Meseji za Vichekesho na Vituko
Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu
Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimuโฆ.kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamake๐๐๐๐๐๐๐
Kiingereza kinashida kweli, Angalia alichokisema huyu mwalimu
Kiingereza shidaaaaโฆโฆ!
Mwalimu wa chakula alipokuwa anaongea na wapishi akiwaeleza maharage kutoungwa vizur
Tcha: these beans are not well connected,,๐๐๐
Wanawake wanavyopenda hela, hadi kutoka kwa nyani na ngedere
Kama Nyani na ngedere wangekuwa na pesaโฆ
Trust me Kuna wanawake wangekuwa wanaishi misituni mda huuโฆ..
Wanavyopenda hela
๐๐๐๐๐๐๐๐
Huyu Jamaa kaona bora afe kuliko mke wake ajue Siri zake
Jamaa Mmoja Alimwambia Mke Wake Wasiliana Na Kitengo Cha Dharura Hospitali, Niko Taabani Nahisi Kama Ninakufa.
Mke Akamwambia Nipe Namba Yako Ya Siri Nifungue Simu Yako.
Mume Akasema๐๐ Basi Acha Tu; Kila Nafsi Itaonja Mauti
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Aina mojawapo ya watoto ambao ni hasara kuwa nao
Alipelekwa Hospitali na baba yake, baada ya vipimo Doctor akawa anamuandikia dawa, baba yake akatoka nje kuongea na cm.
Mtoto akamwinamia Doctor na kusema kwa sauti ya chini:- “Doctor Kwenye dozi ya dawa niandikie na FANTA BARIDII, CHIPS na MISHIKAKI kutwa mara 2 kwa siku 30.
BREAKING NEWS!!! Nyoka wa ajabu agundulika
HABARI MPASUKO..
jana katika taasisi ya wanyama pori ya Nat Geo ilitangazwa kuwa ametokea Nyoka hatar san Ambaye hajawah kutokea duniania.. wanadai kwamba nyoka huyo anaongezeka ulrefu wa 0.5sm kila akila chakula na huwa anakula chakula kuanzia sekunde 30 kurudi nyuma.. mpaka sasa hakuna siraha ya kuweza kumuua nyoka huyo isipokuwa akiji uma mwenye ndo anaweza kufa, wanasayansi hao walieleza japo uchunguz zaid bado unaendeleaโฆ huyu ni nyoka anayeua kuliko nyoka wote waliowah kutokea katika historia ya maisha ya mwanadam..
nyoka huyu hupatikana katika simu pekee za nokia toch katika sehem ya game inaitwa snake xenzia..
asanteni kwa kufurah na umakin mkubwa katika usomaji wa matini hiiโฆ
haya ni mambo ya wikiend jaman na iwe njema kwenu wote
Haya mawazo ya huyu Mtu kuhusu Shetani ni kiboko
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniโฆunaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniโฆ๐๐๐๐
Angalia huyu jamaa alivyomuweza huyu binti wa chuo
๐๐๐๐ .. TABU KUDATE NA MADEMU WA CHUO
Demu ;ย Baby Safari Hii Nataka Pale Hostel Niwafunike Mashoga Zangu Wote.
Jamaa ;ย Poa Sweetie Ondoa Shaka Nitakununulia #Turubai Utawafunika Woteโฆ!!!
Demu:ย Mxiuuuuuuuu Lione Sura Kama Goti La mbuzi Na Namba yangu futa Nakublock Mpaka Sanduku la postaโฆ!!!
๐๐๐๐nmecheka adi nmelazwa
Sababu ya mke kupewa dawa badala ya mumewe
Dokta: Mama tumemchunguza mumeo kwa makini sana, jopo lote la madaktari tumekubaliana mumeo anahitaji mapumziko japo ya mwezi. Sasa tafadhali chukua hivi vidonge vya usingizi vitasaidia sana.
Mama: Asanteni sana, sasa niwe nampa mara ngapi?
Dokta: Unatakiwa wewe uwe unakunywa vidonge hivi kutwa mara tatu kwa mwezi mzima, mumeo atapona.
Dunia ina mambo! Angalia kilichotokea baada ya mgonjwa kuwekewa macho ya paka
Kuna jamaa alipata ajali akapofuka macho๐, akaenda hospital akawekewa macho ya paka๐๐ฑ,
dokta akamuuliza: vipi saizi unaona?
jamaa: naona ila naona panya tu
๐๐๐๐๐






































































I’m so happy you’re here! ๐ฅณ








Recent Comments