Ni kweli kwamba kupata hedhi ni dalili ya mwili wa msichana kuwa tayari kwa kubeba mimba, lakini kupata hedhi hakuna maana kwamba msichana yupo tayari kwa kuanza kujamii ana au kubeba mimba. Uke wa mwanamke ambaye ni mtu mzima ni madhubuti na unavutika, lakini uke wa msichana ni mwembamba na hauwezi kutanuka sana. Hivyo uke wa msichana unaweza kuchanika vibaya wakati wa kujifungua. Vilevile nyonga ya msichana huwa bado nyembamba sana kuweza kumpitisha mtoto wakati wa kujifungua.
Kwa kuongezea, kupata mtoto siyo suala tu la mwili kuwa tayari kubeba mimba na kujifungua. Inamaanisha pia kuwa tayari kuwa na mwenzio wa kushirikiana naye katika malezi ya mtoto, kuwa na kipato cha kutosha cha kutunza familia na kuwa na nyumba ya kuishi. Kwa vyovyote vile kubeba mimba mapema kunamkosesha msichana kuendelea na masomo na hivyo kumyima nafasi nyingi nzuri za mafanikio.
Hivyo kupata hedhi kila mwezi ni dalili tu ya kuelekea kwenye utu uzima. Haimaanishi kwamba mwili wake umekua vya kutosha kuweza kujifungua mtoto na haimaanishi kwamba amepanga maisha yake kikamilifu kuwa mzazi.
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments