Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Mapishi mazuri ya Chapati za maji

Mahitaji

Unga wa ngano (plain flour) ( 1/4 kilo)
Yai (egg 1)
Sukari (sugar 1/4 kikombe cha chai)
Chumvi (salt 1/4 kijiko cha chai)
Hiliki (ground cardamon 1/4 kijiko cha chai)
Maji kiasi
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Tia unga kwenye bakuli, kisha weka sukari, chumvi, hiliki na maji kiasi. Kisha koroga mpaka mchanganyiko wako uwe mzito. Baada ya hapo tia yai na ukoroge tena. hakikisha mchanganyiko hauwi mzito sana au mwepesi sana.Baada ya hapo onja kama kila kitu kimekolea. Injika chuma cha kupikia chapati (fry-pan) jikoni katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia nusu kijiko cha chakula cha mafuta katika fry-pan na kisha yatandaze. Hakikisha chuma kinapata moto na weka upawa mmoja wa unga wa chapati na uutandaze mpaka uwe flat. Baada ya hapo subiri mpaka chapati ikauke juu na kisha igeuze upande wa pili tia mafuta kijiko 1 kikubwa cha chakula kwa upande wa chini na wa juu kisha uanze kuikandamiza kwa juu na kijiko ili iweze kuiva vizuri kwa chini. Ikisha kuwa ya rangi ya brown igeuze na upike upande wa pili kiasi kisha iipue na uiweke kwenye sahani yenye kitchen towel ili kukausha mafuta. Rudia hii process kwa unga wote uliobakia. Na chapati zitakuwa tayari

Madhara ya nyama nyekundu kwa mtu mwenye VVU

Kuna nyama za aina mbili, nazo ni nyama nyeupe na nyama nyekundu.

Nyama nyeupe

Hizi ni nyama zitokanazo na samaki, kuku, ndege wa aina zote, bata, wadudu

Nyama nyekundu

Hutokana na ngโ€™ombe, mbuzi, kondoo,nguruwe na wanyama wa porini.

Nyama ina virutubishi vingi muhimu kwa afya ya binadamu kama protini, vitamini na madini. Madini ya chuma yanayopatikana kwenye nyama ni rahisi sana kusharabiwa (kufyonzwa) mwilini na ni muhimu kwa kuongeza wekundu wa damu.
Uwezo wa miili ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuyeyusha chakula na kusharabu (kufyonza) virutubishi hupungua. Utumiaji wa nyama nyekundu kwa wingi unaweza kuwaletea matatizo hasa katika uyeyushwaji tumboni kwani nyama nyekundu si rahisi kuyeyushwa ukilinganisha na nyama nyeupe.

Hata hivyo katika nchi yetu watu walio wengi wanatumia nyama kwa kiasi kidogo sana na mara chache. Si vyema watu hawa waache kabisa nyama nyekundu. Jambo la muhimu ni kutumia njia mbalimbali ili kuifanya nyama hii iyeyushwe kwa urahisi tumboni.

Namna ya kusaidia uyeyushwaji ni pamoja n a : –

โ€ข Kutafuna vizuri au kutumia nyama ya kusaga (kwa wanaoipata).
โ€ข Kupika nyama na viungo vinavyosaidia kulainisha kama vile papai bichi, limao, vitunguu saumu n.k.
โ€ข Kula nyama pamoja na papai

Kwa hiyo, kwa anayepata nyama nyekundu kwa wingi, kupunguza kiasi cha nyama hiyo na kuongeza kiasi cha nyama nyeupe. Na kwa yule asiyepata nyama nyeupe, apatapo nyama nyekundu asiache kutumia kwani ina umuhimu mwilini mwake.

Jinsi ya kutengeneza Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga

Mahitaji

Muhogo – 3

Tui La Nazi – 2 vikombe

Chumvi – kiasi

Pilipili mbichi – 2

Mafuta – 1 kijiko moja

Kitunguu maji – 1 kidogo

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chambua muhogo ukatekate au tumia iliyo tayari.
Chemsha muhogo katika sufuria kwa maji kidogo na chumvi, funika uive muhogo.
Karibu na kukauka maji tia tui, kitunguu maji ulichokatakata na pilipili mbichi.
Unaupika moto mdogo mdogo hadi ukauke tayari kuliwa na samaki au kitoweo chochote kingine

Upishi na Matunda ya Mzabibu: Vitamu vyenye Antioxidants

Upishi na Matunda ya Mzabibu: Vitamu vyenye Antioxidants ๐Ÿ‡

Habari za leo wapenzi wa chakula na afya! Leo nataka kuzungumzia faida ya upishi na matunda ya mzabibu. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, matunda haya matamu yanajulikana kuwa na virutubisho na antioxidants nyingi ambazo zinaweza kuleta manufaa makubwa kwa afya yetu. Kama AckySHINE, nina ushauri muhimu na maelezo kuhusu jinsi ya kufurahia vitu hivi vyenye faida ya ajabu. Soma makala hii ili kujua zaidi!

  1. ๐Ÿ‡ Faida ya kwanza ya matunda ya mzabibu ni kwamba yana antioxidants nyingi ambazo husaidia kupambana na athari za radicals huru katika mwili wetu. Hii husaidia kulinda seli zetu dhidi ya uharibifu na kuimarisha mfumo wetu wa kinga.

  2. ๐Ÿ‡ Kula matunda ya mzabibu kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo. Antioxidants zilizopo katika matunda haya husaidia kupunguza viwango vya cholesterol mbaya na kuboresha afya ya moyo.

  3. ๐Ÿ‡ Matunda ya mzabibu yana kiwango kizuri cha vitamini C, ambayo ni muhimu kwa afya ya ngozi yetu. Vitamini C husaidia kujenga collagen, ambayo ina jukumu kubwa katika kuifanya ngozi yetu ionekane nzuri na yenye afya.

  4. ๐Ÿ‡ Kwa kuwa na kiwango cha juu cha maji, matunda ya mzabibu yanaweza kusaidia katika kudumisha afya ya figo. Maji ya kutosha mwilini ni muhimu kwa kazi nzuri ya figo.

  5. ๐Ÿ‡ Pia, matunda haya yana kiwango kikubwa cha resveratrol, ambayo inajulikana kwa uwezo wake wa kupambana na uchochezi. Hii inaweza kuwa na manufaa sana kwa watu wenye matatizo ya uchochezi kama vile ugonjwa wa arthritis.

  6. ๐Ÿ‡ Kwa kuwa ni chanzo kizuri cha nyuzi za chakula, kula matunda ya mzabibu kunaweza kusaidia katika kudumisha afya njema ya utumbo wetu. Nyuzi hizi husaidia katika kuzuia matatizo ya kuvuja kwa utumbo na kuboresha mwendo wa utumbo.

  7. ๐Ÿ‡ Je, umewahi kusikia kuhusu mafuta ya mbegu za mzabibu? Mafuta haya yana virutubisho muhimu kama vile asidi ya linoleiki na vitamini E ambavyo husaidia kulinda ngozi yetu dhidi ya madhara ya mazingira na kuifanya iwe laini na yenye afya.

  8. ๐Ÿ‡ Kulingana na utafiti, matunda ya mzabibu yameonyeshwa kuwa na uwezo wa kuboresha kumbukumbu na afya ya ubongo. Polyphenols katika matunda haya yana jukumu katika kuboresha afya ya ubongo na kuzuia uharibifu wa seli za ubongo.

  9. ๐Ÿ‡ Matunda ya mzabibu ni chanzo kizuri cha nishati. Kwa sababu ya sukari asili iliyomo, matunda haya yanaweza kutoa nguvu na kuongeza kiwango chako cha nishati katika siku yako.

  10. ๐Ÿ‡ Kwa wale wanaopenda kupunguza uzito, matunda ya mzabibu yanaweza kuwa msaada mzuri. Kwa kuwa yana kiwango cha chini cha kalori na mafuta, yanaweza kusaidia katika kudhibiti hamu ya kula na kusaidia katika kupunguza uzito.

  11. ๐Ÿ‡ Kumbuka, ingawa matunda ya mzabibu ni yenye manufaa kwa afya, ni muhimu kula kwa kiasi. Kula matunda mengi sana ya mzabibu kunaweza kuwa na athari hasi kama vile kuongeza uzito na kuathiri viwango vya sukari mwilini.

  12. ๐Ÿ‡ Kwa upande mwingine, unaweza pia kufurahia faida za matunda ya mzabibu kupitia juisi yake. Juisi ya mzabibu inaweza kuwa chaguo nzuri kwa wale ambao hawapendi kula matunda yenyewe.

  13. ๐Ÿ‡ Je, umewahi kufikiria kutumia matunda ya mzabibu kwenye sahani yako ya salad? Matunda haya yanaweza kuongeza ladha na ladha ya kipekee kwenye saladi yako na pia kuongeza faida ya kiafya.

  14. ๐Ÿ‡ Unaweza pia kuongeza matunda ya mzabibu kwenye smoothie yako ya asubuhi. Itakupa ladha tamu na virutubisho muhimu kwa mwili wako.

  15. ๐Ÿ‡ Kwa kuhitimisha, matunda ya mzabibu ni chakula kizuri sana kwa afya yetu na inaweza kuongeza ladha katika milo yetu ya kila siku. Kama AckySHINE, napendekeza kujumuisha matunda haya matamu katika lishe yako na kufurahia faida zake nyingi!

Je, umewahi kula matunda ya mzabibu? Una maoni gani kuhusu faida zake? Tuambie katika sehemu ya maoni hapa chini! ๐Ÿ‡๐Ÿ˜Š

Jinsi ya kupika Vileja

VIPIMO

Unga wa mchele 500g

Samli 250g

Sukari 250g

Hiliki iliyosagwa 1/2 kijiko cha chai

Arki (rose flavour) 1/2 kijiko cha chai

Baking powder 1 kijiko cha chai

Mayai 4

Maji ya baridi 1/2 kikombe cha chai

NAMNA YA KUTAYRISHA NA KUPIKA

1. Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari.

2. Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki.

3. Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri.

4. Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri.

5. Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu.

6. Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa

Jinsi ya kupika Mkate wa sinia

Mahitaji

Unga wa mchele (rice flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 3/4 ya kikombe cha chai)
Hamira (dried yeast 3/4 kijiko cha chakula)
Hiliki (cardamon powder 1/2 kijiko cha chai)
Ute wa yai 1(egg white)
Tui la nazi (coconut milk kikombe 1 na 1/2 cha chai)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Changanya unga wa mchele, hamira, hiliki na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastic kisha koroga vizuri. Ufunike na uwache katika sehemu ya joto mpaka uumuke.(ambayo inaweza kuchukua kama dakika 30-45. Ukisha umuka tia sukari na ute wa yai kisha ukoroge vizuri. Baada ya hapo washa oven katika moto wa 200ยฐC kisha chukua chombo cha kuokea na ukipake mafuta na umimine mchanganyiko. Kisha utie katika oven na uoke kwa muda wa dakika 40. Hakikisha unaiva na kuwa rangi yabrown juu na chini. Na hapo mkate utakuwa tayari.

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Cornflakes

MAHITAJI

Unga – 1 Kikombe

Sukari ya kusaga – 3/4 Kikombe

Siagi – 125 gms

Yai – 1

Baking powder – 1/2 kijiko cha chai

Zabibu kavu – 1/2 kikombe

Cornflakes iliyovunjwa (crushed) – 2 Vikombe

Vanilla – 1 kijiko cha chai

MAANDALIZI

Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri.
Tia baking powder, zabibu na unga na changanya vizuri.
Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni.
Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Weka cornflakes katika sahani ya chali (flat) na zungusha viduara humo kisha upange katika sinia ya oveni.
Pika katika moto wa 350ยบF kwa muda wa dakika 20-25 hadi vigeuke rangi na viwive.

Mapishi ya Wali Wa Nazi Wa Adesi, Bamia Na Mchuzi Wa Kamba

Mahitaji

Mchele – 2 vikombe

Adesi -1 ยฝ vikombe

Nazi ya unga – 1 Kikombe

Maji (inategemea mchele) – 3

Chumvi – Kiasi

Vipimo Vya Bamia:

Bamia – ยฝ kilo

Vitunguu maji – 2 vya kiasi

Nyanya iliyosagwa – 1 kubwa

Nyanya ya kopo – 2 vijiko vya chai

Pilipili manga – ยฝ kijiko cha chai

Mafuta – 3 vijiko vya chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

Wali wa adesi

Osha na roweka mchele na adesi .
Chuja nazi kwa vikombe 3 vya maji tia chumvi kisha weka jikoni.
Tui la nazi likishachemka tia mchele na adesi pamoja. Punguza moto, funika wali upikike kwa moto mdogo mpaka ukauke vizuri.

Bamia

Katakata bamia vipande vya kiasi/ Katakakata vitunguu weka kando.
Katika sufuria tia mafuta na kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi.
Tia nyanya ilosagwa na nyanya ya kopo na pilipili manga na chumvi.
Kisha Tia bamia punguza moto mdogo mdogo mpaka ziwive.

Vipimo: Mchuzi Wa Kamba

Kamba – 1Lb

Vitunguu vilokatwa katwa – 2

Nyanya ilokatwa katwa – 2

Pilipili mbichi iliyosagwa – 1 Kijiko cha chai

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 Kijiko cha chai

Bizari ya mchuzi (curry powder) – ยฝ Kijiko cha chai

Haldi โ€“ bizari ya manajano – ยฝ kijiko cha chai

Nyanya ya kopo – ยฝ Kijiko cha chai

Ndimu – 1

Chumvi – Kiasi

Mafuta ya kukaangia – 2 Vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Kaanga vitunguu kidogo hadi vilainike,
Tia nyanya, thomu na piilipili mbichi. Endelea kukaanga, tia nyanya ya kopo, chumvi, bizari zote.
Tia tia kamba na huku unakoroga mpaka wabadilike rangi na kuwiva. Kamulia ndimu na mchuzi uko tayari.

MAANA YA MANENO YANAYOTUMIKA KATIKA MASUALA YA LISHE

1. Chakula

ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na kuupatia mwili virutubishi mbalimbali Chakula huupatia mwili nguvu, kuulinda na kuukinga dhidi ya maradhi mbalimbali .Mfano wa chakula ni ugali, wali, maharagwe, ndizi, viazi, mchicha, nyama, samaki.

2. Lishe

ni mchakato unaohusisha hatua mbalimbali za jinsi mwili unavyokitumia chakula kilicholiwa, hatua hizi ni kuanzia chakula kinapoliwa, jinsi mwili unavyokisaga na kukiyeyusha, umetaboli, na hatimaye virutubishi kufyonzwa na kutumika mwilini.

3. Virutubishi

ni viini vilivyoko kwenye chakula ambavyo vinauwezesha mwili kufanya kazi zake, karibu vyakula vyote huwa na kirutubishi zaidi ya kimoja ila hutofautiana kwa kasi na ubora. Kila kirutubishi kina kazi yake mwilini na mara nyingi hutegemeana ili viweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. Hakuna chakula kimoja chenye virutubishi vya aina zote isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto, ni mhimu kula vyakula vya aina mbalimbali ili kuwezesha mwili kupata virutubishi mchanganyiko vinavyohitajika.

4. Mlo kamili

ni ule ambao hutokana na chakula mchanganyiko kutoka katika makundi yote ya chakula na una virutubishi vyote muhimu kwa ajili ya lishe na afya bora. Mlo huu unapoliwa kwa kiasi cha kutosha kulingana na mahitaji ya mwili angalau mara tatu kwa siku huupatia mwili virutubisho vyote muhimu.

5. Ulaji unaofaa

hutokana na kula chakula mchanganyiko na cha kutosha (mlo kamili) ili kukidhi mahitaji ya mwili. Ulaji unaofaa pia huzingatia matumizi ya kiasi kidogo cha chumvi, mafuta, sukari, ulaji wa nyama nyekundu kwa kiasi kidogo. Ni muhimu kuzingatia ulaji wa mboga mboga, matunda, na vyakula vya jamii ya kunde kwa wingi ili kudumisha uzito wa mwili unaotakiwa na kupunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

6. Nishati- lishe

ni nguvu inayopatikana baada ya virutubishi (kabohaidreti, mafuta) kuvunjwa vunjwa mwilini. Mwili huitumia nguvu hiyo kufanya kazi mbalimbali Kama kulima, kutembea, kupumua, kuziweka seli za mwili katika hali inayotakiwa n.k.

7. Kalori au kilo kalori

ni kipimo kinachotumika kupima nishati -lishe

8. Makapi mlo

ni sehemu ya chakula ambayo mwili hauwezi kuyeyusha lakini ni muhimu katika uyeyushwaji wa chakula. Mfano wa vyakula venye makapi mlo kwa wingi ni mboga za majani, matunda( maembe, machungwa, mapera, machenza, mafenesi, unga usiokobolewa( dona) na vyakula vya jamii ya kunde.

9. Lehemu

ni aina ya mafuta yanayopatikana hasa kwenye vyakula vya asili ya wanyama na pia hutengenezwa mwilini. Lehemu inayotokana na vyakula ikizidi mwilini huleta madhara ya kiafya. Vyakula venye lehemu kwa kiasi kikubwa ni pamoja na maini, figo, mayai, nyama iliyonona kama nundu, nyama ya nguruwe yenye mafuta, mkia wa kondoo, samli, siagi, ngozi ya kuku n.k.

10. Utapiamlo

ni hali ya kupungua au kuzidi kwa baadhi ya virutubishi mwilini ambapo husababisha lishe duni au unene uliozidi.

11. Antioxidants

ni viini ambavyo vina uwezo wa kukinga seli za mwili zisiharibiwe na chembe chembe haribifu (free radicals) ambazo huweza kusababisha saratani. Viini hivyo huungana na chembechembe hizo haribifu na kuzidhibiti ili zisisababishe madhara. Mifano ya antioxidants ni pamoja na beta-carotene, lycopene, vitamin C, E, na A.

Jinsi ya kupika Roast ya biringanya na mayai

Mara nyingi biringanya hutumika kama kiungo cha nyongeza katika mchuzi. Hata hivyo, kiungo hiki kinaweza kupikwa chenyewe na kutoa mchuzi wenye ladha ya kipekee.

Baadhi ya wapishi wameweza kubuni aina hii ya upishi ambayo huweza kupikwa kwa dakika tano tu na kukupa chakula kitamu chenye ladha ya kuvutia.

Uzuri wa chakula hi ni kwamba kinaweza kuliwa wakati wowote na kwa chakula chochote kulingana na matakwa ya mlaji.

Kwa mujibu wa wataalamu wa maswala ya mapishi, biringanya ni miongoni mwa vyakula vyenye mapishi mengi kama ilivyo kwa mchele.
Hapa tutaenda kuona jinsi ya kupika roast ya biringanya na mayai.

Mahitaji:

Biringanya 2 kubwa
Nyanya 4 kubwa
Kitunguu maji kilichosagwa kijiko 1 cha mezani
Mayai 2
Mafuta ya mzeituni vijiko vitatu vya mezani
Chumvi kiasi
Pilipili 1 (kama unatumia)
Hoho 1
Karoti 1
Kitunguu swaumu kilichosagwa 1
Kotimili fungu 1

Maadalizi:

Chukua biringanya ioshe vizuri na kasha katakata vipande vidogo vidogo.
Osha na menya nyanya hapafu katakata. Fanya hivyo kw akaroti na hoho pia.
Weka mafuta kwenye sufuria na weka jikoni kwenye moto kiasi
Yakishachemka maji na kasha weka kitunguu maji na kasha swaumu huku ukikaanga taratibu.
Weka hoho na karoti huku ukiendelea kukaanga. Baada ya hapo weka nyanya na baadae chumvi. Funika hadi ziive kabisa na kasha weka majani ya kotimili.
Weka biringanya. Acha vichemke hadi viive. Koroga ili kuruhusu mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.
Kwa kuwa biringanya ina majimaji huhitaji kuweka maji ya ziada, weka pilipili.
Acha kwa muda wa dakika tatu hadi dakika tano. Pasua mayai na kisha miminia huku ukikoroga taratibu. Fanya hivyo hadi yaive kabisa na kuwa mchuzi mzito. Roast yako ya biringanya iko tayari kwa kuliwa
Unaweza kula aina hii ya mboga na mikate, maandazi na hata ugali

Mapishi ya Pilau Ya Sosi Ya Soya Na Mboga

Viambaupishi

Kuku (mkate mkate vipande) 1

Mchele wa Basmati (rowanisha) 3 magi

Mdalasini 1 mchi mmoja

Vitunguu maji (vilivyokatwa vyembamba) 6

Mchanganyiko wa mboga za barafu 1 magi

(karoti, mahindi, njegere)

Kabichi (iliyokatwa katwa nyembamba) 1 magi

Pilipili mbichi (iliyosagwa) 3

Pilipili boga iliyokatwa vipande vidogo vidogo 1

Pilipili manga 1 kijiko cha chakula

Chumvi 1 kijiko cha chakula

Sosi ya soya (soy sauce) 5 vijiko vya chakula

Kotmiri iliyokatwa katwa 1 magi

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa 2 vijiko vya chakula

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Tia mafuta ndani ya karai. Yakipata moto kiasi, mimina vitunguu maji na mdalasini 1 mzima kaanga. Itachukua muda kidogo. Kaanga mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown). Viepue na uweke kando.

2. Ndani ya sufuria kubwa, mimina kuku, chumvi, thomu na tangawizi, sosi ya soya, pilipili manga, pilipili mbichi, chemsha mpaka kuku awive na maji yakauke.

3. Changanya vitunguu ulivyokaanga, kabichi, pilipili, mboga, kotmiri, mchanganyiko wa mboga za barafu na weka kwa muda wa dakika tano au kumi. Tia na mafuta kidogo uliyokaangia vitunguu .

4. Chemsha mchele na chumvi uwive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja. Ukishauchuja umwagie katika masala ya kuku.

5. Nyunyizia mafuta kidogo uliokaangia vitunguu.

6. Weka moto mdogo mpaka wali ukishawiva. Uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa.

KIDOKEZO:

Unaweza kuupika wali huo ndani ya jiko, yaani badala ya kutia masala kwenye sufuria ukayatia katika bakuli au treya ya jiko (oven), kisha ukamwagia wali uliouchuja humo na kuupika kaitka moto wa 400-450 Deg kwa muda wa dakika 15-20.

Jinsi ya kuandaa Wali Wa Hudhurungi Na Kabeji

VIPIMO VYA WALI

Mchele wa hudhurungi (brown rice)

na (wild rice kidogo ukipenda)Osha na Roweka – 2 Vikombe

Kitungu maji – 1 Kiasi

Kitunguu saumu – 1 Kijiko cha supu

Bizari ya manjano – 1/2 Kijiko cha chai

Mdalasini nzima – 1 kijiti

Iliki iliyosagwa – 1/4 Kijiko cha chai

Chumvi – Kiasi

Pilipili manga – 1/4 Kijiko cha cha

Mafuta – 2 Vijiko vya supu

Majani ya Bay(bay leaves) – 1

Mbegu ya giligilani iliyoponwa (coriander seeds) – 1 Kijiko cha chai

Supu ya kuku ya vidonge – 1

Maji ya wali – 4 vikombe

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Kaanga kitungu, kabla ya kugeuka rangi tia thomu.
Kisha weka bizari zote na ukaange kidogo.
Tia mchele kisha maji na ufunike upike katika moto mdogo.
Na ikishawiva itakuwa tayari kwa kuliwa na kabeji na kuku wa tanduuri.

VIPIMO VYA KABEJI

Kabeji iliyokatwa katwa – 1/2

Karoti iliyokwaruzwa – 1-2

Pilipili mboga kubwa – 1

Figili mwitu (celery) iliyokatwa – 1 au 2 miche

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa – 1 Kijiko cha supu

Pilipili mbichi – 1

Kisibiti (caraway seed) – 1/4 Kijiko cha chai

Bizari ya manjano ya unga = 1/2 Kijiko cha chai

Giligani ya unga – 1 Kijiko cha chai

Chumvi – Kiasi

Kitungu maji kilichokatwa -1

Kotmiri – upendavyo

Mafuta ya kukaangia – Kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Kwenye sufuria kaanga kitungu, figili mwitu kisha tia thomu na pilipili zote.
Halafu tia bizari zote na ukaange kidogo.
Kisha weka kabeji na chumvi, ufunike moto mdogo ilainike kidogo na sio sana
Tia karoti na usiwache motoni sana, kisha zima moto na inyunyizie kotmiri juu.

Mapishi ya Ndizi mzuzu

Mahitaji

Ndizi tamu (plantain) 3-4
Tui la nazi (coconut milk) kikombe 1 cha chai
Sukari (sugar) 1/4 ya kikombe cha chai
Hiliki (Ground cardamon) 1/4 ya kijiko cha chai
Chumvi (salt) 1/4 ya kijiko cha chai

Matayarisho

Menya ndizi kisha zikwangue utomvu wote. Baada ya hapo zikate kati (kiurefu) na kisha kata tena kati katika kila ndizi vitoke vipande 4. baada ya hapo toa moyo wa katikai wa ndizi. Zioshe na kisha zikaushe maji na uziweke kwenye sufuria ya kupikia. Baada ya hapo tia tui la nazi, sukari, chumvi na hiliki. Ziinjike jikono na uziache zichemke uku ukiwa unalikoroga tui ili lisikatike. Baada ya dakika 10 tui la nazi litakuwa limepungua na kubaki kidogo na hapo ndizi zitakuwa zimeshaiva. Ziache zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa. Zinaweza kuliwa kama mlo (main meal) au kitinda mlo (dissert) au mlo wa pembeni (side dish) haswa kwa futari.

Mapishi ya Mihogo ya nazi na kuku

Mahitaji

Mihogo kilo 1
Kidali cha kuku 1 kikubwa
Nyanya 1 kubwa
Kitunguu maji 1 cha wastani
Swaum/tangawizi i kijiko cha chai
Nazi kopo 1
curry powder 1 kijiko cha chai
Binzari manjano 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili 1
Chumvi kiasi

Matayarisho

Saga pamoja nyanya, kitunguu na swaum/ginger pamoja na vimaji kidogo. Kisha vitie kwenye sufuria isiyoshika chini na uvishemshe mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta na upike ktk moto mdogo mpaka viive.Baada ya hapo tia spice na uzipike kidogo kisha tia mihogo na kuku (kuku na mihogo vikatwe vipande vya wastani) vichanganye vizuri kisha tia nazi na vimaji kiasi,limao chumvi na pilipili na ufunike kisha punguza moto. Pika mpaka mihogo na kuku viive na ibaki rojo kidogo kisha ipua na mihogo yako itakuwa tayari kwa kuliwa

Mapishi ya Mandazi Matamu

Mahitaji

Unga wa ngano (nusu kilo)
Sukari (Kikombe 1 cha chai)
Chumvi (nusu kijiko cha chai)
Hamira (kijiko kimoja cha chai)
Yai (1)
Maziwa ya unga (vijiko 2 vya chakula)
Butter (kijiko 1 cha chakula)
Hiliki (kijiko1 cha chai)
Maji ya uvuguvugu ya kukandia
Mafuta ya kuchomea

Matayarisho

Tia unga kwenye bakuli kisha tia sukari, chumvi, yai, maziwa ya unga, butter na hiliki kisha uchanganye pamoja mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia maji ya uvuguvugu kiasi na uanze kuukanda. Ni vizuri ukaukanda kwa muda wa dakika 15 ili kuhakikisha donge lote la unga limelainika vizuri.
Baada ya hapo Tawanyishaa unga uliokwandwa katika madonge 4. Tia unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze kusukuma donge moja katika shape ya chapati na hakikisha haiwi nyembamba sana wala nene sana yani inatakiwa iwe ya wastani.Ukishamaliza kusukuma unatakiwa ukate shape uipendayo na uyatandaze katika kitu kilichopo flat na kiwe kimenyunyuziwa unga wa ngano ili kuyazuia yasigandie. Rudia hiyo process kwa madonge yote yaliyobakia. Baada ya hapo yaweke mandazi katika sehemu iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka (inaweza kuchukua masaa 3 kuumuka). Yakisha umuka unatakiwa uweke mafuta katika karai la kuchomea. Yakisha pata joto la kiasi unatakiwa utumbukize mandazi na unaze kuyachoma mpaka yawe ya brown. Yakisha iva yaipue na uyaweke kwenye kitchen towel iliyakauke mafuta. Yakisha poa yatakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kupika Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

VIPIMO:

Unga wa Visheti

Unga 4 Vikombe vya chai

Siagi 1 Kikombe cha chai

Hiliki ยฝ Kijiko cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.

2. Changanya vizuri isiwe na madonge.

3. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.

4. Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.

5. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .

6. Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili

7. Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.

8. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.

Shira:

Sukari 2 Vikombe vya chai

Maji 1 Kikombe cha chai

Vanilla ยฝ Kijiko cha chai

(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.

Upishi wa Afya kwa Watoto: Milo Mzuri na Lishe Bora

Upishi wa Afya kwa Watoto: Milo Mzuri na Lishe Bora ๐ŸŽ๐Ÿฅฆ

Habari za leo wapendwa wasomaji! Leo nataka kuzungumzia kuhusu umuhimu wa upishi wa afya kwa watoto. Kama AckySHINE, ninalo jukumu la kusaidia kila mtu kupata lishe bora na kuishi maisha yenye afya tele. Kwa hivyo, leo nitalenga katika upishi wa afya kwa watoto na umuhimu wa milo mzuri na lishe bora.

  1. Milo mzuri ni muhimu sana kwa watoto kwani hutoa nishati wanayoihitaji kwa shughuli zao za kila siku. Kwa mfano, mlo mzuri unaweza kuwa na ugali, maharage, samaki, na mboga mboga kama karoti, pilipili, na mchicha.

  2. Lishe bora ni msingi wa ukuaji na maendeleo ya mtoto. Kwa kuwapa watoto lishe bora, tunajenga mwili wenye nguvu na mfumo wa kinga imara.

  3. Matunda na mboga mboga ni mhimu sana katika upishi wa afya kwa watoto. Matunda kama ndizi, machungwa, na embe hutoa vitamini na madini muhimu kwa miili yao. Mboga mboga kama karoti, kabichi, na spinach zinaongeza nyuzi, vitamini, na madini muhimu.

  4. Kwa kuwa watoto hupenda vitafunwa, tumia wakati mzuri kuwapa vitafunwa vyenye afya kama vile karanga, parachichi, na tambi za mchele. Vitafunwa hivi vina lishe bora na hutoa nishati kwa watoto wetu.

  5. Kama AckySHINE, napendekeza kuwa na milo ya kawaida na kufanya kila mlo kuwa wa kufurahisha na wa kuvutia kwa watoto. Unaweza kujaribu kutengeneza milo yenye rangi mbalimbali ili kuwavutia watoto kula na kufurahia chakula chao.

  6. Kwa watoto ambao hawapendi mboga mboga, unaweza kujaribu kuzipika kwa njia tofauti ili kuongeza ladha na kufanya ziwe za kuvutia kwa mtoto wako. Kwa mfano, unaweza kuzikaanga mboga mboga kwenye mafuta kidogo na kuongeza viungo vinavyopendwa na mtoto wako.

  7. Pia, ni muhimu kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata protini ya kutosha katika milo yao. Protini husaidia katika ukuaji wa misuli na kuboresha afya ya ngozi. Unaweza kuwapa watoto wako nyama kama kuku au samaki, au hata maharage na karanga.

  8. Kama mzazi, ni muhimu kuwa mfano mzuri kwa watoto wako. Kwa kuwa unakula lishe bora, watoto wako watafuata mfano wako na wataona kuwa ni kitu cha kawaida na muhimu.

  9. Pia, hakikisha watoto wako wanakunywa maji ya kutosha. Maji ni muhimu katika kuweka mwili kuwa na afya. Badala ya vinywaji vyenye sukari, chagua maji safi na salama kwa watoto wako.

  10. Ni vizuri kuwashirikisha watoto katika upishi. Wanaposhiriki katika maandalizi ya chakula, wanakuwa na hamu ya kula chakula hicho na wanafurahia kujaribu vitu vipya. Unaweza kuwapa majukumu kama vile kukata mboga au kuchanganya viungo.

  11. Kama AckySHINE, napendekeza kutumia vyombo vya kuvutia na rangi mbalimbali katika kuwawekea watoto chakula chao. Hii itawavutia na kuwafanya wafurahie chakula chao.

  12. Kumbuka kuwa kila mtoto ni tofauti, na wanaweza kuwa na upendeleo tofauti katika chakula. Sio kila mtoto atapenda vitu vyote. Jaribu kuelewa mapendezi ya mtoto wako na kujaribu kuwapa chakula wanachopenda, bila kusahau lishe bora.

  13. Pia ni muhimu kuzungumza na watoto wako kuhusu umuhimu wa lishe bora na jinsi inavyowasaidia kuwa na afya bora. Eleza umuhimu wa matunda na mboga mboga na jinsi zinavyojenga miili yao.

  14. Kuwa na ratiba ya milo na muda maalum wa kula pia ni muhimu. Hii itawasaidia watoto wako kuwa na mfumo mzuri wa chakula na kuzuia matumizi ya vyakula visivyo na lishe.

  15. Mwisho lakini sio kwa umuhimu, nataka kusikia maoni yako. Je! Una mbinu yoyote ya kuwafanya watoto wako wapende kula chakula chenye lishe bora? Je! Unapika nini kwa watoto wako ili kuhakikisha wanapata milo mzuri? Na je! Unadhani upishi wa afya ni muhimu kwa watoto? Naamini kuwa tukiweka umuhimu katika upishi wa afya kwa watoto, tutaweza kuwajengea msingi imara wa afya na ustawi. Tafadhali shiriki maoni yako hapa chini! Asante sana na nakutakia siku njema! ๐ŸŒŸ๐ŸŽ๐Ÿฅฆ

Mapishi ya Viazi vitamu na kachumbari

Mahitaji

Viazi utamu 3
Nyanya 2 kubwa
Kitunguu
Tango
Limao
Chumvi
Pilipili
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Menya viazi na kisha vikate katika vipande. Tia mafuta kwenye chuma cha kukaangia, yakisha pata moto tia viazi nauviache vikaangike mpaka upande mmoja uwe wa brown na kisha geuza upande wa pili na upike mpaka uwe wa brown. Vikisha iva ipua na uweke kwenye kitchen towel ili vikauke mafuta.
Kachumbali: Katakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili tango na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja .Baada ya hapo viazi na kachumbali vitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka

Vipimo

Wali:

Mchele – 3 Vikombe

Kitunguu kiichokatwa – 1

Pilipili boga nyekundu iliyokatwa vipande – 1

Mafuta – ยผ Kikombe

Zaafarani – 1 kijiko cha chai tia kwenye kikombe na maji robo roweka

Chumvi – 1 kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katika sufuria, tia mafuta, kaanga kitunguu mpaka kiwe kidogo rangu ya udongo (brown)
Tia pili pili boga.
Tia mchele, kaanga kwa muda wa dakika 3, tia zaafarani na chumvi.
Tia supu uliyochemshia kuku iwe imoto.
Pika wali katika moto mdogo hadi uwive.

Kuku

Kuku Mzima -1

Mayai ya kuchemsha – 6

Namna Ya Kupika Kuku

Mchemshe kuku mzima na chumvi mpaka uhakikishe ameiva vizuri.
Mtowe na muweke pembeni. Supu yake tumia katika wali kama ilivyo hapo juuu.
Chemsha mayai, menya na kata vipande viwili kila yai moja weka kando

Vipimo Vya Sosi Ya Kuku Ya Nazi

Kitunguu – 1

Nyanya iliyokatwa vipande – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi – 1 kijiko cha supu

Garam Masala – ยฝ kijiko cha supu

Bizari ya manjano – ยฝ kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Pilipili masala ya unga – ยฝ kijiko cha chai

Nyanya ya kopo – 1 kijiko cha supu

Nazi ya unga – 1 kikombe

Maji ya ukwaju – ยผ kikombe cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Tia Mafuta vijiko 2 vya supu katika sufuria
Kaanga kitunguu maji mpaka kiwe rangi ya udongo (brown).
Tia thomu na tangawizi.
Tia nyanya nzima iliyokatwa katwa.
Tia garam masala, manjano, pilipili ya unga, nyanya ya kopo, kaanga vizuri.
Changanya kwenye sufuria na ukwaju. Iache ichemke vizuri.
Changanya nazi ya unga na maji vikombe viwili.
Mtie kuku mpike vizuri na hilo tui.
Mtie kwenye oveni kidogo.

Kupakuwa katika Sinia

Pakuwa wali kwanza katika sinia
Muweke kuku juu ya wali.
Pambia mayai

Mapishi ya Muhogo Na Mbatata Za Nazi Kwa Nyama Ngombe

Vipimo – Mahitaji Ya Nyama

Nyama ya nโ€™gombe ya mifupa – 3ย lb

Tangawizi mbichi ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Kitunguu thomu – 1 kijiko cha supu

Bizari ya pilau/jira/uzile (cumin) – 1 kijiko cha supu

Ndimu – 1

Kitunguu kilokatwakatwa (chopped) – 1 cha wastan

Pilipili mbichi – 3 Zilizosagwa

Chumvi – Kiasi

Vipimo – Muhogo Na Mbatata/Viazi

Muhogo menya na ukate vipande pande – 2

Mbatata/Viazi menya ukate vipande vikubwa kiasi – 5 kiasi

Tui la nazi zito – 1 gilasi

Nyanya ilokatwakatwa au kusagwa – 1

Kitunguu kilokatwakatwa (chopped) – 1 kiasi

Bizari ya mchuzi – kiasi

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha nyama kisha weka katika pressure cooker au sufuria.
Tia viungo vyote vya nyama uchanganye vizuri, kisha ikorogekoroge mpaka maji yake yakaribie kukauka. Usifunike.
Tia maji kiasi ya kuivisha nyama na kubakisha supu yake kiasi ya kuivisha muhogo na mbatata. Muda wa kuivisha nyama inategemea nyama yenyewe na kama unatumia pressure cooker ni takriban dakika 35-40. Ikiwa sufuria ya kawaida utakuwa unaikoroga.
Mimina ndani ya supu, muhogo, mbatata, nyanya, kitunguu, bizari ya mchuzi, chumvi.
Acha ichemke uive muhogo na viazi.
Tia tui la nazi, changanya vizuri acha kwenye moto dakika chache tu.
Epua ikiwa tayari. Tolea na achari.

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About