Vihoja Vya Kukuchekesha

Angalia huyu msichana alichonifanyia

Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa.
Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba.
Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- “Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3.”
SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGINE

Eti wanadamu walikuja vipi duniani

Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa.
Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto
wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika
akamfuta mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na
manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi
kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa
manyani mwanzo?Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo
wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo wao😂😂🚶🏼🚶🏼🚶🏼

Soma huyu mtoto anachosema sasa, Ndoto za watoto bwana! Kazi ipo!

Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?

ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe Nehemiah ??
Nehemiah : mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……”
Akameza mate kisha akaendelea….
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa Nehemiah .!!

Cheki tabia za kuandika vimaneno vya ajabuajabu kwenye pikipiki na bodaboda ilivyomponza huyu

Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU” 😂😂😂 Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapo *Sipendagi Ujinga mimi* 🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About