SMS Nzuri: Meseji za Vihoja Vya Kujienjoy Leo

Angalia huyu msichana alichonifanyia

Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa.
Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba.
Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- “Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3.”
SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGINE

Kuna watu makauzu ila huyu kazidi.. Soma hii!

Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisa…. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli.
Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeye……
Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji.
“Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatoka… sorry bae sitaweza kuja kwa leo… sooo sorry!”
Mshkaji jiii! hajajibu kitu…..

Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.

“CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5”

Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji.
“BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI”

#dada wa watu mashavu yakamshuka… hakuamini kilichotokea…. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwa……

Baadhi ya misemo mikali ya leo

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi kufunika sufuria.

Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?

Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”

Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”

Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About