Vichekesho Vya Kuadisia

Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga

Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?

MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?

Angalia nilichokifanya Jana kumkomoa x-wangu

Mwenzenu nilikatiwa umeme jana basi leo si nikaamua kwenda kununua luku ya 10,000. Kufika njiani nikatamani fursana nikaingia kijisupermarket mara sindo nakutana na ex wangu! Mshenzi yule kaniona mimi sijui alikua na mpango wa kununua vocha ya jero eti kabadili kanunua vocha ya buku tano ilimradi nione maisha yake safi tangu tuachane. Mambo ya kijinga spendi kudadeky nimetoa buku kumi nikanunua mipampers nami nijifanye nimeowa nina mtoto halafu huyoo nikashika njia yangu.

Sasa washkaji zangu tafadhalini mwenye mtoto au shida ya pampers naomba anunue kwangu maana leo nalala tena kiza ๐Ÿ™†โ€โ™‚

Cheka na methali

1.Simba mwendapole =Huyo ni Sharobaro
2.Asiyefunzwa na Mamae= Ujue Mama hajapitia Ualimu
3.Zimwi likujualo= Lilikuona Sehemu.
4.Chelewa Chelewa= Ukizikusanya utapata Ufagio.
5.Hakuna Masika= Wakati wa Kiangazi.
6.Mpanda Ngazi= Asiwe Mwoga kuanguka
7.Dua la kuku=
Bismilah rahman rahim
11.Penye wengi= Pana Ajali au Tukio
12.Ukiona vyaelea= Ujue ni vyepesi.
13.Mwenye nguvu= amekula ugal wa dona(โ€ฆ..)

Kingereza sio mchezo, angalia huyu anavyojichanganya

Jamaa fulani alikuwa ame2lia beach mzungu akapita akamuliza “Are u relax ? Jamaa akawa hamuelewi akamjibu No! Mzungu mwengine akapita akamuliza vilevile akajibu No!

Akaona hapa anasumbuliwa akasogea mbele kidogo ya maji akamuona mzungu mmoja alikuwa ame2lia. Akamuliza “are u relax? Mzungu akajibu yes jamaa akamkata makofi mawili na kumwambia kumbe we ndo relax inuka unatafutwa na wenzakoโ€ฆ..Shenz mkubwa mie nasumbuliwa na wenzako kule we umejikausha!!

Baada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta

MUME: Fungua mlango!

MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.

MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.

MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!

MUMEย kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!

MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.

MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.

MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.

Wanaume wote ni waaminifu

Hii ni kwa wanaume ila mwanamke anaweza kusoma na kujifunza kuwa wanaume wote ni waaminifu.

Mwanaume mmoja alienda kukata miti kwa ajili ya mkaa, bahati mbaya panga likadondokea mtoni, akaanza kulia sana. Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia. Jamaa akajibu; “Panga langu limedondokea mtoni na ndilo ninalotegemea kuendeshea maisha yangu”.

Malaika akazama mtoni na kuibika na panga la DHAHABU na kumuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena na kuibuka na panga la SHABA na kuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena mara hii akaibuka na panga la CHUMA na kuuliza ndio hili?

Jamaa: NDIYO.

Malaika akafurahishwa sana na uaminifu wake hivyo akampa mapanga yote matatu. Jamaa akafurahi sana.

Siku nyingine jamaa alikuwa anatembea na mkewe njiani ghafla mke akadondokea mtoni, jamaa akaanza kulia. Malaika akatokea na kumuuliza: Kwanini unalia?

Jamaa: Mke wangu kadondokea mtoni na nampenda sana.

Malaika akazama mtoni akaibuka na WEMA SEPETU na kuuliza; “huyu ndiye mkeo?”

Jamaa: NDIYO.

Malaika akakasirika sana na kumuuliza: kwa nini umenidanganya?

Jamaa: Nimesema ndiyo kwa sababu ningesema hapana ungezama tena na kuibuka na AUNT EZEKIEL na ningesema hapana tena ungezama na kuibuka na MKE wangu alafu ningesema ndiyo ungenipa wote watatu!

Sasa mimi maskini sina uwezo wa kuhudumia wote hao, ndio maana nikasema NDIYO kwa Wema Sepetu.

*FUNDISHO*
Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu na inakuwa sababu maalumu kwa faida ya wote.

WANAUME WOTE NI WAAMINIFU. Hii ndiyo kauli mbiu yetu.
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About