SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Vijana
Jamaa mpenda michepuko kapatikana
…Upo kazini umeacha familia yako nyumbani mara ghafla unapigiwa simu kutazama unakutana na no ngeni na kuamua kuipokea ndipo unakutana na Sauti ya msichana ya kuvutia lakin kabla hajasema shida yake anaamua kukata simu. Unashikwa na hamu ya kujua ni nani. Tamaa ya mchepuko inakujia ghafla na kuamua kuipiga ile no tena kwa mara nyingine inakuwa haipatikani.
Siku hiyo hiyo usiku ukiwa umelala chumba kimoja na mkeo meseji inaingia tena kwenye cm yako kwa ile namba iliyokupigia mchana ikikuomba umpigie kwa mida ule na kusisitiza kuwa ana hamu ya kukufahamu. kila ukimtumia meseji ya kumdanganya upo sehemu mbaya hasikii anakubipu mara nyingi. Uzalendo unakushinda, unamuangalia pembeni mkeo kalala fofofo kajifunika shuka hadi usoni. Unaamua kuondoka kwa kunyata mpaka sebuleni kwenda kuipiga Ile namba kwa lengo la Kumwambia kesho mkutane. Ile unafika sebuleni na kuanza kuipiga ile cm ndipo unakutana na sauti hii:- MUME WANGU ACHA MCHEPUKO, NILIKUWA NAKUPIMA TU RUDI TU CHUMBANI TULALE 😋😋😋😋😋😋😋😋 Hapo ndo utajua kwann bata hata ale kokoto anaharisha 😂😂😂😂😂😂😂😂
Nani Mkali Hapa kati ya DEMU na MSHIKAJI?
“MAENEO FLANI ya KISHUA”
-Mshikaji kamwona demu mkali
anakatiza kitaa akamkubali akaamua
amfuate amtemee cheche
MSHIKAJI- mambo dada?
DEMU- pouwa
MSHIKAJI-
umependezaa!!!
DEMU- asante.
MSHIKAJI- unaweza ukanisaidia
namba
yako ya simu……..
maana duh
nmekukubali
kinyama.
Demu baada ya kuambiwa vile
akazama kwenye pochi lake akatoa
noti ya
sh.10000 akaandika namba yake
kwenye
noti akampa mshikaji.
Mshikaji kapokea ile noti kachana
sehem
iliyoandikwa namba halafu
kamrudishia
Demu noti yake..!!!
NANI ANA DHARAU
NA NANI JEURI..
DEMU AU MSHIKAJI??!
Kizungu nacho ni sheeeedeer
Mtalii: Do you have vegetables here.
Mtafsiri: Mnavyo vijimeza hapa.
Waiter: Vijimeza vidogo hatuna.
Mtafsiri: No sir, they don’t have.
Mtalii: OK, fine, do you have hot dogs.
Mtafsiri: Sawa, je mnao mbwa wa moto.
Waiter: Loh! Bwana we, hatupiki mbwa hapa.
Mtafsiri: They don’t cook here
Mtalii: What type of snacks do you have here.
Mtafsiri: Aina ngapi ya nyoka mnao hapa,
Waiter: We bwana we hapa hatupiki aina yeyote
ya nyoka, mwache akale nyumbani kwao.
Mtafsiri: They don’t cook any type of snacks
here,
maybe you can go back and eat at home.
Mtalii: OK, at least give us a cocktail juice.
Mtafsiri: OK, tupatie hata juisi ya mkia wa jogoo.
Waiter: Hebu tokeni na bangi zenu hapa, tena
sasa hivi kabla sijakasirika.
Mtafsiri: Lets get out of here
😝😝😝😂😂😂
Usicheke pekeyako
Dogo alivyomchomea dada wa kazi kwa mama yake kuhusu baba
Dogo: mama hivi malaika si wanapaa?
Mama: ndiyo wanapaa, kwanini umeniuliza hivyo?
Dogo: nimesikia baba jana anamuita dada (housegir) malaika wangu, kwa hiyo nae atapaa?
Mama: ndiyo atapaa kuelekea kijijini kwao kesho, pumbavu zake.
Kama mpezi wako akikuita MAMITO Unatakiwa umjibu hivi
Akina dada mpenzi wako akikuita MAMITO usikubali
na yeye mwite MAFORONYA kama mbwai na iwe mbwai🤪🤪🤪🤪🤪🤪
Huyu Jamaa kaona bora afe kuliko mke wake ajue Siri zake
Jamaa Mmoja Alimwambia Mke Wake Wasiliana Na Kitengo Cha Dharura Hospitali, Niko Taabani Nahisi Kama Ninakufa.
Mke Akamwambia Nipe Namba Yako Ya Siri Nifungue Simu Yako.
Mume Akasema👉👉 Basi Acha Tu; Kila Nafsi Itaonja Mauti
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Baadhi ya misemo mikali ya leo
1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.
2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.
3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?
4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.
5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.
6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.
7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.
8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.
9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.
10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi kufunika sufuria.
Usichokijua kuhusu shamba lako
Je wajua?.. Shamba lako likipatikana na dhahabu ni mali ya serikali..ila likipatikana na bangi ni mali yako
😂😂😂😂
Wazo la jioni hii
📢WAZO LA JIONI HII 📢
KAMA MWAKA JANA ULIPIGA HATUA NA HUJAFIKIA MALENGO MWAKA HUU PIGA MSAMBA😝
Vituko vinavyoandikwa kwenye daladala
Huwa naenjoy sana kusoma yaliyoandikwa nyuma ya daladala hasa ninapokuwa kwenye foleni. Misemo maarufu
ya kwenye daladala.
1.Yatima hadeki
2.Utamu wa chips mimba
3.Ukitaka kujua ugumu wa kudai kopesha ukweni
4. Usiyempenda kaja
5. Kobe hapimwi joto
6. Acha kazi uone kaz kupata kaz
7. Ukichezea koki utalowa
8. Heshima pesa kipara kovu tu!
9. Mtumbwi hauna saitmira.
9. Silaha pesa bastola mzigo
10. Hata uoge mjini huendi
11. Chezea mshahara usichezee kazi.
12. Ukiona manyoya ujue kishaliwa
13. Ikisimama Panda
14. Pombe pombe tuu kunywea bar mbwebwe
15. Njia ya chooni haioti nyasi
16. Likizo ya maskini ugonjwa
17. When i grow up i want to be a scania
18. Hata bibi alikuwa binti
19. Kisigino hakikai mbele
20. Kama mapenz pesa kaolewe na benki
21. Hata barabara ina matuta lakin huwez panda viazi
22. Mavi hayana miba lakin ukikanyaga lazma uchechemee
23. Paka haishi kwa msela
24. Ukipendwa ujue kuna boya kaachwa
25. NIPO NIPO KWANZA
26. Mchana nzi ucku mbu
27. Ucmshangae funza kukata viuno ndio mwendo wake
28. Kama umelipenda(gari) bonyeza nyota liwe lako
29. Supermarket hawauzi mkaa
30. We nisubiri mi nakungoja.
31. Zetu dagaa kuku tamaa
32. Hata uwe na heshima vipi huwezi kumpokea askari bunduki
H
😆😆😆😆😜😜😜😝😝😝
Share na wenzako kuongeza siku za kuishi
Angalia nilivyookoa maisha ya mtu leo
Nmeokoa maisha ya mtu asubuhi ya leo huwezi amini.Nmekutana na ombaomba nikamuuliza atajisikiaje nikimpa sh.30,000/-
Akasema ATAKUFA kwa furaha.Nikaondoka bila kumpa ili ASIFE.😃😃😃😃
KICHEKESHO: Ukiona masikini Kachinja kuku
Ukiona masikin kachinja kuku basi kat ya kuku au yeye kuna mmoja atakua mgonjwa 😆😆😆😆
Tabia za Kimama kwa wanaume
1, mwanaume kuoga haraka haraka ili uwahi kuangalia igizo, huo ni UMAMA..😂
2, mwanaume kupiga picha umeng’ata Lips na Unapiga na Camera Beauty Plus huo ni UMAMA..😂
3, Mwanaume kuangalia tamthilia na Jamai Raja na Maigizo kwenye chanel ya sinema zetu wakati mechi za kombe la dunia zinaendelea, pia nawe ni MMAMAA…😂😂
4, Mwanaume kuandika ‘Jomon’ badala ya Jamani, kuandika ‘Pw’ badala ya Poa, kuandika ‘Thatha’ badala ya Sasa, kumwandikia mwanaume mwenzio ‘Mambo my’ Huu ni UDADA, tena UDADA wa CHUO..😂
.
5, Mwanaume kunywa soda au Juice na kubakisha, kununua chakula halafu unakibakisha, kubagua bagua chakula na kujamba hovyo hovyo baada ya kushiba, huo nao ni UMAMAA..😂
.
6, Mwanaume kumuuliza mwanaume mwenzio anapata faida gani kuangalia Mpira, pia nawe ni MMAMA…
.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Kilichompata sista duu bishoo wakati akijidai kununua pete
Mwanamke mmoja aliingia duka la vito vya thamani, akaona pete moja ya dhahabu nzuri sana amabayo ilikuwa kwenye shelf ya chini, wakati anainama apate kuitazama vizuri kwa bahati mbaya (au nzuri!), shuzi likamtoka- druuuuuu, soni ikamuingia huku akigeuka haraka kuangalia kama kuna yeyote dukani pale ameliskia shuzi lake, macho yakagongana na mwenye duka ambaye alikuwa karibu huku uso ukiwa umejaa tabasamu zito, mwana mama hakuwa na uhakika kama amesikika au hakusikika, akaona atumie nafasi ile kuyeyusha…Akauliza “Hii pete bei gani?” . Jamaa mwenye duka, huku akiangua kicheko, akajibu “Umeiona tu umejamba, je nikikuambia bei yake si utakunya kabisa?”
Duh! Wanaume jamani…
Lakini sisi wanaume hatuko fair … Yani demu anang’ng’ana kujipodoa uso na sisi tunaangalia matako. 😆😆😆mungu anatuona jaman😆😆😆😆😆😆Makeup ya matako iletwe
Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili
MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday
MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?😂😂😂😂😂
Cheka kidogo na wewe hapa
*Kama mtaani kwenu mambo yamekuwa tait , usikimbilie mtaani kwetu kwani huku yamekuwa dera kabisa*😂😂😂😂😂
Jana nilipeleka viatu kwa fundi sasa hivi nimekutana nae amevivaa namuuliza ananiambia eti ni ROAD TEST” 😂😂😁
Angalia huyu jamaa alivyomuweza huyu binti wa chuo
😁😁😁😁 .. TABU KUDATE NA MADEMU WA CHUO
Demu ; Baby Safari Hii Nataka Pale Hostel Niwafunike Mashoga Zangu Wote.
Jamaa ; Poa Sweetie Ondoa Shaka Nitakununulia #Turubai Utawafunika Wote…!!!
Demu: Mxiuuuuuuuu Lione Sura Kama Goti La mbuzi Na Namba yangu futa Nakublock Mpaka Sanduku la posta…!!!
😂😂😂😂nmecheka adi nmelazwa
Kuwa na mahusiano na msichana kama huyu ni changamoto, Mabinti bwana!
Binti: Hallow mpenzi, Mambo
Jamaa: Poa baby
Binti:Uko wapi?
Jamaa: Niko town napata lunch
Binti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi
Jamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?
Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.
Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.
Binti: Kwanini dear?
Jamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli!
Recent Comments