Vichekesho Vya Kutumia Watu

Hii ndio maana ya Matatizo, usiombee hili likukute

Matatizo ni nini???

`Matatizo ni pale unapokuwa umefika ukweni usiku na haja kubwa ikakubana na hukuwa unajua choo kilipo, ukatoka nje na kujisaidia kwenye majani kumbe ni mboga asubuhi ukasikia mama mkwe anasema kuna mjinga kajisaidia kwenye mboga na kaangusha pochi yake hapohapo haa! Vile unajisachi pochi hamna na kulikuwa na passport,vitambulisho, kadi ya benki, pesa zaidi ya laki 2 na nusu, funguo za nyumba yako, `
🤒🤒🤒🤒🤒🤒🤒🤒🤒

Walahi haya ndo matatizo😅😅😅😅😅😅

Staili nyingine za michepuko ni shida

Mtu na mkewe walikuwa bado wamelala asubuhi, mtu akapiga hodi mke akaenda kufungua mlango, si akakuta mchepuko wake,
MKE: Unataka nini we mpumbavu?

MUME: Nani huyo unamtukana?
MKE: Kuna mtu hapa anakichwa kama nenda urudi badae
MCHEPUKO:Nawewe pua kama poa
MKE:Miguu kama masaa mawili
MCHEPUKO:Masikio kama sichelewi
MKE: Ondoka hapa mjinga we. …… Akafunga mlango
MUME: mwambie ana macho kama sitoki leo ng’oo
SIPENDI UJINGA MM nikiwa na my love pr

Alichofanya maasai baada ya kupanda Tax

Baada ya kupanda daladala aina ya DSM kutoka Mbagala chalambe mpaka Mwenge na kulipa sh 500.Masai akachukua tax wakati wa kurudi.walipofika sasa shughuli ilikuwa hivi.

Masai: we dureva? Naulisa Ng’ombe na mbusi ipi ngali?
Dereva: Ni ng’ombe ghali Masai.
Masai: kwanini Ng’ombe ngali?
Dereva: kwa sababu ni mkubwa zaidi ya mbuzi
Masai: umepata..na mbusi na kuku ipi ngali
Dereva: ni mbuzi kwa sababu nae ni mkubwa kuliko kuku.
Masai: Umepata..
Masai: sasa me nimekwenda kule mwenge kwa ngali kubwa nikalitoa sh. 500 hii yko ndogo unasema nikupe 40,000 wewe acha wizi.. Nitakupa 250 Tu..wee acha lbia morani…!!!

Kuwa na mahusiano na msichana kama huyu ni changamoto, Mabinti bwana!

Binti: Hallow mpenzi, Mambo

Jamaa: Poa baby

Binti:Uko wapi?

Jamaa: Niko town napata lunch

Binti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi

Jamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?

Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.

Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.

Binti: Kwanini dear?

Jamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli!

Utani wa wahindi, cheka kidogo

Mhindi afaulu mtihani wa Kiswahili

(1) Mfa maji ?……………….. Tampa life jacket.
(2) Mwenda pole?………… Tachelewa fika.
(3) Usipoziba ufa ?……….. Mizi taona mpaka dani.
(4) Usilolijua ?……………… Uliza google.
(5) Mbio za utelezini ?……. Chafua guo yako.
(6) Ukipenda boga ?……… Ngoja mezi ya ramzani tapata.
(7) Ukiona vinaelea ?…….. iko nyepesi hiyo.
(8) Maji yakimwagika ?…… Mambie dada tapiga deki.
(9) Chelewa chelewa ?……… Takosa guo ya sikukuu…
(10) Kila ndege ?………….. …Hutua Airport
(11) Bandu bandu ?….. …….Rafiki yake Jecha
(12) Mtaka cha Mvunguni ?… Ondoa tanda
(13) Simba mwenda kimya?….Kama sio gonjwa basi haina njaa.
(14) Aisifuye mvua ?………. Najua iko Mkulima hiyo
(15) Barabara ndefu ?…….. Ongeza mwendo au tachelewa fika.
(16) Mlanawe hafi nawe ila?…. Takimbia
(17) Asie sikia la mkuu ? …….. Tapeleka jela
(18) Hasira za mkizi ? …………..Tatafuna veve
(19) Mchamba wima ?…….. Karibu ya Hurumzi
(20) Akumurikae mchana ?….Kipofu hiyo
(21) Mficha maradhi ?…….. Taenda Loliondo
(22) Mkataa wingi ? ……….Taenda Chadema
(23) Bendera ?……………. Kama sio ya CCM, ya CUF
(24) Baniani mbaya ?……. Peleka Bombay Lakini sio HB kweli, naonea tu
(25) Akili nyingi ?………. Tapasi mtihani yote
(26) Penye kuku wengi ? …….. Chija bili tatu ivi, hapana mtu najua.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About