Visa Vya Kukuchekesha

Baada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta

MUME: Fungua mlango!

MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.

MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.

MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!

MUME kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!

MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.

MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.

MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.

Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti

Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenzi…

😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?

Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”

Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”

Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”

Wachaga wana mambo mbele ya hela, angalia hii bili ilivyomchanganya MASSAWE

MASSAWE alienda na marafiki zake bar kunywa, baada ya kumaliza kutumia akaletewa bili kama ifuatavyo:
Manka 35,000
Marieta 20,000
Kekuu 30,000

Kitime 15,000
Kinabo 10,000
TOTAL 110,000/=
MASSAWE akaicheki akasema “Wote nitawalipia lakini huyo “TOTAL” Yesuu simlipii.
Kwansa anamiliki sheli kibao sa mafuta hapa bongo. Shensi taip ! Na amekunywa nyingi kuliko wote alipe mwenyewe…

Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu

Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimu….kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamake😀😀😀😀😀😀😀

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About