Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Kuwa na msimamo katika mahusiano

Sio Kila EX Wako Anayeomba Mrudiane Anamaanisha! Wengine Huomba Kurudi Ili Wakutesti Tu Jinsi Ulivyo Mbulula,Jinsi Usivyo Na Msimamo Na Jinsi Ulivyo CHEAP Na Huna Misimamo Wala Future.

Jitu Mmeachana Miezi 6,Leo Linakutesti Lirudishe Majeshi,Na Wewe Ulivyo Kiazi,Upo-Upo Tu,Ina Maana Miezi Yote Hii Ulikuwa Umeganda Unasubiria Rehema Zake Ama?? Kurudia Matapishi Ya EX Ukitegemea Amebadilika Ni Sawa Na Kupika Sufuria La Makande Kwa Mshumaa,Utaambulia Masizi Tu..
.
Kipi Kipya Kakiona Kwako Hadi Arudi??Nini Kilimshinda Huko Nyuma Ambacho Leo Anakiweza Anataka Kurudi??Akafie Mbele Huko.
.
KUWA NA MSIMAMO,Ukisema Its Over Umaanishe,Sio Unakuwa Na Hisia Zinapepea Tu Kama Bendera Ya Katibu Kata Wa Kishumundu… Mtu Kama Hajielewi Achana Nae,Siku Akijirudisha Mwambie Kwanza Akapimwe Minyoo Ya Kinyarwanda.
.
Umekazana Kuwaambia Marafiki Zako ‘Siku Hizi Hakuna Mapenzi Ya Dhati Watu Wote Majanga Tu’,Nani Amekwambia Hayapo?? Yapo Sana Ila Wewe Unatumia Mbinu Tofauti..
.
Huwezi Kusoma Degree Ya Law Halafu U-Apply Kazi Ya Chief Accountant Wa Bodi Ya Tumbaku…Kila Siku Utasingizia Balance Sheet Haina Jurisprudence..Lawyersl
Mmenielewa! Acha Kudate Watu Wasiojielewa,Usidate Kwa Sababu Uko Lonely,Usiwe Desperate Kuingia Mahusiano Kwa Sababu Shosti Zako Wanakusimulia Walivyopelekwa Ruwenzori Waterfalls..
.
Ingia Kwenye Mahusiano Pale Moyo Wako Ukiwa Tayari Na Mtu Uliyemfia Kihisia Na Amekuwa Approved Na Veins,Auricles,Na Aorta Za Moyo Wako Kwamba He/She Is Really The One.. Unadate Na Mtu Ambaye Mustakabali Wake Mwenyewe Haujui,Ukimuuliza Anataka Kuwa Wapi Ndani Ya Miaka 5 Ijayo Anakwambia Mungu Anajua Dont Worry,Halafu BBM Na Instagram Unajiita Baby Ake Mie Iam In Love..
Utaishia Kufua Boxer Hadi Kucha Zinukie Gololi! Mbwa Kamwe Hashughuliki Na Kesi Za Paka Kufungiwa Kabatini.Date The Right Person,With Right Reasons,In A Right Time Uone Kama Mapenzi Hayapo…

Na mwenye masikio na asikie😀😀😀😍

Nani Mkali Hapa kati ya DEMU na MSHIKAJI?

“MAENEO FLANI ya KISHUA”

-Mshikaji kamwona demu mkali
anakatiza kitaa akamkubali akaamua
amfuate amtemee cheche

MSHIKAJI- mambo dada?

DEMU- pouwa

MSHIKAJI-
umependezaa!!!

DEMU- asante.

MSHIKAJI- unaweza ukanisaidia
namba
yako ya simu……..
maana duh
nmekukubali
kinyama.

Demu baada ya kuambiwa vile
akazama kwenye pochi lake akatoa
noti ya
sh.10000 akaandika namba yake
kwenye
noti akampa mshikaji.

Mshikaji kapokea ile noti kachana
sehem
iliyoandikwa namba halafu
kamrudishia
Demu noti yake..!!!

NANI ANA DHARAU
NA NANI JEURI..
DEMU AU MSHIKAJI??!

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Cornflakes

MAHITAJI

Unga – 1 Kikombe

Sukari ya kusaga – 3/4 Kikombe

Siagi – 125 gms

Yai – 1

Baking powder – 1/2 kijiko cha chai

Zabibu kavu – 1/2 kikombe

Cornflakes iliyovunjwa (crushed) – 2 Vikombe

Vanilla – 1 kijiko cha chai

MAANDALIZI

Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri.
Tia baking powder, zabibu na unga na changanya vizuri.
Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni.
Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Weka cornflakes katika sahani ya chali (flat) na zungusha viduara humo kisha upange katika sinia ya oveni.
Pika katika moto wa 350ºF kwa muda wa dakika 20-25 hadi vigeuke rangi na viwive.

Cheki huyu jamaa anavyoungama kwa padri sasa

JAMAA: Baba Padri nimekuja kuungama
PADRI: Haya
JAMAA: Niliiba kamba
PADRI: Kamba?
JAMAA: Ndio, kamba lakini kule mwisho kulikuwa kumefungwa ng’ombe
PADRI: Kwa hiyo uliiba ng’ombe?
JAMAA: Kiukweli nilikuwa nina lengo la kuiba kamba, kwa bahati mbaya mwisho kulikuwa na ng’ombe
PADRI: Mi naona mueleze Mungu direct, mi sikuelewi kabisaaa

🙈😃😃😃😀😀😀😂🙊

Tabia za kuepuka ili uweze kuwa tajiri

UKIWA NA HIZI TABIA 9, JIANDAE KUFA MASKINI…………
By Kashindi Edson

“Umasikini hauji kwa bahati mbaya kama ubaguzi wa rangi au ukoloni, umaskini hutokana na matendo ya kila siku ya mwanadamu” (Nelson Mandela, R.I.P)

“Kila mtu anataka kufanikiwa, lakini si kila mtu yuko tayari kushika majukumu na wajibu wa kumpeleka kwenye mafanikio”(Mwl Nyerere, R.I.P).

“Kile unahokifanya muda huu ndicho kinachoashiria na kutoa picha kamili ya baadae yako”(Mahatma Gandhi, R.I.P)

“Ukizaliwa maskini sio kosa lako, ila ukifa maskini hilo ni kosa”(Bill Gate, The richest man in the world).

Mwalimu wangu wa chuo aliwahi kuniambia kuwa, “mstari unaomtenganisha maskini na tajiri ni mwembamba sana, kwa hiyo ni rahisi sana kuwa tajiri pia ni rahisi sana kuwa maskini”. Mpaka leo sijaelewa alimaanisha nini.

Watu wote waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali za maisha, kwenye uongozi, biashara, kilimo, elimu, siasa, michezo, uandishi, muziki, afya, imani, utangazaji, nk huwa hawana hizi tabia 9 nilizokuandalia leo, kwa hiyo kama una kiu ya mafanikio kwa hicho unachopambania, achana na haya mambo 9 yafuatayo;

1. KUTOKUJARIBU.

Katika kutafuta mafanikio huwa kuna vitu viwili tu vya kuchagua. Tambua kuwa maisha ni vita. “Chagua kufa, au kupambana”. “Siogopi kufa, naogopa kutokujaribu'(Jay Z). Hakuna alie zaliwa anajua, jiamini, jaribu utafanikiwa.

2. KUTOKUJIFUNZA.

Che Guava mpaka anafariki library yake ilikuwa na vitabu zaidi ya 2000, mwenzangu na Mimi sijui hata kama una Biblia au Quran ghetoni kwako. Nkwameh Nkrumah library yake ilikuwa na vitabu zaidia ya 3000, Obama anakuambia kila akiamka asbuhi lazima asome kitu kipya. “JOSEPH=Jifunze, Ona, Soma, Elimika, Pitia, Hamasika.(Prof Jay)

3. WOGA & WASIWASI.

“Tunaweza tukamsamehe mtoto anayeogopa gizani, lakini sio mtu mzima anaeogopa mchana”(Plato, R.I.P). Kitu cha kuogopa katika maisha ni woga wenyewe. Kama hujiamini hutakuja kuwa mshindi katika jambo lolote. Fanya hicho unachofikiria kukifanya kwa moyo wa dhati, kama unaamini ni cha harali na kia manufaa kwako na familia yako, na jamii nzima. Acha tabia ya kuogopa kitu ambacho hakijatokea.

4. KUJILINGANISHA.

Kuna baadhi ya watu, huwa wangetamani kuwa kama watu Fulani. Kuwa wewe pia jiamini. Usitamani kuwa Magufuli, Kassim Majaliwa au Paul Makonda. Kila mtu ni wa pekee na maalumu. Jikubali kwanza afu wengine ndo watakukubali wewe. Weka nguvu kwenye ubora wako na sio kwenye madhaifu yako. Ukijilinganisha sana utakosa furaha ya nafsi maisha yako yote.

*5. KUWEKA VINYONGO.**

“Kuweka chuki na konyongo moyoni ni sawa na kunywa sumu ukidhani atakufa mtu mwingine”. Onesha upendo, sambaza upendo, hayo ndo mafanikio ya kweli.

6. UONGO

“Uongo utakupa ushindi wa siku moja, ukweli utaishi milele”(WEUSI), “Muongo hata akiongoea ukweli usimuamini”(FID Q). Ukiwa muongo huwezi kufanikiwa hata siku moja. “Unaweza ukawadanganya watu, lakini huwezi kuwadanganya watu wote, wakati wote”(Bob Marley). Ukweli kama jua, katika safari ya mafanikio huwezi kuvificha.

7. UVIVU & UZEMBE

“Nyumba yenye njaa ukisizi unapata zero”(Fid Q). Mafanikio huja kwa kupenda unachokifanya. Neno “kazi” katika biblia limeandikwa mara 600. Dangote analala masaa 3 tu kila siku, Mohammed Dewj anaamka saa 11 asbuhi kila siku. We kwepa majukumu tu, kesho utakula magodoro. “Uvivu unalipa muda huu, bidii & juhudi vinalipa baadae”.

8. STAREHE & ANASA KUPINDUKIA

Pombe, sigara, ngono, unga, bange, shisha, cocaine, nk vitu vibaya sana. Ni ngumu sana kufikia mafanikio makubwa kama una tabia kama hizi. “Sisi ni kile tunacho kula”. Mafanikio ya kwanza huanzia kwenye afya yako”. Afya ni utajiri. Pia starehe hupoteza muda sana. “Mavuno ya uzee, ni swaga za ujana, kwa ukila ujana kumbuka kula kiungwana”(Nikki Mbishi,).

9. LAWAMA & UMBEA

“Watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiria hujadili kuhusu mawazo, uwezo wa kati hujadili kuhusu matukio na wale wenye uwezo wa chini, hujadili kuhusu watu” We upo kwenye kundi gani? Bora ukawa kundi la kati kuliko hilo la chini kabisa, hilo ni la “wachawi”. Tusilamike, tupambane,lawama hazisaidii chochote.Ukiweka malengo yako, vizuri na ukaacha hizo tabia hapo juu, muda si mrefu itazifikia ndoto zako

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Wigo wa mimea ni kinga nzuri ya mazao shambani. Mimea ya wigo inaweza kutumika kama kizuizi cha wadudu kuhama hama.

Wigo hutatiza vidukari kuhama na kuingia bustanini. Kwa mfano, mimea kama tithonia ni kizuizi kwa aina nyingi sana za wadudu.

Safu za mbaazi zimekuwa zikitumika kulinda nyanya, viazi, kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharage yanaweza kupandwa kati ya mistari ya kabichi yakiwa kama mitego kwani yanasaidia kulinda kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharagwe yanapandwa kama mtego kwenye kabichi lakini yanafanya kazi ya kudhibiti wadudu (mtego), kuboresha udongo, chakula cha mifugo, matandazo au kutengenezea mbolea.

Vile vile wigo wa mimea ni makazi ya wanyama/wadudu wanaowinda.

MAJIBU YA MAKONDA WA DALADALA ZETU GONGOLAMBOTO HUKU

1. wewe Dada unaturingia nini na matiti yako mawili , mbwa pia ana matiti nane na haturingii eboo !!!!

2. Ka wafikiri Una haraka sana Shuka ukimbie.

3. Nauli kulipa lazima ,Chenji ukikumbuka.

4. Kutapika ndani ndani ya Daladala fain 250/= ,ukijamba pia 250/= ,Sasa jamba tukujue viti vina alarm!…

5.Hatujasema wewe ni Mnene ila Ukikalia SITI mbili Lipia….

6. Hio Elfu kumi yako nenda nunua avocado upake alafu uteleze hadi posta ,nauli ya daladala ni 350/=.

7. usifungue dirisha ungetaka upepo ungepanda pikipiki..

8. wewe Dada hebu sogea hukoo, Unaringa nini wakati asubuhi hii umeoga na sabuni ya kuoshea vyombo…

Faida ya kunywa maji yenye limao au ndimu kila siku

Watalam mbalimbali wa afya wanasema ya kwamba kwa kila siku ni vyema unywe maji ya ndimu ili uweze kujitibu magonjwa yafuatayo;

Unachotakiwa kufanya ni;
Weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.

Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula chochote kingine kwa faida zaidi.

Anza leo kwa kunywa maji yenye ndimu kila siku asubuhi na uone mabadiliko ndani ya mwili wako. Mshirikishe mwenzio ili naye afaidike.

1. Huchochea Mmeng’enyo wa Chakula Tumboni

Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.

Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

2. Huboresha Kinga za Mwili

Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

3. Husaidia Kinga Dhidi ya Saratani

Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicalsmwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).

Usafishaji wa Mwili na DamuLimao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo ,ini na mfumo wa chakula.

4. Kurekebisha Sukari katika Mwili

Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili.
Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.

5. Dawa ya Kikohozi na Mafua

Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.

6. Inasaidia Urekebishaji wa Ngozi na Kupona Makovu

Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia. Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.

7. Husaidia Kupungua Uzito

Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale amabao wanataka kupungua uzito.

8. Kuondoa Harufu ya Mdomo

Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.


Madhara ya kunywa pombe wakati wa ujauzito

Kuacha Matumizi ya pombe wakati wa ujauzito ni moja ya njia ya kuzuia kupata matatizo ya kuzaliwa nayo na udhaifu kwa mtoto. Pia kuna matatizo kadhaa yanaweza kutokea kwa kichaga kutokana na matumizi ya pombe wakati wa ujauzito.

Madhara haya ya pombe huweza kuwa ya kujitambua tabia na madhara madhara ya mkusanyiko wa dalili na viashiria kwa mtoto vinavyoitwa fetal alcohol syndrome-FAS. Kutokana na shirika madhara ya pombe yanayoambatana na dalili na viashiria fulani yanaongezeka sana. Pombe imekuwa ikituiwa vibaya sana wakati wa ujauzito ukilinganisha na madawa mengine.

Dalili za mtoto ambaye mama alikuwa akitumia pombe kwa kiasi kikubwa;

  1. Kutokuwa vema kabla na baada ya kuzaliwa
  2. Mtindio wa ubongo
  3. Udhaifu wa kuzaliwa wa kichwa na uso
  4. Magonjwa ya moyo
  5. Tabia zisizoeleweka
  6. Matatizo ya mfumo wa fahamu

Kiasi gani cha pombe ni salama kwenye ujauzito?

Hakuna kiwango salama cha matumizi ya pombe kwenye ujauzito kilichotambuliwa. Kwa usalama ni kutofikiri kutumia pombe wakati wa ujauzito.

Je kuna uhusiano wa kiwango cha pombe na matokea mabaya ya ujauzito?

Hakuna. Miongozi mwa wanawake waliokunywa ounce 5 ya pombe kwa kila siku, 1/3 ya watoto walikuwa na FAS, 1/3 walionesha madhara sumu kabla ya kujifungua, na 1/3 waliobaki walikuwa kawaida. Kundi jingine lililotumia ounce 1-2 kila siku asilimia 10 ya watoto walikuwa na dalili za FAS. Hata kiwango kidogo cha pombe kimekuwa kikisababisha FAS!. Matumizi ya pombe kwa kiasi kidogo bado yamekuwa yakihusika kusababisha mtoto kuwa na IQ kidogo na matatizo ya kujifunza kwa watoto wenye anatomia ya kawaida.

Je pombe husafilishwa kwenye kondo la mtoto?

Kemikali ya ethyl iliyo kwenye Pombe hupita kwenye kondo na kuingia kwa kwenye mzunguko wa damu wa mtoto. Kiwango cha pombe kwenye damu ya mama huwa sawa na kile kwenye damu ya kichanga tumboni.

Je mama aliyekuwa teja wa pombe anatakiwa aache kunywa pombe?

Mama aliyekuwa teja wa pombe anatakiwa apewe msaada wa wataalamu ili kusaidiwa kuacha pombe, madhara a kujifungua kabla ya mda huongezeka kwa watumiaji wa pombe

Dalili za kuacha pombe ghafla zinaonekana wakati gani wa ujauzito?

Dalili za kukatisha kutumia pombe huanza kuonekana upesi pale mtu anapoacha kutumia pombe, Mara nyingi ndani ya masaa 4 hadi 12. Hata hivyo inawezekana dalili za kukatika kutumia pombe kuonekana siku chache baadae. Mtu asipopata tiba hufikia kilele cha dalili ndani ya masaa 48 na huweza kuendelea kufikia miezi 3 hadi 6 na huwa na dalili kiasi kuliko awali. Dalili na viashiria ni kutetemeka, wasiwasi, mapigo ya moyo kwenda kasi, shinikizo la damu la juu, kutokwa jasho, kichefuchefu, kukosa usingizi na hutegemea utegemezi wa pombe na hali ya mgonjwa.

Mara ujauzito unapotambuliwa kuacha kutumia ama kupunguza husaidia kuondoa madhara kwa mtoto?

Kemikali ya ethyl na ethanol iliyo kwenye pombe hupitaka kwenye kondo la nyuma na kuingia kwenye damu na ubongo wa mtoto. Inafikilika kwamba madhara hutokana na sumu iliyo kwenye pombe na mazao ya uchakataji wa pombe mwilini. Kuacha au kupunguza kutumia pombe mara ujauzito unapotambuliwa huweza kupunguza matatizo ya kuzaliwa kwa mtoto hata hivyo kuna uwezekano kwamba inaweza hili lisitokee. Hivyo tafiti zaidi zinatakiwa kufanyika ili kuonyesha usahihi wa jambo hili.

Siri ya mafanikio katika maisha Ni Kutoangalia Watu

Baada ya kusoma makala kuhusu hofu zinazotugharimu katika safari ya mafanikio, Leo nimekuandalia Makala hii ya Siri ya mafanikio.

Katika safari ya mafanikio, watu wanaweza kuwa kikwazo kikubwa kinachosababisha ugumu wa kuendelea mbele. Wanaweza kuleta upinzani, kukosa imani, au hata kuzua vikwazo visivyo na msingi. Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kuwa changamoto hizi zilizoletwa na watu ni sehemu ya mchakato wa kufikia mafanikio. Ingawa inaweza kuwa ngumu kukabiliana na watu wenye upinzani au wasioamini katika safari yetu ya kufikia malengo yetu, tunapaswa kuzingatia kuwa hakuna mafanikio ya kweli ambayo hayakuja na changamoto. Naam, inaweza kuwa rahisi kufanya kazi peke yetu na kuepuka kukabiliana na watu wasioamini au wenye upinzani, lakini hiyo haitatupeleka mbali sana.

Tunahitaji kushughulikia changamoto hizi na kuona jinsi tunaweza kuzishinda. Kukutana na watu ambao hawana imani na malengo yetu inaweza kuwa kama mtihani mkubwa kwetu. Wanaweza kutushawishi kuacha au kuanza kutilia shaka uwezo wetu. Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa imani yetu ndio itakayotuendesha mbele. Tunapaswa kujikumbusha kuwa mafanikio hayangeweza kupatikana ikiwa tungekuwa na imani ndogo ndani yetu wenyewe. Mbali na hilo, tunapaswa pia kutambua kuwa vikwazo visivyo na msingi vinaweza kuwepo katika safari yetu ya mafanikio. Watu wanaweza kuzua vikwazo hivi kwa sababu ya wivu, woga, au tu kutokuelewa malengo yetu. Ni muhimu kutambua kuwa hatuwezi kudhibiti tabia au mitazamo ya watu wengine, lakini tunaweza kujifunza kuweka mipaka na kuendelea kufuata malengo yetu licha ya vikwazo hivyo. Katika safari yetu ya mafanikio, tunapaswa kuwa na uvumilivu na subira.

Tunapaswa kutambua kuwa kila changamoto tunayokutana nayo inatupa fursa ya kukua na kujifunza. Tunapaswa kutumia changamoto hizi kama nguvu ya kuendelea mbele badala ya kutuacha tukata tamaa. Kwa kumalizia, ingawa watu wanaweza kuwa kikwazo katika safari yetu ya mafanikio, tunapaswa kuona changamoto hizi kama sehemu ya mchakato wa kufikia malengo yetu. Tunapaswa kuwa na imani thabiti ndani yetu wenyewe, kuweka mipaka na kuendelea kusonga mbele licha ya vikwazo vinavyoweza kuzuka. Kwa kufanya hivyo, tutapata mafanikio kamili na kuwa bora zaidi katika safari yetu ya kuelekea mafanikio.

Wakati mwingine, tunaweza kukutana na watu ambao hawana imani na uwezo wetu au wanajaribu kutuweka chini kwa sababu ya wivu au tamaa. Ni muhimu kujifunza kuweka mipaka na kuendelea kusonga mbele, kujiamini katika uwezo wetu na kuendelea kufanya kazi kwa bidii kuelekea malengo yetu.

Watu wanaweza pia kuwa vikwazo kwa kuwa na maoni tofauti au kutokuwa na uelewa kamili wa malengo yetu. Katika hali hizi, ni muhimu kuwa na uvumilivu na kuwasiliana kwa wazi ili kuelezea malengo yetu na kutafuta njia za kuwashawishi au kuwashirikisha katika safari yetu ya mafanikio.

Hakikisha pia kuwa unazungukwa na watu wenye mawazo chanya ambao wanakuunga mkono na kukusaidia kufikia malengo yako. Kuwa na timu ambayo inakusaidia na kukutia moyo ni muhimu sana katika safari ya mafanikio.

Kwa hiyo, tunapokabiliana na vikwazo kutoka kwa watu katika safari yetu ya mafanikio, ni muhimu kujifunza kutokana na hilo, kuweka mipaka, kuwasiliana kwa wazi, na kuwa na timu yenye msaada karibu nasi. Hatimaye, tunapaswa kuendelea kuamini katika uwezo wetu wenyewe na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu.

Waziri mkuu wa zamani wa uingereza Sir Wiston Churchill aliwahi kusema;

“huwezi kufika mwisho wa safari yako kama utakuwa unasimama kila mahali kumtupia jiwe kila mbwa anaye kubwekea”

Sir Wiston Churchill

Kauli hii ina maana kwamba kama una picha kichwani ya kule unakokwenda au umekusudia kufikia na kutimiza lengo fulani katika maisha hupaswi kusikiliza, kupambana au kushindana nakila mtu.

Unapokuwa njiani kutimiza lengo lako lazima utakutana na watu wa aina hizi;

  1. Watakaokurudisha nyuma kwa kukuharibia mipango na juhudi zako
  2. Watakaokuvunja moyo na kukukatisha tamaa
  3. Watakaokusema vibaya hata kwa mazuri yako na kukuzushia uongo
  4. Watakaokuchukia kwa sababu ya bidii yako

Unaweza kushawishika kutaka kumjibu kila mtu anayekusema vibaya, kukuchukia au kukukatisha tamaa (hapo ndo unakuwa sawa na yule anayesimama kumtupia jiwe kila mbwa anayebweka).

Unaweza ashawishika kutaka kuona kila mtu anakukubali na kukuunga mkono, kitu ambacho hakiwezekani.
Kuna Msemo usemao “siri kubwa ya kufeli katika maisha ni kujaribu kumpendeza kila mtu”.

Hapa duniani huwezi kumpendeza kila mtu hata ufanye jambo zuri kiasi gani “hata ukichezea maji utaambiwa unatimua vumbi”. Mara nyingi tunajitahidi kufanya mambo mema na kuwa na nia njema, lakini bado kuna watu ambao hawatafurahia jitihada zetu na watatupinga tu. Hii inaweza kuwa changamoto kubwa kwetu kihisia na kijamii, kwani tunatamani kukubalika na kupendwa na kila mtu.

Lakini kumbuka, haifai kuchukulia kila upinzani kibinafsi au kuathiri thamani yako. Watu wana mitazamo tofauti na uzoefu wao binafsi, na huenda hawana ufahamu kamili wa hali yako au malengo yako. Badala yake, ni muhimu kuwa na imani katika nia zako na kuendelea kufanya mambo mema bila kujali jinsi watu wengine watakavyokuona au kukupinga.

Njia bora ya kushughulikia upinzani ni kujielewa na kuweka mipaka. Jifunze kuamini kwamba wewe ni wa thamani na una uwezo mkubwa wa kuathiri mazingira yako. Wacha maadili yako yaongoze vitendo vyako na usiruhusu maneno au maoni ya wengine kukufanya ujisikie vibaya au kupoteza lengo lako.

Kumbuka pia kuwa hakuna mtu aliyeweza kufanya kila mtu awe radhi. Hata watu mashuhuri na viongozi wa kiroho hawakuepuka upinzani. Kina Mandela, Mahatma Gandhi, au Martin Luther King Jr., walikabiliana na upinzani mkubwa, lakini waliendelea kusimama imara kwa imani zao na kufanikisha mabadiliko makubwa.

Ili kufanya mabadiliko katika jamii au ulimwengu, ni muhimu kuwa tayari kukabiliana na upinzani. Upinzani unaweza kukusaidia kukua kibinafsi na kitaaluma, kurekebisha njia zako, na kukuza uvumilivu wako. Ni nafasi ya kujifunza na kujenga hoja zako kwa msingi thabiti.

Hivyo, jinsi unavyokabili upinzani ina athari kubwa kwa maendeleo yako na mtazamo wako kwa maisha. Usikate tamaa na usiruhusu upinzani ukuzuie kufuata ndoto zako na kufanya mambo makubwa. Jiamini, thamini uwezo wako, na endelea kusonga mbele bila kujali kile ambacho wengine wanaweza kusema au kufikiria. Hakuna kitu kikubwa kilichofanyika bila ya upinzani, kwa hiyo endelea na safari yako na uhakikishe kuwa unaamini kwamba una nguvu ya kufanya tofauti.

Wewe fwatilia Mipango yako huku ukitazame hatima yako. Soma hapa mbinu hizi za kukunufaisha maishani.

Lakini haimaanishi uwachukie watu na kuwatendea mabaya ili ufanikiwe mwenyewe. Chuki na Mapambano hayanufaishi bali yanakufanya kuwa dhaifu.

Vivyo hivyo, Sio watu wote ni kikwazo. Kuna watu wa aina nyingine ambao wanaweza kukusaidia kufanikiwa. Unapaswa kuwa makini na kutumia Busara yako kuweza kuwatambua watu unaokuwa nao katika safari ya Mafanikio.

Status za Whatsapp za Wazungu na Wabongo

STATUS ZA WAZUNGU kwenye Whatsapp vere vere kliaaa…
👉sick
👉at movie
 👉 in a meeting2
👉 kind of happy,, 👉busy,,
👉available
👉Driving
👉sleeping

STATUS ZA WABONGO SASA MBUTA NANGA MBONGO NGAFU

“Akutake nani una shepu la Kitorondo utaishia kumegwa na kuachwa

“Watu tuna nyota za Chips Mayai sio wewe mwenye Nyota ya Punda,halulaaa”

👌Kantangazeee ndo Kwanza naanza na ntakukomesha Mwanaharamu we!

😍 I love yu so much ur my only one,No one lyk yu and I mean it 🎶 Yu ma numba1 ma sweet sweet namba1 roho yangu mama,,

👍 Asante 😍 vimenitoshaaa tena kama ulijua 😘😘😘😘😘,

💪 unajifanya simba kumbe nyau mimi ndo maji kama hujanioga utaninywaa,

🙈 nauza Ubuyu kwa bei nafuuu kama unataka inbox me plz

😔 poleee jaman utapona wangu,,,

💪 utalijua jiji na chuki zako walingia na tako wakati hadi nyani analo kitu sura dada…

😡 usinisemeshe usiniongeleshe tena utaniambia vizur ulikuwa wapi..

😷 mdomo kaumbiwa mwanadamu ongeeni nyie me sijali ya wanafiki nafanya yangu huna hadhi ya kujibiwa na mimi
pamoja na ya kwako uloweka🙈😆😆😆

Mambo usiyoyajua kuhusu ugonjwa wa Pumu

Asthma /pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia ya hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu, pia hufanya kuta za ndani ya njia ya hewa kuvimba na hivyo hupunguza kiasi cha hewa kinachoingia na kutoka ktk mapafu, Hali hii husababisha mgonjwa kutoa mlio kama wa filimbi/mluzi wakati wa kupumua, kifua kubana, kushindwa kupumua vizuri na kukohoa sana, watu wa pumu huwa na dalil hizo nyakat za usiku na asubuhi sana pia ugonjwa huu huwaathiri watu wa Rika zote ingawaje Mara nying huwaathiri watoto kwa sababu huanza utoton na hivyo takriban MILION 6 ya watoto wanaumwa pumu na watu takriban 255,000 hufa kila mwaka kwa ugonjwa huu.

KUNA AINA NYINGI ZA PUMU

1 ~PUMU YA UTOTONI (CHILD_ONSET ASTHMA)

Hii ni aina ya pumu inayotokea baada ya mtoto kuzaliwa na kupata mzio (aleji) ambayo hupatkana katika vumbi la wadudu kama mende, pia manyoya ya wanyama kama paka, mbwa pia kutumia baby wipe zenye harufu na sabun zenye harufu kwa watoto huwa ni hatari.
Pumu hii hutokea kwa kuwa mwil wa mtoto hutengeneza Kinga ya mwil (ANTIBODIES) za IgE zinazosababisha pumu.
Ugonjwa wa pumu ni sugu sana kwa watoto wanaozaliwa na uzito mdogo wenye asili ya kiafrka pia pumu ya utotoni huwaathiri Zaidi watoto wa kiume.

2 ~PUMU YA UKUBWANI (ADULT_ONSET ASTHMA)

Pumu hii huanza baada ya kufika miaka 20, PUMU hii huathiri Zaid wanawake kuliko wanaume na pia haitokei sana kama pumu ya utotoni, Vizio pia husababisha aina hii ya pumu kwa asilmia kubwa sana

3~PUMU ITOKANAYO NA MAZOEZ (EXERCISE INDUCED ASTHMA).

Ikiwa utatokewa na Hali ya kukosa pumzi wakati wa mazoez au baada ya mazoezi inawezekana una pumu inayosababishwa na mazoezi pia hata kama sio mwanamichezo kukimbia kwa Kasi angalau dk 10 kunaweza kusababisha kukosa pumzi kwa muda mrefu.

4~PUMU ITOKANAYO NA KUKOHOA (COUGH INDUCED ASTHMA).

Hii ni aina ya pumu iliyo ngumu kwa baadhi ya madaktari kuigundua kwa sababu katika pumu hii inawezekana isitokee hata dalil zingine Zaidi ya kukohoa tu hvyo madaktari wanalazimka kuchunguza Zaidi sababu zingne za kukohoa sana na kuhakiksha sio zinazosababishwa na kukohoa huko.

5~PUMU ITOKANAYO NA KAZI (OCCUPATIONAL ASTHMA)

Aina hii ya pumu humtokea mtu akiwa mahali anapofanya Kazi pia huwatokea sana watumish wa viwandani ambapo kuna Moshi na gesi ya nitrogen oxide.

6~PUMU YA USIKU (NOCTURNAL ASTHMA)

Pumu hii hutokea Kati ya saa sita usiku na saa 2 asubuhi, pumu hii huamshwa na vumbi, harufu za pafyum, harufu za rangi za nyumba na vinyes vya wanyama pia Mara nying wagonjwa wa pumu hii hushtuka usingizini wakat wa usiku wa manane baada ya kukosa pumzi.

7~PUMU KALI ISIYOKUBALI STEROID(SEVERE ASTHMA /STEROIDAL RESISTANT ASTHMA).

Wakat wagonjwa wengi wakipata nafuu baada ya kupata steroid wachache hawapati unafuu na hvyo kuhitaj matibabu makubwa Zaidi.

JE UNAJUA CHANZO CHA PUMU??

Visababishi vya pumu havijulikani waziwazi ila vitu vinavyochangia pumu ni VIZIO mfano MOSHI WA SIGARA, BANGI, GESI, GARI NA KEMIKALI pia kila mgonjwa wa pumu ana mzio, Zaid ya 25%hupatwa na mafua yanayosababishwa na mzio (HIGH FEVER /ALLERGIC RHINITIS) na kuwashwa macho (ALLERGIC CONJUCTIVITY) pia wanaweza kupata pumu.

Pia mzio unaweza kusababishwa na antibodies zilizo ndani ya damu zinazopelekea njia ya hewa kuvimba na kusababisha pumu, pia Moshi wa SIGARA, MARASHI, NK husababisha pumu pia watu wazima wenye uzito unaozid vimo vyao yaani BMI Kat ya 25 na 30 na wanaopata pumu ukilinganisha na wenye mwili mkubwa pia watoto waliozaliwa kwa njia ya upasuaj na Zaidi watu walio katika stress na pia tatizo la ngozi linalosababishwa na mzio /allergc (ECZEMA /ATOPIC DERMATITIS au pumu ya ngozi ni hatar ktk jamii yetu.

DALILI ZA PUMU

Sio watu wote wenye pumu Wana Dalili HIZI na pia sio watu wote wenye Dalili hizi wana pumu.

~KUKOHOA SANA
~KUTOA SAUTI KAMA YA MLUZI /FILIMBI WAKAT WA KUPUMUA
~KUBANWA NA KIFUA
~KUPUNGUKIWA PUMZI

JINSI YA KUTIBU NA KUJIKINGA NA PUMU

~kuna aina mbil za matibabu ya pumu moja ni ya dawa ambayo husaidia kutanua njia za hewa ambazo zimesinyaa (BRONCHOPDILATORS) pia na matibabu mengine ni kutumia dawa za kotikosteroid za kuvuta (INHALED CORTICOSTEROIDS) ila kwa kawaida matibabu haya huwa chanzo cha magonjwa mbalmbal kutokana na dawa za kemikal hivyo si nzur sana.

NJIA YA KUJIKINGA NA PUMU

NI KUJIKINGA NA Vitu vyenye mzio Kama vile PERFUME, DAWA ZA KEMIKAL, RANGI ZA NYUMBA, KUVUTA SIGARA, PIA EPUKA KUNYWA POMBE NA KUCHEZA NA WANYAMA KAMA PAKA NA MBWA PIA WAZAZI MUACHE KUTUMIA BABY WIPES ZENYE HARUFU KWA WATOTO WENU.

MADHARA YA SHISHA

Yafuatayo ni madhara ya shisha;

1.Kansa
Licha ya kupita ndani ya maji, moshi wa shisha huwa na kiwango kikubwa cha carbon monoxide na nicotine ambazo humfanya mtumiaji awe kwenye hatari kubwa ya Kupata Tatizo la kansa ya koo, ama mapafu.

2.Matatizo ya Moyo
Moshi na tumbaku husababisha mishipa ya damu ya artery Kuziba, Matokeo yakemoyo hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi wake.

3.Huharibu Fizi (periodontal disease)
Hii hutokana na kuongezeka kwa kiasi cha sumu ya nicotine kwenye damu na fizi matokeo yake ni kuharibika kwa fizi na kupata matatizo ya meno.

4. Fangasi na Kifua kikuu (TB)
Kutokana na kutosafishwa vizuri kwa bomba za kuvutia shisha (hasa kutokana na wengi kujali kipato kuliko afya za watu) Mtumiaji hujiweka kwenye hatari kubwa ya Kupata magonjwa ya kuambukizwa kama fangasi, au hata vidonda vya tumbo kwa kuvuta kimelea cha helicobacteria.

5.Kuzaa Njiti (mtoto mwenye uzito mdogo)
Hii ni kwa wanawake wanaotumia shisha wakiwa wajawazito. Pia mtoto huyo ni rahisi kuwa na magonjwa yanayohusiana na upumuaji.

6. “Nicotine Addiction”
Hii ni hali ya kuwa mtumwa wa Sumu ya Nicotine. Mtumiaji wa shisha huvuta kiwango sawa cha nicotine kama mvutaji wa sigara hii husababisha sumu hii hatari kuingia kwenye damu yake, matokeo yake hataweza kuishi bila kutumia shisha au sigara.

7.Kupoteza Uwezo za Kujamiiana.
Utafiti unaonesha kuwa, wanawake wanaotumia shisha hupoteza hamu ya kujamiiana kwa kiasi kikubwa. Hali ni mbaya zaidi kwa wanaume kwani huchangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa nguvu za kiume.

8.Kuchakaa kwa ngozi.
Kama ilivyo kwa watumiaji wa sigara, matumizi ya shisha huchangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa ngozi. Mtumiaji wa muda mrefu wa shisha huzeeka haraka zaidi ya asiyetumia.

9.Asthma na Allergy Zingine
Uvutaji wa shisha huharibu utando laini uliopo kwenye njia za pua na koo, uharibifu huu unaweza kusababisha matatizo ya allergy, na asthma.

10.Kwa kuwa Haina Ladha kama ya sigara, watu wengi (hasa vijana) huona shisha ni mbadala mzuri wa sigara, bangi, na madawa mengine ya kulevya wakihisi haina madhara kumbe wanajiangamiza wenyewe!

Faida na namna ya kutumia mafuta ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele

Faida ya Mafuta Ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele.

1. Yanasaidia kufanya mzunguko wa damu kufanya kazi vizuri kwenye ngozi ya kichwa na kupenyeza hadi kwenye shina ya nywele kisha kuifanya nywele inayoota kuwa imara

2. Yanasaidia kupambana na mba kwenye ngozi ya kichwa

3. Yanasaidia uzalishwaji wa mzizi au shina ya nywele

4. Yanasaidia uzalishwaji wa melanin ambayo inafanya kazi ya kutoa rangi ya nywele inayotakiwa.

5. Yanasaidia kuifanya nywele isiwe kavu sana.

NAMNA YA KUZIHUDUMIA NYWELE:

Unaweza kuchanganya na Mdalasini pamoja na Asali.

1. Olive oil vijiko 2 vya chakula

2. Asali kijiko 1 cha chakula

3. Mdalasini kijiko 1 cha chai

Pasha moto olive oil kisha changanya vyote kwa pamoja pakaa kwenye nywele acha kwa muda wa dakika 20 kisha osha nywele zako na upakae mafuta zikishakauka.

Ninashauri utumie mafuta haya kwenye nywele na ngozi ni mazuri sana. Ukiwa na mba pakaa kwenye ngozi mba itaisha na muwasho utaondoka.

MITAGUSO MIKUU YA KANISA KATOLIKI

MITAGUSO MIKUU

Yesu Kristo aliwakabidhi mitume kumi na wawili uongozi wa Kanisa wakiwa kundi moja lenye mkuu wake, yaani Petro. Vilevile waandamizi wao, yaani maaskofu wote, ni kundi moja na Papa wa Roma ndiye mkuu wao. Huyo peke yake, na kundi la maaskofu likiwa pamoja naye na chini yake, ndio wenye mamlaka ya juu katika Kanisa lote. Mamlaka hiyo inatumika kwa namna ya pekee unapofanyika mtaguso mkuu, yaani mkutano maalumu wa maaskofu uliokubaliwa na Papa kuwa unawakilisha kundi hilo lote. Hakuna uamuzi wa kudumu kuhusu ipi ni mikuu kati ya mitaguso yote iliyofanyika katika historia ya Kanisa. Tangu karne XVI Wakatoliki wataalamu wa sheria za Kanisa wanatoa orodha yao, ambayo kwa sasa ni kama ifuatavyo.

ORODHA YA MITAGUSO MIKUU

• Katika milenia ya kwanza ilifanyika mashariki (Uturuki wa leo):
1. Nisea I (mwaka 325)
2. Kostantinopoli I (381)
3. Efeso (431)
4. Kalsedonia (451)
5. Kostantinopoli II (553)
6. Kostantinopoli III (680-681)
7. Nisea II (787)
8. Kostantinopoli IV (869-870)
• Katika milenia ya pili ilifanyika magharibi (Italia, Ufaransa, Ujerumani, Uswisi na Vatikano ya leo):
9. Laterano I (1123)
10. Laterano II (1139)
11. Laterano III (1179)
12. Laterano IV (1215)
13. Lyon I (1245)
14. Lyon II (1274)
15. Vienne (1311-1312)
16. Konstanz (1414-1418)
17. Firenze (1431-1445)
18. Laterano V (1512-1517)
19. Trento (1545-1563)
20. Vatikano I (1869-1870)
21. Vatikano II (1962-1965)

HISTORIA YA MITAGUSO MIKUU

Mitaguso mikuu ya kwanza ilifanyika hasa ili kubainisha katika mafundisho yaliyogongana yapi yanalingana na imani sahihi. Mwisho wake ulikuwa kutangaza dogma fulani na kutenga na Kanisa watakaokataa kuiamini na watakaofundisha tofauti.
Mitaguso iliyofanyika baada ya farakano la mwaka 1054 kati ya Kanisa la mashariki na la magharibi, pamoja na kulenga umoja uliovunjika na kufundisha dogma mpya, ilishughulikia zaidi urekebisho wa Kanisa katika ngazi na nyanja zote. Kwa namna ya pekee Mtaguso II wa Vatikano tangu uitishwe ulijulikana kuwa wa kichungaji, yaani usio na lengo la kufundisha dogma mpya wala kulaani mafundisho mengine.

Mtaguso I wa Nisea (325)

Mtaguso I wa Nisea ndio mtaguso wa kwanza kuitwa (tangu mwaka 338) mtaguso wa kiekumeni, yaani mtaguso wa dunia yote au mtaguso mkuu. Ndiyo sababu inashika nafasi ya pekee kati ya mitaguso yote.
Uliitishwa na kusimamiwa na kaisari Konstantino Mkuu, aliyehofia mabishano kati ya raia wake Wakristo kuhusu Yesu Kristo, ambayo yalihatarisha umoja na usalama wa Dola la Roma lililoanza kuelekea kusambaratika. Yeye aliwaalika maaskofu wote wa dola, waliokuwa kama 1000 mashariki na kama 800 magharibi. Washiriki walitokea hata nje ya dola hilo, kama vile Persia na Armenia. 2
Katika hali hiyo mtaguso ulianza tarehe 20 Mei 325; washiriki walikuwa kama 318, wengi wao wakitokea upande wa mashariki wa dola hilo. Upande wa magharibi uliwakilishwa na watu 4 kutoka Ulaya na 1 kutoka Afrika. Papa Silvesta I (314-335) aliwakilishwa na mapadri wawili.
Asili ya mabishano ilitokea katika Kanisa la Aleksandria (Misri), ambapo kasisi Arios alikuwa amekanusha umungu wa Yesu, na hivyo alihukumiwa na Sinodi ya Aleksandria ya mwaka 321, iliyoitishwa na askofu Aleksanda wa Aleksandria. Hata hivyo Arios hakuacha mafundisho yake, akakimbilia Palestina kwa rafiki yake Eusebio wa Nikomedia.
Basi, mtaguso ulikiri karibu kwa kauli moja kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu kwa maana ana ousìa (yaani dhati) ileile ya Kimungu aliyonayo Baba. Ndiyo kiini cha Kanuni ya imani ya Nisea iliyopitishwa na mtaguso.
Uamuzi mwingine wa mtaguso ulikuwa kupanga siku ya Pasaka, sherehe kuu ya Kanisa, iwe Jumapili inayofuata mbalamwezi ya kwanza ya majira ya Springi, tofauti na kalenda ya Kiyahudi. Pia zilitungwa kanuni 20 kuratibu mambo mbalimbali.
Mtaguso ulipomalizika tarehe 25 Julai 325, Konstantino alifikiri uamuzi juu ya dogma utamaliza mabishano, lakini haikuwa hivyo, kwa sababu Wagiriki wengi, ingawa hawakukubaliana na Arios, hawakuridhika na msamiati uliotumika kuelezea uhusiano wa Baba na Mwana.

Mtaguso I wa Konstantinopoli (381)

Mtaguso I wa Konstantinopoli ndio wa pili kati ya mitaguso ya kiekumene yaliyofanyika wakati wa mababu wa Kanisa. Uliitishwa na kaisari Theodosius I ukafanyika Konstantinopoli mwaka 381.
Maaskofu 150 waliohudhuria walilaani aina mbalimbali za uzushi, hasa ule wa Masedoni wa Konstantinopoli aliyekanusha umungu wa Roho Mtakatifu, wakathibitisha maamuzi ya mtaguso mkuu wa kwanza (Mtaguso I wa Nisea), uliofanyika mwaka 325.
Hivyo walikiri kwamba Roho Mtakatifu pia, kama vile Yesu Mwana wa Mungu, anachanga dhati ileile ya Baba.
Pamoja na hayo, walikamilisha kanuni ya imani ya Nisea ambayo kwa sababu hiyo inaitwa sasa kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli na ambayo inatumika sana hata leo katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, hasa katika liturujia.

Mtaguso wa Efeso (431)

Mtaguso wa Efeso unahesabiwa na Wakristo walio wengi kama mtaguso mkuu wa tatu. Ulifanyika Efeso katika mkoa wa Asia Ndogo, kwa amri ya kaisari Theodosi II; Papa Selestini I (422-432) alimteua Sirili wa Aleksandria kuuendesha; washiriki walikuwa zaidi ya 150 na kujadili vikali hasa uzushi wa Nestori wa Konstantinopoli.
Patriarki huyo alikuwa anasisitiza ubinadamu wa Yesu Kristo kuliko umungu wake, akisema Bikira Maria alimzaa mtu Yesu, si Mungu, wala si Neno wa Mungu aliyehifadhiwa ndani ya nafsi ya Kristo kama hekaluni. Kwa hiyo Kristo alikuwa Theophoros, yaani “mbeba Mungu”, na Maria Christotokos, “Mama wa Kristo” si Theotokos, “Mama wa Mungu”.
Mtaguso huo ulilaani haraka mafundisho hayo ukikiri kwamba nafsi ya Yesu Kristo ni moja tu, ile ya milele ya Mwana wa Mungu, na kwamba nafsi hiyo ilitwaa ubinadamu kamili wenye mwili na roho. Hivyo Maria ni Theotokos kwa kuwa alimzaa Mungu kama binadamu.
Wajumbe wa Papa walipofika walithibitisha uamuzi huo, lakini maaskofu kutoka Antiokia hawakuridhika, na uzushi huo uliendelea Mesopotamia na kuenea hata Asia mashariki.
Mtaguso ulitangaza kuwa Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli ni kamili ukakataza isibadilishwe kwa namna yoyote. Pia ulilaani Upelaji, uzushi kutoka Ulaya magharibi kuhusu uwezo wa binadamu kutenda mema bila kusaidiwa na neema ya Mungu.

Mtaguso wa Kalsedonia (451)

Mtaguso wa Kalsedonia (leo katika nchi ya Uturuki) unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa nne kati ya mitaguso ya kiekumeni iliyofanyika katika historia ya Kanisa.
Mtaguso huo uliitishwa na kaisari Marcianus wa Dola la Roma Mashariki pamoja na mke wake Pulkeria wa Bizanti miaka 20 baada ya Mtaguso wa Efeso.
Hao waliona haja ya kudumisha umoja wa Wakristo, uliokuwa msingi wa uimara wa dola hilo, hasa wakati huo ambapo makabila yasiyo na ustaarabu kutoka Asia yalikuwa yanajaribu kuteka Ulaya.
Umoja huo uliingia hatari ya kuvunjika kutokana na uamuzi wa mtaguso mkuu wa Efeso kuhusu imani sahihi juu ya Yesu Kristo kutoeleweka kwa namna moja.
Hasa baadhi ya walioshinda mtaguso huo walionekana kusisitiza mno umungu wake hata kutia shaka kama wanaamini sawasawa ubinadamu wake.
Vikao vilianza tarehe 8 Oktoba 451 vikiwa na washiriki zaidi ya 350: mara nyingi inatajwa idadi ya 600 hivi. Hatimaye mafundisho ya Eutike na Dioskoro wa Aleksandria yalilaaniwa.
Ufanisi wa mtaguso ulichangiwa na msimamo wa kaisari Valentiniano III wa Dola la Roma Magharibi, binamu wa Pulkeria. Kaisari huyo alimuunga mkono Papa Leo I (440-461) aliyekuwa ametoa msimamo wake na wa Kanisa la Roma tangu mwaka 449 katika Tomus ad Flavianum, yaani Waraka kwa Flaviano, Patriarki wa Konstantinopoli aliyeuawa na wafuasi wa Eutike. 3
Ingawa msimamo huo wa kati ulikubaliwa na wengi, wengine waliuona ni kinyume cha uamuzi wa Efeso, hivyo walishikilia sana mtazamo hao hata walipodhulumiwa na serikali. Ndiyo asili ya farakano la Misri, Syria, Armenia n.k. linalodumu hata leo.
Mtaguso huo ulitunga pia kanuni mbalimbali, kama vile kwa kumpatia Patriarki wa Konstantinopoli nafasi ya pili kati ya maaskofu wote.

Mtaguso II wa Konstantinopoli (553)

Mtaguso II wa Konstantinopoli uliitishwa na kaisari Justiniani I mwaka 553 kwa lengo la kupatanisha tena na Kanisa Katoliki Wakristo wote wa Misri, Syria n.k. waliojitenga miaka 100 iliyopita kufuatana na Mtaguso wa Kalsedonia.
Kwa ajili hiyo kaisari huyo alifanya yalaaniwe maandishi ya Wanestori watatu (Teodoro wa Mopsuestia, Teodoreto wa Kiro na Iba wa Edesa) yaliyochukiwa sana na Wamisri.
Pia mtaguso mkuu huo ulilaani baadhi ya mafundisho wa Origene.
Walihudhuria maaskofu 168; kati yao 11 walitokea magharibi. Kumbe Papa Vigili (537-555) na maaskofu wengine 12 wa magharibi walikataa kuhudhuria ingawa walikuwepo Konstantinopoli, ila mwaka uliofuata alikubali maamuzi ya mtaguso.
Hatimaye Papa Gregori I (590-604) aliutambua kama mtaguso mkuu kwa sababu haukuharibu kitu. Hivyo Wakristo wengi wanauhesabu kuwa wa tano kati ya mitaguso ya kiekumeni, ingawa lengo halikufikiwa, kwa kuwa Wamisri waliendelea kukataa Mtaguso wa Kalsedonia.

Mtaguso III wa Konstantinopoli (680-681)

Mtaguso III wa Konstantinopoli unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa sita kati ya Mitaguso ya kiekumeni.
Kaisari Konstantino IV wa Konstantinopoli ndiye aliyeuitisha na kuuendesha kuanzia tarehe 7 Novemba 680 hadi tarehe 16 Septemba 681.
Suala kuu lililosumbua Wakristo wa karne VII lilimhusu Yesu Kristo upande wa utashi. Ulikuwa unaenea mtazamo wa kwamba hakuwa na utashi wa kibinadamu, bali ule wa Kimungu tu.
Lakini wamonaki Sofronio wa Yerusalemu na Maksimo Muungamadini walipinga vikali jaribio hilo la kuleta upatanisho wa Waorthodoksi wa Mashariki (Wamisri n.k.) kwa kumpunguza Yesu katika ubinadamu wake kamili uliosisitizwa na Mtaguso wa Kalsedonia (451).
Vilevile Papa Martin I (649-655), katika mtaguso uliofanyika Laterani, alilaani mtazamo huo, kinyume cha Kaisari na Patriarki wa Konstantinopoli.
Konstantino IV alikubaliana na Papa Agatoni (678-681), na hivyo Mtaguso III wa Konstantinopoli ulilaani rasmi mtazamo wa kwamba Yesu hakuwa na utashi wa kibinadamu.

Mtaguso II wa Nisea (787)

Mtaguso II wa Nisea uliitishwa na malkia Irene wa Bizanti mwaka 787 ili kujadili matumizi ya sanamu katika Ukristo, kutokana na ombi la Papa Adrian I (772-795).
Wakristo wengi wanauhesabu kuwa wa saba kati ya Mitaguso ya kiekumeni. Ni wa mwisho kufanyika wakati wa mababu wa Kanisa.
Mtaguso mkuu huo ulihitajika ili kumaliza mabishano makali kuhusu sanamu za Kikristo yaliyochukua zaidi ya miaka 100 hasa katika Dola la Roma Mashariki yakimalizika mwaka 843 tu.
Chanzo ni uamuzi wa kaisari Leo III wa Konstantinopoli (717-741) wa kuteketeza sanamu zote ili kujilinganisha na Waislamu waliotishia utawala wake.
Patriarki wa Konstantinopoli alilazimika kujiuzulu, lakini uamuzi wa kaisari ulizidi kupingwa hasa na wamonaki na mwanateolojia Yohane wa Damasko. Mapapa wa Roma pia walipinga uamuzi huo.
Sera ya dola ilibadilika aliposhika uongozi Irene kwa niaba ya mtoto wake mdogo Konstantino VI.
Mtaguso ulianza Konstantinopoli mwaka 786, lakini ulipoingiliwa na jeshi waliowaunga mkono maaskofu wengi waliopinga sanamu, Irene aliuhamishia Nisea ambapo vilifanyika vikao 7 kuanzia tarehe 28 Septemba 787. Cha mwisho kilifanyika katika ikulu tarehe 23 Oktoba 787.
Pamoja na maaskofu 300 hivi wa dola hilo, walihudhuria wamonaki wengi. Papa alituma mabalozi wake wawili na barua moja.
Mtaguso ulitofautisha heshima inayokubalika kwa sanamu na ibada isiyovumilika. Hoja kuu ni kwamba sanamu si kitu, ila inamwakilisha yule aliyechorwa ndani yake. Kimsingi sanamu zinakubalika kutokana na umwilisho wa Mwana wa Mungu uliomfanya atwae sura na kuonekana.
Mtaguso ulichukua pia maamuzi mbalimbali ili kurekebisha Kanisa.

Mtaguso IV wa Konstantinopoli (869-870)

Mtaguso IV wa Konstantinopoli ni jina linalotumiwa na Wakristo kwa namna tofauti, kadiri wanavyokubali au kukataa uhalali na uekumeni wa mitaguso fulanifulani.
Kanisa Katoliki linahesabu kuwa Mtaguso Mkuu IV wa Konstantinopoli ule uliofanyika tangu tarehe 5 Oktoba 869 hadi 28 Februari 870.
Uliitishwa na Kaisari Basili I wa Konstantinopoli na Papa Adrian II (867-872), kwa sababu mwisho wa ikonoklastia katika sinodi ya mwaka 843 ulikuwa umeacha athari kubwa katika Kanisa la Mashariki. 4
Patriarki Metodi wa Konstantinopoli (843-847) alijitahidi kutuliza pande zote, lakini hakufaulu.
Alipofariki, malkia Teodora, akitawala kwa niaba ya mtoto Mikaeli III, alilazimisha nafasi yake ishikwe na Ignas I, mmonaki mwenye msimamo mkali, ambaye hatimaye aliondoshwa.
Badala yake alichaguliwa mlei msomi Fosyo ambaye kwa siku chache alipewa daraja na kutawazwa, lakini kufikia Februari 859 lililotea farakano kati ya waliomkubali yeye na waliomkubali Ignas I.
Ndipo Fosyo alipojitahidi kuungwa mkono na Papa Nikolaus I (858-867), ambaye kwanza alimkubali pamoja na pendekezo la Kaisari Mikaeli III la kuitisha mtaguso uliofanyika Konstantinopoli kati ya Aprili na Agosti 861 wakihudhuria maaskofu zaidi ya 300.
Papa hakupendezwa na maamuzi ya mtaguso huo, akashindana na Kaisari kimaandishi kwa sababu za kiutamaduni na za kisiasa pia.
Hapo Fosyo alipata nguvu dhidi ya Papa akaitisha mtaguso uliovunja umoja kati ya Makanisa ya Mashariki na yale ya Magharibi mwaka 867, akithubutu kwa mara ya kwanza kumhukumu Papa kama mzushi na kutaka kumuondoa madarakani.
Kumbe Kaisari mpya alimrudisha Ignas I kuwa Patriarki na pamoja naye akamuomba Papa atume mabalozi kwa mtaguso mwingine wa kufanyika Konstantinopoli.
Mtaguso ulipoanza tarehe 5 Oktoba 869 walikuwepo tu maaskofu wakuu 5 na maaskofu wengine 7, lakini walikuwepo mabalozi wa Mapatriarki wa Antiokia na Yerusalemu (wale wa Aleksandria walifika baadaye).
Waliokuwa upande wa Fosyo walikubaliwa kuhudhuria kuanzia tarehe 7 Oktoba wakamtetea sana dhidi ya msimamo wa Papa, lakini wakashindwa na kutengwa (29 Oktoba).
Baada ya miezi mitatu mtaguso uliendelea tarehe 12 Februari 870, wakiwepo maaskofu 67 walioongezeka tena hadi kufikia 103 siku ya mwisho (28 Februari), lilipotolewa tamko la imani pamoja na kanuni 26 kuhusu teolojia na sheria, bila kutoa mafundisho mapya. Pamoja na idadi yenyewe kutokuwa kubwa sana, ni muhimu kwamba walikuwepo maaskofu wakuu 37 kati ya 40.
Kwa kuwa mtaguso huu haukukubaliwa sana huko Konstantinopoli (hasa baada ya Fosyo kurudia Upatriarki mwaka 877), na pande mbili zilishindwa zaidi na zaidi kuelewana, uliitishwa mtaguso mwingine, ambapo wafuasi wa Fosyo walikuwa ndio wengi.
Baadhi ya Waorthodoksi wanahesabu mtaguso huo mpya (879-880), uliofuta maamuzi dhidi ya Fosyo, kuwa wa kiekumeni na kuukataa ule wa miaka 10 ya nyuma. Lakini wengine hawakubali kuwa wa kiekumeni kwa sababu haukutoa mafundisho ya imani.
Ingawa wajumbe wa Papa Yohane VIII (872-882) walikubali kwanza maamuzi wa mtaguso huo ili kudumisha amani, na labda hata yeye mwenyewe, waandamizi wake waliukataa, na Fosyo mwenyewe aliondoshwa tena mwaka 886.

Mtaguso I wa Laterano (1123)

Mtaguso I wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki mtaguso mkuu wa tisa katika historia yake, wa kwanza kufanyika Magharibi. Ulianza tarehe 18 Machi ukamalizika tarehe 11 Aprili 1123.
Mahali pake ni kwenye Kanisa Kuu la Roma (Italia) katika mtaa wa Laterano, alipokuwa anaishi askofu wake. Hukohuko baadaye ilifanyika mitaguso mingine minne ya Karne za Kati, halafu umuhimu wake ukapungua Papa alipohamia Vatikano.
Mtaguso uliitishwa na Papa Kalisti II (1119-1124) mnamo Desemba 1122, mara baada ya Mapatano ya Worms, ya kwanza kufanyika kati ya Papa na Dola Takatifu la Kirumi, iliyofurahisha sana wanakanisa, hata mwaka huo ulitajwa kuwa mwanzo wa kipindi kipya.
Mapatano hayo yalikomesha desturi ya walei kuteua viongozi wa Kanisa na wa utawa, yakitenganisha shughuli za kiserikali na zile za kidini, na kukubali kwamba mamlaka ya kiroho inatokana na daraja takatifu.
Ili kuthibitisha mapatano hayo, Papa alialika Roma maaskofu wote wa Magharibi. Waliohudhuria kweli walikuwa zaidi ya 900 kati ya maaskofu zaidi ya 300 na maabati 600 hivi). Papa mwenyewe aliendesha vikao.
Hakuna hati za mtaguso, ila matunda yake. Tunachojua ni kwamba Mapatano hayo yalisomwa yakapitishwa rasmi, pamoja na kanuni 22 au 25, ambazo nyingi zilikuwa zimeshapitishwa zamani.

Mtaguso II wa Laterano (1139)

Mtaguso II wa Laterano, uliofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 11 Aprili 1139 chini ya Papa Inosenti II (1130-1143), unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi. Ni wa pili kufanyika Magharibi, kwenye Kanisa kuu la Roma (Italia).
Mtaguso ulihitajika kutokana na farakano lililotokea mwaka 1130 alipofariki Papa Honori II (1124-1130): hapo makardinali waligawanyika kuhusu Mapatano ya Worms, ambayo mwaka 1122 yalikuwa yamekomesha mashindano kuhusu uteuzi wa maaskofu.
Isitoshe, kulikuwa na ushindani kati ya koo mbili za Roma, yaani Frangipane na Pierleoni.
Tarehe 14 Februari 1130, makardinali 16 waliosimama upande wa familia ya Frangipane walimchagua Gregorio Papareschi, aliyejiita Papa Inosenti II. Saa chache baadaye, Pietro Pierleoni alichaguliwa na makardinali wengine na kujiita Anakleti II.
Hatimaye, kwa msaada wa Bernardo wa Clairvaux, Inosenti II alishinda na kukubaliwa na wengi, ingawa hakuweza kuhamia Roma mpaka baada ya mpinzani wake kufa (1138). 5
Mtaguso ulipaswa kurekebisha matokeo ya farakano hilo. Basi, Inosenti II alifungua kikao na kuondoa madarakani maaskofu waliomfuata mpinzani wake.
Halafu papa alikusudia kuendeleza juhudi za urekebisho za Mtaguso I wa Laterano. Hivyo zikapitishwa kanuni 30, ambazo nyingi kati yake zilikuwa za kurudia zile za zamani kuhusu usimoni, mapadri wenye wake n.k.

Mtaguso III wa Laterano (1179)

Mtaguso III wa Laterano uliitishwa na Papa Aleksanda III (1159-1181) ufanyike huko Roma mwaka 1179, kutokana na Amani ya Venezia kati ya Kaisari Federiko I wa Ujerumani na Lega Lombarda ya Italia kaskazini.
Unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na moja. Ulijadili masuala mbalimbali na kuyatungia kanuni. Kati ya maamuzi muhimu zaidi, mmojawapo ulihusu uchaguzi wa Papa, ukidai thuluthi mbili za kura za makardinali wote, bila kutofautisha haki za makundi yao matatu.

Mtaguso IV wa Laterano (1215)

Mtaguso IV wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na mbili.
Uliitishwa na Papa Inosenti III (1198-1216) kama kilele cha kazi yake.
Ulihudhuriwa na maaskofu zaidi ya 400 (wakiwemo mapatriarki wa Kilatini wa Konstantinopoli na Yerusalemu na wawakilishi wa wale wa Antiokia na Aleksandria), na wakuu wa watawa zaidi ya 800, mbali na mabalozi wa watawala wa nchi mbalimbali.
Mada kuu zilikuwa Vita vya msalaba, Mashindano kuhusu uteuzi wa viongozi wa Kanisa, mamlaka ya Papa, mwenendo wa makleri, mashirika ya kitawa, imani (kuhusu ekaristi n.k.) na wajibu wa Wakristo wote kupokea sakramenti ya kitubio walau mara moja kwa mwaka.
Kutokana na wingi na umuhimu wa mafundisho na maamuzi yaliyotolewa, mtaguso huo unahesabiwa kuwa kati ya ile iliyoathiri zaidi Kanisa hadi leo.

Mtaguso I wa Lyon (1245)

Mtaguso I wa Lyon uliitishwa na Papa Inosenti IV (1243-1254) tarehe 24 Juni 1245 akiwa huko Lyon (Ufaransa), alipokimbilia usalama. Waliushiriki karibu viongozi 150 wa Kanisa Katoliki, ambalo linauhesabu kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tatu.
Baada ya mashindano makali kati ya mamlaka ya kiroho ya Papa na ile ya kisiasa ya kaisari huko Ulaya, mtaguso huo uliitishwa ili kumhukumu moja kwa moja kaisari Federiko II kuwa Mpinga Kristo.
Mtaguso ulianza tarehe 28 Juni 1245 wakiwepo maaskofu 144, halafu ukawa na vikao viwili vingine tena tarehe 5 Julai na 17 Julai. Hatimaye maaskofu walikuwa 225.
Mwanzoni papa alitangaza matatizo 5 yanayotesa Kanisa:
• kuharibika kwa imani na maadili;
• kushindwa kuikomboa Nchi takatifu (Yerusalemu ulitekwa tena na Waturuki mwaka 1244);
• kudumu kwa farakano la Waorthodoksi;
• kujitokeza hatari ya kuvamiwa na Watartari;
• kupambana na Federiko II.
Maamuzi yalitangazwa tarehe 25 Agosti tu, baada ya papa na wasaidizi wake kurekebisha miswada, yakapokewa na kufafanuliwa na vyuo vikuu. Lakini uamuzi wa kumuondoa madarakani kaisari haukuweza kutekelezwa hata kwa vita.

Mtaguso II wa Lyon (1274)

Mtaguso II wa Lyon unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na nne. Ulikusudiwa hasa kurudisha umoja kamili kati ya Wakatoliki na Waorthodoksi, uliotafutwa katika karne XIII yote.
Mnamo Februari 1274, katika ikulu ya Konstantinopoli, kaisari Mikaeli VIII ilifaulu kufanya maaskofu wengi wakiri ungamo la imani lililodaiwa na Papa Klementi IV (1265-1268).
Ndipo Papa Gregori X (1271-1276) alipoitisha mtaguso huko Lyon, ambao uhudhuriwe na wawakilishi wa Waorthodoksi ili kukamilisha umoja.
Papa Gregori X alifungua mtaguso tarehe 7 Mei 1274 akitangaza tena malengo yake matatu:
• kusaidia Wakristo wa Nchi takatifu,
• kuungana tena na Waorthodoksi,
• kurekebisha maadili ndani ya Kanisa.
Vilifuata vikao viwili tarehe 18 Mei na 4 Juni. Halafu tarehe 24 Juni ulifika na kupokewa kwa shangwe ujumbe kutoka Ugiriki, ukiundwa na maaskofu 2 na katibu wa kaisari.
Tarehe 6 Julai kilifanyika kikao cha nne kwa ajili ya muungano na hatimaye tarehe 16 Julai kile cha mwisho kilichopitisha hati mbalimbali za urekebisho. Kesho yake mtaguso ulifungwa.
Muungano haukuweza kudumu, kwa sababu, alivyoandika Papa Paulo VI (1963-1978) tarehe 19 Oktoba 1974, ulifanyika «bila kulipatia Kanisa la Kigiriki nafasi ya kutokeza kwa hiari mtazamo wake kuhusu jambo hilo. Wakristo wa Kilatini ndio waliotunga hati na matamko kufuatana na mafundisho juu ya Kanisa yaliyofafanuliwa na kupangwa magharibi». 6
Mikaeli VIII alijaribu kulazimisha raia zake wapokee mambo wasiyoyakubali kwa moyo, hata akatumia nguvu kuwadhulumu waliokataa; akilaumiwa na watu wa Roma kwa kushindwa kufanikisha muungano, akaja kutengwa na Kanisa. Alipokufa (1282), mwanae Androniko II aliyemrithi, alifuta maamuzi ya baba yake kwa ajili ya muungano.
Vilevile mipango kwa ajili ya vita vya msalaba haikutekelezwa, na hatimaye (1291) Waturuki waliteka Akri, mji wa mwisho kubaki mikononi mwa Wakristo huko Mashariki ya Kati.
Maamuzi mengine yalihusu utaratibu mpya wa kumchagua Papa kwa lengo la kuzuia uchelewaji uliojitokeza hapo nyuma, na katazo la mashirika mapya ya kitawa.

Mtaguso wa Vienne (1311-1312)

Mtaguso wa Vienne unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na tano.
Mtaguso huu ulifanyika Vienne (Ufaransa) baada ya mashindano kati ya Papa Bonifas VIII (1294-1303) na mfalme wa Ufaransa Filipo IV.
Hatimaye mwaka 1309 mwandamizi wake, Papa Klementi V (1305-1314) alikubali kubaki Avignon (leo nchini Ufaransa), karibu na himaya ya mfalme huyo.
Mapapa walibaki huko hadi mwaka 1377, waliporudi Roma.
Kwa shinikizo la mfalme, Papa alitoa hati Regnans in excelsis (12 Agosti 1308) ili kuitisha mtaguso mkuu huko Vienne tarehe 1 Novemba 1310, kwa lengo la kujadili mada 4:
• suala la Wahekalu;
• vita vya msalaba;
• hali ya imani na Kanisa kwa jumla;
• urekebisho wa Kanisa.
Mtaguso ulichelewa kuanza hadi tarehe 16 Oktoba 1311, walipokuwepo washiriki 170 hivi, ambao kati yao Wafaransa walikuwa zaidi ya thuluthi moja. Wengine walizuiwa na mfalme wa Ufaransa.
Vikao rasmi vikawa vitatu hadi Machi 1312.
Kuhusu Wahekalu, mtaguso uliamua kufuta shirika lao kama alivyopenda mfalme, bila kulifanyia utafiti wala kulitolea hukumu.
Kuhusu Vita vya Msalaba, uliamua kuvianza upya na kwa ajili hiyo kutoza zaka kwa miaka sita, lakini mfalme alijitwalia hizo pesa bila kutekeleza ahadi yake ya kuongoza vita hivyo.
Kuhusu imani, ulijadili baadhi ya mafundisho hasa ya makundi kadhaa ya watawa, lakini uamuzi ulichukuliwa baadaye tu.
Kuhusu urekebisho, ulidai haki za Kanisa ziheshimiwe na serikali za nchi. Pia ulijadili kirefu mahusiano ya ndani, hasa kati ya maaskofu, maparoko na watawa.

Mtaguso wa Konstanz (1414-1418)

Mtaguso wa Konstanz (Ujerumani) unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na sita. Uliitishwa na antipapa Yohane XXIII kwa ombi la kaisari Sigismund wa Ujerumani ukathibitishwa na Papa Gregori XII (1406-1415).
Lengo kuu lilikuwa kumaliza Farakano la Magharibi lililofikia hatua ya kuona maaskofu watatu kujidai Papa kwa wakati mmoja. Malengo mengine yalikuwa kung’oa uzushi na kurekebisha Kanisa “katika kichwa na viungo vyake”.
Hatimaye Papa Gregori XII alikubali kujiuzulu, wapinzani wake wawili waliondolewa, na Papa Martin V akachaguliwa.
Ulikuwa mtaguso muhimu kwa wingi wa waliohudhuria (makardinali 29, maaskofu 186, maabati zaidi ya 100 na wataalamu 300 hivi), muda (vikao 55) na mafanikio, ingawa majaribio yake ya mapinduzi yalishindikana, hasa ulipodai kuwa na mamlaka ya juu kuliko Papa.
Kati ya maamuzi mengine kuna hukumu dhidi ya John Wyclif na Jan Hus kama wazushi.

Mtaguso wa Firenze (1431-1445)

Mtaguso wa Firenze uliitishwa na Papa Martin V (1417-1431) mwaka wa mwisho wa uongozi wake ili kutekeleza shingo upande agizo la Mtaguso wa Konstanz la kwamba mtaguso ufanyike mara kwa mara.
Mtaguso ulianza Basel (Uswisi) chini ya Papa Eugenio IV (1431-1447), ukiwa na maaskofu wachache kulingana na mapadri na walei wenye haki ya kupiga kura.
Ingawa mtaguso ulifaulu kupatanisha wafuasi wa Hus na Kanisa, na kutoa sheria kadhaa za urekebisho kwa kibali cha Papa, baadaye ulianza kumshambulia yeye pamoja na makardinali, ukionyesha wazi wengi waliuona una mamlaka ya juu kuliko Papa, kinyume cha mapokeo.
Hapo Eugenio IV aliuvunja halafu akauhamishia Ferrara (Italia), ulipokutanika tarehe 8-1-1438, bila kujali upinzani wa wale ambao walibaki Basel na kumchagua antipapa wa mwisho, Felix V.
Huko Italia ulifika ujumbe mkubwa kutoka Konstantinopoli kwa ajili ya kurudisha umoja kati ya Kanisa Katoliki na Waorthodoksi. Kati ya wajumbe 700 kulikuwa na kaisari na patriarki wa Konstantinopoli, walioogopa Waturuki watateka mji wao (kama ilivyotokea kweli tarehe 29 Mei 1453); hivyo walihitaji msaada wa Wakristo wenzao wa magharibi.
Ferrara iliachwa kutokana na uhaba wa majengo na hofu ya tauni. 7
Mwaka 1439 mtaguso ulihamia Firenze ukafikia makubaliano ya kurudisha umoja (6-7-1439), ingawa uamuzi ukashindwa kutekelezwa kwa kiasi kikubwa kutokana na upinzani wa waumini wa Konstantinopoli.
Vilevile tarehe 22-11-1439 yalifikiwa makubaliano na Waarmenia na tarehe 4-2-1440 yale na Wamisri.
Hatimaye tarehe 24-9-1443 mtaguso ulihamia Roma kwenye Laterano. Huko yalifikiwa makubaliano ya kurudisha umoja na Wasiria kadhaa (30-4-1444) na Wakaldayo na Wamaroni wa Kupro (7-8-1445).
Hakuna hati kuhusu mwisho wa mtaguso. Lakini waliobaki Basel na kujitenga na Papa, kufikia tarehe 19-4-1449 walimkubali Nikolaus V na siku sita baadaye walifunga mkutano wao.
Mtaguso huo ulichochea Wakristo wa magharibi kutamani mawasiliano na wenzao wa Ethiopia na India, jambo lililowafanya waanze zile safari za mbali kupitia baharini zilizowafikisha Afrika Kusini na Mashariki, China na Amerika.

Mtaguso V wa Laterano (1512-1517)

Mtaguso V wa Laterano ulifanyika kuanzia mwaka 1512 hadi 1517 huko Roma. Kanisa Katoliki linauhesabu kama mtaguso mkuu wa kumi na nane.
Uliitishwa na Papa Julius II (1503-1513) ambaye alianza kuusimamia tarehe 3 Mei 1512. Baada ya kifo chake, uliendelezwa na Papa Leo X (1513-1521) hadi kikao cha 12 na cha mwisho kilichofanyika tarehe 16 Machi 1517.
Ulihudhuriwa na maaskofu 100 hivi, wengi wao wakitokea Italia. Kutofika kwa wajumbe kutoka nchi nyingine, pamoja na wengi kukosa nia ya kujirekebisha, kulichangia kufanya utekelezaji wa maamuzi ya mtaguso ushindikane.
Maamuzi hayo yalitolewa kwa hati za Papa. Mengine yanahusu mafundisho ya imani, mengine maagizo ya urekebisho wa Kanisa.
Kabla yake kilifanyika “Kitaguso” cha Pisa: kwa kuwa Papa Julius II alikuwa hatekelezi kiapo chake cha kuitisha mtaguso kwa ajili ya urekebisho, baadhi ya makardinali, wakihimizwa na watawala wa Ujerumani na Ufaransa, waliuitisha huko Pisa (Italia) kuanzia tarehe 1 Septemba 1511. Walikusanyika wachache tarehe 1 Oktoba, halafu katika kikao cha nane walimsimamisha Papa wakahamia Lyon (Ufaransa).
Papa aliitikia “kitaguso” hicho kwa hati ya tarehe 18 Julai 1511, ambayo pamoja na kukipinga na kujitetea aliitisha mtaguso mkuu ukusanyike tarehe 19 Aprili 1512 huko Laterano.
Vita vilichelewesha mwanzo wa mtaguso wenyewe hadi tarehe 3 Mei 1512, walipokusanyika katika basilika la Laterano makardinali 15, mapatriarki 2, maaskofu wakuu 10, maaskofu 56, maabati na wakuu wa mashirika ya kitawa wachache pamoja na mabalozi wa nchi 3. Mwisho walikuwepo makardinali 23 na maaskofu 122.
Upande wa matokeo, utekelezaji wa maagizo ya mtaguso ulikuwa mdogo sana, la sivyo pengine Matengenezo ya Kiprotestanti yasingetokea. Ukweli ni kwamba Martin Luther aliyaanzisha miezi sita tu baada ya mtaguso kwisha.

Mtaguso wa Trento (1545-1563)

Mtaguso wa Trento (uliofanyika kwa kwikwi kuanzia mwaka 1545 hadi 1563), unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tisa.
Mtaguso huo, uliochukua muda mrefu kuliko yote ya historia, ulieneza urekebisho wa Kanisa na kuchukua msimamo kuhusu mafundisho ya Waprotestanti waliojitokeza katika hiyo karne XVI.
Mtu wa kwanza kulilia mtaguso ambao uamue kati yake na papa alikuwa Martin Luther (1517): huko Ujerumani ombi lake liliungwa mkono na wengi, pamoja na kaisari Karolo V aliyeuona kuwa njia ya kurekebisha Kanisa lakini pia ya kujiimarisha kimamlaka. Ndiyo sababu kuu iliyomfanya Papa Klementi VII (1523-1534), aliyesimama upande wa Ufaransa, kukataa kabisa kuuitisha.
Wazo hilo lilipata nguvu tena chini ya mwandamizi wake, Papa Paulo III (1534-1549), ambaye mwaka 1536 aliitia kwanza Mantova halafu Vicenza maaskofu na maabati wote, pamoja na wafalme wadogo wengi wa Dola takatifu la Kijerumani.
Baada ya juhudi mbalimbali kushindikana, mwaka 1542 uamuzi ulifikiwa wa kuitisha mtaguso huko Trento kwa sababu ni mji wa Italia lakini ulikuwa ndani ya mipaka ya dola hilo. Hatimaye (Novemba 1544) papa aliweza kutoa hati ya kuitisha mtaguso inayoitwa Laetare Jerusalem.
Mtaguso ulifunguliwa rasmi tarehe 13 Desemba 1545 katika kanisa kuu la Mt. Vigilio.
Mwanzoni mtaguso ulikuwa na maaskofu wachache, karibu wote kutoka Italia, ukatawaliwa na wajumbe wa papa. Kati ya makardinali wapya (Contarini, Sadoleto, Carafa, Fisher na huyo Pole) wengi walipenda urekebisho.
Zilijadiliwa na kupitishwa hasa dogma dhidi ya mafundisho ya Waprotestanti, kama vile kuhusu utakaso na wokovu. Pamoja na kupitisha tafsiri rasmi ya Biblia katika Kilatini iliyo maarufu kwa jina la Vulgata, kati ya maamuzi muhimu zaidi upo ule wa kudai maaskofu waishi katika majimbo yao ili kufanya uchungaji uliowapasa.
Baada ya mtaguso kuhamishiwa Bologna, Papa Paulo III aliusimamisha mnamo Septemba 1549.
Papa Julius III (1550-1555) aliuitisha tena kuanzia tarehe 1 Mei 1551 na zikatolewa hati juu ya sakramenti za Ekaristi, Kitubio na Mpako wa wagonjwa. Polepole waliohudhuria waliongozeka, 8
wakiwemo Waprotestanti wengi pia, wakidai wanateolojia wao wawe na haki ya kupiga kura na hati zilizokwishatolewa zifutwe. Ndipo ilipoonekana wazi kwamba tofauti katika imani ni kubwa mno.
Majeshi ya Kiprotestanti yalipokaribia Trento, Papa alikubali kusimamisha tena mtaguso tarehe 28 Aprili 1552.
Sehemu ya mwisho ya mtaguso baada ya kuitishwa ilichelewa kuanza hadi tarehe 18 Januari 1562, tena ilikabili matatizo mengi, lakini iliokolewa na kutawaliwa na askofu wa Milano Karolo Borromeo, mpwa wa Papa Pius IV (1559-1565) aliyemalizia haraka mtaguso wakiwemo wajumbe 255.
Katika sehemu hiyo yalitolewa mafundisho rasmi kuhusu Misa, Daraja takatifu na Ndoa, Toharani, sala kwa watakatifu, heshima kwa masalia na rehema. Pia Kanisa la Roma lilikubaliwa kama mama na mwalimu wa makanisa yote. Maaskofu wote walitakiwa kuahidia utiifu kwa Papa, ambaye peke yake ana haki ya kuitisha mtaguso mkuu. Kwa msingi huo, mtaguso ulimuachia Papa kuthibitisha maamuzi yote, naye alifanya hivyo bila kujali upinzani wa maofisa wake huko Roma.
Isitoshe, mwishoni, maamuzi mbalimbali yaliachwa mikononi mwa Papa na ofisi zake, yakachukuliwa miaka iliyofuata; kati yake, urekebisho wa Breviari na Misale, kwa kusawazisha liturujia za majimbo ya magharibi (isipokuwa chache, kama ya Milano na Lyon) kulingana na mapokeo ya Roma. Halafu ikatolewa Katekisimu ya Trento na Orodha ya vitabu vilivyokatazwa (Index librorum prohibitorum).

Mtaguso I wa Vatikano (1869-1870)

Mtaguso I wa Vatikano unatazamwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa ishirini katika historia yake.
Uliitishwa rasmi na Papa Pius IX (1846-1878) mnamo 29 Juni 1867 na vikao vyake viliendelea katika Basilika la Mt. Petro huko Vatikano mjini Roma kuanzia tarehe 8 Desemba 1869 hadi vilipokatika mnamo 1870, kutokana na jeshi la Italia kuteka Roma tarehe 20 Septemba.
Walishiriki maaskofu na mapadri 774 (kati ya 1050 wenye haki ya kuhudhuria), ambao kwa mara ya kwanza walitokea mabara yote. Pia ilikuwa mara ya kwanza ya kutokuwepo wawakilishi wa serikali. Kumbe wajumbe wa Waorthodoksi na wa Waprotestanti walialikwa pia, lakini hawakufika.
Tarehe 24 Aprili 1870, baada ya majadiliano mengi, ilipitishwa hati Dei Filius juu ya Mungu, ufunuo, imani, na uhusiano kati ya imani na akili.
Ingawa lengo halikuwa hilo, tokeo kuu la kazi ya mtaguso huo ni tangazo la dogma ya Papa kuwa na karama ya kutokosea katika mafundisho ya imani na maadili anayoyatoa ili yadumu moja kwa moja pale anapotimiza masharti fulani (kwa kifupi: akisema “ex cathedra”, yaani “kutoka ukulu).
Dogma hiyo iliimarisha mamlaka ya Papa na umoja wa Kanisa dhidi ya maelekeo ya kitaifa ambayo yalitawala karne zilizotangulia yakisababisha matatizo mengi.

Mtaguso II wa Vatikano (1962-1965)

Malengo ya Mtaguso II wa Vatikano

Muda mfupi baada ya kuchaguliwa Papa, mwenye heri Yohane XXIII alitangaza uamuzi wake wa kuitisha mtaguso mkuu akiamini kwamba utaweza kuandaa na kusababisha ustawi mpya wa maisha ya Kanisa. Lengo kuu la mtaguso lilikuwa kuliamsha Kanisa likumbuke wito wake na kwa kujifanya upya kwa ndani lipate msukumo mpya wa kimisionari ili kuwatangazia watu wote ujumbe wa milele wa wokovu, amani na umoja.
Tangazo hilo lilitolewa tarehe 25-1-1959. Baada ya maandalizi, Mtaguso II wa Vatikano ulifunguliwa tarehe 11-10-1962. Vikao vinne vikafanyika mpaka ulipofungwa tarehe 8-12-1965. Kila kikao kilianza Oktoba na kumalizika Desemba ya miaka hiyo.
Kwa kuwa Yohane XXIII alifariki tarehe 2-6-1963, vikao vitatu vya mwisho viliongozwa na mwandamizi wake, Paulo VI, na hati zote kumi na sita zikatolewa chini yake pia kwa kupigiwa kura ya ndiyo karibu kwa kauli moja. Maaskofu na wakuu wa mashirika kadhaa wenye haki ya kupiga kura walikuwa kama elfu tatu, wakiwakilisha karibu Kanisa lote duniani, isipokuwa nchi zile zenye kuwadhulumu Wakristo.
Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About