Visa Vya Kujienjoy Leo

Mtoto ni wa baba au wa mama? Angalia hoja za baba na mama kila mmoja anadai ni wake

Mtoto ni wa baba au wa mama?

Mume alimpa mkewe talaka wakaenda mahakamani ili hakimu aamue nani akae na mtoto.

MME: Akasimama akauliza hivi: Mheshimiwa hakimu hivi nikichukua ATM card nikaingiza kwenye mashine ikatoa pesa, sasa pesa zitakuwa ni za ATM au zakwangu?

MKE: Akasimama na kusema: Mheshimiwa hakimu hivi ukimwaga mbegu ktk shamba la mtu mti ukiota utakuwa wa kwako au wa mwenye shamba?.

Hebu tumsaidie hakimu aamue kesi hii…

Kizungu nacho ni sheeeedeer

Mtalii: Do you have vegetables here.
Mtafsiri: Mnavyo vijimeza hapa.
Waiter: Vijimeza vidogo hatuna.
Mtafsiri: No sir, they don’t have.
Mtalii: OK, fine, do you have hot dogs.
Mtafsiri: Sawa, je mnao mbwa wa moto.
Waiter: Loh! Bwana we, hatupiki mbwa hapa.
Mtafsiri: They don’t cook here
Mtalii: What type of snacks do you have here.
Mtafsiri: Aina ngapi ya nyoka mnao hapa,
Waiter: We bwana we hapa hatupiki aina yeyote
ya nyoka, mwache akale nyumbani kwao.
Mtafsiri: They don’t cook any type of snacks
here,
maybe you can go back and eat at home.
Mtalii: OK, at least give us a cocktail juice.
Mtafsiri: OK, tupatie hata juisi ya mkia wa jogoo.
Waiter: Hebu tokeni na bangi zenu hapa, tena
sasa hivi kabla sijakasirika.
Mtafsiri: Lets get out of here
😝😝😝😂😂😂
Usicheke pekeyako

Kilichotokea baada ya bibi na babu kukumbukia mahaba ya ujanani

Mzee wa miaka 60 alimwambia mkewe, leo nataka tukumbukie enzi zetu kutongozana, mke akajibu sawa, inabidi unisubiri mwembeni saa 1 usiku nitapita, mzee akafika saa 1 alikaa hadi saa 5 usiku, aliporudi nyumbani akamuuliza mkewe kwa hasira; sasa tumepanga nin halafu haujatokea ?
Mke; leo mama alinikataza nictoke nyumbani usiku nijisomee ! Babu hoii…

Alichojibu dalali baada ya kufumwa na mke wa mtu ndani ya nyumba ya kupanga

Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.

Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hivi… njoo ndani uone mwenyewe.

Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,

‘Nyie mnafanya nini hapa?’

Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’

Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu

Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimu….kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamake😀😀😀😀😀😀😀

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About