Magonjwa yatokanayo na sigara

Kuna matatizo na magonjwa mengi na ya aina mbalimbali
unayoweza kuyapata kutokana na utuvaji wa sigara. Kiungo
rahisi kuathirika ni mapafu. Baada ya kuvuta huo moshi, kaboni
na tindikali iliyomo kwenye tumbaku huishia kwenye mapafu.
Malimbikizo haya ya kaboni na tindikali husababisha ugumu
katika kupumua na kusabisha usaha kwenye mapafu. Matatizo
haya ya mapafu humfanya mvutaji awe mwepesi kupata
maambukizo mengine.
Hii inaweza ikawa kikohozi sugu na pia inaweza kusababisha
nimonia (kichomi) pamoja na kifua kikuu na sarakani. Nikotini
vilevile ni mbaya kwa tumbo. Husababisha kupoteza hamu ya
kula na maumivu katika sehemu za chini ya tumbo.

Unaweza ukaona kwamba wavutaji wakubwa wa sigara wakawa na
meno meusi au machafu. Hii ni kwa sababu kaboni imejilimbikiza juu
ya meno, na hivyo kubadilika kwa rangi. Watu wanaovuta mara kwa
mara hutoa harufu mbaya mdomoni na hupata matatizo ya ngozi.

Je, sigara ni sumu kwa binadamu?

Ndiyo. Nikotini iliyo kwenye tumbaku ni sumu. Ukiwa na kiwango
kikubwa cha nikotini katika damu utajisikia kichefuchefu,
kutapika, kujaa kwa mate mdomoni, maumivu ya sehemu za
chini ya tumbo, kuharisha, na kujihisi dhaifu. Dalili nyingine
ni kuumwa na kichwa, kizunguzungu, kuongezeka kwa mapigo
ya moyo, kupata shinikizo la damu, kutetemeka na kutokwa na
jasho baridi. Nikotini nyingi inaweza kusababisha ukosefu wa
umakini na pia ukosefu wa usingizi.

Je, ni kweli kuwa madhara ya uvutaji moshi wa sigara yako ni kidogo kuliko yale yatokananyo na kuvuta moshi kutoka kwa mvutaji?

Uvutaji wa aina zote una madhara. Kama utavuta sigara na
kuvuta moshi kwa kutumia mdomo hadi kwenye mapafu yako
utapata madhara moja kwa moja kwenye viungo vyako.
Kama nitasimama karibu na mvutaji na kuvuta moshi, kuna
madhara ambayo siyo ya moja kwa moja. Kwa upande mwingine
kama jirani wa mvutaji unaweza kuvuta sumu nyingi itokanayo
na tumbaku kwa sababu hakuna kitu cha kuichuja. Sigara za
viwandani zina kishungi ambacho huchuja tindikali mbalimbali
zenye sumu, kama vile kaboni na asidi ya magamba ya miti,
ambazo zina madhara kwa mapafu.

Je, gongo na sigara husaidia uyeyushaji wa chakula?

Ni imani na fikra potofu kwamba, ukinywa gongo au kuvuta
sigara kwa kiasi kidogo baada ya chakula itasaidia kuyeyusha
baadhi ya vyakula vya mafuta. Pombe inaweza hata kupunguza
mtiririko wa kawaida wa kimiminika muhimu kwa uyeyushaji wa
chakula (tindikali) na hivyo kuchelewesha kuliko kurahisisha
uyeyushaji wa chakula.
Nikotini ya sigara kwa upande mwingine inaongeza kazi katika
utumbo mpana na hivyo kurahisisha uyeyushaji wa chakula.
Lakini kwa upande mwingine nikotini huchochea utengenezaji
wa tindikali tumboni ambayo husababisha maumivu ya tumbo.

Je, ni kweli kwamba mtu anayekunywa pombe anaishi kwa muda mrefu kuliko yule ambaye hanywi kabisa?

Si kweli. Mpaka sasa wanasayansi hawajathibitisha kwamba
mtu anayekunywa pombe kidogo ndiye anayeishi kwa muda
mrefu. Kwa ujumla, watu wanaoishi katika hali ya usafi, afya
njema na maisha yenye furaha ndio wanaoishi kwa muda
mrefu kuliko wale ambao hawajijali kimwili na kiakili. Kimsingi,
kunywa pombe ni kutojijali. Unywaji wa pombe kwa kiasi hauna
madhara, lakini inakupasa kuwa macho katika unywaji huo ili
usizidishe kupita kiasi.

Je, ukinywa pombe unaongeza damu?

Si kweli.
Pombe haiongezi damu, vitamini wala nguvu. Ukweli ni kwamba unywaji pombe kupita kiasi huvuruga ufyonzaji wa vitamini na madini kutoka kwenye chakula kuingia mwilini.

Vitamini ni muhimu kwa kuimarisha kinga ya mwili ambayo inasaidia kujikinga na magonjwa, pamoja na maradhi kama UKIMWI. Kwa hivyo, unatakiwa uhakikishe unakula matunda na mboga za majani kwa sababu vinakuongezea vitamini.

ATHARI ZA ULEVI KATIKA JAMII

Watu wanokunywa kupitia kiasi huathiri jamii kwa njia
mbalimbali. Madhara mengine hutokea kwa kuwa wanafanya
vitu ambavyo wasingevifanya iwapo wasingekuwa wamelewa.

Watu wakilewa, huweza kuwa na hasira, wagomvi hivyo basi
huwadhuru wengi kiakili na kimwili. Isitoshe, ajali nyingi za
kazini na barabarani hutokea watu wakiwa wamelewa. Mara
nyingi watu wasiokuwa na hatia na vilema hupoteza maisha yao
kutokana na ajali zinazohusiana na ulevi.

Watu wanaokunywa
pombe kupita kiasi hupunguza uangalifu na hivyo basi kuchangia
katika kuenea kwa VVU kwenye jamii. Watu wanaokunywa pombe
wanaweza pia kufanya ujambazi katika jamii. Pia wanaokunywa
kupita kiasi si wafanyakazi wa kutegemewa kwani hutumia
muda mwingi nje ya sehemu zao za kazi.

Watu waliozoea kunywa pombe nyingi hupoteza pesa zao nyingi
kununua pombe na muda wao mwingi kufikiria jinsi ya kupata
pesa za kunywea pombe.

Kutokana na gharama za kununua
pombe familia zao hukosa pesa za vitu muhimu kama kodi ya
nyumba, ada na sare za shule na chakula.

Vijana wanaokunywa pombe huanza kuiba pesa nyumbani kwao
ili kununulia pombe. Matumizi mabaya ya pombe mara nyingi
husababisha matatizo au kuvunjika kwa familia, au urafiki.

Vilevile husababisha matokeo mabaya shuleni au kuacha kabisa
shule, hali ambayo inaweza kusababisha kukosa nafasi za kazi,
kujitegemea wewe mwenyewe na kusaidia famila yako na jamii.

Madhara ya sigara na pombe kwa mtoto

Watoto hawatakiwi kunywa pombe wala kuvuta sigara!

Watoto hasa ndio wapo katika hatari zaidi ya kupata madhara
yatokanayo na uvutaji sigara na unywaji pombe, kwa sababu
bado wanaendelea kukua. Wanaweza wakaathiri miili yao na ubongo
kwa maisha yao yote. Wana hatari zaidi ya kuathirika katika
maendeleo yao ya kijamii na kisaikolojia. Matumizi mabaya ya pombe
na sigara yanaweza yakaleta madhara katika makuzi ya mtoto.

Wanawake wanaweza kulewa haraka kuliko wanaume?

Wasichana na wanawake wanaweza kulewa kwa ujumla.
Mara nyingi, hulewa pombe haraka kuliko wanaume. Hii
inatokana na uzito mdogo wa miili yao, na kiasi cha mafuta na
maji katika miili yao. Kilevi husambaa kiasi kikubwa katika miili
ya wanawake. Maini yao huharibika kirahisi zaidi kuliko maini
ya wanaume.

Kutokana na kilevi, wanawake au wasichana huwa wepesi
kufanya vitu ambavyo wasingefanya kama wasingelewa.
Wanaume hutumia nafasi hii kuwashawishi kufanya mapenzi
bila kuchukua tahadhari yoyote kama vile kutumia kondomu ili
kupunguza maambukizo ya VVU.

Madhara ya pombe kwa mwili na akili

Pombe huingia kwenye damu na kuzunguka mwili mzima pamoja
na kwenye ubongo wako. Ina madhara kwa viungo vya mwili
wako na ubongo wako na hivyo huathiri tabia na hisia zako.

Unywaji wa pombe kupita kiasi unaweza kuathiri viungo vingi
kwa mfano, ini ambalo ndilo huathirika zaidi. Ini hilo linafanya
kazi ya kufyonza kilevi katika mwili wako. Kama ukinywa zaidi
utaathiri ini kiasi kwamba halitaweza kufanya kazi kikamilifu au
litashindwa kabisa hatimaye utakufa. Kilevi kingi husababisha
kansa ya ini na tumbo.

Hatari kubwa siku hizi ni kupata na kusambaza virusi vya
UKIMWI. Mlevi mara nyingi huwa mzembe na husahau kinga
muhimu kama vile kutumia kondomu wakati wa kufanya mapenzi.
Anaweza pia kufanya mapenzi na watu ambao hafahamu afya
zao, kama ni wagonjwa au la. Zaidi ya hayo mlevi mara nyingi
huwa dhaifu, hivyo ni rahisi kushambuliwa na magonjwa
mbalimbali pamoja na VVU.

Pombe inaathiri pia uwezo wa kufanya tendo la ndoa. Huwa ni
vigumu kwa uume kusimama. Pia huathiri ubongo hasa sehemu
zile zinazomiliki ufahamu na mihemko.

Kwanza unaweza kujisikia mchangamfu na huru, lakini mara
tu unaanza kujisikia taabu na kushindwa kutembea vizuri.
Utakuwa na matatizo ya kutoona vizuri na matatizo ya kutoa
uamuzi sahihi. Watu huanza kuwa na vijitabia vya ajabu na
vipya baada ya kulewa. Kugombana na watu wengine na kufanya
mambo yasiyokubalika kama vile kujikojolea mbele za watu.
Kama utaendelea kunywa kuna uwezekano mkubwa wa kupata
madhara. Kila dhara huharibu mamilioni ya seli za ubongo wa
binadamu.

Kwanza hutakuwa na kumbukumbu ya nini kimetokea, lakini
unaweza pia kupoteza kabisa kumbukumbu zako. Kama ukinywa
pombe kupita kiasi kwa muda mrefu unaweza kupungukiwa
akili na mwisho kuharibu kabisa akili. Pombe pia ni dawa ya
kulevya kwani huweza kukutawala. Watu waliotawaliwa na
pombe, hutumia pesa nyingi na muda mwingi kwenye pombe,
hali ambayo inaweza kuwa ni mzigo mzito kwa familia na jamii,
na pindi mtu anapotawaliwa, ni vigumu kunywa kidogo au kuacha
kabisa. Kama mtu atajaribu kuacha, hupata matatizo kama
kutetemeka, mapigo ya moyo kuongezeka, kutokwa na jasho
jingi, na kukosa usingizi wakati wa usiku. Hali hiyo husababisha
maumivu na ni hatari kwa watu ambao wametawaliwa na pombe.

Je, Uvutaji wa sigara unafurahisha na kuchangamsha?

Ndiyo, lakini ni mwanzo tu na kwa muda mfupi; hii ni kwa
sababu mwanzoni nikotini iliyomo katika sigara inasababisha
damu kumiminika kwa wingi kupita kwenye ubongo wako. Hivyo,
husababisha msisimko na kukufanya ujisikie raha. Nikotini
pia inasababisha misuli mwilini kujichua na hivyo kukufanya
ujisikie mchangamfu.

Baada ya muda utajisikia kinyume na ulivyojisikia mwanzoni.
Kama utavuta zaidi na zaidi damu na oksijeni kidogo vitatiririka
mwilini na kwenye ubongo. Hii itakufanya ujisikie mchovu na
mwenye huzuni.

Kwa bahati mbaya baadhi ya matangazo ya biashara au
marafiki watakushawishi kwamba, uvutaji wa sigara ni safi, poa
na hukufanya kujisikia mkubwa. Lakini hawaongelei madhara
mabaya kiafya yatokanayo na uvutaji wa sigara na ugumu wa
kuacha uvutaji huo pale utakapoizoea.

Nikotini mara nyingi
huitwa kianzisho. Hii inamaanisha kwamba wakati mwingine
vijana wanaanza kuvuta sigara na kisha kuhamia kwenye
utumiaji wa dawa za kulevya. Hata hivyo uvutaji ni gharama.

Kwa nini watu wanakunywa pombe?

Unywaji wa pombe ni sehemu ya utamaduni wa Tanzania na nchi
nyinginezo duniani.

Watu hupendelea kunywa pombe katika
sherehe za kidini, kijamii, nyumbani na vilabuni. Wanakunywa
pombe ili kujiburudisha, lakini pia kuongeza ujasiri, kuondoa
aibu au kusahau matatizo yao kwa kipindi fulani au kwa muda
mfupi.

Vijana wengi, hasa wavulana, hudhani kwamba kunywa
pombe ni ishara ya kujionyesha kuwa wamekuwa watu wazima.
Kimsingi, unywaji pombe kidogo hukubalika kijamii na hauna
madhara, lakini ulevi wa kupindukia ni hatari na huweza
kusababisha vifo na haukubaliki katika jamii zetu kwa sababu
hudhoofisha na kufanya watu kusahau majukumu yao, hupunguza
heshima na afya njema.

Iwapo msichana atajamiiana wakati wa siku salama anaweza kuepuka kupata mimba?

Siku salama ni siku ambazo hakuna yai ambalo lipo tayari kwa kurutubishwa. Iwapo mwanamke atajamii ana katika siku salama tu, yaani wakati ambapo hakuna yai lililo tayari kurutubishwa, anaweza asipate mimba. Hata hivyo, i inatakiwa ajue kwa uhakika lini yai linakuwa tayari kurutubishwa.
Kwa vile wasichana wengi mzunguko wa siku zao hubadilika kila wakati, ni vigumu kujua kama kuna yai ambalo lipo tayari kwa kurutubishwa. Mzunguko na siku za hedhi za msichana unaweza kuathirika na mfadhaiko, huzuni, maradhi, safari au mabadiliko mengine katika maisha ya msichana. Hata kama msichana atakuwa na mzunguko ambao haubadilikibadiliki anaweza kupata mabadiliko ya ghafla katika kipindi fulani.
Kwa hiyo, kuhesabu siku salama siyo njia salama ya kuepuka kupata mimba. Kwa upande wa wasichana hakuna siku salama kutopata mimba, kwa sababu mzunguko wa siku zao za hedhi unabadilika badilika hata zaidi kuliko ule wa wanawake watu wazima!

Je, kwa nini unasema kwamba wasichana vijana hawapo tayari kubeba mimba?

Ni kweli kwamba kupata hedhi ni dalili ya mwili wa msichana kuwa tayari kwa kubeba mimba, lakini kupata hedhi hakuna maana kwamba msichana yupo tayari kwa kuanza kujamii ana au kubeba mimba. Uke wa mwanamke ambaye ni mtu mzima ni madhubuti na unavutika, lakini uke wa msichana ni mwembamba na hauwezi kutanuka sana. Hivyo uke wa msichana unaweza kuchanika vibaya wakati wa kujifungua. Vilevile nyonga ya msichana huwa bado nyembamba sana kuweza kumpitisha mtoto wakati wa kujifungua.
Kwa kuongezea, kupata mtoto siyo suala tu la mwili kuwa tayari kubeba mimba na kujifungua. Inamaanisha pia kuwa tayari kuwa na mwenzio wa kushirikiana naye katika malezi ya mtoto, kuwa na kipato cha kutosha cha kutunza familia na kuwa na nyumba ya kuishi. Kwa vyovyote vile kubeba mimba mapema kunamkosesha msichana kuendelea na masomo na hivyo kumyima nafasi nyingi nzuri za mafanikio.
Hivyo kupata hedhi kila mwezi ni dalili tu ya kuelekea kwenye utu uzima. Haimaanishi kwamba mwili wake umekua vya kutosha kuweza kujifungua mtoto na haimaanishi kwamba amepanga maisha yake kikamilifu kuwa mzazi.

Je, wasichana wana viungo gani vya uzazi na kazi zake ni zipi?

Viungo vya uzazi vya ndani vinaonekana katika michoro inayofuata:

Ukiangalia mchoro huu hapo juu, ambao unaonyesha via vya uzazi vya ndani, utaona uke, mfuko wa uzazi, kokwa za mayai na mirija ya kupitisha mayai. Uke ni mfereji ulio kati ya mfuko wa uzazi na sehemu ya nje ya via vya uzazi. Uke unatumiwa wakati wa kujamii ana, damu ya hedhi na mtoto hupita hapa. Urefu wa uke kwa wastani ni sentimita 7 hadi 8. Mfuko wa uzazi kwa kawaida huwa na ukubwa unaofikia embe ndogo. Yai moja lililorutubishwa hujishikilia kwenye kuta zake nazo huitunza mimba mpaka siku ya kuzaliwa mtoto. Wakati wa ujauzito mfuko wa uzazi hukua taratibu ukistahimili ukuaji wa mtoto. Kila upande wa mfuko wa uzazi i i ipo kokwa ya mayai, ambayo i ina ukubwa kama mbegu ya harage. Kila mwezi yai moja hukomaa kwa upande wa kulia au kwa upande wa kushoto na husafiri kwa kupitia katika mrija wa falopia. Kazi ya mirija ni kupitisha yai lililopevuka kila mwezi kutoka kwenye kokwa za mayai mpaka mfuko wa uzazi. Yai hutungishwa ndani ya mirija hii.

Ukiangalia mchoro huu unaoonyesha via vya uzazi vya nje, utaona midomo ya nje na midomo ya ndani, halafu kisimi, tundu la mkojo, sehemu ya haja kubwa na mlango wa uke. Midomo ya nje na ya ndani ni mii nuko ya ngozi na i iko hapo kuhifadhi sehemu za ndani za uke. Kisimi (au kinembe) ni sehemu ya juu kabisa ndani ya uke na ni sehemu ya uke ambayo humsaidia mwanamke awe na msisimko au asikie utamu wakati wa kujamii ana. Kama tulivyoona hapo juu, mlango wa uke ni tundu ambalo damu hutokea wakati wa hedhi. Pia ni sehemu unapoingia uume wakati wa kujamii ana na mtoto hutokea sehemu hii anapozaliwa. Tundu la mkojo ni juu ya mlango wa uke na ni tundu ambalo mkojo hutokea. Sehemu ya haja kubwa ni sehemu i inapopita haja kubwa (kinyesi).
Kama wewe ni msichana, unaweza kuamua kutumia kioo kujiangalia sehemu zako za via vya uzazi vya nje. Kwa njia hii unaweza kuyaelewa vizuri maumbile yako.

Mabadiliko gani yanatokea kwenye miili ya wavulana Wakati wa makuzi au wakati wa kubalehe?

Wakati wa makuzi au kipindi cha kubalehe, wavulana hupitia mabadiliko mbalimbali ya kimwili, kihisia, na kiakili. Mabadiliko haya yanaletwa na ongezeko la homoni, haswa testosterone. Hapa chini ni mabadiliko muhimu yanayotokea kwenye miili ya wavulana wakati huu wa kubalehe:

  1. Ukuaji wa Viungo vya Uzazi: Testicles (korodani) na uume hukua na kuongezeka kwa ukubwa.
  2. Uzalishaji wa Manii: Wavulana huanza kuzalisha manii, na hivyo kuweza kutungisha mimba.
  3. Ukuaji wa Nywele: Nywele huanza kuota katika sehemu mbalimbali za mwili kama usoni, kwapani, sehemu za siri, na kifuani.
  4. Sauti Ya Kunong’ona: Kuna mabadiliko ya sauti ambapo sauti huanza kubadilika na kuwa nzito.
  5. Ukuaji wa Misuli na Mifupa: Kunakuwa na ongezeko la ukuaji wa misuli na mifupa, na mara nyingi wavulana hukua urefu na mapana.
  6. Mwili Kujaa: Wavulana hupata ongezeko la uzito na uwezo wa mwili kufanya kazi za nguvu unaimarika.
  7. Mabadiliko ya Kihisia na Kiakili: Wavulana hupitia mabadiliko ya kihisia, ikiwemo kuanza kuvutiwa kimapenzi na wenzao, pia huweza kupitia mihemko isiyo thabiti.
  8. Chunusi: Kwenye uso na sehemu nyingine, chunusi zinaweza kutokea kutokana na mabadiliko ya homoni.

Ukuaji huu ni sehemu ya kawaida ya kukua na kila mvulana hupitia mabadiliko kwa kasi na namna yake mwenyewe.

Mabadiliko ya kimwili

  • Utaongezeka urefu na uzito, mikono na mabega yatakuwa na nguvu zaidi, uume na korodani zitaongezeka ukubwa;
  • Ngozi yako i takuwa na mafuta zaidi na unaweza kuota chunusi usoni;
  • Kuota nywele sehemu za siri, makwapani na hatimaye usoni na kwenye kifua
  • Kubadilika sauti na kuwa nzito; na
  • Uume kusimama / kudinda mara kwa mara na utaanza kuota ndoto nyevu

mabadiliko ya kihisia

  • Utaanza kuwa na hisia za kutaka kujamii ana, moyo kwenda mbio, na kuwa na msisimko ukimwona msichana unayekuvutia
  • Mvutio kwa wasichana utaongezeka na utaanza kujali namna unavyotaka kuonekana; na
  • Kuanza kujiamini, kutotaka kulazimishwa kufanya mbaadhi ya vitu na wewe kutaka kuonekana kama mtu mzima anayeweza kufanya maamuzi pekee yake

Mabadiliko haya ni jambo la kawaida kwa mvulana balehe. Kumbuka, kila mvulana anapitia mabadiliko haya katika nyakati tofauti na ukali / nguvu tofauti.

Wakati wa makuzi/ kubalehe/ kuvunja ungo, ni mabadiliko gani yanatokea kwenye miili ya wasichana?

Balehe ni kipindi cha mpito kati ya utoto na utu uzima, ambapo watoto wa kike na wa kiume wanapitia mabadiliko mbalimbali ya kimwili, kiakili, na kihisia. Kwa wasichana, mabadiliko haya yanaweza kujumuisha yafuatayo:

  1. Ukuaji wa Viungo vya Uzazi: Ovari zinaanza kutengeneza mayai na homoni za kike kama estrogen na progesterone, ambazo husababisha mabadiliko mengine.
  2. Hedhi (Menstruation): Wasichana wanaanza kupata hedhi, ambayo ni kumwagika kwa utando wa kizazi kila mwezi, isipokuwa kipindi cha ujauzito.
  3. Ukuaji wa Matiti: Huanza kama vimbe vidogo chini ya chuchu na baadaye kukua zaidi.
  4. Ongezeko la Urefu na Uzito: Kuna spurt ya ukuaji ambapo wasichana hukua haraka kwa urefu na kuongezeka uzito.
  5. Mabadiliko ya Mwili: Mafuta ya mwili huongezeka hasa kwenye hips, makalio, na matiti, kusababisha umbo la mwili kubadilika na kuwa la kike zaidi.
  6. Nywele za Mwili: Uotaji wa nywele katika sehemu za siri, kwapani, na nyakati nyingine kwenye mikono, miguu na uso.
  7. Mabadiliko ya Ngozi: Ngozi inaweza kuwa yenye mafuta zaidi na kusababisha chunusi.
  8. Mabadiliko ya Hisia na Tabia: Hisia zinaweza kubadilika haraka kutokana na mabadiliko ya homoni na mihadhara mingine ya kisaikolojia ya kipindi hiki.

Hizi ni baadhi tu ya mabadiliko yanayotokea wakati wa balehe kwa wasichana. Ni muhimu kuzungumza na watoto kuhusu mabadiliko haya na kuhakikisha wanapata usaidizi na taarifa sahihi kadri wanavyokua.

Kuna mabadiliko mengi ya kimwili ambayo yanatokea kwa msichana wakati anaingia utu uzima. Baadhi ya mabadiliko hayo ni kama yafuatayo:

Mabadiliko ya mwili

  1. Kuongezeka urefu na kupanuka mwili haswa nyonga na matiti kuanza kukua;
  2. Ngozi yako i taanza kuwa na mafuta mengi, unaweza pia kuota chunusi usoni;
  3. Kuota nywele sehemu za siri (mavuzi) na makwapani; na
  4. Kupata damu ya hedhi (kuvunja ungo).

Mabadiliko ya hisia

  1. Kuanza kuwa na muhemko wa kutaka kujamii ana na wakati mwingine mwili wako unaweza kusisimka ukimwona mvulana anayekuvutia;
  2. Mihemuko ya kupenda wanaume huongezeka na wewe kupenda kujipamba i li kuwa na mwonekano wa kupendeza; na
  3. Kuanza kujiamini, kutotaka kulazimishwa kufanya baadhi ya vitu na wewe kutaka kuonekana kama mtu mzima anayeweza kufanya maamuzi pekee yake.

Mabadiliko haya ni jambo la kawaida kwa msichana balehe. Kumbuka, kila msichana anapitia mabadiliko haya katika nyakati tofauti na ukali / nguvu tofauti.

Kutubu na Kusamehewa dhambi

Usiogope wala usisite kutubu na kuomba msamaha kwa Mungu. Uwe na Amani na Matumaini katika Huruma ya Mungu itokayo katika Upendo wake wa Mfano wa baba awapendavyo wanawe. Mungu anasubiri kukupokea kwenye mikono yake Ili akutunze kama mtoto wake kama utatubu na kumrudia yeye. Amua kumwendea leo! Anakungoja ni wewe tuu…

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About