Tenda Wema Uende Zako
Nimekuta panya ana struggle kuingia chini ya mlango wa jirani yanguโฆ
Nikagonga mlango Jirani kafungua panya akapenya mi nkaenda zanguโฆ..
Tenda Wema Uende Zako!!! Sipendi Ujinga mimi kwanini panya wa watu apate shida
Nimekuta panya ana struggle kuingia chini ya mlango wa jirani yanguโฆ
Nikagonga mlango Jirani kafungua panya akapenya mi nkaenda zanguโฆ..
Tenda Wema Uende Zako!!! Sipendi Ujinga mimi kwanini panya wa watu apate shida
Mtoto alimwuuliza baba yake,
Mtoto: Baba unaweza kumwachia hilo gari lako house boy/girl akaliendesha?
Baba: siwezi kumwachia gari langu hili aliendeshe ni ghali sana.
Mtoto: je mnaweza kumwachia chumba chenu house boy/girl kikiwa wazi na mkaenda kazini?
Baba: haiwezekani kamwe kuna vitu vya gharama na pia heshima haitakuwepo.
Mtoto: unaweza ukampa house boy/girl ATM CARD yako na namba ya siri ukakuchulie pesa?
Baba: mtoto unatafuta balaa sasa, unataka siku akiiba hii card akachukue pesa zote tuwe maskini, sithubutu.
Mtoto: aahaaaaaa, kumbe hauwezi kumkabidhi chochote chenye thamani house boy/ girl, sasa kwa nini mnanikabidhi mimi kwa house boy/girl na nyie mnaenda kazini mpaka mnarudi kumbe mimi sina thamani kwenu eeeeh!
Baba na mama baada ya kurudi safari pamoja wakakuta BARUA iko mezani SEBULENI ikisemaโฆ. “Baba na mama, ni matumaini yangu kuwa mtasoma ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka
juu ya meza, naomba msishtuke mana ni mambo ya kawaida kwenye maisha tunayoishi, najua mtaumia kwa vile bado nasoma na ndiyo nipo kidato cha kwanzaโฆ” Napenda kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii barua sipo nyumbani, nimetoroka mana nimegundua
nina uwezo wa kujitegemea kwa sababu mi ni kijana mwenye umri wa miaka 14 na ninajua kipi chema na kipi kibaya.
Tangu mwezi mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano nabinti mmoja aliyeitwa Rachel, mwenye umri wa miaka 27 na kwa sasa
ndo naishi naye kwenye chumba alichopanga. Nilipokuwa nyumbani sikuwa napata hela za kutosha ila sasa nimeanza kushika noti za shilingi 10,000โฆ Msichana niliyenaye ni mzuri sana wa umbo na ninampenda sana, amenifundisha njia za kutafuta hela.
Amenipangia kazi ya kuuza madawa ya kulevya na yeye ikifika
usiku anaenda kuuza mwili wake, basi kila siku tunapata hela ya kutosha, huyu mchumba wangu ni msichana mwenye bidii, kwa siku analala masaa 6 tu maana mwanaume yeyote akija lazima awe naye
chumbani kwa muda wa masaa 3.
Msiwe na hofu, nipo salama kabisa na nimeamua kumwoa Rachel mana ni kila kitu kwangu. Pia amenunua gari la kubebea mbao kwahiyo biashara inaenda vizuri.
Rachel ameenda kupima afya na amekutwa na upungufu wa kinga
mwilini, mara nyingi namridhisha anapotaka kitu flani, iwe kufanya naye mazoezi ya viungo au kufanya naye mapenzi, si mnajua unapokuwa na mgonjwa unakuwa naye karibu.
Ila mi pia sijihisi vizuri mana kila saa nakohoa tu na sina uhakika kama nimeathirika. Tumepanga baada ya miaka miwili tutawatembelea, nadhani mpaka miaka miwili iishe atakuwa
ameshajifungua, na ni furaha yangu mtamwona mjukuu wenu. Wazazi wangU, sina la kuongeza kwaherini Mungu
akipenda tutaonana.
NB: “Baba na mama, mimi nipo chumbani kwangu najisomea,
mnachokisoma ni h/work ya mwalimu wa kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi ya kusisimua, naomba muiangalie kama kuna
makosa!”
Ingekuwa wewe hapo ndi baba au mama ungefanyaje? SHARE na wenzako wasome.
Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenziโฆ
๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Leo kuna mdogo wangu nimemtumia meseji nimemuomba aniazime chaja yake ya simu. Akanijibuย 21002ย Nikawa mkali nikamuambia kuchajia mara moja tu ndio HELA yote hio si bora nikanunue Chaja yangu mpya. Akaniambia nimesema TUMIA TU ๐๐mtatuua na lugha zenu๐
Bibi kapigwa mtama na Kibaka na kuporwa simu,
Kainuka na kuanza kumkimbiza kibaka,
Kibaka kuona Bibi hakati tamaa akatupa simu,
Bibi kaikota na kuendelea kumkimbiza kibaka,
Kibakaย “Bibi kama ni simu yako si tayari umechukua”,
Bibi kajibuย “Bado Mtama”
bibi ujinga hapendagi”๐ก๐ก๐ก๐ก๐ก
Tofauti ya Binti wa Kizungu na Binti wa Kibongo pale ambapo Mwanaume wake atokapo kuoga.
Binti wa Kizungu:ย Baby you look nice and fresh.ย
Binti wa Kibongo:ย Naona safari imeiva, Mwanaume hupumziki kama nesi wa zamuย
๐๐๐๐
Recent Comments