wa protini, wanga na mafuta. 🍽️

  11. Panga vinywaji vyako: Hakikisha unakunywa maji ya kutosha kwa siku nzima. Weka chupa ya maji karibu nawe ili uweze kuinywa mara kwa mara. 🚰

  12. Fikiria kuhusu uchumi: Kujiandaa kwa chakula cha wiki nzima kunaweza kukusaidia kuokoa pesa, kwani huwezi kutumia pesa nyingi kununua chakula nje. 🪙

  13. Saidia familia na marafiki: Unaweza kuwahimiza familia na marafiki wako kujiunga na wewe katika kuandaa chakula cha wiki nzima. Inaweza kuwa ni jambo la kufurahisha na kuwapa motisha. 👨‍👩‍👧‍👦

  14. Uwepo wa akili: Kujiandaa kwa chakula cha wiki nzima kunahitaji subira na nidhamu. Kuwa na akili nzuri na uzingatia lengo lako. 💪

  15. Badilisha mapishi yako: Usiogope kubadilisha mapishi yako na kujaribu vitu vipya. Hii itakupa uzoefu mpya na kuongeza furaha yako ya kula chakula chako cha wiki nzima cha lishe bora. 🌟

Kwa hivyo, kama AckySHINE, na mtaalamu wa lishe, ninaamini kuwa kujiandaa kwa chakula cha wiki nzima cha lishe bora ni njia nzuri ya kuboresha afya yako na kufurahia chakula chako kwa njia ya kipekee. Je, umeshawahi kujaribu kuandaa chakula chako cha wiki nzima? Je, unayo mbinu zako za kujiandaa? Nishirikishe mawazo yako katika sehemu ya maoni hapa chini! 👇

Asante kwa kusoma, na kuwa na wiki njema ya lishe bora! 🥗✨

Mapishi ya wali kuku wa Kisomali

Mahitaji ya wali

Mchele – 3 vikombe

Vitunguu (viliokatwa vidogo vidogo) – 2

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa – 1 kijiko cha chai

Bizari ya pilau – 1 kijiko cha supu

Mdalasini – 1 kijiti

Hiliki – 3 chembe

Pilipili manga nzima – chembe chache

Siagi – Vijiko 2 vya supu

Chumvi – kiasi

Mahitaji kwa kuku

Kuku kidari (Breast) kata vipande vipande – 2 LB

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa – 1 kijiko cha supu

Kotmiri iliyokatwa ndogo ndogo – kiasi

Bizari ya pilau (cummin au jiyrah) – 1 kijiko cha chai

Pilipili kubwa tamu la kijani – 1

Pilipili kubwa tamu nyekundu – 1

(zikate vipande vipande)

Karoti iliyokunwa – 1 – 2

Chumvi – Kiasi

Mapishi ya Wali:

Roweka mchele kwa muda fulani kutegemea mchele
Katika sufuria tia mafuta na kaanga vitunguu hadi vibadilike rangi kidogo.
Tia thomu iliyosagwa, mdalasini, bizari ya pilau, hiliki, pilipili manga na chumvi, kaanga kidogo.
Tia mchele kaanga kidogo, kisha tia maji ya moto kiasi kutegemea na aina ya mchele kama kawaida ya kupika wali kama pilau.
Tia sigai, funika upikike wali hadi uwive.

Mapishi ya Kuku:

Mchanganye kuku pamoja na thomu/tangawizi iliyosagwa, chumvi, pilipili mbichi.
Katika karai tia mafuta yapate moto vizuri.
Mtie kuku, bizari ya pilau (jiyrah) na ukaange, karibu na kuiva tia vitunguu.
Tia mapilipili makubwa, kotmiri, na kaanga kwa dakika moja tu uzime moto na epua weka kando.

Jinsi ya kutengeneza biskuti za Matunda Makavu Na Cornflakes

VIAMBAUPISHI

Unga – 4 Vikombe

Sukari – 1 Kikombe

Baking powder 1 kijiko cha chai mfuto

Siagi – 454 gms

Mayai – 2

Matunda makavu (tende, zabibu, lozi) – 1 Kikombe

Vanilla – 2 Vijiko vya chai

Cornflakes – ½ kikombe

JINSI YA KUANDAA

Changanya sukari na siagi katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy)
Tia yai moja moja huku unachanganya mpaka iwe laini kama sufi. (fluffy)
Tia unga, baking powder, matunda makavu, changanya na mwiko.
Chota mchanganyiko wa biskuti kwa mkono kama (kiasi cha kijiko kimoja cha supu) fanya duara na uchovye katika cornflakes iliyopondwa kwa mkono (crushed)
Zipange katika treya ya kupikia na zipike (bake) katika moto wa 375°F kwa muda wa kiasi dakika 15 huku unazitazama tazama.

Mapishi ya Wali Mweupe Kwa Mchuzi Wa Kuku Wa Balti

Vipimo

Kuku 1 mkate vipande vipande

Vitunguu 3 katakata (chopped)

Nyanya 5 zikatekate (chopped)

Tangawizi mbichi ilokunwa au ilosagwa 1 kijiko cha kulia

Thomu (kitunguu saumu) kilosagwa kijiko 1 cha kulia

Bizari mchanganyiko (garam masala) kijiko 1 cha chai

Jira/bizari ya pilau (cummin powder) kijiko 1 cha chai

Dania/gilgilani ilosagwa (coriander powder) kijiko 1 cha chai

Mtindi/maziwa lala (yoghurt) vijiko vya kulia 4 mjazo au paketi moja ndogo.

Malai ya kupikia (cooking cream) kikombe 1

Kasuri methi (majani makavu ya uwatu/dried fenugreek leaves) 1 kijiko cha kulia

Mafuta ya kupikia ½ kikombe

Chumvi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha kuku vizuri mwache achuje maji.
Weka mafuta katika sufuria kaanga vitunguu mpaka vianze kugeuka rangi ya brown hafifu. Kisha tia tangawizi na thomu ukaange.
Tia kuku ukaange mpaka ageuke mweupe kisha tia nyanya endelea kukaanga ziwive.
Piga mtindi vizuri katika kibakuli uwe nyororo.
Epua sufuria weka kando kisha tia mtindi uchanganye vizuri pamoja na kuku.
Rudisha katika moto acha uchanganyike na kuku kidogo kisha mwagia malai ya kupikia (cooking cream)
Tia kasuri methi/majani makavu ya uwatu yaliyovurugwa. Acha katika moto dakika 1 tu.
Epua umimine katika chombo na nyunyizia ikiwa tayari kuliwa na wali mweupe.

Jinsi ya kupika Keki Ya Maboga

Viamba upishi

Unga wa ngano vikombe vikubwa 3
Boga lililopondwa kikombe 1
Baking powder vijiko vidogo
Sukari kikombe kikubwa 1
Blue band kikombe ½
Vanilla kijiko kidogo 1
Mayai 2
Maji kiasi/ maziwa
(kama nilazima)

Hatua

• Osha boga, Kata, ondoa mbegu, kisha kata vipande vikubwa, chemsha na maji mpaka vilainike.
• Kwangua boga la ndani ukiacha maganda na ponda sawasawa.
• Chekecha unga (kila kikombe 1, vijiko vidogo 2 vya baking powder) kwenye bakuli kubwa.
• Ongeza blue band na changanya sawasawa na vidole.
• Ongeza sukari na changanya.
• Ongeza mayai na koroga na mwiko.
• Ongeza boga lililopondwa na koroga njia moja mpaka ilainike.
• (Kama haikulainika ongeza yai /mayai au maziwa/ maji kidogo).
• Ongeza vanilla na koroga.
• Paka mafuta chombo cha kuokea au sufuria kisha chekecha unga kidogo wa ngano.
• Mimina rojo la keki kwenye sufuria au chombo cha kuokea.
• Oka kwenye oven au tumia sufuria na weka mkaa wa moto juu na chini moto kidogo mpaka iive.
• Jaribu kuchoma kisu katikati, kama ni kavu keki imeiva, epua, pozesha kata tayari kwa kula, kama kitafunio.

Mapishi ya Tende Ya Kusonga Ya Lozi Na Cornflakes

VIAMBAUPISHI

Tende zilizotolewa kokwa – 1 Kilo

Cornflakes – 1 ½ kikombe

Lozi Zilokatwa katwa – 1 kikombe

Siagi – ¼ kilo

MANDALIZI

Mimina tende na siagi kwenye sufuria bandika motoni moto mdogo mdogo mpaka zilainike. Kwa muda wa dakika 10.
Isonge kidogo kwa mwiko au kuikoroga ichanganyike vizuri.
Changanya Cornflakes na lozi kwenye tende mpaka zichanganyika vizuri.
Pakaza treya au sinia mafuta au siagi kidogo.
Mimina mchanganyiko wa tende, zitandaze vizuri na ukate vipande saizi unayopenda. Zikiwa tayari kuliwa kwa kahawa.

Namna ya kutengeneza Visheti Vya Nazi Na Njugu (Sudani)

VIAMBAUPISHI

Unga – 3 mug za chai

Samli – ½ mug ya chai

Maziwa – 1¼ mug ya chai

Baking powder – 2 vijiko vya chai

VIAMBAUPISHI VYA MJAZO

Njugu zilizomenywa vipande vipande – 2 vikombe cha chai

Sukari – ½ kikombe cha chai

Iliki – 1 kijiko cha chai

Nazi iliyokunwa – 2 vikombe vya chai

VIAMBAUPISHI VYA SHIRA

Sukari – 2 vikombe vya chai

Maji – 1 kikombe cha chai

Ndimu – 1

JINSI YA KUVIANDAA

1-Changanya unga na samli kisha tia baking powder na maziwa. Ukande ulainike kisha

uwache kama dakika 5 uumuke.

2-Kwenye bakuli nyingine changanya njugu, sukari na iliki.

3-Kata madonge madogo dogo sukuma kila donge duara jembamba, kisha tia kijiko cha mchanganyiko wa njugu juu yake ifunikie juu yake na ibane pembeni.

4-Panga kwenye treya isiyoganda (non stick) kisha choma kwenye oven kwa moto wa chini

(bake) 350° C kwa dakika kama 15-20.

5-Chemsha maji na sukari katika sufuria ndogo kisha tia ndimu acha ichemke mpaka inatenate unapoigusa.

6-Kwenye sahani ya chali mimina nazi iliyokunwa.

7-Vibiskuti vikiwa tayari vya motomoto chovea kwenye shira kisha zungushia katika nazi iliyokunwa,

panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma (Grilled)

Mahitaji

Mchele wa Basmati /Pishori – 4 vikombe

Kuku

Vitunguu – 3

Nyanya/Tungule – 2

Tangawizi mbichi ilosagwa – 2 vijiko vya supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi nzima – 3

Ndimu – 2

Garama Masala/bizari mchanganyiko – 1 kijiko cha supu

Haldi/tumeric/bizari manjano – 1 kijiko cha chai

Pilipilu ya unga nyekundu – 1 kijiko cha chai

Mtindi /yoghurt – 3 vijiko vya supu

Mafuta ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele, roweka.
Safisha kuku vizuri, mkate vipande vya saizi ya kiasi weka katika bakuli.
Katika kibakuli kidogo, changanya tangawizi mbichi, thomu, bizari zote, pilipili nyekundu ya unga, chumvi, mtindi, kamulia ndimu.
Punguza mchanganyiko kidogo weka kando.
Mchanganyiko uliobakia, tia katika bakuli la kuku uchanganye vizuri arowanike (marinate) kwa dakika chache hata nusu saa au zaidi.
Weka kuku katika treya ya kuoka au kuchoma katika oveni kisha mchome (grill) uwe unageuzageuza hadi aive.
Epua, weka kando.
Katakata vitunguu, nyanya/tungule, pilipili boga weka kando.
Katika sufuria ya kupikia biriani, tia mafuta, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
Tia nyanya na pilipili mbichi, pilipili boga na mchanganyiko uliopunguza awali.
Tia kuku uchaganye vizuri.
Wakati unakaanga vitunguu ili uokoe muda, huku chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji, chuja.
Punguza masala nusu yake weka kando.
Mimina wali kiasi juu ya masala, kisha mimina masala yaliyobakia kisha juu yake tena mimina wali.
Funika upike katika oveni hadi uive.
Changanya unapopakua katika sahani.

Mapishi ya Kidheri – Makande

Mahitaji

Nyama (kata vipande vidogodogo) – ½ kilo

Maharage – 3 vikombe

Mahindi – 2 vikombe

Kitunguu – 1

Nyanya – 2

Kabichi lililokatwa – 2 vikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko cha chai

Vidonge vya supu – 2

Chumvi – kiasi

Mafuta -1au 2 vijiko vya chakula

Namna Yakutayarisha

Chemsha mahindi mpaka yawive na maji yakauke kiasi.
Chemsha maharage pembeni nayo mpaka yawive na maji yakaukie kiasi.
Tia mafuta kwenye sufuria anza kukaanga vitunguu , thomu na vidonge vya supu koroga kiasi.
Kisha mimina nyama iliyokatwa vipande acha ikaangike kidogo na chumvi.
Nyama ikishakaangika tia nyanya funika kwa moto mdogo mpaka nyama iwive.
Kisha mimina mahindi na maharage yaliyochemshwa na maji yake kiasi koroga mpaka ichanganyike na mwisho mimina kabichi funikia mpaka kabichi iwive onja chumvi kama imekolea
Halafu malizia kukoroga mpaka ichanganyike na ikaukie kisha pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Pilau Ya Samaki Wa Tuna Na Mboga

Mahitaji

Mchele – 2 Mugs

Mboga mchanganyiko za barafu (Frozen veg) – Mug

Tuna (samaki/jodari) – 2 kopo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi -2 vijiko vya supu

Garam masala – 1 kijiko cha supu

Nyanya – 2

Kitungu maji – 1

Mdalasini nzima – 2 vijiti

Karafuu – 6 chembe

Pilipili mbichi – 1

Chumvi – kiasi

Viazi – 3

Maji – 2 ½ Mugs

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Maandalizi

Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20
Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga.
Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive.
Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu.
Tia maji, yatakapochemka tia mchele.
Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.

Mapishi ya samaki aina ya salmon

Mahitaji

Salmon fillet 2
Potatao wedge kiasi
Lettice kiasi
Cherry tomato
Limao 1
Swaum
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Mmarinate samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kutengeneza Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga

Mahitaji

Muhogo – 3

Tui La Nazi – 2 vikombe

Chumvi – kiasi

Pilipili mbichi – 2

Mafuta – 1 kijiko moja

Kitunguu maji – 1 kidogo

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chambua muhogo ukatekate au tumia iliyo tayari.
Chemsha muhogo katika sufuria kwa maji kidogo na chumvi, funika uive muhogo.
Karibu na kukauka maji tia tui, kitunguu maji ulichokatakata na pilipili mbichi.
Unaupika moto mdogo mdogo hadi ukauke tayari kuliwa na samaki au kitoweo chochote kingine

Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai

Viambaupishi

  1. Mchele (Basmati) – 3 vikombe
  2. Mbogamboga za barafu (karot, njegere, spring beans na mahindi) – 1 kikombe
  3. Kuku Kidari – 1 LB (ratili)
  4. Mayai – 2 mayai
  5. Vitunguu (vikubwa) – 2 au 3 vidogo
  6. Pili pili manga – 1 kijiko cha chai
  7. Paprika – 1 kijiko cha chai
  8. Chumvi – Kiasi
  9. Mafuta – 1/3 kikombe cha chai
  10. Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko cha supu
  11. Tangawizi – 1 kijiko cha chai
  12. Kidonge cha supu – 1
  13. Soy sauce – 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku

Kata kidari cha kuku vipande vidogo vidogo vya kiasi.

Tia mafuta kidogo katika wok (karai ya kichina)

Kisha mtie kuku, thomu, tangawizi, soy sauce, pilipilimanga, paprika chumvi.

Tia mboga za barafu, kidonge cha supu, kaanga kuku na mboga viwive yitu vyote na mchanganyiko ukauke.

Namna Ya Kutayarisha Na kupika Wali

Roweka mchele wa basmati kwa muda wa saa au zaidi.

Halafu chemsha mchele pamoja na chumvi

Wacha uchemke asilimia 70%

Chuja maji na weka kando

Katika sufuria, tia mafuta kidogo tu

Kisha tia mayai mawili ukaange haraka haraka (crumbled egg)

Changanya mchanganyiko wa kuku na mboga

Kisha tia wali changanye vizuri

Rudisha katika moto, funika upikike kidogo hadi uive

Kisha pakua katika sahani na tolea na mayai ya kuchemsha ukipenda.

Mapishi ya Wali maharage,mchuzi wa samaki na spinach

Mahitaji

Mchele (rice 1/2 kilo)
Maharage yaliyochemshwa (boiled red kidney beans 1 kikombe cha chai)
Samaki waliokaangwa ( 2 fried fish)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2 ya tin)
Vitunguu vilivyokatwa (onion 2)
Kitunguu swaum (garlic 3 cloves)
Tangawizi (ginger kiasi)
Limao (lemon 1/2)
Chumvi (salt)
Pilipili (scotch bonnet pepper 2)
Mafuta (vegetable oil)
Spinach
Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai)

Matayarisho

Saga nyanya, kitunguu, tangawizi na kitunguu swaum pamoja. Tia kwenye sufuria na upike mpaka maji yakauke kisha tia curry powder, mafuta na chumvi na upike tena mpaka mchanganyiko uive kisha tia samaki na limao na maji kiasi na uache uchemke kiasi. Na hapo mchizi utakuwa tayari.
Osha na uzikate spinach kisha kaanga kitunguu na mafuta kiasi (hakikisha visiwe vya brown kisha tia spinach na chumvi. zipike kwa muda wa dakika 3-4 na hapo zitakuwa tayari zimeshaiva.
Wali: Chemsha maji kiasi kisha tia, chumvi, pilipili nzima(isikatwe) mafuta na tui la nazi. Baada ya hapo koroga na utie mchele na maharage na ufunike uache uchemke mpaka maji yakauke. Kisha geuza na ufunike tena na uuache mpaka uive. Baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuseviwa.

Jinsi ya kupika Biskuti Ya Keki Kavu kwa kizungu Shortcake

Viamba upishi

Unga 2 Magi (vikombe vya chai)

Sukari iliyosagwa 2/3 Magi (kikombe cha chai)

Siagi   220 g

Unga wa mchele ½ Magi

Yai 1

Vanilla 1 kijiko cha chai

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Changanya vitu vyote hivyo kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.

2. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in)

3. Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa saa nzima au mpaka ibadilike kuwa rangi ya dhahabu.

4. Epua acha ipoe kisha kata vipande kama mstatili, weak kwenye sahani tayari kunywewa na chai.

Jinsi ya kupika Biskuti Za Tende Na Ufuta

Viambaupishi

Unga 3 Vikombe vya chai

Baking powder 1 ½ Vijiko vya chai

Sukari 1 Kikombe cha chai

Siagi 1 Kikombe cha chai

Mayai 2

Maji kiasi ya kuchanganyia

Tende 1 Kikombe

ufuta ¼ kikombe

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika bakuli

2. Tia mayai, na maji kidogo uchanganye vizuri.

3. Sukuma kiasi kama unavyosukuma chapati duara kubwa.

4. Tandaza tende juu yake halafu kunja hadi mwisho.

5. Paka mayai juu yake halafu mwagia ufuta kisha kata kata vipande kama katika picha.

6. Vipange kwenye treya ya oveni kisha choma(bake)moto wa 350°F kwa muda wa nusu saa takriban.

7. Ziepue katika moto naziache zipowe. Panga katika sahani.

Mapishi ya Tambi na nyama ya kusaga

Mahitaji

Tambi (Spaghetti)
Nyama ya kusaga
Kitunguu maji
Nyanya ya kopo
Kitunguu swaum
Tangawizi
Carrot
Hoho
Lemon
Chumvi
Curry powder
Mafuta
Fersh coriander

Matayarisho

Katakata vitunguu maji, carrot, hoho, kisha weka pembeni. Saga vitunguu swaum na tangawizi pamoja kisha weka pembeni. Baada ya hapo injika sufuria jikoni, tia mafuta. Yakisha pata moto tia vitunguu maji kaanga mpaka vigeuke rangi ya kahawia kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.baada ya hapo tia nyanya ya kopo na iache ichemke mpaka iive. Baada ya nyanya kuiva tia curry powder na chumvi. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia nyama ya kusaga na uiache ichemke mpaka iive.Baada ya nyama kuiva tia Corrot na hoho na uzipike kwa muda wa dakika 2.Na baada ya hapo mboga itakuwa imeivaa, iipue na katia fresh coriander. Baada ya hapo injika sufuria yenye maji jikoni. Yaache yachemke na kisha tia chumvi na mafuta ya mzaituni (olive oil) na tambi. Acha zichemke mpaka ziive kisha zichuuje maji na chujio na baada ya hapo zitakuwa tayari kuseviwa na nyama.

Mapishi ya tambi za kukaanga

Kupika tambi ni kama ifuatavyo

VIAMBA UPISHI

Tambi pakti moja

Sukari ¾ kikombe cha chai

Mafuta ½ kikombe cha chai

Iliki kiasi

Maji 3 Vikombe vya chai

Vanilla / Arki rose 1-2 Tone

Zabibu Kiasi (Ukipenda)

JINSI YA KUPIKA TAMBI ZAKO

1. Zichambue tambi ziwe moja moja.

2. Mimina mafuta kwenye sufuria yakisha pata moto mimina
tambi,zigeuzegeuze mpaka zibadilike rangi na kuwa brown.

3. Punguza mafuta kwa kuyachuja na zirudishe jikoni.

4. Nyunyizia iliki zilizosagwa koroga kidogo na mimina maji na tia arki
na acha zichemke mpaka maji yakikaribia kukauka mimina sukari
koroga kidogo na punguza moto.
5. Kisha tia zabibu ukipenda, zifunike ili zikaukie vizuri.

6. Zikishakauka pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa

Kidokezi: Itategemea na aina za Tambi unazopika kwa kukisia maji, kama utaona hazijaiva unaweza kuongeza maji kidogo.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About