SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

πŸ€£πŸ˜ƒπŸ˜‚

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo

Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangi… kiberiti kikawaishia… wakamtuma mwenzao akatafute kingine… bangi lilikuwa limemkolea… akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweni…

MSHIKAJI:Β oyaaa wanangu eeeh… niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe …..

WENZAKE:Β baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.

Angalia nilichokifanya Jana kumkomoa x-wangu

Mwenzenu nilikatiwa umeme jana basi leo si nikaamua kwenda kununua luku ya 10,000. Kufika njiani nikatamani fursana nikaingia kijisupermarket mara sindo nakutana na ex wangu! Mshenzi yule kaniona mimi sijui alikua na mpango wa kununua vocha ya jero eti kabadili kanunua vocha ya buku tano ilimradi nione maisha yake safi tangu tuachane. Mambo ya kijinga spendi kudadeky nimetoa buku kumi nikanunua mipampers nami nijifanye nimeowa nina mtoto halafu huyoo nikashika njia yangu.

Sasa washkaji zangu tafadhalini mwenye mtoto au shida ya pampers naomba anunue kwangu maana leo nalala tena kiza πŸ™†β€β™‚

Unakumbuka haya enzi za shule?

Kama umesoma st Kayumba utakuwa una aidia na haya…

1.Unaenda shule umechelewa unakuta mwalim anakamata wachelewaj unaamua urudi nyumbani
2.unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni af unamuunguza mwenzio
3.mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu y kurudia nyumban
4.MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule)
5.MTU akikunyima kitu chake unamwambia “Ahaa eeh utaona sa nne”
6.wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao
7.ukiibiwa daftar jipya unalia kuliko hata uliloandika
8.unajaza mapeni kwenye mkebe(compass) na mengine hayaandiki
9.vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwibaπŸ˜‚
10.hakuna habari nzur kama kuambiwa Leo hamna shule mwalim haupo
11.habari mbaya zaidi n kurud nyumban kutoka shule una njaa af unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa
12.mtoto wa mwalim utamgundua tu kwanzia sweta begi na viatu vyake
13.usiombee umpige mtoto wa mwalim utataman uache shule
14.unatengeneza kifutio cha ndala af unatishia eti kinafuta hadi peniπŸ˜‚
15.ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu af unaongeza kijiti katikati
16.siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na naji wanakagua kuni au mboleaπŸ˜†
πŸ˜‚
Dah shule zetu hizi kiboko!!

Ipi umeipitia wewe
Share na wengine

Faida 13 za kunywa juisi ya miwa

Unapopita maeneo mengi ya mijini na pembezoni wa miji utakutana na wafanyabiashara wa miwa wanaouza miwa na juisi yake. Wengi hununua juisi ya miwa kwa kuwa hufurahia utamu wake. Lakini umeshajiuliza juisi miwa ina faida gani kiafya?

Kuna faida nyingi za juisi ya miwa. Baadhi ya faida hizo ni kama zifuatazo;
1. Juisi ya miwa ina uwezo mkubwa wa kuipatia miili nguvu kwa haraka na kukata kiu ya maji. Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari β€œsucrose” ambayo kazi yake kuu ni kutengeneza nguvu mwilini. Kwa hiyo wakati mwingine ukiwa na uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya viwandani tafuta juisi ya miwa.

2. Ingawa juisi ya miwa ina utamu lakini inafaa sana kwa watu wenye kisukari. Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari halisi ambayo ina uwezo mdogo wa kuzidisha kiwango cha sukari mwilini au kitaalamu inaitwa β€œLow Glycemic Index”. Kutokana na hilo juisi ya miwa inashauriwa kutumiwa kama mbadala wa vinywaji vingine vya viwandani. Ni muhimu pia kwa watu wenye kisukari kutumia juisi hii kwa kiasi kidogo au kulingana na ushauri wa Daktari.

3. Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya calcium, magnesium, potassium, chuma na manganese. Madini haya yana uasili wa ualkali ambao husaidia kupunguza uwezekano wa kupata kansa kama vile kansa ya Tezi dume β€œProstate cancer” na kansa ya maziwa β€œBreast Canser”.

4. Juisi ya miwa inasaidia kuongeza kiwango cha protein mwilini na ku-imarisha ufanyaji kazi wa figo.

5. Juisi ya miwa iliyochanganywa na maji ya Nazi husaidia kupunguza maumivu hasa yanayosababishwa na maambukizi ya ngono β€œSTDs” na kidney stones.

6. Juisi ya miwa husaidia kulinda maini yasipate maambukizi. Hii ndo maana Madaktari hushauri matumizi ya juisi ya miwa kwa watu wenye ugonjwa wa Homa ya Manjano.

7. Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya potassium ambayo husaidia kuimarisha mmeng’enyo wa chakula.

8. Husaidia kuzuia maambukizi katika tumbo na utumbo.

9. Vilevile husaidia katika kutibu matatizo ya choo kigumu au kitaalamu inaitwa β€œconstipation”.

10. Uchunguzi unaonyesha juisi ya miwa husaidia kuzuia meno kuoza na matatizo ya kupumua kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha madini. Kwa hiyo kama unafikiria kwenda kwa daktari kung’arisha meno yako, kunywa juisi ya miwa mara kwa mara.

11. Juisi ya miwa husaidia katika kupambana na mabaka mabaka na kung’arisha ngozi.

12. Juisi ya miwa huweza kutumika kama ” face mask na scrub” kwa kuipaka kwenye ngozi na hivyo kusaidia katika kuing’arisha na kuiimarisha uso.

13. Juisi ya miwa ina faida nyingi mwilini, ni muhimu kuhakikisha usafi katika utengenezaji wake.

Kumbuka: Juisi ya miwa isiyokuwa salama inaweza ikawa ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya tumbo na kuhara.

Chanzo, dalili na matibabu ya chunusi

Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.

Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris.Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni kumi na sa-ba..Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wa-kati wa balehe (adolescents) .

Karibu asilimia 85 ya vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na zaidi ya asilimia 20 ya wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.

Chunusi ni ugonjwa unaoathiri vifuko au glandi za ngozi.Katika ngozi ya binadamu kuna glandi ziitwazo Sebaceous ambazo zipo chini ya ngozi na kazi yake kubwa ni kutoa mafutamafuta yaitwayo Sebum ambayo hu-saidia kuiweka ngozi kuwa nyevu na yenye mvuto.

Wakati wa balehe mwili wa binadamu hutoa Sebum kwa wingi na kwa sababu wakati huu vikemikali vya mwili yaani sex hormones hutolewa kwa wingi hasa hormone ya kiume iitwayo androgen husababisha utoaji wa sebum kuwa mwingi zaidi kuliko kawaida. Sebum inapotolewa kwa wingi huungana na seli za ngozi zilizo-kufa na kutengeneza mchanganyiko mzito kama nta uitwao comedo ambao huziba vishimo vya kutolea joto.

Maambukizi zaidi hutokea pale ambapo vijidudu yaani baktaria vinaposhambulia vishimo vilivyoziba hapo kivimbe ambacho watu wengine huita Pimple hujitokeza pale ambapo Sebum, bacteria, seli za ngozi na seli nyeupe za damu zinapo-changanyika na kujikusanya katika vishimo vya jasho vilivyoziba na eneo husika hupata vivimbe au vipele ambavyo tunaviita chunusi.

Ukubwa wa kipele hutegemea ngozi ya mtu au kiasi cha mchanganyiko nilioeleza hapo juu katika eneo husika.Vipele vinaweza kuwa vidogo au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.

Ngozi mpya hutengenezwa kirahisi tu mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha mlingano usiosahihi wa ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni kwa sababu maeneo hayo yana vifuko au glandi za Sebaceous nyingi.

CHANZO CHA CHUNUSI

Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;

UMRI – Kama nilivyosema hor-mone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubale-he.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
VIPODOZI –Baadhi ya vipodozi kama Make-up za kina dada na Sprays za ny-wele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufan-ya chunusi kuwa nyingi zaidi.
DAWA-Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na ma-kusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana.
MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
JINSIA-Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.
FAMILIA- Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.
HOMONI- Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
USAFI WA MWILI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele hu-sababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwi-lini au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi
MAWAZO AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi vimkemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huwe-za kuchangia au kusababisha chunusi

DALILI ZA CHUNUSI

Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza kujitokeza kama baka dogo na wakati mwingine mtu anaweza utambuzi wa chunusi unaweza kuwa mgumu kutokana na watu walivyomakini au wanavyojenga wasiwasi kubwa katika mwonekano wao hasa usoni.Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana.

Daktari kuzigundua, japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu akaenda kumwona daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya chunusi.Pale inavyotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu chakula, ngozi, dawa unazotumia na vitu vingine vinavyowe-za.kuchangia mtu kupata chunusi

MATIBABU

Matibabu ya chunusi yanajumuisha kupunguza utoaji wa anta (sebamu ), kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.

Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingia au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyoeleza hapo juu.

DAWA ZA KUPAKA

Kuna dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi. Dawa hizi hupatikana kama cream,lotion,gel au pad.

Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu. Mojawapo ya dawa hizi ni antibi-otic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin na betamethasone au dexame-thasone kama vile Gentrisone au Gentriderm cream, Erythromycin,B-Tex na kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa ukianza na asilimia ndogo (2.5%) na kuen-delea kadri ngozi yako inavyohimili dawa. Gentamycin huua wadudu wanaosababisha chunusi wakati dawa nyingine huondoa mwasho.

Dawa nyingine ni zile zinzolainisha nta au Comedolytics na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi.

Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi na sabuni ya kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.

DAWAZA KUMEZA

Wakati mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa kutumia dawa za kumeza kulingana na wingi au ukubwa wa tatizo.

Dawa kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi ,dawa hizo ni kama vile Erythromycin topical, Accutane (isotret-inoin), Benzamycin Cleocin T (clindamycin phosphate), Desquam-E (benzoyl peroxide) Minocin (minocycline hydrochloride) na ”Si vema kujinunulia mwenyewe tu na kuanza kutumia bila ushauri wa daktari au mtaal-amu wa magonjwa ya ngozi.”

Wanawake wenye chunusi zisizotibika wanaweza kupewa Anti-androgens kama vile baadhi ya vidonge wa uzazi wa mpango.Chunusi sugu hutibiwa kwa ciorticosteroids na anti-iflammatory drugs ambazo hutibu chunusi sugu ambazo huitwa Acne fulminans na hupatikana zaidi kwa vijana.

MATIBABU MENGINE

Kwa nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata upasuaji mdogo (skin grafting) au plastic surgery kama chunusi imesaba-bisha baka kubwa na kuna njia kama vile Chemical peel ambapo kemikali hupakwa kwenye ngozi na inapokauka kipande au gamba la juu la ngozi huondolewa na kuondoa baka.

MATIBABU MBADALA

Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.

Watu wenye chunusi wanashauriwa kulAa mlo kamili wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi, matunda, mboga za ma-jani,vitamin B complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa, tumbaku, sukari, vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi

MUHIMU

Chunusi haziwezi kutibika kabisa japokuwa iwapo matibabu Yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.

MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI

  1. Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
  2. Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu.
  3. Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na mafuta mgando
  4. Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
  5. Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
  6. Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
  7. Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
  8. Punguza mawazo

Ingekua wewe ndio baba au mama ungefanjaje?

Baba na mama baada ya kurudi safari pamoja wakakuta BARUA iko mezani SEBULENI ikisema…. “Baba na mama, ni matumaini yangu kuwa mtasoma ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka
juu ya meza, naomba msishtuke mana ni mambo ya kawaida kwenye maisha tunayoishi, najua mtaumia kwa vile bado nasoma na ndiyo nipo kidato cha kwanza…” Napenda kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii barua sipo nyumbani, nimetoroka mana nimegundua
nina uwezo wa kujitegemea kwa sababu mi ni kijana mwenye umri wa miaka 14 na ninajua kipi chema na kipi kibaya.

Tangu mwezi mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano nabinti mmoja aliyeitwa Rachel, mwenye umri wa miaka 27 na kwa sasa
ndo naishi naye kwenye chumba alichopanga. Nilipokuwa nyumbani sikuwa napata hela za kutosha ila sasa nimeanza kushika noti za shilingi 10,000… Msichana niliyenaye ni mzuri sana wa umbo na ninampenda sana, amenifundisha njia za kutafuta hela.

Amenipangia kazi ya kuuza madawa ya kulevya na yeye ikifika
usiku anaenda kuuza mwili wake, basi kila siku tunapata hela ya kutosha, huyu mchumba wangu ni msichana mwenye bidii, kwa siku analala masaa 6 tu maana mwanaume yeyote akija lazima awe naye
chumbani kwa muda wa masaa 3.

Msiwe na hofu, nipo salama kabisa na nimeamua kumwoa Rachel mana ni kila kitu kwangu. Pia amenunua gari la kubebea mbao kwahiyo biashara inaenda vizuri.

Rachel ameenda kupima afya na amekutwa na upungufu wa kinga
mwilini, mara nyingi namridhisha anapotaka kitu flani, iwe kufanya naye mazoezi ya viungo au kufanya naye mapenzi, si mnajua unapokuwa na mgonjwa unakuwa naye karibu.

Ila mi pia sijihisi vizuri mana kila saa nakohoa tu na sina uhakika kama nimeathirika. Tumepanga baada ya miaka miwili tutawatembelea, nadhani mpaka miaka miwili iishe atakuwa
ameshajifungua, na ni furaha yangu mtamwona mjukuu wenu. Wazazi wangU, sina la kuongeza kwaherini Mungu
akipenda tutaonana.

NB: “Baba na mama, mimi nipo chumbani kwangu najisomea,
mnachokisoma ni h/work ya mwalimu wa kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi ya kusisimua, naomba muiangalie kama kuna
makosa!”

Ingekuwa wewe hapo ndi baba au mama ungefanyaje? SHARE na wenzako wasome.

Faida za kila kitu kwenye mti wa papai

Watu wengi hulitumia tunda la papai kwa sababu ya utamu wake. Hata hivyo mbali na kuwa na ladha nzuri, tunda la papai lina faida lukuki kwa afya ya mwanadamu.

Utajiri wa vitamin.

Tunda la papai lina vitamini A,B,C,D, na E jambo linalo liweka tunda hili katika kundi la matunda na vyakula vyenye utajiri mkubwa wa vitamin.

Faida zitokanazo na papai kiafya.

Tunda la papai lina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa :

Mbegu za Papai:

1. Kutibu tatizo la Shida ya kusaga chakula tumboni.

2. Kutibu Udhaifu wa tumbo.

3. Kutibu Kisukari na asthma au pumu.

4. Kutibu Kikohozi kitokacho mapafuni.

Mizizi Ya Papai:

Β· Kutibu Kifua kikuu

Β· Tunda hili huleta afya nzuri ukitumia kila siku

Β· Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda

Β· Vilevile yanasaidia kutibu sehemu palipoungua moto

Β· Kama hiyo haitoshi, maziwa yanayotoka katika jani la mpapai yanatibu kiungulia na Ugonjwa wa colon (njia ya haja kubwa ndani)

Majani Ya Mpapai:

Β· Pia yanasaidia kutofunga choo

Β· Maganda ya tunda la papai yanasaidia kutibu tatizo la kuungua, vipele na saratani ya ngozi.

Β· Mbegu zake zinatibu ini zikitafunwa 10 – 12 kwa siku 5.

Β· Majani yake yakaushie ndani, yanatibu pumu. Inapoanza kubana yachome majani yaliyokaushwa kisha jifukize, kule kubanwa kutakisha.

Β· Majani yake yanasaidia katika kutibu shinikizo la damu.

Β· Papai likimenywa na kupondwa linafaa Sana katika masuala ya urembo kwani linaweza kutumika Kama vile unavyotumia lotion kulainisha uso.

Β· Mbegu za papai zina uwezo wa kutibu homa. Meza mbegu za papai kiasi cha kijiko cha chakula mara 3 kwa ajili ya kutibu homa.

Β· Mbegu za papai zilizokaushwa ndani kisha zikasagwa kuwa unga zinatibu malaria, tumia kijiko 1 cha chai changanya na uji, kunywa mara 3 kwa siku 5 Mgonjwa wa kifua kikuu akila matunda haya kwa muda mrefu atapona bila dawa nyingine.

Β· Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa, lita 2 na nusu kwa dakika 15, yanatibu figo, bladder, yanazuia kutapika.

Baada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta

MUME: Fungua mlango!

MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.

MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.

MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!

MUMEΒ kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!

MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.

MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.

MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.

Umuhimu wa kula fenesi kiafya

Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee huku likiwa na ladha tamu isiyomithilika. Licha ya sifa hii, tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki endapo litaliwa na mwanadamu.

Kwanza, linatajwa kuwa na virutubisho kadha wa kadha vyenye kazi mbalimbali mwilini. Baadhi ya virutub
isho hivyo ni pamoja na vitamini za aina mbalimbali, madini, protini, mafuta, uwanga na nyuzinyuzi.

Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na lehemu. Si hivyo tu, bali pia ni chakula chenye virutubisho vya kuondosha sumu mwilini vinavyoweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa mengine kadha wa kadha.

Uwepo wa viondosha sumu ndani ya tunda hili kunasaidia pia kuongeza uwezo wa kuona. Tunda hili pia linatajwa kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya potassium yanayosaidia kuimarisha mifupa na afya ya ngozi.

Wataalamu wa mambo ya afya wamezitaja faida nyingine za tunda hili kuwa ni pamoja na:

Kinga:

Fenesi ni chanzo kizuri cha vitamini C. Uwepo wa kiasi kikubwa cha vitamini hiyo pamoja na viondosha sumu kunaongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini. Husaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi.

Nishati:

Ni tunda salama kiafya, halina lehemu licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha mafuta. Pia, lina wanga na kalori kwa kiasi kikubwa. Sukari iliyomo ndani yake huchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mwili.

Hurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza.

Asthma:

Inasadikika pia kuwa tunda hili lina uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu.
Si hivyo tu, fenesi lina vitamini muhimu katika utengenezaji wa damu mwilini.

Matumizi ya juisi ya limao kutibu shinikizo la chini la damu

Juisi hii ni nzuri sana katika kutibu shinikizo la juu la damu.

Lakini inaweza pia kutumika kutibu shinikizo la chini la damu hasa ikiwa hili shinikizo la chini la damu limesababishwa na upungufu wa maji mwilini (dehydration).

Kutibu shinikizo la chini la damu unaweza kuchanganya juisi ya limau na chumvi kidogo na sukari au unaweza kutumia maji maji ya miwa.

Shopping Cart
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About