Vichekesho Vya Kukuparaha

Cheki kilichonipata sasa, ungekua wewe ungefanyaje?

Siku moja katika pitapita zangu nikakutana na mtoto mmoja mkali balaa yaani ni mzuri sanaaaa, moyo ukanituma nimuimbishe mtoto akakubali kwamba nitafute siku tukae tuongee vizuri akasema nimpe namba yangu ya simu.

 

Ebwana si akatoa simu hiyo inauzwa laki sita mimi hapa nina kisimu cha tochi tena nimefunga na rababendi
Je, wewe ungeendelea kumtajia namba zako!!!

Baada ya kumkuta mwanamme mwingine chumbani kwake na mke wake cheki huyu anachokifanya

NAKUA(BABA) karudi kazini mwanae mdogo akamuwahi,
DOGO: Baba usiingie ndani kina jini chumbani kwenu
NAKUA: Hakuna kitu kama hicho
DOGO: Kweli baba kuna jini liko kwenye kabati lenu la nguo….

NAKUA kaingia ndani kamkuta mkewe kalala kitandani kajifunika shuka gubigubi hadi kichwani. Kaenda kwenye kabati kufungua mlango , akamkuta rafiki yake wa miaka mingi yuko uchi ndani ya kabati
NAKUA: Aise unajua we fala sana, we rafiki yangu miaka yote hiyo halafu unamtisha mwanangu eti wewe jini, hebu toka huko nenda kwenu kacheze michezo hiyo na mwanao.

Haya mapenzi jamani! Umewah kumpenda kwa kihivi??

Sijui Kama ushawai fall in love ile haswaa..

yani unampenda mtoto hadi akikupigia ile sauti ilivo tamu unajiskia kutafuna na kuimeza hiyo simu

Akikuita tu “my love”unajiskia tu kuvua nguo mwenywe
..
hicho kiupendo ukiwa nae unajskia unaweza piga wanaume 8 kwa pamoja

Yani ile love mtashinda pamoja kutwa nzima afu usiku unakopa salio umpigie muongee

Yani yale mapenz kiasi ukiona love story za romeo na Juliet unaona hakuna wanachofanya coz mapenz yao hayafikii yenu..

ile true love akikuangalia machoni akuguse mashavu afu akwambie,”I love u”
Unajishikilia kwenye ukuta usizimie..

yani ukimfikiria unaweza kulala chini ya kitanda Ku dilute hiyo feeling coz ni too much..

Umewahi kufeel hivyo??

Kama ushawai experience hivyo?? Basi HIYO SIYO “LOVE” NI “BANGI” PLZ ACHA KUTUMIA!
#ishakua_biashara_kichaa

Kilichotokea baada ya babu mzee kuibiwa nauli kwenye daladala

Mzee mmoja alipanda Gari Stend;
Wakati wa kugombania Siti,
Akaibiwa Nauli.

Akasimama katikati ya Gari-Akasema; “Jamani Naomba Aliyeniibia Pesa yangu Arudishe Haraka,
Tena Fasta kabla Sijafanya Tukio kama Nililofanya 1977″
Abiria kuskia hivyo wakaogopa.
Ikabidi Mwizi Ajitokeze,
Akarudisha Pesa na Kuomba Msamaha! Mtu Mmoja akauliza,
Mzee,
Kwani 1977 Ulifanya nn?
Si nilienda kwa Miguu mpaka Nyumbani!
Uscheke Peke Yako, wa2mie na wengine ili nao wacheke!

Usichokijua kuhusu sungura, panya na jamii yao

JE WAJUA?

Sungura, panya na Jamii zao huwa na mwendo wa kukimbia na kuruka muda wote na umri wao wa kuishi ni miaka 15. Kobe ni mnyama mwenda pole, asiye na papara wala pilika, muda mwingi hujificha na kupumzika ndani ya jumba lake akikwepa maadui. Umri wa kuishi kobe hufikia hadi miaka 300.
FUNZO: Mazoezi ni kiinimacho na uongo mtupu. Jipumzikie mwaya!!!
🏃🏾🏃🏿‍

Hii ndiyo Ladha ya bia zote usiyoijua

Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..

Kwa wanywaji wazuri wa bia,

chupa ya kwanza 🍺 huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

chupa ya pili 🍺🍺 kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi….

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu 🍺🍺🍺 huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…..

Bia ya nne 🍺🍺🍺🍺 huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano 🍺🍺🍺🍺🍺 ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu……na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita 🍺🍺🍺🍺🍺🍺 na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. ……. …Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.

Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika…….

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About