Vichekesho Vya Wikiendi
Upendo wa kweli ni nini?
*Upendo wa kweli ni nini?*
*๐Upendo wa kweli ni pale mwanaume anapomfumania mwanamke wake na kisha kumwambia baby vaa nguo twende nyumbani*
*Kifo ni nini?*
*๐Kifo ni pale mwanamke anapokubali kwenda nyumbani na mwanaume yule.*
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Kichekesho cha mtalii na mbongo
Duh! Sikubali bora mbavu zituume wote!
Watalii wana dharau sana bana, Mtalii alikodi boti akazunguka nayo kwenye mto Rufiji kuangalia mandhari, akamuuliza kijana anayeongoza boti, “Do you know Biology, Psychology and Anthropology?” Kijana akajibu “NO,” Mtalii akamwambia “nothing you know under the sun? You are useless, and u’ll die with your illiteracy!” baada ya muda boti ikaanza kuzama, kijana akamwambia mtalii “Do you know kuogelealogy and kusepalogy from mambalogy? Mtalii akajibu huku ametoa macho “No” kijana akamwambia “You will kufalogy and mambalogy wil eat your matakology because of your bad-mdomology..๐๐๐๐๐๐
Kilichotokea kati ya mkaka na mdada walipokutana hotelini
Mkaka aliingia kwenye hoteli moja akaketi meza moja na mdada mrembo maarufu sana;
MKAKA: Samahani dada sijui saa ngapi?
MDADA: Nani kakwambia saa yangu ndio ya kuangalia kila mtu?
MKAKA: Samahani sanaโฆ.jamaa akachukua Galaxy yake akapiga simuโฆ.aise saa ngapi saa hizi? mi ndio nimeingia toka USA nataka kurekibisha saa yangu ifwate muda wa huku. Na wewe uwahi kuchukua iPad nimekuja nazo tatu tu za zawadi. Halafu ntafutie mtoto mzuri nimumwagie midola niliyokuja nayo, ok ciao tuonane badae.
MDADA: Kaka samahani saa hizi ni saaโฆ..
MKAKA: Achana na mimi wewe
Ha ha ha ha haaaaa!!
Sasa Hawa wadada Wapo in Relationship Na Nan!!??
Asilimia 76% Ya Wasichana Kila Ukiwatongoza Wanakwambia Wapo In relationship SAWA ATUKATAIโฆ
Asilimia 98% Ya Mamen Wapo SINGLEโฆ HAPA NDIPO HESABU ZANGU ZINAFELI..
Sasa Hawa wadada Wapo in Relationship Na Nan!?.
Angalia huyu polisi kitu alichonijibu
Nimefika hapa Polisi Station nimefarijika sana na Kustuka baada ya kumkuta Askari hapa Kaunta anasoma Biblia nikajisikia fahari kuona anasoma neno kituo cha Polisi. Nikamuukiza Afande ni Nani alimuua Goliathi? Akasema Muulize Afande Mwita mlango namba 2 ndo anausika na Kesi za Mauaji.๐๐
Sifa 10 za mwanaume ambaye kila binti anayetaka aolewe angependa aolewe naye!!
1. Awe na pesa nyingi
2.Siyo lazima awe mzuri wa sura
3. Ajenge ukweni
4.Awe mpole
5.Asimuonee wivu mke wake
6.Awe mwenye upendo wa dhati
7.Asishike simu ya mke wake.
8.Akimkuta na mwanaume apite tu, akitaka kujua ni nani asubiri nyumbani
9.Awe anamskiliza mke wake kwa kika kitu.
10.Asipende mwanamke mwingine zaid yake
UKIMPATA MWANAUME MWENYE SIFA HIZO KAPIME DNA LAZIMA ATAKUWA NI BABA AKO.
๐๐๐๐๐๐๐๐
Kweli mitandao imeharibu watu, angalia huyu anachokisema sasa
๐๐ kweli nimeamin mitandao inahribu watu
Leo kuna jamaa kamuona Dada akipita barabaran kapendeza jamaa kamwendea Dada akamwambia!
Dada nice photoย ๐๐๐๐
Huyu mwanamke kazidi sasa
Jamaa: Mambo honey, upo ok?
Mrembo: Sipo ok my dear
Jamaa: Una tatizo gani baby?
Mrembo: Nimetoka hospitali kupima, nna mimba.
Jamaa: Weeh usiniletee balaa hiyo mimba imeingiaje wakati huwa tunatumia kinga?
Mremboย Kwani nani kakwambia mimba ni yako, hebu tuliza mshono huo.
๐๐๐๐๐๐๐
MTATUUA
Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo
Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangiโฆ kiberiti kikawaishiaโฆ wakamtuma mwenzao akatafute kingineโฆ bangi lilikuwa limemkoleaโฆ akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweniโฆ
MSHIKAJI:ย oyaaa wanangu eeehโฆ niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe โฆ..
WENZAKE:ย baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.
Tabia za wachepukaji
WACHEPUKAJI WENGI WANATABIA HIZI
1.Hachezi mbali na simu yake kila wakati.
2.Inbox na sending items hufutwa kila
wakati.
3.Ukimuomba simu yake ghafla lazima
akwambie hebu
kwanzaโฆโฆ.
4. Kamwe haiiti always vaibration.
5. Namba nyingi ha save.
6. Kuna simu hapokei hata
iwejeโฆ.anapenda sms zaidi
7.Majina mengi kwenye simu yameseviwa
kwa majina ya
kufikirika.
8.Muda mwingi ni mtu wakujihami.
9.Anapenda password na anabadili mara
kwa mara.
10.Akiazima simu yako, akitumia tu
anafuta dial no
haraka.
11.Always yuko na simuโฆ..hadi bafuni
ikibidi.
12. Anajazba ukimuuliza chochote kuhusu
simuโฆ.anajishtukia.
13. Akiwa anachati anakuangalia mara kwa
mara
kiwiziwizi
14. Hana jeuri ya kukuweka profile picture
na akikuweka
humalizi masaa anakudampu huko
Hapa kuna ukweli asilimia millioni moja
kabisa
Share na washikaji zako๐๐๐๐๐
Recent Comments