Utani kwa wadada wembamba
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Wadada wembamba hebu nenepeni basi mnatupa tabu kusoma maneno ya kwenye kanga jamanii โฆโฆโฆmnaviringisha kanga mwili mara 3 mpaka maandishii hayaonekanii
๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Mbangi mwitu au kwa kisayansi ni African marigold / (Tagetes erecta) Unazuia Bakteria, fungusi na wadudu kama vile Siafu, bungo pamoja na aina nyingine za wadudu.
Siku moja jioni katika mji flani, kulikuwa na basi likisafiri kutoka mji huo kuelekea mji mwingine. Lilikuwa ni basi kubwa na limejaa abiria. Wakati wakiendelea na safari, ghafla, mvua kubwa iliyoambatana na radi ikaanza kunyesha. Dereva hakuogopa, wala abiria, wakaendelea na safari. Mara wakati wanaenda, radi ikaanza kufuatilia gari. Kila wakienda, radi inapiga karibu na basi kana kwamba inalifuata basi. Likisimama, radi inapiga pembezoni mwa basi.
Dereva kuona hivyo, akasimamisha gari mita 5 kutoka kwenye mtiโฆ Akawaambia abiria, “Humu ndani ya basi, kuna mtu ambaye leo ni siku yake ya kufa, tena kufa kwa radi. Ili tusife wote, nataka kila abiria ashuke akaguse mti ili anayepigwa na radi, apigwe wengine wasife kwa ajili yake. “Abiria wakitetemeka, wakaanza kushuka mmoja mmoja. Unaenda unagusa mti , kisha unarudi kwenye basi. Abiria wote pamoja na dereva mmoja mmoja, wakaenda, wakagusa mti na kurudi bila dhara lolote! Akawa kabaki abiria mmoja tu, ambaye alikuwa hajagusa mti. Abiria wote kwa macho ya hasira wakamwambia akaguse mti. Akawa anaogopa kufa. Akagoma. Wakamlazimisha kwa nguvu sana na kumtoa njeโฆโฆ. โฆโฆ.. Yule abiria akiwa amefumba macho, akaenda akagusa mti. Hamadi bin Vuu! Radi kali sana ikalipiga basi, abiria na wote waliokuwamo, wakafa palepale. Kumbe uwepo wake ndio ulikuwa unazuia abiria wengine wasidhurike na radi.
MAFUNZO
1. Unapofanikiwa, huwezi jua uwepo wa nani umefanikisha mafanikio yako, usichukue sifa zote peke yako. Wapatie na wengine bila kumsahau MUNGU.
2. Unaweza kujiona huna thamani sehemu ulipo, iwe kwenye kundi la WhatsApp, darasani, kazini, kwenye basi, barabarani bila kujua kama uwepo wako ni wa muhimu sana kwa ustawi wa wengine.
3. Usimtenge wala kumnyanyasa mtu au jirani yako, huwezi jua uwepo wake ni kwa ajili gani.
Unga wa ngano (plain flour 1/2 of kilo)
Siagi (butter vijiko 2 vya chakula)
Yai (egg 1)
Chumvi (1/2 ya kijiko cha chai)
Hiliki (ground cardamon 1/4 ya kijiko cha chai)
Maji ya uvuguvugu (warm water)
Mafuta (vegetable oil)
Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri. Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri sasa unaweza kutia maji ya uvuguvugu kidogo, kidogo huku ukiwa unauchanganya ili kupata donge. Baada ya hapo anza kukanda hilo donge mpaka mabuje yote yapotee na unga uwe mlaini, ambapo itakuchukua kama dakika 15. Baada ya hapo tawanyisha unga katika madonge ya wastani (yasiwe makubwa sana au madogo sana) Ukimaliza hapo, andaa kibao cha kusukumia chapati kwa kukitia unga kidogo ili chapati isinatie kwenye kibao. Sukuma donge moja la chapati mpaka liwe flat na kisha weka kijiko kimoja cha mafuta na usambaze. ukisha maliza ikunje (roll). Fanya hivyo kwa madonge yote yaliyobakia.
Baada ya hapo andaa chuma cha kuchomea (fry-pan) katika moto wa wastani. Kisha anza kusukuma chapati (ni vizuri ukaanza na zile ulizozikunja mwanzo ili kuzipa nafasi zile za mwisho ziweze kulainika) ukiwa unasukuma hakikisha zinakuwa flat (na zisiwe nene sana au nyembamba sana) Ukishamaliza hapo tia kwenye chuma cha kuchomea. Acha iive upande mmoja then igeuze upande wa pili. Tia mafuta ama kijiko kimoja kikubwa upande wa chini wa chapati na uanze kuukandamiza kwa juu uku ukiwa unaizungusha. fanya hivyo uku ukiwa unaigeuza kuiangalia kwa chini ili isiungue. ikishakuwa ya brown, geuza upande wa pili na urudie hivyohiyvo mpaka chapati iive. Rudia hii process kwa chapati zote zilizobakia.
Siri ya chapati kuwa laini ni kutia siagi au mafuta ya kutosha kipindi unazikanda na pia kuzikanda mpaka unga uwe laini.
Ukwaju ni tunda maarufu sana ambalo hupatikana katika maeneo yenye uoto wa kitropiki. Kwa kingereza hujulikana kama tamarind, na kwa kitaalamu (botanical name) huitwa tamarindus indica, waarabu huita tamru alhind. Katika baadhi ya maeneo hutumiwa kama kiungo katika mboga.
Ukwaju umetunukiwa viambata muhimu na madini ambayo ni muhimu sana kwa mustakabali wa afya zetu. Una viambata kama calcium, vitamin C, copper, phosphorus, madini ya chuma, magniziam, na pyridoxine. Wataalamu wa afya wanasema kila gramu 100 za ukwaju kuna 36%za thiamin, 35% Iron, 23% magnesium ,na 16%phosphoras.
Pia ukwaju una kiwango kikubwa cha tartic acid Ma citric acid
Namna ya kuutumia ukwaju, tengeza juisi nzuri ya ukwaju, tumia kama kiungo katika chakula, unaweza kutafuna majani yake yenye ladha ya chumvichumvu, au kuyakausha majani ya mkwaju kivulini na kuweka katika uji, au supu au juisi ya matunda.
Husaidia kuongeza uwezo wa macho kuona (improving eyesight). Matumizi ya ukwaju kwa kula au kutumia kama juisi huondoa matatizo ya macho na kukufanya uwe na macho yenye afya.
Husaidia kwa wenye kisukari, kwa sababu ukwaju unaviambata muhimu kama polyphenols na flavonoids ambavyo ni madhubuti katika kurekebisha sukari mwilini na kupunguza vitambi.
Husaidia kwa wenye shinikizo la damu .unashauriwa kunywa juisi ya ukwaju Mara kwa mara. Kwasababu ukwaju hupunguza kiwango kikubwa cha lehemu mwilini (cholesterol). Pia unakiwango kikubwa cha madini ya potasiam .licha ya hayo ukwaju unafaida ya kusafisha damu.
Huondoa tatizo la nywele kukatika, na kuzipa mng’aro halisi, chemsha ukwaju, kisha tumia maji yake, changanya na vijiko viwili vya bizari, oshea nywele zako. Kisha ziache nusu saa na uzioshe kwa maji ya vuguvugu.
kuboresha mfumo wa mmeng ‘enyo na kuondoa gesi, tumia juisi ya ukwaju.
Mengineyo ni kupunguza uzito
Kuboresha ngozi yako
Unga 3 Vikombe vya chai
Baking powder 1 ยฝ Vijiko vya chai
Sukari 1 Kikombe cha chai
Siagi 1 Kikombe cha chai
Mayai 2
Maji kiasi ya kuchanganyia
Tende 1 Kikombe
ufuta ยผ kikombe
1. Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika bakuli
2. Tia mayai, na maji kidogo uchanganye vizuri.
3. Sukuma kiasi kama unavyosukuma chapati duara kubwa.
4. Tandaza tende juu yake halafu kunja hadi mwisho.
5. Paka mayai juu yake halafu mwagia ufuta kisha kata kata vipande kama katika picha.
6. Vipange kwenye treya ya oveni kisha choma(bake)moto wa 350ยฐF kwa muda wa nusu saa takriban.
7. Ziepue katika moto naziache zipowe. Panga katika sahani.
Wiki ya kwanza
Status:”Location flani amazing”
“Having fun”
“I love my life”
“sijali mnayosema nafanya nachotaka”
BAADA YA MIEZI MIWILI
STATUS:”Binadamu wengi ni wasaliti”
“trust nobody”
“Na hili nalo litapita”
BAADA YA MIEZI SITA
Status:”Yesu wewe ndio rafiki wa kweli”
“Bwana ndiye mchungaji wangu”
BAADA YA MIEZI TISA NA KIDOGO
STATUS: “Nakupenda mwanangu๐
๐
๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita tangazo kama ifuatavyo:
Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania.
Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake
Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa haraka na furaha kuwa:
Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata kuwaka haitawaka!
Nyama vipande – 3 LB
Mtindi – ยฝ kopo
Kitunguu (thomu/galic) – 1ยฝ kijiko cha supu
Tangawizi – 1ยฝ kijiko cha supu
Nyanya – 2
Pilipili mbichi – kiasi
Nyanya kopo – 4 vijiko vya supu
Vidonge supu – 2
Pilipili nyekundu paprika – kiasi
Bizari zote saga – 2 vijiko vya supu
Viazi – 4
Mafuta – 2 mug
Samli – ยฝ kikombe
Vitungu – 6
Kwenye sufuria tia nyama, saga nyanya na thomu, pilipili mbichi, tangawizi. Mimina kwenye nyama na mtindi, tia na nyanya kopo, bizari paprika, vidonge vya supu, chumvi kisha changanya vyote pamoja weka motoni.
Katika sufuria nyengine tia mafuta na samli kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi toa weka pembeni.
Kanga viazi weka pembeni.
Chukua mafuta kidogo uliyokangia tia kwenye nyama acha katika moto wa kiasi mpaka nyama iwive na maji ya punguke.
Tia viazi na vitunguu vivunje vunje tia ndani ya nyama acha moto mdogo.
Mchele – 5 mug
Maji – kiasi
Chumvi – kiasi
Mafuta uliyokaanga vitungu – kiasi
Rangi ya biriani – ยผ kijiko cha chai
*Zafarani – ยฝ kijiko cha chai
*roweka rangi na zafarani
Osha mchele roweka muda wa saa.
Chemsha maji kama magi 10 hivi na chumvi tia mchele.
Uache uchemke ukishaiva kiini nusu, mwaga maji chuja.
Mimina juu ya nyama tia rangi na mafuta kwa juu funika.
Aacha kidogo katika oveni kwa muda wa dakika 20 hivi kisha epua ikiwa tayari.
Mchele – 3 Vikombe
Kitunguu kiichokatwa – 1
Pilipili boga nyekundu iliyokatwa vipande – 1
Mafuta – ยผ Kikombe
Zaafarani – 1 kijiko cha chai tia kwenye kikombe na maji robo roweka
Chumvi – 1 kiasi
Katika sufuria, tia mafuta, kaanga kitunguu mpaka kiwe kidogo rangu ya udongo (brown)
Tia pili pili boga.
Tia mchele, kaanga kwa muda wa dakika 3, tia zaafarani na chumvi.
Tia supu uliyochemshia kuku iwe imoto.
Pika wali katika moto mdogo hadi uwive.
Kuku Mzima -1
Mayai ya kuchemsha – 6
Mchemshe kuku mzima na chumvi mpaka uhakikishe ameiva vizuri.
Mtowe na muweke pembeni. Supu yake tumia katika wali kama ilivyo hapo juuu.
Chemsha mayai, menya na kata vipande viwili kila yai moja weka kando
Kitunguu – 1
Nyanya iliyokatwa vipande – 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi – 1 kijiko cha supu
Garam Masala – ยฝ kijiko cha supu
Bizari ya manjano – ยฝ kijiko cha chai
Chumvi – kiasi
Pilipili masala ya unga – ยฝ kijiko cha chai
Nyanya ya kopo – 1 kijiko cha supu
Nazi ya unga – 1 kikombe
Maji ya ukwaju – ยผ kikombe cha chai
Tia Mafuta vijiko 2 vya supu katika sufuria
Kaanga kitunguu maji mpaka kiwe rangi ya udongo (brown).
Tia thomu na tangawizi.
Tia nyanya nzima iliyokatwa katwa.
Tia garam masala, manjano, pilipili ya unga, nyanya ya kopo, kaanga vizuri.
Changanya kwenye sufuria na ukwaju. Iache ichemke vizuri.
Changanya nazi ya unga na maji vikombe viwili.
Mtie kuku mpike vizuri na hilo tui.
Mtie kwenye oveni kidogo.
Pakuwa wali kwanza katika sinia
Muweke kuku juu ya wali.
Pambia mayai
Wachambuzi wa mambo ya saikolojia wanasema kwamba kwa kuchukua tai na kulivaa ile rangi ndiyo itakayoweza kupeleka ujumbe wa wewe unataka nini au unataka watu wakutambue kwa namna gani.
Wakati Joshua Blue, Makamu mkuu wa shule ya Kennedy mjini Hong Kong, anapoendesha baraza la wanafunzi anavaa tai lenye rangi ya light violet ili kumpa mamlaka.
Tai la rangi ya bluish-purple anasema ni โcolourful yet mutedโ, anaamini kwamba rangi ya bluu inawafanya wanafunzi wasiboreke wakatiw anasikiliza, anajizuia kutumia brighter purples na pinks wakati akiwa mbele ya wanafunzi.
โHuhitaji kuwa na rangi nyingi zinazongโaa kwani watoto watajivuruga,โ anasema Blue mwenye umri wa miaka 35.
Hakika inaweza kuwa kama kichekesho lakini wataalamu wanasema kwamba uchaguzi wa rangi ya tai inasaidia sana kupeleka ujumbe unaotakiwa kwa wahusika. Na hii haijalishi ni mteja, mdau wafanyakazi au watoto.
โRangi hutoa aina Fulani ya ishara,โ anasema David Zyla, Mwandishi mwenye makao makuu yake New York anayeandika Color Your Style.
โSuti ile ile inaweza kubadilishwa kimtindo yaani salamu zake kwa kubadili rangi ya tai, na kila mvao ukawa na ishara na salamu tofauti.โ
Baada ya kusoma maelezo yote hayo, nikuulize je sasa unaweza kufikiria unataka kuvaa tai gani katika mkutano wako ujao.Labda nikusaidie kwa namna hii.:
Si bahati mbaya au kitendo cha kubahatisha kwa wanasiasa wengi kuvaa tai lenye rangi nyekundi ndani ya suti zilizo dark na mashati mepesi.
โTai nyekundu inaonesha mamlaka,โ anasema Mark Woodman, mchambuzi wa mambo ambaye amejifunza masuala ya huko Laurel, Maryland, Marekani. โKuna kitu Fulani kipo ndani ya rangi nyekundu ambacho mara zote kinajitokeza kumuimarisha mtu na kumpa mvuto wa pekee.โ
Ofisa Mtendaji wa JPMorgan, Jamie Dimon huvaa tai nyekundu anapozungumza na wananchi
Hata hivyo wataalamu wanasema kwamba kuna rangi nyekundu na rangi nyekundu.Nyekundu iliyokoza kwa miondoko ambayo wazungu wanasema ni burgundy, husaidia kuleta imani na matumaini wakati ile nyekundu nyepesi na pink inakuwa zaidi onesho la ubunifu na namna ulivyo kistaili.Katika miaka michache iliyopita rangi ya pink inaweza kuonesha mshikamano na wamama anasema Woodman.
Wakati unaendesha mradi au unataka kupeleka ujumbe Fulani kwa kruu yako fikiria kuvaa tai la rangi nyekundu iliyokoza ambayo inashaini.Tai la rangi nyekundi unaweza kuwa njia bora ya kuonesha mamlaka.
Ross Znavor, Mtendaji katika moja ya taasisi za kifedha mjini New York yeye huvaa tai la rangi ya purple na si nyekundu katika mikutano ya kibiashara,Rangi hii huonesha kujiamini na humsaidia watu kuendelea kumkumbuka.
Anasema kuvaa tai hilo kunampatia mtu mwingine kukubali kwamba wewe unaweza kushirikiana naye na kujenga uhusiano wa kudumu.
Lindsay anasema purple, kiasili ni rangi ya utiifu na utajiri na kwa sasa inaaanza kukubalika maeneo ya kazi.
Arnold Schwarzenegger huonesha kujiamini kwa kuvaa tai rangi ya purple.
โWanaume wanaovaa mashati ya lighter purple na tai za darker purple, hutaka kutambulika haraka katika kundi bila kuleta ushawishi mwingine wa kipuuzi unaovurugaโ.
Inawezekana huvai kila siku au kila mahali lakini ukivaa tai nyeusi katika mikutano ya watendaji, kwenye dhifa unakupa wewe hali ya muondoko mweroro wenye utanashati mkubwa , anasema Zyla.
Muigizaji sinema Leonardo DiCaprio huvaa tai nyeusi katika mikutano au maeneo ambayo ni ya kikazi zaidi.
Lakini ni kweli kuwa rangi nyeusi inakufanya kuwa na ujeuri wa aina Fulani na wengine wanasema kusema kwamba inakuwa overdressed katika mazingira mengi. โRangi hii inafaa kutotumika kama wewe unataka kuendelea kupanda ngazi, wapandisha ngazi wanaweza kufikiria kwamba wewe ni jeuri wa aina Fulani hivi,โ anasema Zyla.
Ni vyema sana kama mtu atakuwa amejipatia grey shades, anaongeza Woodman. Tai la rangi ya grey linaweza kukupa mwonekano wenye mvuto mweroro usio na jeuri na usiojinata anasema Woodman.
โGrey iko poa, iliyotulia na ya kisasa zaidi,โ anasema.Ili kuifanya iwe imetulia zaidi piga tai hili na shati ambalo ni lighter, pastel-coluored. Tafadhali angalia lighter grey shades na malizia na shaini ili kukupa muonekano ambao ni polished.
Rangi ya kijani ina maana nyingi kuanzia kuzaliwa upya hadi rangi ya fedha kwa mataifa Fulani.Lakini cha ajabu ni rangi yenye โkeleleโ nyingi katika maeneo ya kazi.
Wakati mwingine kijani inakuwa too much.
โJe unataka kukumbukwa akwa ajili ya tai au kama wewe binafsi?,โ anauliza Woodman .Anasema kuchagua rangi ya kijani inayostahili ni kazi kubwa.Kijani inayowaka inavuruga kutokana na mwako wake na pia inakuwa na taabu sana kupata suti inayoambatana nayo au hata shati. Hata hivyo tai la light green likiwa na subtle print linaweza kuwa jema katika shati ambalo rangi yake ni neutral.
Tai ya rangi ya njano, ni tai la kiasili kwa nchi nyingi hata waingereza wanaliheshimu kwa sababu linakupa uhakika, kukuweka mngโavu na mwenye siha hasa ya kufaa.
Ni rangi inayoonesha jua, hivyo watu wengi wanaweza kuwa na kishawishi cha kuzungumza nawe kwa sababu ya ukweli kuwa ni rangi yenye mvuto wa kipekee. Kwa wengi kuvaa tai la rangi ya njano kunaonesha kwamba maisha yeye anayaangalia katika dunia chanya zaidi, anasema Eve Roth Lindsay, mshauri wa masuala ya muonekano wa Hong Kong.
Lakini kiukweli kuwa unapaswa kuwa mwangalifu usije ukafanya kosa la uasili na utamaduni wa eneo lenu inapokuja suala la rangi.
Mathalani rangi ya njano nchini india ina maananisha kwamba wewe ni mfanyabiashara wakati rangi nyeupe nchini China inamaana upo katika kipindi cha maombolezo.
Unahofu ya kupeleka ujumbe ambao uhuhitaji kwa kutumia tai uliyovaa yaani rangi yake?basi ni vyema ukafikiria kutumia tai ya rangi ya bluu.
Rangi hii hutumika katika matukio yote.
Rangi ya bluu ni rangi bomba kwa kuwa inawakumbusha watu anga na bahari, vitu vyenye kutuliza maisha ya binadamu anasema Lindsay.
โRangi ya bluu hakika ni salama zaidi kuivaa,โ anasema.
Tai ya Patterned blue hutoa hali ya kutulia na kitaalamu zaidi na inaweza kutumiwa katika mikutano ya kimataifa ya kibiashara na mazingira bila kupeleka ujumbe usiotakiwa.
Tai ya subtle blue inaweza kuwa na mvuto na kujionesha undani wakati cobalt au royal blue hukufanya ujiachie ndani ya kundi kwa namna Fulani. โBluu iliyokoza ni rangi ya marubani watukuka. Bluu bahari ni rangi inayoaminika, inayokupa imani na kiburi cha uwezo,โ anasema Lindsay .
โKabati lako likiwa na rangi rafiki za asili kama tan, kahawia, earthy colours, salmon na njano hufaa sana kwa watu wanaojishughulisha na wengine kama wafanyabiashara (mauzo), walimu na watu wa huduma mbalimbali,โ anasema Lindsay.
Hakikisha kwamba tai la rangi ya kahawia haiku pekee kwani inaweza kuonesha ugoigoi katika wajihi. Hata hivyo tai la beige linaweza kukuonesha kwamba huna matatizo, yuko huru.
Epuka kuvaa tai la rangi ya udongo na shati linalofanana nalo. Na kama unataka kujishebedua na kuonekana kweli katika eneo la kazi rangi hizi za asili achana nazo kabisa.
Tafakari na ujumbe huuuu!!!โฆ
DAKTARI :- Unajisikiaje?
CHIZI:-Kila siku naota nyani wanacheza mpira wa miguu.
DAKTARI :- Nitakupa dawa leo hautaota tena.
CHIZI:-hiyo dawa nipe kesho sababu leo wanacheza fainali. na nilibet
๐๐๐๐
Ni hizi
1. Mvuta sigara hazeeki
2. Mvuta sigara haumwi na mbwa
3. Mvuta sigara nyumbani kwake haingii mwizi
UFAFANUZI
1. Hazeeki kwa sababu hufa mapema kwa kifua kikuu
2. Haumwi na mbwa kwa vile kifua na mapafu yanapooza na hulazimika kutembea na bakora
3. Nyumbani kwake haingii mwizi kwa kuwa inafika wakati ambapo halali:
atakohoa usiku kucha hivyo mwizi anajua yupo macho
kumbe kikohozi tu!
1 kilo unga wa ngano
240 ml maji ya vugu vugu
2 olive oil kijiko kikubwa cha chakula
2 asali kijiko kidogo cha chai
1 chumvi kijiko kidogo cha chai
1 hamira ya chenga kijiko kidogo cha chai
Chukua bakuli weka maji ya uvugu vugu, amira ya chenga, asali na chumvi kisha koroga ichanganyike vizuri acha itulie kwa dakika 10.
Kisha chukua olive oil na unga wa ngao mimina kidogo kidogo changanya mpaka ichanganyike safi kabisa kisha anza kukanda kama mchanganyiko wa chapati au maandazi.
Baada ya mchanganyiko wako kua mgumu safi kabisa funika bakuli lako na mfuko wa plastiki au cling film kwa muda wa saa 1 katika joto la chumba na mchanganyiko wako utaumuka baada ya muda huo. kisha ukandamize mchanganyiko huo wa unga na kua flati kama mwanzo.
Kata mafungu matano hadi saba ya ujazo sawa inategemea na ukubwa wa piza unaopenda we mlaji kisha sukuma umbo la duara.
Tengeneza mchuzi mzito wa nyanya kisha weka juu ya kitako cha piza na kuitandaza vizuri kwenye pizza yako kama unavyopaka siagi kwenye mkate. Usisahau kuweka chumvi na sukari kidogo katika mchuzi wa nyanya ili kukata uchachu.
Katakata nyanya, kitunguu, pili pili hoho, na bilinganya na kuziweka juu ya pizza yako kwa mpangilio ukitanguliza biringanya, ikifuatiwa na pili pili hoho, kitunguu maji na nyanya.
Kisha chukua mozarella cheese ikwaruze katika mkato mdogo rahisi kuyeyuka kwa kutumia kwaruzo la karoti linafaa.
kisha chukua mkwaruzo wa mozarella cheese na unyunyizie juu ya hizo mboga.
Weka pizza yako kwenye sahani ya bati au pizza pan ili isaidie kuiva upande wa chini.
Weka pizza yako kwenye oven ambayo imeshawashwa na ina joto 400 – 450ย F. Choma kwa dakika 20 hadi 25 iwe kaukau na rangi ya kahawia pia cheese itakua imyeyuka na kusambaa vizuri juu ya pizaa.
NB: Unaweza weka mchanganyiko wa nyama yeyote ile kama salami, nyama ya ngombe, nyama ya kuku au samaki kwa kufata maelekezo sawa sawa na hii piza ya mboga, tofauti yake itakua huweki mboga unaweka nyama.
Kushindwa jambo sio Makosa, bali kuacha kufanya jambo kabisa ni makosa makubwa.
Ckia ckupend, cktaki na wala ckhitji tena ww ni kikwzo
ktka maisha yangu ucnizoee! Mwmbie shtan maneno hya kabla
hjalala. g9t
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Recent Comments