SMS Nzuri: Meseji za Visa Vya Msimu

Huyu mchaga kazidi sasa, angalia anavyomfanya huyu mbuzi

Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.

Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. Chezeya mchaga!

Cheki kilichotokea stesheni ya treni, mambo mengine ukipaniki inakula kwako kama huyu jamaa

Jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondokaโ€ฆ

Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka. Watu wakamuullza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu: “kinachonichekesha, yule aliyepanda alikuwa ananisindikiza.

Ulevi noma! Angalia huyu mlevi alichomfanyia huyu jamaa usiku! Ungekua wewe ungefanyaje?

Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.

Tofauti kati ya mwanamke na mwanamme

UTOFAUTI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME
1. Kwenye mshituko; mwanaume hushituka halafu huangalia nini kimemshitua, mwanamke hushituka halafu huzimia hivyo ataambiwa na mwanaume kilichomshitua๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
2. Kwenye kupenda; mwanaume huanza kutamani alafu hupenda, mwanamke huanza kupenda moja kwa moja bila kumjua vizuri huyo ampendae๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
3.Kwenye kusaidia; mwanaume hutoa msaada alafu uhuzunika, mwanamke huuzunika badae ndo anakumbuka km msaada unahitajika๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
4.Kwenye maamuzi; mwanaume hufikiri ndipo hutenda, mwanamke hutenda halafu hufikiri๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
5.Kwenye kudanganya; Mwanaume hudanganya ili kumlinda mwanamke, mwanamke hudanganya ili kumkomoa mwanaume๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
6.Kwenye ugomvi; wanaume hupigana halafu hueshimiana, wanawake hupiga mikelele alafu kila mmoja hurud kwake, kexho tena๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
7.Kwenye ndoa; mwanaume hutafuta maixha ndipo huoa, mwanamke huolewa ndipo atafute maisha๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
8.Kwenye kukata tamaa; mwanaume hukata tamaa mapema ili jambo lisimsumbue, mwanamke hajui kukata tamaa hadi aumizwe๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
9.Kwenye kula;Mwanaume hushiba alafu huanza madoido, mwanamke huanza na madoido alafu badae hujilaumu hakushiba๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
10.Kwenye siri; Mwanaume hutunza siri hasa za aibu, mwanamke humueleza shoga yake badae hugombana nae baada ya kumrudia mwenyewe kwa siku 2 tu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Hizi ni baadhi tu ya sifa tofauti kati ya mwanaume na mwanamkeโ€ฆ.. VIVA GENTLEMEN๐Ÿ‘Š๐Ÿฝ๐Ÿ‘Š

Analia kilichompata huyu jamaa baada ya kubadili jinsia yake kichawi

Jamaa alimpa ujauzito mwanafunzi akashtakiwa kumbe yule jamaa ana bibi yake mtaalam wamambo yetu ya Jadiโ€ฆ

Jamaa akaongea na bibi yake amuwekee jinsia ya kike ili akashinde Mahakamani na akitoka arudishiwe mambo yake kama kawaida.

Bibi akampachika jamaa jinsia ya kike alipofika mahakamani kuhojiwa akasema mi sijampa ujauzito kwasababu minina jinsia ya kike piaโ€ฆ!
Kwa kuthibitisha akajifunua nguo, basi jamaa akashinda kesi.

Jamaa akawa anarudi Home, lakini wakati anakaribia kufika akaona watu wengi wamejaa home wanalia akauliza kulikoni akaambiwa “Bibi amefariki”!

Vuta picha hapoโ€ฆ!!!

Vichekesho vya kukuondoa mawazo leo

Soma vichekesho hivi;

Mwizi wa atm

Jamaa aliibiwa kadi yake ya benk akaulizwa kama ameripoti polisi akajibu “sijaripoti bado, mwizi mwenyewe hamfikii matumizi kama mke wangu.

Cheka kidogo

Njia rahisi kusahau matatizo yako (japo kwa muda mfupi) vaa viatu vinavyokubana.

Mlizi mbio mbio

Tulikuwa bar moja jana mlinzi kaingia spidi, akamwambia jamaa mmoja aliyekaa kaunta, Mlinzi: Mzee gari lako limeibiwa Mzee: Umemtambua aliyeiba? Mlinzi: Hapana lakini nimeandika namba za gari hizi hapa.

13, 13โ€ฆ

Jamaa alikuwa anapita nje ya wodi ya vichaa akasikia mtu anasema, 13, 13, 13, 13, 13, 13,โ€ฆ.. akaamua kuchungulia kwenye kitundu alichokiona ajue kuna nini, ile kuchungulia tu akamwagiwa mchanga wa machoni, sauti ikabadili ikaanza 14,14,14,14,14โ€ฆโ€ฆ

WATAALAM

Jamaa alikuwa anaumwa sana, mkewe akamwita daktari, alipofika akamkuta jamaa kafumba macho;
Dokta: Huyu mbona amekwisha kufa?
Jamaa: Sijafa bwana
Mke: Hebu nyamaza bwana acha kubishana na wataalamu.

Ya leo mgonjwa

Dokta alipotembelea wodi ya mgonjwa wake aliyepata ajali. Mgonjwa akiwa amening’inizwa mikono juu akauliza “dokta ntaweza kweli kupiga kinanda nkitoka hospitali?”
Dokta: Bila shaka utaweza, wewe ni mpiga kinanda mzuri enh?
Mgonjwa: Hapana sijawahi kabisa bado.

4WD

Mwanaume alimnunulia pete ya almasi mkewe, rafiki akauliza “si ulisema anapenda gari yenye four wheel drive, mbona umenunua pete?” Mume akajibu “unadhani wapi ntapata rav4 feki?”

Ajali ilivyotokea

Trafiki polisi akihoji palipotokea ajali “ahaa! Sasa naanza elewa embu nielezee jinsi ajali ilivyotokea wewe ukiwa kama dereva mhusika.” Dereva akajibu “hata sikumbuki nlifumba macho”

Faini ya kukojoa

Polisi alimdaka jamaa anakojoa pembezoni mwa ukuta.
Polisi: Wewe unajua panakatazwa kukojoa hapa?
Jamaa: Sasa nimebanwa nifanyaje?
Polisi: Faini yake elfu tano.
Jamaa akatoa noti ya elfu 10.
Polisi: Sasa chenji tunaipataje?
Jamaa: Tafuta chenji unipe changu.
Polisi: Basi kojoa tenaโ€ฆ

Mume anaenda kazini

Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang’ang’ania kuwa anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong’oneza mkewe aliyekuwa usingizini; “Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana” Mke: Si ndio nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kaziniโ€ฆ

Hasira za mtoto

Baba na mtoto:
Baba: Mwanangu ukiwa na hasira unafanya nini?
Mtoto: Naenda chooni.
Baba: Chooni? Kufanya nini?
Mtoto: Kusafisha.
Baba: Halafu ndio hasira zinaisha?
Mtoto: Ndio. Nasafisha choo kwa mswaki wako.

Mgonjwa na Dokta

Mgonjwa: Dokta nimekuja nahisi ninaumwa Malaria na kifua.
Dokta: Sasa ushajua unaumwa nini hapa umefuata nini kwangu?
Mgonjwa: Sasa si nimekuja kwa dokta.
Dokta: Wanaojua kuwa wanaumwa kama wewe wanapitiliza maabara.

Pilau la bachela

Bachela mmoja aliyekua akiishi kwa muda mrefu peke yake kwenye nyumba aliyopanga siku moja alitaka kupika pilau kwa mara ya kwanza. Sasa asijue nini kinachobadilisha rangi ya wali kuwa rangi ya brown, yeye akapika kama kawaida (wali) kisha wakati wa kula akavaa miwani yenye rangi ambayo ukiuangalia wali unauona kama pilau wakati anakula.

Mwizi na chizi

Mwizi kaiba TV na kuanza kukimbia nayo, kumbe ile nyumba mlikuwa na chizi, akaanza kumkimbiza yule mwizi. Kila mwizi akiongeza mbio chizi nae huyo, mwishowe mwizi akasalimu amri na kusimama, yule chizi akamsogelea na kumwambia.. Daah umesahau remote hii hapa mwizi kafleti.

Chemsha bongo

Baba akimuuliza chemsha bongo mwanae anayesoma shule ya chekechea “haya niambie kitu gani hakiwezi kuliwa wakati wa breakfast?” Mtoto akajibu “hiyo mbona rahisi baba, si lunch na dinner”

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About