SMS Nzuri: Meseji za Visa Vya Katikati Ya Wiki

Alichokifanya jamaa baada ya kuokota wallet yenye pesa za kumwaga

Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station

“Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hiviโ€ฆ”

Mtangazaji akasema:- Akhasante sana John, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama ana kusikiliza akutafute kwa No. Gani!?

John: Hapana, mi nilikuwa namshukuru tu maana amenitoa kwenye matatizo na ninapenda kumuombea Dedication wimbo wa Snura “MAJANGA” umfikie popote pale alipoโ€ฆ!!!

Huyu mchaga kazidi sasa, angalia anavyomfanya huyu mbuzi

Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.

Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. Chezeya mchaga!

Mzee wa kichaga na hela zake. Angalia anachofanya

Mzee moja alikuwa kila usiku anapita mbele ya bank anasimama,kisha anapiga honi,akitoka askari mlinzi,anaondoka.Hilo jambo likamkera sana askari mlinzi, askari akawa na mvizia yule mzee wa kichaga ,siku alipokuja tena akamkamata, akamuuliza kwa nini unakuja unapiga honi kisha unakimbia? Mzee akasema: Haki ya mungu babaangu , Nina pesa zangu ktk account hapa bank naogopa usilale usingizi ndo maana kila siku usiku napita kukuangalia kama umelala!!
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Jinsi ya Kubana matumizi X-mass

Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.

๐ŸŽ€โœจMarry Xmas & Happy new year.โœจ๐ŸŽ€

Sababu ya mwanaume kunya kitandani alipokuwa kalala na mke wake

Jamaa flani alikuwa amelala na mkewe. Mara akamuona mtu amesimama kitandani.

Jamaa akafoka, “Toka hapa, we ni nani mpaka unakuja kitandani mwangu?”

Yule mtu akajibu, “Mi ni malaika na hapa sio kitandani mwako uko mbinguni!”

Jamaa, “Huh! Inamaana nimekufa,mbona mi bado kijanaโ€ฆ naomba nirudishwe!”

Malaika, “Inawezekana lakini siwezi kukurudisha kama mtu labda urudi kama mbwa ama kuku.”

Jamaa akakumbuka mbwa wanavyopata taabu ya kulinda, akaonelea arudi kama kuku.

Malaika akamgeuza kuku, akamwambia ajifunze kutaga kabla hajapelekwa duniani.

Akachuchumaa na kuanza kujikamua; yai la kwanza likatoka. akajikamua tena, yai la pili likatoka. Akajikamua tena mara ya tatu.

Wakati yai la tatu linatokaโ€ฆ akashtukia amepigwa konde ikifuatwa na sauti ya hasira ya mkewe, “Pumbav*! Balaa gani hiiโ€ฆ. unakuny* kitandani!!”

Wanaume wote ni waaminifu

Hii ni kwa wanaume ila mwanamke anaweza kusoma na kujifunza kuwa wanaume wote ni waaminifu.

Mwanaume mmoja alienda kukata miti kwa ajili ya mkaa, bahati mbaya panga likadondokea mtoni, akaanza kulia sana. Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia. Jamaa akajibu; “Panga langu limedondokea mtoni na ndilo ninalotegemea kuendeshea maisha yangu”.

Malaika akazama mtoni na kuibika na panga la DHAHABU na kumuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena na kuibuka na panga la SHABA na kuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena mara hii akaibuka na panga la CHUMA na kuuliza ndio hili?

Jamaa: NDIYO.

Malaika akafurahishwa sana na uaminifu wake hivyo akampa mapanga yote matatu. Jamaa akafurahi sana.

Siku nyingine jamaa alikuwa anatembea na mkewe njiani ghafla mke akadondokea mtoni, jamaa akaanza kulia. Malaika akatokea na kumuuliza: Kwanini unalia?

Jamaa: Mke wangu kadondokea mtoni na nampenda sana.

Malaika akazama mtoni akaibuka na WEMA SEPETU na kuuliza; “huyu ndiye mkeo?”

Jamaa: NDIYO.

Malaika akakasirika sana na kumuuliza: kwa nini umenidanganya?

Jamaa: Nimesema ndiyo kwa sababu ningesema hapana ungezama tena na kuibuka na AUNT EZEKIEL na ningesema hapana tena ungezama na kuibuka na MKE wangu alafu ningesema ndiyo ungenipa wote watatu!

Sasa mimi maskini sina uwezo wa kuhudumia wote hao, ndio maana nikasema NDIYO kwa Wema Sepetu.

*FUNDISHO*
Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu na inakuwa sababu maalumu kwa faida ya wote.

WANAUME WOTE NI WAAMINIFU. Hii ndiyo kauli mbiu yetu.
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Safari ni safari

FUNDISHO : SAFARI NI SAFARI

Maisha ni ya ajabu sana, wakati mwingine maisha ni mazuri na mwingine ni mabaya, katika maisha yetu tumeshapitia safari nyingi sana na za aina mbalimbali kwa nyakati mbalimbali. Lakin kiukweli kila safari ni safari tuu.

Japokua kila safari ina changamoto zake lakini mwisho wake ni ule ule , kila safari ina uzuri na upekee wake.

Vile vile kila safari ina ubaya wake, kwa mfano kila safari ina gharama yake kulingana na upekee wake.

Usiwe na wasiwasi na mashaka na aina ya safari ulionayo, jipe moyo utaimaliza na kupata ulichokitarajia. Haya ndio maisha na wote tunatakiwa tuyafurahie.

Ingawa kila mtu ana safari yake bado wote tunatakiwa tufurahie pamoja kwa safari tuliyo nayo. Hata Uwe Na safar ya aina gani wewe furahi tuu. Hii ni kwa sababu safari mwisho wake ni mmoja kwa wote burudani ni ile ile

Safari๐Ÿบ ni safari ๐Ÿบhata kama ni ya chupa au ya kopo mwisho wake ๐Ÿ’ค๐Ÿ’ค

๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Ulijua ni nn??

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About