Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Ufuta Na Jam

VIAMBAUPISHI

Unga vikombe 2

Sukari ya kusaga 1/4 Kikombe

Siagi 250 gms

Jam kisia

Ufuta kisia

Vanilla 1 kijiko cha chai

MAPISHI

Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai, sukari na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri.
Tia baking powder, na unga na changanya kwa mkono vizuri.
Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni.
Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam, halafu juu yake paka mayai na unynyuzie ufuta.
Pika katika moto wa chini 350ºF kwa muda wa dakika 20-25.
Tayari kwa kuliwa.

Nia yako isishindwe

Nimejifunza jambo kubwa sana ambalo sote tuna lijua nalo ni “NIA”.
Nimemtazama mwendesha pikipiki anaiwasha pikipiki kwa muda mrefu kwa kupiga kiki kwa kurudia rudia, akiamini lazima iwake ili aende anakotaka kwenda. Anajaribu kuwasha kwa kiki ikikataa anajaribu kwa starter, ikigoma anajaribu kuchomoa plug na kuangalia kama kuna tatizo, anajaribu tena na tena mpaka inawaka, anaanza safari yake.

Ingawa ametumia muda mwingi kuhangaika kuiwasha pikipiki yake lakini hakuzimia moyo na kuamua kuitelekeza ili atembee kwa miguu, ila alikua na “NIA” isiyozimika haraka mpaka atakapoona imewaka kwakua anaamini jana iliwaka, lazima na leo iwake hata kama imelala kwenye hali ya hewa ya namna gani.

Ikiwa tunakua na “NIA” ya kufanya mambo madogo madogo yatokee, na tunayasimamia kwa “IMANI” kabisa mpaka yanakua kweli, kwanini tunaogopa kusimamia mambo makubwa yatokee maishani mwetu?. Kwanini unadiriki kusema kwenu hakuna aliyewahi kufanikiwa, hakuna anae miliki gari ya thamanani, hakuna aliyejenga nyumba ya kifahari, hakuna…hakuna….

Kwanini “NIA” yako uilinganishe na kushindwa kwa hao wengine kwenu? Wewe ni mmoja wa tofauti, na ukiamua kujitenga kifikra mbali nao, na kufanya mambo makubwa kwa bidii bila kuzimia moyo, hakika utakua wewe kama wewe kuitwa MABADILIKO ya mafanikio katika hao wengi walioshindwa.

“NIA YAKO ISISHINDWE”

Mapishi ya wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Nyama Ng’ombe Na Mchicha

Wali Wa Mpunga

Mchele wa mpunga – 4 Vikombe

Tui la nazi – 6 vikombe

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele kisha

Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi.

Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.

Mchuzi wa nyama Ng’ombe

Nyama – 1 kilo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa -2 viijiko vya supu

Viazi/mbatata – 2

Kitunguu maji kilokatwakawa (slice ndogo) – 2

Nyanya/tungule – 4

Nyanya kopo – 3 vijiko vya supu

Majani ya mchuzi/mvu – 3 msongo (bunches)

Bizari ya mchuzi (simba 2) – I kijiko cha chai

Ndimu – 1 kamua

Mafuta – ¼ kikombe

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Weka nyama katika sufuri, tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi, ndimu na chemsha nyama hadi iwive na ibakie supu yake kidogo.
Weka mafuta katika sufuri nyingine, kaanga kitunguu. Vinapogeuka rangi tia majani ya mchuzi endelea kukaanga hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown)
Tia nyanya/tungule, viazi/mbatata, endelea kukaanga mpaka nyanya ziive.
Tia nyama na supu yake kisha tia nyanya ya kopo, kotmiri, bizari ya mchuzi, chumvi uache mchuzi kidogo katika moto hadi viazi viive vikiwa tayari.

Mboga Mchicha

Mchicha – 4 michano/vifungu

Kitunguu – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 3

Nyanya/tungule – 2

Tui la nazi zito – 1 kikombe cha chai

Chumvi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mboga iache ichuje maji.
Ikatekate kisha weka katika sufuria.
Katika kitunguu maji, kitunguu thomu kisage au kikatekate kidogodogo (chopped), nyanya.
Weka jikoni ipikike kwa maji yake na mvuke.
Tia tui endelea kuweka katika moto mdogomdogo hadi ikaribie kukauka ikiwa tayari.

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia asali

Asali hasa asali mbichi ya asili ni dawa nzuri sana ya kutibu chunusi. Asali ni antibiotiki ya asili ambayo husaidia kupunguza ukubwa wa chunusi na maumivu ya chunusi.

Asali inaweza pia kuzuia ngozi yako isipatwe na maambukizi mengine ambayo yangeweza kusababisha matatizo kwenye ngozi au makovu.

Hivyo asali inachukuliwa kama moja ya dawa za asili nzuri za kutibu chunusi unazotakiwa kuzijaribu.

Kwanza safisha ngozi yako vizuri na maji ya uvuguvugu kasha jipake asali moja kwa moja sehemu yenye chunusi. Iache kwenye ngozi kwa dakika 30 kisha jisafishe na maji safi ya uvuguvugu.

Jinsi ya kupika Donati

Viamba upishi

Unga
2 Magi (kikombe kibuwa cha chai)

Sukari
1/3 Kikombe cha chai
Mayai 5

Siagi 4 Vijiko vya chakula

Hamira 1 Kijiko cha chakula

Baking Powder 1 Kijiko cha chai

Vanilla 1 Kijiko cha chai

Hiliki zilizosagwa 1 Kijiko cha chai

Sukari ya laini ya unga

(icing sugar) 1 Magi

Jinsi ya kuandaa na kupika

Unavunja mayai, unatia sukari, hamira, baking powder, vanilla na hiliki ikisha unapiga kwa kutumia mchapo wa kupigia keki. Unapiga mchanganyiko kwa muda wa dakika tano.

Unatia siagi kwenye sufuria na unaiyayusha na kuipasha moto mpaka iwe moto ikisha unaimimina kwenye mchanganyiko na unapiga tena kwa dakika mbili tu.

Unatia unga kwenye sinia au bakuli kubwa ikisha unamimina ule mchanganyiko kwenye unga na unaukanda kutumia mkono, mpaka ulainike.

Ukiona unga mwingi basi ongeza maziwa kidogo mpaka uwe sawa, na ukiona unga mwepesi sana basi unaweza kuongeza unga kidogo pia mpaka ukae sawa mfano wa unga wa maandazi.

Sukuma na ukate madonge kama unavyoyaona hapo juu. Tumia kifuniko cha chupa kwa kukatia kiduara kidogo katikakti ya madonge.
Ukimaliza kukata madonge yote, yaweke kidogo yavimbe halafu teleka mafuta na uyachome.
Ukitoa kwenye mafuta yachuje moto na kabla ya kupoa yawe moto moto yarovye kwenye icing sugar na uhakikishe yote yameenea sukari juu.
Ukimaliza tia kwenye sahani acha zipowe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Kichekesho cha mtalii na mbongo

Duh! Sikubali bora mbavu zituume wote!

Watalii wana dharau sana bana, Mtalii alikodi boti akazunguka nayo kwenye mto Rufiji kuangalia mandhari, akamuuliza kijana anayeongoza boti, “Do you know Biology, Psychology and Anthropology?” Kijana akajibu “NO,” Mtalii akamwambia “nothing you know under the sun? You are useless, and u’ll die with your illiteracy!” baada ya muda boti ikaanza kuzama, kijana akamwambia mtalii “Do you know kuogelealogy and kusepalogy from mambalogy? Mtalii akajibu huku ametoa macho “No” kijana akamwambia “You will kufalogy and mambalogy wil eat your matakology because of your bad-mdomology..😂😂😂😂😂😂

Jinsi ya kutengeneza saladi

Mahitaji

Tango 1/2
Kitunguu 1/2
Cherry tomato 8
Lettice kiasi
Green olives kidogo
Black olives kidogo
Hoho jekundu 1
Carrot
Giligilani kidogo

Salad dressing
Yogurt 1/2 kikombe
Swaum 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili ya unga 1/4 kijiko cha chai
Chumvi kidogo
Olive oil kiasi

Matayarisho

Osha vitu vyote kisha vikaushe maji. Baada ya hapo ktk bakuli kubwa katakata, lettice, tango,hoho, kitunguu,giligilani na kisha ikwangue carrot na utie bila kusahau nyanya zote pamoja na olives.Baada ya hapo ichanganye vizuri, kisha tengeneza salad dressing kwa kuchanganya vitu vyote vilivyo (kwenye list ya salad dressing) kisha koroga vizuri.Baada ya hapo ichanganye na salad.Na hapo salad yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila na chochote upendacho kama vile chips, nyama choma au au chakula kikuu.

Jinsi ya kupika pizza ya mboga mboga na cheese

MAHITAJI

1 kilo unga wa ngano
240 ml maji ya vugu vugu
2 olive oil kijiko kikubwa cha chakula
2 asali kijiko kidogo cha chai
1 chumvi kijiko kidogo cha chai
1 hamira ya chenga kijiko kidogo cha chai

JINSI YA KUPIKA

Chukua bakuli weka maji ya uvugu vugu, amira ya chenga, asali na chumvi kisha koroga ichanganyike vizuri acha itulie kwa dakika 10.
Kisha chukua olive oil na unga wa ngao mimina kidogo kidogo changanya mpaka ichanganyike safi kabisa kisha anza kukanda kama mchanganyiko wa chapati au maandazi.
Baada ya mchanganyiko wako kua mgumu safi kabisa funika bakuli lako na mfuko wa plastiki au cling film kwa muda wa saa 1 katika joto la chumba na mchanganyiko wako utaumuka baada ya muda huo. kisha ukandamize mchanganyiko huo wa unga na kua flati kama mwanzo.
Kata mafungu matano hadi saba ya ujazo sawa inategemea na ukubwa wa piza unaopenda we mlaji kisha sukuma umbo la duara.
Tengeneza mchuzi mzito wa nyanya kisha weka juu ya kitako cha piza na kuitandaza vizuri kwenye pizza yako kama unavyopaka siagi kwenye mkate. Usisahau kuweka chumvi na sukari kidogo katika mchuzi wa nyanya ili kukata uchachu.
Katakata nyanya, kitunguu, pili pili hoho, na bilinganya na kuziweka juu ya pizza yako kwa mpangilio ukitanguliza biringanya, ikifuatiwa na pili pili hoho, kitunguu maji na nyanya.
Kisha chukua mozarella cheese ikwaruze katika mkato mdogo rahisi kuyeyuka kwa kutumia kwaruzo la karoti linafaa.
kisha chukua mkwaruzo wa mozarella cheese na unyunyizie juu ya hizo mboga.
Weka pizza yako kwenye sahani ya bati au pizza pan ili isaidie kuiva upande wa chini.
Weka pizza yako kwenye oven ambayo imeshawashwa na ina joto 400 – 450 F. Choma kwa dakika 20 hadi 25 iwe kaukau na rangi ya kahawia pia cheese itakua imyeyuka na kusambaa vizuri juu ya pizaa.

NB: Unaweza weka mchanganyiko wa nyama yeyote ile kama salami, nyama ya ngombe, nyama ya kuku au samaki kwa kufata maelekezo sawa sawa na hii piza ya mboga, tofauti yake itakua huweki mboga unaweka nyama.

Maswali na Majibu kuhusu Mafumbo ndani ya Kanisa Katoliki

Neno hili kuwa nafsi tatu kwa Mungu mmoja laitwaje?
Laitwa fumbo la Utatu Mtakatifu. (Lk, 3:21-22)


Kanisa linafafanuaje fumbo la umwilisho?
Linatamka kuwa Yesu Kristo ni Mungu kweli na Mtu kweli. (Ebr 4:15)


Nini maana ya neno “Fumbo”?
Fumbo ni ukweli ambao hatuwezi kuelewa kikamilifu, lakini tunasadiki kwa kuwa Mungu hutufumbulia. (Math 11:27)


Katika dini yetu yapo mafumbo hasa mangapi?
Mafumbo matatu
1. Fumbo la Utatu Mtakatifu
2. Fumbo la Mungu Kujifanya mtu
3. Fumbo la Ukombazi wetu

Mapishi ya Wali, Mchuzi Wa Nazi Wa Samaki Nguru

Mahitaji

Mchele – 3 vikombe

Samaki Nguru (king fish) – 5 vipande

Vitunguu – 2

Nyanya/tungule – 4

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Tui la nazi zito – 2 vikombe

Pilipili mbichi – 5-7

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 7-9 chembe

Kotmiri – 1 msongo (bunch)

Bizari ya samaki – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 2-3

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha samaki, kata vipande kiasi weka kando.
Katakata kitunguu na nyanya vipande vidogo vidogo sana (crush) .
Katakata kotmiri weka kando.
Saga pamoja, pilipili mbichi, kitunguu thomu, ndimu na chumvi.
Changanya pamoja na bizari ya samaki kisha paka katika vipande vya samaki acha kidogo vikolee.
Weka mafuta katika sufuria au karai, kaanga vitunguu kidogo tu kisha tia nyanya/tungule endelea kukaanga hadi vilainike na kupondeka.
Tia kikombe kimoja na nusu cha tui la nazi, kisha tia vipande vya samaki na masala yake, acha mchuzi uchemke samaki aive. Ongeza chumvi, ndimu, pilipili ikihitajika.
Ongezea tui lilobakia acha motoni kwa daika chache tu.
Epua mwagia kotmiri mchuzi ukiwa tayari.

Pika wali wa maji/mweupe kama kawaida utolee na mchuzi.

Kwa nini watu wanapenda pesa

Watu wengi tunapenda sana Pesa lakini hatuko tayari kuzifanyia Pesa kazi nikiwa na maana kutumia njia sahihi kuzipata na tunapozipata hatuna Akili ya kuweza kuwa nazo muda mrefu zisiondoke.
Kama tujuavyo katika maisha yetu haya Pesa ndio kila kitu,tunahitaji Pesa ili tuweze kufanya mambo mengi mazuri na makubwa.Kitu kinachotukwamisha hatujui tufanye nini ili tuweze kuzipata hizi Pesa na tunapozipata tunakosea tena cha kuzifanyia ili zisipotee tena au zisiishe.

Kitu kikubwa kinachotugharimu ni kwamba hatuna elimu ya Pesa.Wengi wetu tumesoma tena sana lakini huko shuleni na vyuoni hatufundishwi jinsi gani ya kuzitafuta Pesa,uzifanyie nini,na nini kifanyike ili zisiishe.
Elimu hii kuhusu Pesa haitolewi shuleni zaidi ni ya kujifunza kutoka mtaani hasa kwa watu wanaomiliki Pesa nyingi au ambao wamefanikiwa ndio watakupa utaalam halisi na elimu kuhusu Pesa.

Kuna watu wengi sana tumeshawahi kuwasikia wamepata Pesa nyingi sana lakini sasaivi hawana kitu.Wengi tumewasikia kwenye bahati nasibu wamejishindia Pesa nyingi,wengine kwenye mashindano mbalimbali wamejishindia Pesa kibao lakini cha kujiuliza hao watu mpaka sasa wapo wapi?hela zao ziko wapi?wamezifanyia kitu gani?bado wanazo??Jibu rahisi ni hapana na hii ni kutokana na kwamba hawakupata elimu ya Pesa ndio maana.

Inatakiwa kabla ya kuwapa watu Pesa lazima wapate elimu kuhusiana na Pesa hapo ndipo watakapokuwa na ujuzi Wa kuweza kuzifanyia kazi na kuziongeza.
Matajiri wote unaowafahamu wana elimu juu ya Pesa ndio maana Pesa zinazidi kuwafuata wao na sisi ambao hatuna elimu ya Pesa tunazidi kuhangaika kuzitafuta.

Lakini sifa nyingine ya Pesa kadiri unavyotoa ndivyo unavyozidi kuzipata yaani ni kama vile unabarikiwa….kama unajua au unavyoona matajiri wengi sana ni watoaji Wa hela kusaidia sehemu mbalimbali hasa kwa wasiojiweza au miradi ya kimaendeleo ndio maana unaona wanazidi kufanikiwa.

Watu wengi tunazifanyia Pesa kazi badala ya Pesa kutufanyia sisi kazi. Hii ni kutokana na kwamba hatujaelewa au hatujui jinsi gani ya kutengeneza mfumo utakaokuwa unakuingizia tu Pesa hata kama haupo.Umeshawahi kujiuliza hicho unachokifanya kama ukipumzika kwa muda Wa kama miezi sita utaendelea kupata kiasi kilekile cha Pesa ulichokuwa unakipata kabla ya kupumzika?Kama huwezi hivyo basi wewe unazifanyia Pesa kazi.

Kwa muajiriwa ukipumzika miezi sita utaendelea kulipwa mshahara wako?
Kwa mfanyabiashara labda Wa duka ukipumzika wiki moja bila kufungua duka lako utapata kipato kile kile unachokitengeneza kila siku?Kama hauwezi basi ujue unazifanyia Pesa kazi.

Tukiangalia kwa upande mwingine wafanyabiashara wakubwa wanaweza kupumzika hata mwaka mzima na wakaendelea kupata hela zilezile kwani wameshatengeneza mfumo ambao sisi wengi hatunao na ndio watu ambao Pesa zinawafanyia kazi.Ana uwezo Wa kwenda kupumzika Marekani mwaka mzima na Pesa zikaendelea kuingia huu ndio Uhuru Wa Pesa.

Jiulize wewe unazifanyia Pesa kazi au Pesa zinakufanyia wewe kazi?
Unaufanyia mfumo kazi au mfumo unakufanyia wewe kazi?
Kipato chako ni endelevu au sio endelevu?
Ukipumzika mwaka mzima bila kufanya au kugusa chochote utaendelea kupata kipato hichohicho?

Kama jibu ni hapana basi ni muda muafaka Wa kubadilika na kubadilisha unachokifanya.

……Shtuka na changamkia fursa……

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About