Vituko Vya Wikiendi

Kilichotokea kwa binti na mvulana wake walipotaitishwa na baba yake msichana

Msichana alikuwa amekaa na baba yake kibarazani, mara akamuona MVULANAfriend wake akija, yule mvulana alipokaribia tu, yule msichana akamwambaia:

MSICHANA: Umekuja kuchukua kile kitabu chako, kinachoitwa “DADDY IS AT HOME?” by Ngozi Okafor
MVULANA: Hapana!, Nimekuja kuazima kitabu cha Maombi kama kinaitwa “WHERE SHOULD I WAIT FOR YOU?” by Ngũgĩ wa Thiong’o
MSICHANA: Aaah! Icho sina ila ninacho kimoja kinaitwa “UNDER THE MANGO TREE” by Chimamanda Adichie
MVULANA: Ooh! Vizuri, Basi usisahau kuja nacho kesho kitabu cha Okot p’Bitek kile kinachoitwa “CALL ME IN 5 MINUTES BEFORE” Utakapokuja shule.
MSICHANA: Usijali, tena nina kitabu kipya kinaitwa “I WON’T LET YOU DOWN” by Chinua Achebe
Baba mtu akawatazamaaaa kisha akasema
BABA: Vitabu vyote hivyo, mbona vingi sana, atavisoma vyote kweli
MSICHANA: Ndio Daddy, huyu mvulana hupo smart sana na ana akili atavisoma vyote hivyo!
BABA: Sawa! Usisahau kumpatie na kile ambacho nimekiweka pale juu ya meza, kinaitwa “I AM NOT STUPID, I UNDERSTOOD EVERYTHING YOU’VE BEEN SAYING” by Shakespeare!
Na kuna kingine nimekiweka juu ya kabati la vyombo, kinaitwa “IF YOU GOT PREGNANT PREPARE TO GET MARRIED”

Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?

Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”

Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”

Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”

Cheki huyu mwanamke anavyomkomoa mme wake baada ya kumsaliti

MKE: Mbona unanukia pafyumu ya kike?
MUME: Yaa kuna mwanamke tulikuwa tumeminyana ndani ya daladala
MKE: Na lipstiki kwenye shati?
MUME: Tulikumbatiana na wageni toka Zambia walitembelea ofisi yetu
MKE: Na ile kondom iliyotumika kwenye mfuko wa suruali?
MUME: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi
MKE: Lazima niulize mie huwa nahakikisha nimeacha kila kitu hukohuko ndio narudi nyumbani
MUME: Umesema nini wewe?
MKE: Bwana ee acha maswali ya kijinga mi nalala nina usingizi. 😄😄

Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga

Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?

MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?

Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili

MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday

MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?😂😂😂😂😂

Shopping Cart
3
    3
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About