Vichekesho Vya Weekend
Jinsi ya Kubana matumizi X-mass
Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.
🎀✨Marry Xmas & Happy new year.✨🎀
Mshahara usiobadilika
PAMOJA NA HALI NGUMU YA UCHUMI NCHINI HUWEZI AMINI MSHAHARA WA DHAMBI HAUJABADILIKA HATA KIDOGO…BADO NI MAUTI VILEVILE
😊😊😊😊
Angalia huyu msichana alichonifanyia
Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa.
Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba.
Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- “Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3.”
SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGINE
Tenda Wema Uende Zako
Nimekuta panya ana struggle kuingia chini ya mlango wa jirani yangu…
Nikagonga mlango Jirani kafungua panya akapenya mi nkaenda zangu…..
Tenda Wema Uende Zako!!! Sipendi Ujinga mimi kwanini panya wa watu apate shida
Kisa cha mzaramo na mchaga
MZARAMO V/S MCHAGA.
Mzaramo alitangaza anatibu magonjwa yooooooote
kwa tsh. 100,000/=
Na kama akishindwa kukutibu anakurudishia laki
yako nakukuongeza laki nyingine.
MCHAGA akaona hii fursa yakujipatia hela aiwezi mpita akaenda kutibiwa.
MZARAMO: “unaumwa nini?”
MCHAGA: “Sisikii ladha ya aina yoyote mdomoni kabisaaaa..”
MZARAMO: “sawa, toa laki kabisa..”
Mchaga akatoa.
MZARAMO akamuagiza msaidizi wake; “Naomba kikopo no.27 mpe anywe huyu..”
MCHAGA akanywa akatema faster; “Puh puu puu, Aisee huu si mkojo huu..?”
MZARAMO: “Umepona karibu tena..”
Mchaga aka-mind sana Kesho yake akarudi tena hakuamini ameliwa pesa yake.
MCHAGA: aisee nina tatizo la kumbukumbu nasahau
sanaaaaa..”
MZARAMO akamwambia “hakuna tabu, toa laki tukupe tiba..’
MCHAGA akatoa pesa akijua leo lazima afanikiwe..’
MZARAMO: “nesi naomba kikopo no.27..”
MCHAGA: “ASA CHALII ANGU HICHO SI CHA JANA CHA MKOJO HICHO AISEE..?”
MZARAMO: “UMEPONA KUMBUKUMBU UNAYO.
😄😄😄😄😁😁😁😁😁😁
Angalia nilichomfanyia huyu dereva sasa
Tulikua kwa basi tunaelekea arusha,ile namcheki dereva kumbe ni best yangu na basi ilikua kwenye spidi hatari, nikaenda kumziba macho nkamuuliza otea mi ni nani, kabla hajanijibu nikasikia kishindo kikubwa sana
NA SASA HIVI NIMEZINDUKA NIMEONA ABIRIA WOTE TUPO WODI NAMBA 3 HAPA KCMC MOSHI. 🤕🤕🤕🤕
SODA ZA WAGONJWA PLIIIZ!!! 🙏🙏🙏🙏🙏
Wanawake hii nayo ni romantic ?💞
Alaf wale Madem wanaowavua maboy wao KOFIA alaf wanakimbia nayo thinking its FUNNY and ROMANTIC.. Hiv nyie mkivuliwa MAWIGI wakakimbia nayo mtajiskiaje?🐸🐸
Hawa Machizi wamezidi sasa
Chizi kakaa ukingoni mwa bahari analia kwa masikitiko na huku kakamata kijiko cha chai. Mwezake akamuuliza mbona unalia mwenzangu. Chizi akajibu nimetia vijiko vitatu vya sukari baharini, kila nikionja bado ina chumvi. Mwenzake akacheka sanaaaaaa akamwambia. Hujakoroga!!!!😂😂😂😂😂😂
Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!
JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.
Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,
Wakapiga magoti…:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emen…
MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emen…
MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimya…
MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: …….!!
MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.
Chezea mawaifu walokole wewe!
Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe James??
JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……”
Akameza mate kisha akaendelea….
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!
Angalia haya mazungumzo ya msichana na mvulana, mapenzi ya ajabu haya
Demu: Hny mambo jamani!
Man: Safi nipe habari wangu wa moyo
Demu:Wafanya kazi gani vile wangu?
Man: Ni fundi wa kufunga ATM
Demu: Wow dont tel me i love you myn mwa mwa mwaaaaah
Man: Mbona wafurahia?
Demu: Nami natamani kuja kufanya kazi za kibenki.
Man: Itakua poa sana nami natamani pia
Demu: Hee si umesema wafanya kazi ya kufunga ATM?
Man: Hukunielewa mie ninafunga mashine na za kunulia condom kwenye bar
Demu: nipishe huko
Alichokisema mtoto baada ya kusikia baba na mama wakiongea mambo yao usiku
MUME: Mke wangu naomba nikubusu
MKE: Sitaki
MUME: Ntakununulia pete ya gold
MKE: Staki
MUME: Ntakununulia gari
MKE: Sitaki….mtoto wao aliyekuwa kalala alisikia haya maneno ya mwisho
MTOTO: Baba basi nibusu mimi uninunulie baiskeli
BABA: Pumbafu lala huko mjinga mkubwa
Cheki huyu mtoto anachomjibu mwalimu wake, kufundisha watoto ni kazi kweli kweli
Mwanafunzi wa darasa la 2 kaulizwa na mwalimu wake
Hivi:je ukipewa maandazi 5 ukiambiwa kula 3 tu yatabaki mangapi?
Akamjibu hivi:nikipewa na chai hakibaki kitu mwalimu.
Huu ndio uhondo na raha ya kupanda daladala wajameni
Wasiopanda dalaladala wanakosa uhondo wa kauli hizi
1. nitakupa
2. Atapewa mbele
3. Hujapewa mbele?
4. Utapewa nyuma
5. Nitakupa nikikaa vizuri
6. Ngoja isimame nikupe
7. subiri asimamishe nikupe
8. hivi nlivyo kaa ntakupaje?
9. Utapewa tulia
10. Nikupe mara ngapi?
Muda ambao unaweza kumzoea dingi
Muda pekee ambao unaweza kumzoea DINGI ni pale unapomfundisha kutumia SMARTPHONE….
Wanakuwaga wapole sana aisee unaweza hata kumuagiza maji ya kunywa akakuletea….
😂😂😂😂😂😂😂
MAMBO KUMI YA KUFURAHISHA NA HUWEZI KUYAFANYA
1. Huwezi kuosha Macho kwa Sabuni;
2. Huwezi kuhesabu Nywele zako;
3. Huwezi kupumua kwa Pua na huku umetoa Ulimi;
4. Unajaribu kufanya namba 3
6. Umeona inawezekana, sanasana unakuwa Kama Jibwa;
7. Unatabasamu kwa kuwa umejiona Mjinga!
8. Umeruka namba 5;
9. Unahakikisha Kama kweli 5 haipo.
10. Unacheka kwa kuwa nimekubamba!
Wachaga kweli kiboko: Mcheki huyu mchaga na mbuzi!!!
Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.
Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. 😄😄
Huyu Jamaa bwana! Cheki anavyojibu sasa
*Mdukuzi:* _halloo massai unasemaj_
*Massai:* _safi rafiki_
*Mdukuzi:* _nikikuuliza swali unaakili ya kujibu?_
*Massai:* _ulisa acha maneno yako._
*Mdukuzi:* _nitajie wanyama kumi wa porini_
*Massai:* _swala watatu na tembo saba_😆😆😆😆😆😆👆🏿
Mkalimani alivyoharibu ibada ya leo
Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji kutoka Bulgaria, Mahubiri yameanza saa 1 asubuhi hali ikawa kama hivi:
MCHUNGAJI: My name is Pastor Livingstone
MKALIMANi: Kwa jina naitwa mchungaji Jiwe linaloishi
MCHUNGAJI: We thank God for All goals we set by our hands
MKALIMANI: Tunamshukuru Mungu kwa Magoli yote tuliyoweka kwa Mkono
Hivi navyoongea kanisa halina viti waumini wote tumekimbia nje naona Mkalimani amebaki na kiatu cha kushoto tu.
Sunday joke
Recent Comments