Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mapishi ya Mseto wa choroko

Mahitaji

Mchele 2 vikombe vya chai
Choroko kikombe 1 na 1/2
Nazi kopo 1
Swaum 1 kijiko cha chakula
Kitunguu 1 kikubwa
Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai
Chumvi
Mafuta

Matayarisho

Loweka choroko usiku mzima, pindi ukianza kupika loweka mchele nusu saa kisha katika sufuria kubwa, kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia swaum na binzari nyembamba kisha tia choroko, mchele, chumvi,nazi na maji mengi kiasi yakuivisha choroko pamoja na mchele. Pika mpaka vitu vyote viive na viwe vilaini kisha upondeponde kiasi.Baada ya mseto wako kuiva utakuwa unaonekana kama uji wa mchele vile. Na Baada ya hapo mseto wako utakuwa tayari kwa kuliwa na mboga yoyote uipendayo.Inapendeza zaidi kuliwa vile tu ukishamalizwa kupikwa

Namna nzuri ya kuhudumia nywele zako za asili kirahisi

Kwa wale ambao tuna nywele asilia (natural hair), tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo. Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia, karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu.

Katika mada ya leo, nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi. Je,unazifahamu nywele zako vizuri?Una nywele za aina gani? Zina tabia gani? Zinataka nini?

Zifuatazo ndizo njia ya kuzihudumia nywele zako;

1. Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda.

Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi. Mwingine oh..nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwaniโ€ฆhazishikiki.T atizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako. Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri. Jenga mahusiano mazuri tu na nywele zako,zielewe,ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua.

2. Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe.

Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele.Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri.Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki( โ€˜friendlyโ€™) .Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi.Unapoziacha chafu,ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia,kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri.

3. Linda unyevu wa nywele zako

Kila mtu akisikia kiu hunywa maji.Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu.Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu.Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri,na zikikauka zinakua kavu sana.Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri,ukazi-โ€™conditionโ€™.Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache,pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.

4. Zifahamu nywele zako

Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi. Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu .Unajuaje?

Chukua kikombe,kijaze maji safi.Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi.

Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi.

Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida.

(Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)Ni kwamba โ€˜cuticleโ€™ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka.

Kwa hiyo ukifanya โ€˜deep conditionerโ€™ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye โ€˜hot oil treatmentโ€™ itakusaidia โ€˜cuticleโ€™kufunguka na unyevu kupita.

Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya vuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana.

Mimi nina aina gani?..Nina nywele zinazonyonya unyevu haraka.

5. Mafuta ya Kupaka kichwani.

Ni ya muhimu mnoo!.Nimefanya utafiti wa kina nimeona mafuta ya nazi yanaweka afya nzuri kwa nywele aina nyingi hivyo na mimi nikaanza kuyatumia. Kwangu mimi,mafuta ya nazi ya kutengeneza mwenyewe yamenikubali sana. Japo huwa nanunua pia mafuta kama ya olive(extra virgin) na ya tea tree.

6. Kuzichambua vizuri kabla ya kuchana.

Uwe mkarimu na mwenye subira kwa nywele zako. Mimi zikijifunga huwa nazichambua kwa mikono taratibu wakati mwingine nazilowesha na maji kwa mbali halafu nachana kwa chanuo lenye mapana sio ambalo reli zake zimebanana. sio kitana. Chanuo kubwa(wide toothed comb).

7. Usizisumbue mara kwa mara na usuke mitindo ya kuzitunza zikue.

Kama unataka zikue haraka, usizisumbue sana. Unaweza ukasuka mitindo mizuri tu ukakaa nazo wiki nzima au kadri zitakavyodumu. Au upunguze kuzichana mara kwa mara lakini utafute siku kama wikiendi ukae uzichambue taratibu na vidole kuondoa mafundo. Kuchana mara kwa mara zinapukutika,zinaanguka. Zitakua lakini sio kwa kasi ya kama ukizisuka ukaziacha kwa muda.

8. Punguza matumizi ya vitu vya moto kwenye nywele zako kama pasi ya nywele na vingine vya hivyo.

Mimi dryer la nywele situmii zaidi ya mara mbili kwa mwezi. Mara nyingi naziacha zikauke na hewa hata kama nimezifunga rollers natoa kesho baada ya masaa 24

Cheki huyu jamaa anavyoungama kwa padri sasa

JAMAA: Baba Padri nimekuja kuungama
PADRI: Haya
JAMAA: Niliiba kamba
PADRI: Kamba?
JAMAA: Ndio, kamba lakini kule mwisho kulikuwa kumefungwa ng’ombe
PADRI: Kwa hiyo uliiba ng’ombe?
JAMAA: Kiukweli nilikuwa nina lengo la kuiba kamba, kwa bahati mbaya mwisho kulikuwa na ng’ombe
PADRI: Mi naona mueleze Mungu direct, mi sikuelewi kabisaaa

๐Ÿ™ˆ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Š

Angalia huyu baba alichowafanya mtoto wake wa kike na boyfriend wake

BABA OYEEEEEE๐Ÿ’ช๐Ÿ’ช
Soma hiiโ€ฆ

Msichana alikuwa amekaa na baba yake kibarazani, mara akamuona MVULANA friend wake akija, yule mvulana alipokaribia tu, yule msichana akamwambia hivi:-

MSICHANA: Umekuja kuchukua kile kitabu chako, kinachoitwa “DADDY IS AT HOME?” by Ngozi Okafor

MVULANA: Hapana!, Nimekuja kuazima kitabu cha maombi kama kinaitwa “WHERE SHOULD I WAIT FOR YOU?” by Ngลฉgฤฉ wa Thiong’o

MSICHANA: Aaah! Hicho sina ila ninacho kimoja kinaitwa “UNDER THE MANGO TREE” by Chimamanda Adichie

MVULANA: Ooh! Vizuri, Basi usisahau kuja nacho kesho kitabu cha Okot p’Bitek kile kinachoitwa “CALL ME IN 5 MINUTES BEFORE” Utakapokuja shule.

MSICHANA: Usijali, tena nina kitabu kipya kinaitwa “I WON’T LET YOU DOWN” by Chinua Achebe

Baba mtu akawatazama kisha akasema

BABA: Vitabu vyote hivyo, mbona vingi sana, atavisoma vyote kweli

MSICHANA: Ndio Daddy, huyu mvulana yupo smart sana na ana akili atavisoma vyote hivyo!

BABA: Sawa! Usisahau kumpatia na kile ambacho nimekiweka pale juu ya meza, kinaitwa “I AM NOT STUPID, I UNDERSTOOD EVERYTHING YOU’VE BEEN SAYING” by Shakespeare!

Na kuna kingine nimekiweka juu ya kabati la vyombo, kinaitwa “IF YOU GET PREGNANT PREPARE TO GET MARRIED” by Wole Soyinka.

Vidokezo vya kukusaidia ule mboga za majani zaidi

Ulaji wa mboga za majani ni muhimu kwa sababu zina vitamini na madini mengi na viwango vidogo vya kalori. Ili uongeze mboga zaidi za majani katika milo yako, fuata vidokezi hivi vifuatavyo;

Gundua njia za kupika haraka

Pika mboga mpya za majani au zilizogandishwa kwa barafu katika wimbi mikro kwa mlo wa haraka na rahisi kuongeza kwa mlo wowote. Pika maharagwe ya kijani, karoti, au brokoli kwa mvuke katika bakuli na kiwango kidogo cha maji katika wimbi mikro kwa mlo wa haraka.

Kuwa mbele ya mambo

Katakata bechi ya pilipili hoto, karoti, au brokoli.Ziweke ili uzitumie wakati zimeadimika. Unaweza kuzifurahia kwenye saladi, na mboji au sandwichi ya mboga za majani.

Chagua mboga za majani zilizo na rangi nyingi

Ngโ€™arisha sahani yako na mboga za majani zilizo na rangi nyekundu, ya machungwa, au kijani. Ziko na vitamini na madini. Jaribu boga ya tunda la muoka, nyanya cheri, viazi vitamu, au kale (sukuma wiki). Hazionji vizuri tu bali ni nzuri kwako pia.

Angalia mpangilio wa friza

Mboga za majani zilizogandishwa kwenye barafu hutumika haraka na kwa urahisi na ziko na lishe kama mboga mpya za majani. Jaribu kuongeza mahindi, dengu, maharagwe ya kijani, spinachi, au mbaazi barafu kwa milo yako kadhaa uipendayo au au ule kama mlo wa kando.

Weka mboga nyingi za majani

Mboga za majani za mkebe ni ongezo muhimu kwa mlo wowote, kwa hivyo weka nyanya, maharagwe mekundu, uyoga, na viazisukari vya mkebe tayari. Chagua zilizo na lebo kama โ€œsodiamu iliyo punguzwa,โ€ โ€œsodiamu kidogo,โ€ au โ€œhakuna chumvi imeongezwa.โ€

Fanya saladi yako ya bustani ingโ€™ae kwa rangi

Ngโ€™arisha saladi yako kwa kutumia mboga za majani zilizo na rangi nzuri kama vile maharagwe meusi, pilipili hoho zilizokatakatwa, figili zilizokatakatwa, kabichi nyekundu iliyokatakatwa au wotakresi. Saladi yako haitapendeza tu lakini pia itaonja vizuri.

Kunywa supu ya mboga za majani

Ipashe moto na uile. Jaribu supu ya nyanya, boga kikazio, au mboga za majani za bustani. Tafuta supu iliyopunguzwa sodiamu au iliyo na kiwango cha chini cha sodiamu.

Ukiwa nje

Kama chakula cha jioni ni nje ya nyumbani, usijali. Unapoagiza, itisha mboga zaidi za majani au saladi zaidi badala ya mlo wa kawaida wa kando uliokarangwa.

Onja ladha ya mboga za majani za msimu

Nunua mboga za majani ambazo ni msimu wake kwa ladha ya kiwango cha juu kwa bei ya chini. Angalia bidhaa zilizo na bei maalumu katika duka kuu la karibu kwa ununuzi wa bei nafuu. Au tembelea soko la wakulima lililokaribu.

Jaribu kitu kipya

Huwezijua unachoweza kupenda. Chagua mboga mpya ya majani โ€“ iongeze kwa mapishi yako au tafuta mtandaoni jinsi ya kuipika.

Angalia jinsi muda wako unavyopotea

Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka.

Katika hayo masaa 24 unayoyapata kila siku unayatumiaje katika suala zima la kukufikisha katika ndoto na malengo au mafanikio yako?

Kwa nini kuna matajiri na maskini na wote tunapewa masaa 24???
Tucheki mgawanyo Wa masaa 24 ulivyoโ€ฆ.katika masaa 24 unayopewa kwa siku masaa 8 ni ya kazi,masaa 8 ni ya kulala na masaa 8 ni ya kufanya mambo yako mengine.

Tuseme katika Masaa 8 kwa ajili ya mambo yako mengine labda masaa manne yanapotea katika foleni au purukushani za maisha kama kula nk.
Je haya mengine manne yanaenda wapi?Tunayapotezea wapi?
Kwenye mpira?kwenye movie?kwenye TV?kwenye mitandao ya kijamii?kukaa na kuwajadili wengine na mashosti?

Hivi unajua kwa siku una wastani Wa kupoteza masaa manne kwenye masaa yako 24??
Kwa wiki unapoteza masaa 28 hali kadhalika masaa 112 kwa mwezi hupotea.
Kwa mwaka mmoja wenye masaa 8760 una wastani Wa kupoteza masaa 1344 ambayo ni sawa na siku 56 kwa mwaka kwa makadirio ya haraka haraka.

Kwa maana nyingine kwa kutumia hii “concept” kila miezi 12 ya mwaka mzima unapoteza miezi miwili kwa mambo ambayo sio “productive”.
Hii ni sawasawa na kupoteza mwaka mmoja ndani ya miaka 6โ€ฆkwa maana nyingine kwa “the same concept” ya masaa 4 kwa siku kupotea ni kwamba unapoteza mwaka mmoja kwa mambo ambayo hayakusaidii chochote.

Hebu jiulize hapo ulipo una umri gani?umeshapoteza miaka mingapi kwa mambo ambayo sio productive??
Kama wewe ni mfanyakazi au muajiriwa ukifanya kazi kwa muda Wa miaka 40 au kwa muda Wa miaka 40 unapoteza miaka 6.6.

Je hebu jiulize muda wote huo unaoupoteza kwenye mambo ambayo sio “productive” ungekuwa ni muda ulioutumia vizuri kwa mambo ya uzalishaji mfano kuanza kidogo kidogo kujenga biashara yako sasaivi tungekuwa na mamilionea na mabilionea wangapi?
Ili uweze kujenga biashara ambayo ni “strong” inakuhitaji angalau uijenge kwa muda Wa miaka mitano kwa maana nyingine kwa kutumia masaa manne tu kwa siku ndani ya miaka 40 utakuta tayari wewe ni milionea na baada ya kustaafu ajira usingeanza kuangaishana na pensheni (kwanza ni shilingi ngapi) au kuanza kubembeleza kuomba uongezewe mkataba au kwenda kufanya tena part time employmentโ€ฆ..kwa concept hiyo ni mamilionea wangapi tumewapoteza??

Ndio maana katika hii dunia yetu tunayoishi matajiri wote ni 3% na 97% ya watu waliobakia wanawafanyia kazi matajiri.
Matajiri waliweza kuiona hii concept kwa jicho la Tatu na wakaanza kuifanyia kazi and the rest is history.
Huwezi kumkuta tajiri anapoteza muda wake kwa mambo ya kizembe yasiyomuingizia chochote ndio maana matajiri wanazidi kuwa matajiri na maskini wanaendelea kuwa maskini.

Lakini bado muda na nafasi unayo sasa ukiamua na ukianza kuutumia muda wako ulio nao kwa ajili ya kuyatengeneza maisha yako.
Watu wengi hawako tayari kuumia na kujifunza biashara na kuielewa ndani ya miaka mitano itakayowapelekea kuwa matajiri na kuweza kuyafikia malengo na ndoto zao lakini wapo tayari kuajiriwa na kufa maskini ndani ya miaka 40.

Muda mzuri ndio sasa Wa kufanya maamuzi sahihi Wa kuyawekeza masaa manne kwenye biashara ili uje upate matokeo chanya.

Mapishi mazuri ya Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku

Vipimo vya Wali:

Mchele – 3 vikombe

*Maji ya kupikia – 5 vikombe

*Kidonge cha supu – 1

Samli – 2 vijiko vya supu

Chumvi kiasi

Hiliki – 3 chembe

Bay leaf – 1

Vipimo Vya Kuku

Kidari (chicken breast) – 1Kilo

Kitunguu – 1

Tangawizi mbichi – ยฝ kipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 7 chembe

Pilipili mbichi – 3

Ndimu – 2

Pilipilimanga – 1 kijiko cha chai

Mdalasini – ยฝ kijiko cha chai

Jira/Cummin ya unga – 1 kijiko cha chai

Maji – ยผ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Wali:

Osha na roweka mchele kisha weka sufuria katika moto tia samli ipashe moto.
Tia hiliki, bay leaf, kaanga, kisha tia mchele ukaange kidogo.
Tia maji, chumvi na kidonge cha supu, upike wali kama unavyopika pilau.
*Maji kisia kwa kutegemea mchele ulivyo.
*Unaweza kutumia supu yoyote badala ya kidonge.

Kuku:

Katakata kidari cha kuku vipande vya kiasi, weka katika sufuria, tia ndimu, bizari zote, chumvi.
Katakata kitunguu vipande vidogodogo, pilipili, na kitunguu thomu (chopped), tia katika kuku.
Chuna tangawizi mbichi tia katika kuku. Changanya vitu vyote vizuri.
Tia maji kiasi ยผ kikombe tu kiasi cha kumkaushia kuku. Weka katika moto mpike huku unageuzageuza. Anapokaribia kukauka epua akiwa tayari kuliwa na wali (na saladi upendayo)

Mapishi ya Kabichi

Mahitaji

Kabichi 1/2 kilo
Nyanya ya kopo 1/2
Kitunguu 1
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.

Maana ya Kumuamini Mungu

Kumuamini Mungu ni kuwa na uhakika na uwepo na uwezo wa Mungu. Ni kutambua na kukubali kwa uhakika kuwa Mungu yupo na anaweza kutenda. Unaweza kuwa na Imani lakini ukakosa kuamini yaani unaamini kwa Mungu lakini huamini kama atakutendea.

Kuamini kunakua na sifa zifuatazo

1. Kutokuwa na mashaka kama Mungu atatenda au hatatenda

2. Kuwa na subira. Kusubiri Mungu atende wakati unaofaa

3. Kuwa na matumaini hata kama hujatendewa.

Mara nyingi watu wanakuwa na imani lakini hawaamini ndio maana wanashindwa kuelewa mapenzi ya Mungu, mipango na matendo yake.

Kuwa na Imani tuu bila Kuamini huwezi kuendelea mbele kiroho. Kukosa Kuamini ndiyo sababu inayokwamisha maendeleo ya kiroho kwa watu wenye imani.

Dalili za kukosa au kupungukiwa Kuamini ni kama ifuatavyo

1. Kutokuwa na uhakika kama sala zako zitajibiwa.

2. Kukosa subira na matumaini.

3. Kuwa na maswali kama, Hivi Mungu yupo na mimi au hayupo na mimi??. Kujiuliza Hivi Mungu amenisikia?, Ananikumbuka?, Atafanya kweli??

Kukosa Kuamini kukizidi kunaleta hali ya kuhisi kuwa Mungu yupo na anaweza kutenda chochote lakini hatendi. Utakua sasa unaanza Kujiuliza kwa nini. Mtu akifika katika hali hii, Imani huporomoka na kupotea Mara nyingine mtu hufikia Kukosa imani kabisa na Mungu japokuwa anajua yupo na anaweza.

Ili kuondokana na hali hii ya kuwa na Imani lakini unakua na Kukosa kuamini, jitahidi kusali /kuomba neema ya kuamini, Jitahidi kusoma Biblia itakujengea kuamini na pia omba ushauri kwa watu wenye imani na wanaoamini.

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Chumvi

VIAMBAUPISHI

Unga – 3 Vikombe vya chai

Siagi – 250 gms

Baking powder – 3 Vijiko vya chai

Mayai – 2

Chumvi – 1 kijiko cha chai

Maziwa – 1/2 Kikombe

Pilipili manga ya unga 1 Kijiko cha chai

MAANDALIZI

Katika bakuli la kusagia (blender) au mashine ya keki, tia siagi, chumvi na mayai, piga mpaka iwe kama malai (cream).
Tia Unga, baking powder, pilipili manga.
Tia maziwa.
Kata usanifu (design) unayotaka na sokota au kunja kwa usanifu unaopenda.
Pika (bake) katika moto wa 350ยบ C โ€“ usiviache vikawa rangu ya udongo (brown) sana.

Amri ya Tano ya Mungu: Kutunza uhai wetu na wa watu wengine

Katika Amri ya Tano ya Mungu tumeamriwa nini?

Tumeamriwa tutunze uhai wetu na wa watu wengine tangu mwanzo hadi mwisho. (Mwa 4:10-11)


Kwa nini ni lazima kutunza uhai wetu na wa wenzetu?

Kwa sababu uhai wa watu wote umetoka kwa Mungu


Haki gani ya Binadamu ni ya msingi kupita zote?

Haki ya binadamu iliyo ya msingi kupita zote ni uhai wake ambao ni lazima uheshimiwe na kulindwa tangu siku ya kutungwa mimba


Nani anatenda dhambi dhidi ya amri ya tano ya Mungu? Mambo yanayovunja Amri ya Tano ya Mungu

Anayetemda dhambi dhidi ya amri ya tano ya Mungu ni yule;-

1. Anayemuua mtu au anayejiua mwenyewe
2. Anayemdhuru mwingine kwa namna yoyote ile
3. Anayeua Mimba na kuharibu nguvu za uzazi
4. Anayesaidia kuua, kumdhuru mtu au anayesaidia kutoa/kuharibu mimba
5. Anayeharibu mazingira yaliyomuhimu kwa uhai
6. Anayetetea au kuendeleza mifumo ya ya dhuluma, uhasama na vita.

Matumizi ya maji kutibu shinikizo la chini la damu

Matumizi ya maji ya kunywa ni moja ya dawa rahisi kabisa ya shinikizo la chini la damu.

Hii ni kwa sababu Maji ni mhimu kwa kila ogani ndani ya mwili iweze kufanya kazi zake sawa.

Kwa hiyo sababu kuu ya mtu kuwa na shinikizo la chini au hata la juu ni matokeo ya mishipa ya damu kutokuwa na vimiminika vya kutosha.

Mishipa ya damu imeundwa kwa maji maji ya damu (serum) na seli za damu.

Maji yanapopungua kwenye mwili hata vipenyo vya mishipa yako navyo hupungua ukubwa wake jambo linaloleta kushuka kwa shinikizo la damu.

Matatizo yote haya ni matokeo ya kutokunywa maji ya kutosha kila siku.

Kwa sababu hii, ili kupandisha juu shinikizo la damu unahitaji kunywa zaidi maji sambamba na juisi nyingine za matunda au za mboga mboga kila siku.

Hii inasaidia kuongeza vimiminika katika mishipa ya damu.

Sababu ya meno kubadilika rangi

Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao yamekuwa na rangi, hivyo kuwafanya watu hao kuona aiabu. Pia watu wengi wakiona meno yana rangi ya njano hudhani ni machafu, meusi yanahitaji kusafishwa ili yawe meupe.

Meno kubadilika rangi huweza kuwa ni sababu moja au muunganiko wa sababu mbalimbali kama ifuatavyo;

Matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye kaboni, sigara na mvinyo (wine) kwa muda mrefu husababisha kubadilika kwa rangi ya meno kwa juu (extrinsic staining).

Utumiaji wa maji yenye madini mengi ya fluoride katika kipindi cha utoto (dental fluorosis).

Matumizi ya dawa aina ya tetracycline kwa mama mjamzito ambaye tayari meno ya mtoto aliye tumboni yameanza kuumbwa lakini hayapata madini ya kutosha.

Maumbile yasiyo sahihi ya sehemu ya juu ya jino (amelogenesis imperfecta). Iwapo sehemu hii imeumbwa ikiwa laini kuliko inavyotakiwa huwa rahisi kufyonza rangi na jino huota likiwa limebadilika rangi au hubadilika baada ya muda.

Kufa kwa sehemu hai ya jino hasa kutokana na kuumia kwa jino au ajali (pulp necrosis), hali hii huweza huchukua miaka mingi mpaka kutokea kubalika rangi ya jino..

Jino liliozibwa kwa kutumia material aina ya amalgam huweza kubadilika rangi na kuwa nyeusi.

Mara nyingne jino lililotibiwa kwenye mzizi wa jino (root canal treatment ) huweza kubadilika rangi baada ya miaka mingi.

Kuna njia mbalimbali ambazo hutumika kuyafanya meno yaliyo na rangi isiyo ya kawaida kuwa meupe.

Njia hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu kutokana na jinsi alivyoathirika. Kuna njia nyingi ambazo huweza kuyangโ€™arisha kwa ndani (internal bleaching) au kuyangarisha kwa nje (external bleaching).

Endapo una tatizo la meno yaliyobadilika rangi, muone daktari wa kinywa na meno kwaajili ya ushauri na matibabu kwani kinywa kizuri na chenye afya huongeza kujiamini.

Namna wazazi wanavyoongea na mabinti katika umri tofauti

Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya.
Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena!
Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako?
Miaka 26: Wenzio wanaolewa.
Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha
kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia!
Miaka 33: Kuna mtu wa Mungu yupo kule
anaombea unaweza kupata mchumba
Miaka 36: At least pata mtoto mmoja.
Miaka 39: We will take care of all the wedding
billsโ€ฆyeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu .
Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ changamkia fulsa umri ukifika

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About