Visa Vya Wikiendi

Cheki kilichonipata sasa, ungekua wewe ungefanyaje?

Siku moja katika pitapita zangu nikakutana na mtoto mmoja mkali balaa yaani ni mzuri sanaaaa, moyo ukanituma nimuimbishe mtoto akakubali kwamba nitafute siku tukae tuongee vizuri akasema nimpe namba yangu ya simu.

 

Ebwana si akatoa simu hiyo inauzwa laki sita mimi hapa nina kisimu cha tochi tena nimefunga na rababendi
Je, wewe ungeendelea kumtajia namba zako!!!

Read and Write Comments

Huyu mke kwa kupenda hela! Cheki anachomwambia mume wake

Jamaa karudi toka kazini mpole na hana furaha!
MKE; Vipi leo mbona mpole?
MUME; Ofisi yetu imeungua na watu wote waliokuwemo wamekufa.
MKE; Ilikuaje wewe ukapona?
MUME; Nilikua chooni jirani na ofisi najisaidia.
MKE; Loh maskini, familia zao itakuaje?
MUME; Watalipwa million 100 kila mfiwa.
MKE; KWA HASIRA, Ona sasa na wewe kunya kunya kwako umetukosesha mihela.. Ungeenda kunya akhera.Read and Write Comments

Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!

JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.

Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,

Wakapiga magoti…:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emen…

MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emen…

MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimya…

MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: …….!!

MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.

Chezea mawaifu walokole wewe!Read and Write Comments

Staili nyingine za michepuko ni shida

Mtu na mkewe walikuwa bado wamelala asubuhi, mtu akapiga hodi mke akaenda kufungua mlango, si akakuta mchepuko wake,
MKE: Unataka nini we mpumbavu?

MUME: Nani huyo unamtukana?
MKE: Kuna mtu hapa anakichwa kama nenda urudi badae
MCHEPUKO:Nawewe pua kama poa
MKE:Miguu kama masaa mawili
MCHEPUKO:Masikio kama sichelewi
MKE: Ondoka hapa mjinga we. …… Akafunga mlango
MUME: mwambie ana macho kama sitoki leo ng’oo
SIPENDI UJINGA MM nikiwa na my love pr

Read and Write Comments

Wabongo ni noma! Angalia huyu mbongo anachokifanya

Basi juzi kati hapa sehemu ndogo ya ukuta wa Ikulu ya Magogoni ilianguka!..
Wakapelekwa contractors watatu ili achaguliwe mmoja atakayejenga vzr na kwa bei nafuu!..
Wakwanza alikuwa MUHINDI, wa pili MCHINA na MBONGO!…

MUHINDI: “ntajenga kwa milioni 90!.., 40 za vifaa, 40 za mafundi na milioni 10 faida yangu”

MCHINA: “mi ntajenga kwa milioni 70!.., 30 za vifaa, 30 za mafundi na milioni 10 faida yangu”

MBONGO kuona vile akamvuta chemba msimamizi wa Magogoni!..
MBONGO: “mi ntajenga kwa milioni 270”

MSIMAMIZI WA MAGOGONI: “we una wazimu nn!.. yaani unathubutu kusema hivyo na unaona wenzako wametaja kiwango kidogo?!.”

MBONGO: “milioni 100 zako, 100 zangu alafu hiyo milioni 70 tunaajiri yule mchina”Read and Write Comments

Ulevi noma! Angalia huyu mlevi alichomfanyia huyu jamaa usiku! Ungekua wewe ungefanyaje?

Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.Read and Write Comments

Je, hii ni kweli kwa wale wasichana wasiojibu meseji WhatsApp!!!?

Ukiona hivyo ujue ndio hivi

Mwanaume mwenzangu ukiona unamtext msg msichana WhatsApp kaisoma hajajibu, umetuma ya pili kasoma hajajibu, ukatuma ya tatu hajajibu mmmmmh😨😨 hapo ujue mwenzio kaangalia kwenye profile yako, kakagua picha weee mwishoni akajisemea tu “Huyu.mkaka hapana kwa kweli”🤣🤣🤣🤣🤣🤣

🏃‍♂🏃‍♂🏃‍♂🏃‍♂🏃‍♂🏃‍♂

Read and Write Comments

Shopping Cart