Vichekesho Vya Kimjin Mjini

Kilichotokea baada ya bibi na babu kukumbukia mahaba ya ujanani

Mzee wa miaka 60 alimwambia mkewe, leo nataka tukumbukie enzi zetu kutongozana, mke akajibu sawa, inabidi unisubiri mwembeni saa 1 usiku nitapita, mzee akafika saa 1 alikaa hadi saa 5 usiku, aliporudi nyumbani akamuuliza mkewe kwa hasira; sasa tumepanga nin halafu haujatokea ?
Mke; leo mama alinikataza nictoke nyumbani usiku nijisomee ! Babu hoiiโ€ฆ

Angalia alichokifanya huyu mtu baada ya kuokota wallet ya thamani

Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station “naitwa Juma nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki7, ATM card na karatasi yenye PIN ya ATM card na kijimfuko cha dhahabu” Mtangazaji akasema, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama anakusikiliza? Jamaa akajibu; hapana, ninaomba kumuombea dedication wimbo wa R.Kelly usemao “U SAVED ME” umfikie popote alipo!!

Kichekesho cha mwalimu na wanafunzi

Mtoto: Mwalimu mimi nataka nisome darasa la nne kwani hili la3 halinifai.

Mwalimu: Kwa nini unasema hivyo?

Mtoto: Nina akiliโ€ฆ

Basi mwalimu akamueleza mkuu wa shule na mkuu kaitisha interview kwa dogo. Maswali ni hayaโ€ฆ.

Mwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 20 tukitoa moja tukalidondosha chini yatabaki mangapi?

Dogo: Yatabaki 19.

Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo kwenye friji.

Dogo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha unafunga.

Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani kwenye friji.

Dogo: Unafungua friji unamtoa tembo ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga friji.

Mwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro mmoja. Ni nani na kwa nini?

Dogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka kwenye friji.

Mwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga na mamba na viboko wakali, aliwezaje?

Dogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa simba.

Mwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto, baadae alikufa. Unadhani ni kwanini alikufa?

Dogo: Alidondokewa na lile tofali tulotoa kwenye ndege na kutupa chini.

Mwalimu mkuu: Huyu dogo akasome chuo kikuuโ€ฆ.
๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About