SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

🤣😃😂

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Jinsi ya kutengeneza mishumaa

MALIGHAFI ZINAZO HITAJIKA WAKATI WA UTENGENEZAJI WA MISHUMAA.

1. Paraffin Wax
2. Utambi
3. Mould ( Umbo )
4. Stearine au mixture
5. Rangi
6. Jiko la mafuta ya taa au mkaa.
7. Sufuria.
8. Boric acid.

VIDOKEZO MUHIMU :

1. Paraffin Wax :

Hii inatokana na nta na sega ya nyuki iliyo changanywa na mafuta ya taa. Ina rangi nyeupe na katika utengenezaji wa mishumaa ina ubora kuliko bee wax.

* Bee Wax : Inatokana na masega ya nyuki yaliyo changanywa na mafuta ya petroli na diesel na rangi yake ni ya njano.

2. STEARINE

Hii dawa maalumu inayo fanya mishumaa iungane ama ishikamane.

3. BORIC ACID :

Hii ni maalumu kwa ajili ya kuufanya utambi usiishe mapema na uwake bila kutoa moshi.

4. RANGI :

Rangi nzuri zinazo tumika katika utengenezaji mishumaa ni rangi za chakula na nyingi huwa ni za maji.

JINSI YA KUTENGENEZA

Andaa mould ( umbo lako ) utakalo litumia baada ya kuyeyusha ( paraffin wax ) na kuchanganya na michanganyo yote.

Kwa Mfano : ( Kipimo cha stearine )

1. Wax kilo moja – Stearine vijiko vinne vya chakula.
2. Wax nusu kilo – Stearine vijiko vinne vya chakula
3. Wax robo kilo – Stearine kijiko cha chakula.

Baada ya mould ( umbo ) kuwa tayari , chemsha wax mpaka iyeyuke na itoe kwenye vyombo ambavyo umetayarisha na usubiri ikauke ili uanze kutoa mishumaa.

Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!

JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.

Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,

Wakapiga magoti…:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emen…

MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emen…

MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimya…

MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: …….!!

MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.

Chezea mawaifu walokole wewe!

Kingereza sio mchezo, angalia huyu anavyojichanganya

Jamaa fulani alikuwa ame2lia beach mzungu akapita akamuliza “Are u relax ? Jamaa akawa hamuelewi akamjibu No! Mzungu mwengine akapita akamuliza vilevile akajibu No!

Akaona hapa anasumbuliwa akasogea mbele kidogo ya maji akamuona mzungu mmoja alikuwa ame2lia. Akamuliza “are u relax? Mzungu akajibu yes jamaa akamkata makofi mawili na kumwambia kumbe we ndo relax inuka unatafutwa na wenzako…..Shenz mkubwa mie nasumbuliwa na wenzako kule we umejikausha!!

Usiyoyajua kuhusu pesa haya hapa

Habari za Leo Rafiki yangu wa Muhimu sana. Ni furaha yangu kujua unaendelea vyema sana na majukumu yako.

Ni wakati mwingine tena tunaenda kujifunza pamoja juu ya mambo mbalimbali ili tuweze kufikia mafanikio kila siku. Leo tunakwenda kujifunza kuhusu pesa na utajua mambo mengi sana juu ya pesa.

Ni siri gani ipo ndani ya fedha na wengi hawaijui?

Kwanini watu wengi wanakua matajiri halafu wanapoteza utajiri wao wote na kuwa maskini tena?

Ulishawahi kuona watu maarufu wamekua na pesa nyingi lakini baada ya muda wanapotea na pesa zao zinapotea na kurudi kuwa watu wa kawaida kabisa?

Hujawahi kuona watu wakiuza mashamba ya urithi kwa mamilioni ya pesa na wakabadilisha aina ya maisha wanayoishi lakini baada ya muda pesa zinapotea na wanarudia hali yao ya zamani?

Hujakutana na vijana waliochimba madini wakajikuta wamepata mawe wakawa milionea lakini ghafla baada ya muda Fulani wanarudi kule kule walipokua?

Wengi wakiona hayo utawasikia wanasema pesa za mashamba hazika! Pesa za madini zina mashetani! Ni siri gani ipo kwenye hii pesa?

Inawezekana umeshajiuliza sana maswali haya na hata kuogopa kuwa nayo. Ukaamua kuwa mtu wa kawaida tu kwasababu ya hofu hizi zinazokujia unapofikiri kuwa tajiri kisha uje upoteze pesa zako zote!

Watu wengi wamekuwa na fikra kwamba pesa ni mbaya, zinaharibu watu, zinawafanya watu kuwa wachoyo, zinawafanya watu kuwa na tamaa pamoja na mengine mengi unayoyafahamu.

Ukweli ni kwamba pesa haina tatizo lolote pesa haina shetani wala pepo lolote linaloifanya imharibu mtu anapokuwa nayo nyingi. Pesa sio kiumbe hai. Pesa tunaitumia kununua bidhaa mbalimbali au kulipia huduma tunazozihitaji katika maisha yetu ya kila siku.

Ukweli kuhusu pesa ni huu hapa. Kwanza pesa haimbadilishi mtu bali inamfanya awe Zaidi ya vile alivyokuwa mwanzo yaani kama mtu alikuwa ni mchoyo akipata pesa atakuwa mchoyo maradufu, kama alikua mlevi akipata pesa anazidisha kuwa mlevi Zaidi.

Na wengine wakiwa hawana pesa kuna tabia nyingi wanakuwa nazo ndani zimejificha hawazionyeshi wakishapata pesa zile tabia zinafunguka na kuwa wazi.

Kama mtu alikuwa Malaya akipata pesa ndio utaona anaanza kubadilisha wanawake. Pesa zinabaki kuwa pesa na tabia za mtu zinabakia kuwa tabia za mtu.

Kama mtu alikua mtoaji akipata pesa atakuwa mtoaji Zaidi.
Kama alikua mcha Mungu akipata pesa atakwenda kuabudu Zaidi.
Hivyo pesa sio tatizo watu ndio wenye matatizo ndani yetu.

“Having more money won’t change you as a person. It will, however, magnify
the person you already are.” – Bob Proctor

Huwa napenda kuutumia mfano wa chombo. Watu wengi wanaopata pesa nyingi ghafla na kuzipoteza zote ni kama maji yaliyojaa kwenye ndoo utake kuyaweka yote kwenye kikombe cha chai.

Ukweli ni kwamba kikombe kitajaa lakini yale yaliyobaki yatamwagika yote chini hivyo hivyo na pesa zinazopatikana ghafla ni sawa na kuziweka kwenye kikombe ambacho ni uwezo wa akili yako.

Kama Akili yako bado haijaweza kupangilia milioni ishirini hivyo hata ukipewa leo zote zitapotea na zitabaki kile kiwango ambacho akili yako inaweza kutawala na kuendesha. Hivyo njia sahihi ya wewe kuweza kumiliki mamilioni ya shilingi na kubakia nayo ni kuanza kubadili ufahamu wako. Kuza ufahamu wako kidogo kidogo ili uweze kuendesha utajiri mkubwa. Na hili halitokei ndani ya siku moja ni kadiri unavyojifunza kila siku. Kwa kusoma vitabu na kufanyia kazi yale unayojifunza.

Jambo moja na muhimu la kufanya ni kutokuweka akili yako yote kwenye pesa. Usiweke malengo yako kwenye pesa unapofanya biashara unafanya ili upate pesa lakini siku zote pesa hazikai huwa zinaisha hivyo badala ya wewe kuweka nguvu zako na mawazo yako kwenye pesa weka Zaidi katika kuwasaidia watu kama unauza nguo kazana Zaidi katika kuwafanya watu wafurahie huduma yako pesa zitakuja.

Kama unatoa huduma hakikisha unatoa huduma bora ili kuvutia wateja Zaidi kila siku. Pesa utaziona kwako na zitaongezeka kila wakati.

Wekeza pia muda wako kwenye kutengeneza mifumo mbalimbali ambayo itakuwa inakuingizia pesa bila kuwa na kikomo. Unapotegemea mfereji mmoja wa kipato lazima utabakia pale pale siku zote.

Jambo la muhimu la kufanya ili uweze kubakia juu kwenye mafanikio siku zote ni kujifunza na kujijengea misingi ambayo itakuwezesha wewe usiyumbe na ubakie na utajiri wako.

Kuwa mwaminifu, kua mtoaji, wapende wengine, kuwa muadilifu, usidhulumu mtu, kabla hujafanya lolote angalia lina manufaa gani kwako na kwa wengine.

Nikutakie wakati mwema Asante sana kwa kusoma Makala hii.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About