Vichekesho Vya Katikati Ya Wiki
Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu
Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimuβ¦.kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamakeπππππππ
Baada ya kuumizwa kimapenzi haya ndiyo maneno
Mkishaumizwa ndo utasikia, Moyo sukuma damu sio mengine. wakati mnapenda mlizani moyo ulikuwa unasukuma kinyesi!!!!!??????ππππ
Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe James??
JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiweβ¦β¦”
Akameza mate kisha akaendeleaβ¦.
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!
Cheki huyu dingi alivyo mnoko
Unamtumia baba ako meseji ukiwa shule “Baba naomba unitumie 100,000 ya pckt mny” anakuuliza “pckt mny” ndo nini? Unamjibu ni kifupi cha “pocket money” af ankutumia 10,000, unamuuliza hiyo hela ni ya nini? Anakwambia ni kifupi cha 100,000.
Hapo ndo unatamani kuchoma shule ufe.
Wadada acheni hizo
Mfalme Sulemani alikuwa na wake 700 na alichepuka(cheated)na vimada 300 . Mpenzi wako/Mume wako unamfumania na kimada mmoja tu ugomvi na amani imapotea ndani ya nyumba,unasimulia kuanzia padri,mchungaji,ukoo wako mzima,mashoga, stress,vidonda vya tumbo,inapelekea mpaka unaokoka,eti kisa kamuonjesha mmojaβ sasa akionjesha 700 si utakutwa MirembeοΏ½
Wadada acheni HIZO
ππππππ.
Cha kufanya mpenzi wako akikuacha
Kumkomoaβ¦
MPENZI WAKO AKIKUACHA BILA SABABU CHUKUA SIMU MPIGIE MAMA AKE MWAMBIE MWANAO AMEKUFA UWEZIβ¦. KULIA PEKE YAKOπ€
Hii ndiyo sababu ya kumfanya huyu jamaa kujiita fara
MZEE:”sasa huyu mgeni sijui alale wap?”
MKE:”saa hizi ni usiku akalale na Bebi.”
jamaa akaona huyo Bebi pengne mtoto anakojoa kitandani au akalia asije msumbua usiku
JAMAA:”msipate tabu mi ntalala hapa kwenye kochi” akalala
asubh wanakunywa chai akaibuka mrembo,jamaa akapigwa bumbuwazi almanusra ajimwagie chai.
BINTI:”Naitwa BEBI,we unaitwa nani?”
Jamaa akasema mimi naitwa Faraβ¦..!
Angalia huyu mwalimu alichokifanya
Mwalimu aliingia darasani akiwa amechoka kinoma
akawambia wanafunzi.
‘leo tutajifunza kipindi cha
dini ” wanafunzi wakiwa wanajiandaa ili kuendelea
na kipindi mwalimu akajiegesha kwenye kiti klichokua
karibuu yake baada ya dakika kadhaa mwalimu alipitiwa
na usingizi, ghafla alingia mkurugenzi na
kusimama pembeni mwa kile kiti alichokalia mwalimu
ghafla kmya kikatawala darasani kiasi cha kunfanya
mwalimu ashtuke usingizini aliamka huku akipiga
miayo alpotupa jicho pembeni alimuona mkurugenzi
kasimama pemben! akiwa anababaika alifungua
kinywa na kusema ‘ Hivi ndivyo walivyolala wanafunzi
wa YESU walipokua wakimsubli kule mlimani, je
kuna mwenye swal? mkurugeni pale alipokua
akapiga makofi na kumsifia mwalimu kwa kufundisha
kwa vitendo.
Je % Ngapi unampa mwalimu kwa
kusolve kibarua chake.????
Angalia uhuni wa huyu dereva
Dereva alikamatwa kwa kosa la kusababisha ajari ya watu wa5 aliowagonga. Trafik akamuliza kwanin umewagonga awa watu? Jamaa akajibu,”nilikua mwendo wa kasi sana, alafu nimejaza abiria ndani, gari likawa linakuja mbele yangu nilipokanyaga breki zikakatika, sasa ningefanya nin?” Trafki akamwmbia, kwanin ucngeenda upande ambao una watu wachache ili uokoe wengi? Jamaa akajibu, “nilifanya hivo, huku kushoto alikua m1 na kulia walkua wa4, nikamfuata uyu wa kushoto et akakambilia upande wakulia akazani cjamwona, nikamfata huko huko alipoenda, nikampa kitu mbwa yule”
Kilichompata huyu jamaa akiwa anaangalia mpira mechi kali na mke wake
WIFE: Baibie, yule ni nani? Ni Chris Brown??
HUSBAND: Yule ni Theo Walcott
WIFE: ile Yellow Card ni ya nini?
HUSBAND: ile ni ya Onyo, na Red Card inamaanisha mchezaji awache kucheza na atoke inje ya uwanja.
WIFE: Oooooh! Inakaa kama traffic light! Yellow- Ilani na Red – Simama
HUSBAND: Yeah yeah swity! Ndio hivyo.
WIFE: Na je Green Card??
HUSBAND: Aaaah! Hakuna kitu kama hicho.
WIFE: Nataka Arsenal ishinde world cup.
HUSBAND: [kimya]
WIFE: Ni nani yule mzee anakaa kama Mr. Bean??
HUSBAND: Yeees swity, yule ni kocha wa Arsenal, anaitwa Arsene Wenger.
WIFE: Oooooh! inamaanisha yule kocha mwengine ni Chelsea Wenger??
HUSBAND: [Kabadilisha channel]
Recent Comments