SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Krismass
Kisa cha mzaramo na mchaga
MZARAMO V/S MCHAGA.
Mzaramo alitangaza anatibu magonjwa yooooooote
kwa tsh. 100,000/=
Na kama akishindwa kukutibu anakurudishia laki
yako nakukuongeza laki nyingine.
MCHAGA akaona hii fursa yakujipatia hela aiwezi mpita akaenda kutibiwa.
MZARAMO: “unaumwa nini?”
MCHAGA: “Sisikii ladha ya aina yoyote mdomoni kabisaaaa..”
MZARAMO: “sawa, toa laki kabisa..”
Mchaga akatoa.
MZARAMO akamuagiza msaidizi wake; “Naomba kikopo no.27 mpe anywe huyu..”
MCHAGA akanywa akatema faster; “Puh puu puu, Aisee huu si mkojo huu..?”
MZARAMO: “Umepona karibu tena..”
Mchaga aka-mind sana Kesho yake akarudi tena hakuamini ameliwa pesa yake.
MCHAGA: aisee nina tatizo la kumbukumbu nasahau
sanaaaaa..”
MZARAMO akamwambia “hakuna tabu, toa laki tukupe tiba..’
MCHAGA akatoa pesa akijua leo lazima afanikiwe..’
MZARAMO: “nesi naomba kikopo no.27..”
MCHAGA: “ASA CHALII ANGU HICHO SI CHA JANA CHA MKOJO HICHO AISEE..?”
MZARAMO: “UMEPONA KUMBUKUMBU UNAYO.
ππππππππππ
Mimi ndio nimeelewa hivi!
Leo nimepishana na Vitz imeandikwa, “Never trust women”
Nikajua huyu mtu lazima alikuaga na Range Rover
ππππππ
Huu ndio uchawi unaweza kufanyika siku mpenzi wako akikutambulisha kwao
πππππ
*UCHAWI* ni nini?
`Uchawi ni pale mpenzi wako anapokupeleka kwao kufika tyu ghafla unakutana na dada yake getini ambaye alikuwa ni mpenzi wako wa zamani, ile kuingia ndani unamuona kaka yake ambaye mlipigana baada ya kukufumania na mke wake, hujakaa vizuri unamuona mama yake ambaye ndiye jimama shangingi lako anayekuweka mjini akupaye jeuri ya kutamba ambapo hata gari unalolitumia alikupa yeye na hataki upajue anapoishi, wakati unataka kuondoka unakutana uso kwa uso na baba yake ambaye alikuwaga wakili wako kwenye kesi ya ubakaji`
π€£πππππ€£
Angalia huyu boyfriend alivyomuweza huyu msichana wake
Siku moja msichana alikuwa anapita maeneo ya A.T.M gafla
akamuona boyfriend wake anatoa pesa kwenye A.T.M binti
akaamua kujificha na kumtumia boyfriend wake sms ya
kimahaba
“Honey kama upo nyumbani umelala naomba unitumie ndoto
zako,
Kama unakula nitumie chakula, Kama unacheka nitumie kicheko
chako,
Kama unalia nitumie machozi yako,Kama unatoa pesa kwenye
A.T.M nitumie pesa.” Boyfriend akajibu “NIKO CHOONI LABDA
NIKUTUMIE KINYESI MPENZI!!
Biashara ambayo imefeli
*TEACHER*: _nielezee biashara ambayo imefeli kutokana na uzembe
*STUDENT*: Changudoa akipata mimbaβ¦
*TEACHER*: _get Out!!!!!!!!!!!!!!_
ππ
Hii ndiyo Ladha ya bia zote usiyoijua
Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..
Kwa wanywaji wazuri wa bia,
chupa ya kwanza πΊ huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza kooβ¦ Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.
chupa ya pili πΊπΊ kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihiβ¦.
Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.
Bia ya tatu πΊπΊπΊ huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sanaβ¦. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokezaβ¦..
Bia ya nne πΊπΊπΊπΊ huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikiaβ¦.. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.
Bia ya tano πΊπΊπΊπΊπΊ ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipuβ¦β¦na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; βMi sipendwi mpaka leo sijaolewaβ au β Mume wangu sijui yukoje hanijaliβ
Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.
Kuanzia bia ya sita πΊπΊπΊπΊπΊπΊ na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. β¦β¦. β¦Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.
Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjikaβ¦β¦.
Cheki jamaa alivyoumbuka baada ya kuhudhuria semina isiyomuhusu
Jamaa kavamia semina ya wasomi iliyokua inafanyika maeneo ya ubungo plaza bas wakaanza kujitambulisha
1. Naitwa Anna niko SUA mwaka3 nasoma agriculture
2. Naitwa Stella niko UDSM mwaka2 nasoma public relation
3. Naitwa Emmanuel niko UDOM mwaka3 nasoma computer science
bas jamaa nae akainuka kwa kusuasua huku akijishtukia akasema”Naitwa Elisha niko Tanesco mwaka wa 7 nasoma mita”
Kilichotokea baada ya polisi wa kibongo kukutana na mwizi mzungu
POLISI KAKAMATA MZUNGU ‘yestaday I saw u at ze maize shop..(jana nilikuona dukani kwa muhindi) when u saw me u started 2 six six.(uliponiona ulianza ku-sitasita) u ran n decided 2 plant a car.(ulikimbia na ukaamua kupanda gari) zen u pot-cry me through ze window.(kisha ukanichungulia dirishani) now sleep down n snake well b4 I cut u a millet.(sasa lala chini kisha nyooka vizuri kabla sijakukata mtama) Chezea lugha wewe..!!!
Alichokifanya jamaa baada ya kuokota wallet yenye pesa za kumwaga
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station
“Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hivi⦔
Mtangazaji akasema:- Akhasante sana John, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama ana kusikiliza akutafute kwa No. Gani!?
John: Hapana, mi nilikuwa namshukuru tu maana amenitoa kwenye matatizo na ninapenda kumuombea Dedication wimbo wa Snura “MAJANGA” umfikie popote pale alipoβ¦!!!
Angalia huyu house girl wa mzungu alichokifanya na anachokisema
House girl mmoja alipewa kazi na mzungu mara akavunja sahani.
Mzungu aliporejea,kazin akamuuliza ‘what happened to my plate?
House girl akajbu: ‘The dog wow wow friji paaa, mchuzi mwaaaa the vyombo pangalapangala the sahan ngelengenjeeβ¦β¦the pasuka paaaaaaaa
ππππhadi saiz mzungu bado anasoma dictionary hajui lugha gani imetumika
Madenge hakosi visa. Soma hii
MADENGE
HAKOSI
VISA
baada ya kumaliza form four baba akamwambia achague zawadi yoyote aipendayo
MADENGE: naomba pesa nikamuoe bibi maana siku nyingi amekuwa akiniita mchumba wake.
BABA: Shenzi, yule ni mama yangu mzazi huwezi kumuoa.
MADENGE: Mbona wewe umemuoa mama yangu mzazi sijasema kitu ww inakuuma? lazima nilipize kisasi ikikuuma muache mama yangu kila mtu akae na mamayake. πππ
Huyu mwanafunzi kweli kiboko
Ticha: Wa kwanza kujibu swali langu ataenda Home mapema..
John kusikia hivyo….Karusha begi la daftari nje…..`Β
`Ticha akauliza: Nani karusha begi nje!?!`*
`John: Mimi….. Kwa herii Mwalimu……` ππ,ππ
Sitasahau mwaka huu
Sitasahau mwaka ule ambapo nilipeleka barua ya maombi yangu ya kazi kwenye kampuni moja maarufu. Wakati nasubiri majibu siku moja nikaenda kwa mama ntilie kununua maandazi akanifungia vizuri, kufika nyumbani hamu yote ya maandazi iliniishia pale nilipogundua karatasi iliyofungiwa maandazi ni barua yangu ya kuombea kaziππ
Maswali ya kijinga yakijibiwa vizuri
Haya ndiyo majibu mazuriππππππππππ
Q: Umenyoa nywele?
A: *Hapana, nimebadilisha kichwa.*
Q: Hiyo simu umenunua?
A: *Hapana nimeitengeneza mwenyewe.*
Q: Utakula mboga na nini?
A: *Mdomo*
(Simu inaita usiku,then aliyepiga anauliza) Q: Nimekuamsha?
A: *Hapana nilikuwa naota jua hapa nje.*
Q: Gazeti la leo linasemaje?
A: *Sijaongea nalo.*
Q: Gari limejaa, nitakaa wapi?
A: *Usijali dereva anashuka kituo kinachofata utapata kiti.*
Q: Hiyo ni ajali?
A: *Hapana ni driver ameamua kupark gari upside down* .
Q: Umepause movie?
A: *Hapana wamechoka kuact wanarest.*
ππππππ
πββπββπββπββπββπββ
Hii ya mamba na kiboko kali, Wewe unaonaje?
Eti kati yaΒ MAMBAΒ naΒ KIBOKOΒ nani kiboko???ππππ
Mi naonaΒ MAMBAΒ ndoΒ kiboko!π³
Ujinga mbele kwa mbeleπππππππ»ππ»ππ»ππ»ππ»
Cheki hawa wachungaji
CHEKA KIDOGO
Wachungaji watatu walikutana kwa siri na kuelezana matatizo yao ili waweze kuombeana.
MCHUNGAJI WA KWANZA: mimi tatizo langu ni wizi, kila nikimaliza ibada lazima niibe pesa za sadaka.
WA PILI: Mimi tatizo langu ni wanawake yani nimeshalala na wana kwaya wote pamoja na mke wa ASKOF.
WA TATU akaanza kulia badala ya kuongea.WENZAKE:
We vp unatatizo gani mbona unalia???
AKAJIBU: jamani mimi tatizo langu ni “umbea” haya yote tuliyoongea lazima nikaseme!
πππππππ»ππ
Misemo 17 ya kuchekesha
1) gari la kuvutwa halina overtake
2) kisigino hakikakai mbele
3) wimbo wa taifa haupgwi disko
4) feni haiwashwi beach
5) mshkaki hauchomwi kwa jiko la ges
6) mganga haagiz tembele
7) hata bibi alikuwa bint
8) mke wa mtu sumu,mume wamtu maziwa
9) kipara bila pesa ni kovu
10) mbwa hanenepi migiuu
11) picha ya rais haina bodyguard
12) mjini shule kijiji tuition
13) saa ya ukutani haivaliwi mkonon
14) heshima pesa shkamoo makelele
15) ulinz pesa bastora mzgo
16) kuku ni kuku jogoo mbwembwe
17) kusoma kuelewa kukesha mbwembwe
Kichekesho cha mtalii na mbongo
Duh! Sikubali bora mbavu zituume wote!
Watalii wana dharau sana bana, Mtalii alikodi boti akazunguka nayo kwenye mto Rufiji kuangalia mandhari, akamuuliza kijana anayeongoza boti, “Do you know Biology, Psychology and Anthropology?” Kijana akajibu “NO,” Mtalii akamwambia “nothing you know under the sun? You are useless, and u’ll die with your illiteracy!” baada ya muda boti ikaanza kuzama, kijana akamwambia mtalii “Do you know kuogelealogy and kusepalogy from mambalogy? Mtalii akajibu huku ametoa macho “No” kijana akamwambia “You will kufalogy and mambalogy wil eat your matakology because of your bad-mdomology..ππππππ
Recent Comments