Vichekesho Vya Asubuhi Hii

Kilichompata sista duu bishoo wakati akijidai kununua pete

Mwanamke mmoja aliingia duka la vito vya thamani, akaona pete moja ya dhahabu nzuri sana amabayo ilikuwa kwenye shelf ya chini, wakati anainama apate kuitazama vizuri kwa bahati mbaya (au nzuri!), shuzi likamtoka- druuuuuu, soni ikamuingia huku akigeuka haraka kuangalia kama kuna yeyote dukani pale ameliskia shuzi lake, macho yakagongana na mwenye duka ambaye alikuwa karibu huku uso ukiwa umejaa tabasamu zito, mwana mama hakuwa na uhakika kama amesikika au hakusikika, akaona atumie nafasi ile kuyeyusha…Akauliza “Hii pete bei gani?” . Jamaa mwenye duka, huku akiangua kicheko, akajibu “Umeiona tu umejamba, je nikikuambia bei yake si utakunya kabisa?”

Sababu za kumuacha mke kama umemchoka

Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi

_
1. Missed calls 16? Umeua betri la simu yangu. Kwa hiyo hata mimi unaweza kuniua… It’s Over!!!
_
2. Hata hunieshimu. Mi naongea na wewe lakini we upo bize unavuta pumzi? It’s over!
_
3. Nimekupigia umepokea simu hapohapo. Huna subira. It’s over!!
_

4. Nilikwambia huwa napenda chakula cha moto lakini hujanipashia ice cream. Hunijali. It’s over!
_
5. Nimekupa mayai mawili, moja uchemshe jingine ukaange. We umekaanga ambalo ulitakiwa kuchemsha na umechemsha ulilotakiwa kukaanga. Huniheshimu, It’s over!
_
6. Nimekuita DARLING na wewe ukaniita HONEY. Yani kwa maana nyingine unamuita mama yangu NYUKI. Huheshimu wazazi wangu, fungasha kilicho chako. its over.

😄😂😄😂😄😂😄😂😄

Hii ndio ndoto ya harusi ya kila msichana anayotamani

GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enhee…
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng’ombe napeleka kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia Range Rover Sport na mama mkwe ntampa Range Rover Evoque
GIRL: Baby u are awesome…
BOY: Halagu mdogo wako wa kiume ntampa Prado Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo sijaanza kula….
GIRL: Enhee…na sisi??

BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti
Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu, itatupeleka hadi Maldives
GIRL: Baby I love you
BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon Bahamas….halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ua electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani
GIRL: Ooh my sweetheart…halafu tukitoka huko??
BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo

Jamaa anayependa kuwafanyia watu uhuni leo kapatikana na huyu mdada

Mdada alienda super-market kununua
kuku, bahati mbaya kwenye frij
kulikuwa na kuku mmoja tu, muuzaji
akamtoa akamuweka kwenye
mzani, akaonekana ana kilo moja na robo.

Mdada akamuuliza
muuzaji,’Huna mkubwa zaidi?’ Muuzaji
akamchukua yule kuku na
kujifanya kamrudisha kwenye friji, halafu
akamtoa tena kwenye friji na
kumrudisha kwenye mzani, safari hii
akagandamiza mzani kwa gumba,
kuku akaonekana ana kilo mbili. Mdada
akasema ‘Duh afadhali huyu
mkubwa kidogo, naomba unifungie
nawachukua wote wawili

Mamaaaaa muuzaji sijui atatoa wap kuku wa pili😂

😅😅😅😅😅Hapo ndipo utagundua kwa nini MUWA co TUNDA 🚶🏽🚶🏽

Makonda wana mambo, Kila mtu ni ndugu yao

Hakuna m2 mwenye ndugu wengi kama konda wa daladala.

Utasikia,
“HAYA, DADA HAPO MBELE, MJOMBA KULE MWISHO.
MA-MDOGO UNAENDA?,
NGOJA ASHUKE BIBI.
HAYA SHEMEJI UMEIKUTA YA KUWAH.
Babu njoo ukae!
Baba angu hapo tusogee kidogo,

Shangazi maliza ngazi,
Swaiba geukia mbele,
Kaka hapo shika upande wa pili,
Mdogo wangu mpishe Ma Mkwe akae.
Subiri Shemeji yako apande…

Duh… makonda noma…!!

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About