Vituko Vya Kukuchangamsha

Cheki kilichonipata sasa, ungekua wewe ungefanyaje?

Siku moja katika pitapita zangu nikakutana na mtoto mmoja mkali balaa yaani ni mzuri sanaaaa, moyo ukanituma nimuimbishe mtoto akakubali kwamba nitafute siku tukae tuongee vizuri akasema nimpe namba yangu ya simu.

 

Ebwana si akatoa simu hiyo inauzwa laki sita mimi hapa nina kisimu cha tochi tena nimefunga na rababendi
Je, wewe ungeendelea kumtajia namba zako!!!

Haya ndiyo madhara ya kulala kanisani

Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema
” SIMAMA”
Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama
Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri
” kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA”
Binti akazimia

Cheki nilichomfanyia boss wangu

Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..

Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallah…!!
sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!!
Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu..
Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.

Simu ilivyozua utata

Mama alichukuwa simu akampa mwanawe. Mama..Mpigie babako mwambie chakula tayari. (Mtoto akachukuwa na kupiga) Mtoto…Mama simu ya baba imepokelewa na mwanamke. (Mama kwa hasira) Akirud atanitambua leo. (Baada ya muda kidogo baba akarud,kufika mlangon tu kapokewa na sufuria ya kichwa. Hajakaa vzur mwiko wa pua) Mama..Mwanangu ulipopiga simu ya babako mwanamke wake alisemaje?? Mtoto..Alisema mteja unaempigia hapatikan kwa sasa…..

Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?

Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”

Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”

Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”

Tofauti ya mke na mchepuko!!!

Mke ni kama Tv na Mchepuko ni kama Simu.
Nyumbani unaangalia Tv lakini ukitoka unatoka na simu.

Mara chache unafurahia Tv lakini Muda mrefu unacheza na simu yako.

Tv ni bure kwa maisha yako yote, lakini Simu kama hujalipia hupati huduma.

Tv ni kubwa nzito na wakati wote ni ya zamani. Lakini simu ni nzuri, nyembamba, na ni rahisi kubeba.

Gharama za huduma za tv ni ndogo sana, Lakini gharama za huduma za Simu ni kubwa na pia ni lazima kuzitimiza.

Tv ina remote lakini Simu haina.

Kitu muhimu zaidi simu ina njia mbili za kuwasiliana unaongea na unasikiliza lakini Tv unalazimika kusikiliza hata kama hutaki au unataka.

Unaweza kununua Tv mara moja na ukatumia kwa kipindi kirefu lakini Simu mara zote unabadilisha inategemea na fasheni.

Ya mwisho na ya kuzingatia

Tv haina Virusi lakini Simu inayo.

KUWA MAKINI.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About