Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Sala ni Hazina

Sala ni Hazina. Kusali ni muhimu sana. Sala unayosali leo inaweza kukusaidia hata miaka kumi ijayo au ikasaidia watoto wa watoto wako. Mungu ni mwenye fadhila na anakumbuka yote. Mwombe Mungu akulinde ukiwa mzima ili uwapo hatarini akukumbuke hata kabla hujamwomba.

Jinsi ya kupika Mchuzi Wa Ngogwe Na Bamia

Viamba upishi

Ngogwe ½ kg
Kitunguu 2
Bamia ¼ kg
Karoti 2
Mafuta vijiko vikubwa 8
Maji vikombe 3 Mayai 2
Nyanya 2
Chumvi

Hatua

• Osha, menya na katakata nyanya na vitunguu.
• Osha, menya na kata karoti virefu virefu.
• Osha, kata ncha za bamia pande zote na kama ndefu sana kata
vipande viwili.
• Osha, kata vikonyo vya ngongwe, kama ni kubwa kata vipande viwili.
• Kaanga vitunguu, ongeza nyanya, korogoa mpaka zilainike.
• Ongeza ngogwe, karoti, bamia na chumvi, koroga mpaka
zionekane kukolea rojo.
• Ongeza maji vikombe 2 koroga na funikia kwa dakika 10-15 au
mpaka ziive. Punguza moto.
• Koroga mayai kwenye maji mpaka iwe kama maziwa, ongeza
kwenye mboga na koroga polepole usiponde ngogwe wala bamia
kwa dakika 5.
• Onya chumvi, pakua za moto kama kitoweo.

Mapishi ya Viazi vya nyama

Mahitaji

Viazi (potato) 1 kilo
Nyama ya ng’ombe 1/2 kilo
Nyanya ya kopo iliyosagwa 1/2 tin
Vitunguu maji 2
Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chai
Hoho 1
Curry powder 1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Chumvi
Coriander
Mafuta ya kupikia

Matayarisho

Safisha na katakata nyama ktk vipande vidogovidogo kisha weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia nyama, swaum/ tangawizi, chumvi na limao. Ichanganye vizuri kisha funika na uipike mpaka iive na maji yote yakauke yani yabaki mafuta tu. Baada ya hapo tia viazi vilivyokatwa vipande vya wastani vikaange kwa muda wa dakika 10 kisha tia pilipili na curry powder na nyanya. Funika na punguza moto.Pika mpaka nyanya iive vigeuze kisha tia vimaji kidogo vya kuivishia viazi. Viazi vikikaribia kuiva(hakikisha vinabaki na rojo kidogo) tia hoho na upike kwa muda wa dk 5 kisha malizia kwa kutia coriander. Changanya vizuri kisha ipua na viazi vyako vitakuwa tayari kwa kuliwa.

Angalia jinsi maamuzi yako ya jana na ya leo yanavyoweza kukuathiri

By Malisa GJ,
Nimeitoa kwa Comrade Markus Mpangala na kuitafsiri kwa Kiswahili (kisicho rasmi sana).
Mwaka 1998 “Google” walitaka kuiuza kampuni yao kwa “Yahoo” kwa dola Milioni 1 (sawa na Shilingi Bilioni 2) lakini Yahoo wakakataa. Yani Yahoo wakakataa kuinunua Google.

Mwaka 2002 Yahoo wakagundua kwamba walifanya makosa kuikataa Google kwahiyo wakarudi na kutaka kuinunua kwa dola Bilioni 3 (sawa na Trilioni 6). Lakini Google wakataka wapewe Dola Bilioni 5 (sawa na Trilioni 10). Yahoo wakagoma.

Mwaka 2008 kampuni ya Microsoft ikataka kuinunua Yahoo kwa Dola Bilioni 40 (sawa na Trilioni 80) lakini Yahoo wakakataa offer hiyo. Wakaona ni “ndogo”

Lakini Yahoo ikazidi kuporomoka kwenye soko na ilipofika mwaka 2016 hatimaye ikauzwa kwa dola Bilioni 4.6 (sawa na Trilioni 9) kwa kampuni ya Verizon.

#MyTake:

Unajifunza nini kupitia kisa hiki cha Yahoo? Binafsi nimejifunza mambo kadhaa:

#Mosi ni kuhusu fursa. Ukipata fursa leo itumie huwezi kujua kesho itakuaje. Yahoo wamechezea fursa nyingi sana. Kama wangekua makini huenda wao ndio wangekua wamiliki wa Google leo. Au wangeuzwa kwa bei kubwa (Trilioni 80) kwa Microsoft mwaka 2008. Lakini maringo yao yamewafanya kuja kuiishia kuuzwa bei ya “mbwa” (trilioni 9). Usifanye makosa ya Yahoo.!

#Pili ni kuhusu Thamani. Ukiwa kwenye nafasi leo usijione una thamani kuliko asiye na nafasi hiyo. Huwezi kujua kesho itakuaje. Maisha ni kupanda na kushuka. Unaweza kumnyanyasa mtu leo kwa sababu una nafasi fulani, kesho ukaenda kuomba kazi ukakuta ndio “boss” anayeajiri. Unayemuona leo yupo chini kesho aweza kuwa juu, na aliye juu akawa chini. Yahoo ilikua juu sana miaka ya 1990’s lakini kwa sasa imebaki “skrepa”. Hata sijui kama kuna watu wanaitumia siku hizi zaidi ya wale wabibi waliofungua email kipindi kile cha zama za kale za mawe.

Yahoo ilijiona juu kuliko wengine kwahiyo ikadharau kampuni zingine. Hata Google ilipotaka kuuzwa kwa Yahoo mwaka 1998, Yahoo iliona kama vile kuinunua Google ni kupoteza fedha. Leo inatamani kuwa hata “department” ya Google lakini haiwezekani. Usifanye makosa ya Yahoo.!

#Tatu nimejifunza majuto ni mjukuu. Wamiliki wa Yahoo huenda wanajuta sana kwa kupoteza fursa zote zilizokuja mbele yao. Vivyo hivyo katika maisha kuna maamuzi unaweza kufanya leo kesho ukayajutia. Mwanadada anaweza kukataa kuchumbiwa na kijana kwa sababu hana kazi, hana nyumba wala gari. Lakini baada ya miaka kadhaa anamuona yule kijana amefanikiwa kuliko alivyofikiri. Anatamani awe hata mchepuko wake lakini haiwezekani.
Usifanye makosa ya Yahoo.!

#Nne nimejifunza kuwa ukichagua sana nazi utapata koroma. Yahoo walijifanya kuchagua sana. Kila aliyekuja na “Offer” walikataa. Matokeo yake wakaja kuuzwa bei ya kuku za kienyeji kutoka Singida. Mwaka 2008 Microsoft walitaka kuinunua Yahoo kwa Dola bilioni 40 wakagoma. Lakini miaka 8 baadae (2016) wamekuja kuuzwa Dola bilioni 4.6 (yani 10% ya kile walichokua wapewe mwaka 2008).

Vivyo hivyo na binadamu ndivyo tulivyo. Ngoja nitumie mfano wa akina dada ili unielewe vzr. Kuna kina dada kuringa kwao ni fahari. Sisemi kina dada wasiringe. Ni vizuri kuringa lakini isiwe “too much”. Sasa wewe unaringa wanaume zaidi ya 10 waliokuja kukuposa, wote unawakataa unataka uolewe na nani?

Mwenye elimu umemkataa, mwenye gari umemkataa, mwenye nyumba umekataa, mwenye biashara umekataa. Umewakataa wote. Ukija kuhamaki umekuwa kama “Yahoo”… una miaka 35 na huna hata mchumba wa kusingiziwa. Unaanza kwenda kwenye mikesha ya maombi ili upate muujiza. Miaka mitatu inaisha hakuna muujiza wala mazingaombwe.

Unaamua kuweka tangazo gazetini “natafuta mchumba mwenye miaka 40 na kuendelea. Hata kama hana kazi mimi nina kazi tutasaidiana”. Miaka miwili inapita hupati. Unagundua ulikosea kama Yahoo. Hakuna mwanaumwe wa miaka 40 ambaye yupo single. Unarekebisha na kusema kuanzia miaka 25, wakati wewe una 40.

Unaamua kujilipua kama Jackline Wolper na Harmonizer. Au Zari na Diamond. Au Wema na Idris. Hujui wakati Wema anachukua taji la Miss Tanzania Idriss alikua form one?? Lakini leo wanamitana mababy?? Kwahiyo unaona miaka 25 kwa 40 sio issue. Na wewe unaamua kuingia kwenye kundi la “akina bibi wanaolea wajukuu zao”

Lakini hupati “husband material”. Unawapata “maplay boy” wa mjini. Wanakuja wanakuta ni bibi wa miaka 40 wanakuuliza “umemaliza eddah” wakidhani ni mjane umefiwa na mume unataka kuolewa tena. Kumbe hujawahi kutolewa mahari hata mara moja. Wanakuambia ngoja tufikirie, halafu haoooo wanapotea kama Microsoft ilivyopotea mbele ya uso wa Yahoo. Hawarudi ng’o.

Baadae baba yako anaamua kuondoa tangazo la “Jihadhari mbwa mkali” lililokuwa getini anaweka tangazo jipya “tunauza barafu” Na hapo ndipo utakapogundua kuwa vifusi vya mchanga wa mgodini vinaweza kutumika kupiga “plasta” nyumba yenu.

My dear Life is too short to be complicated. Live your life. Enjoy every moment of your life. Tumia fursa zote muhimu unazozipata. Usiringe. Usimdharau mtu. Heshimu kila mtu. Mche Mungu. Usifanye makosa ya “Yahoo”.!

Mambo Ya Kuzingatia Kuongeza Utagaji Wa Kuku

Inafahamika kuku kutaga mayai mengi hutokana na aina ya mbegu ya kuku, ila jua kwamba hata aina ya mbegu ya kuku yenye sifa ya kutaga mayai mengi kama haitapewa matunzo mazuri  basi sifa yake ya utagaji itapotea.

Kwa kawaida Tetea anatumia muda wa masaa 24 – 27 (siku moja) kutengeneza yai. Hakuna njia ya kupunguza muda huu (yaani atengeneze mayai miwili katika siku moja). Hiyo ndio asili yake. Njia Nzuri ya kumfanya kuku atage muda mrefu ni kumfanya awe na furaha na afya.

Njia za kuwafanya kuku wawe na furaha na afya:

1. Wape chakula bora chenye virutubisho vya kutosha. Usichakachue chakula chao hawatataga.

2. Viota vyao viwe safi. Safisha viota vyao mara kwa mara ili watage sehemu safi.

3. Wawe na sehemu ya wazi ya kuzunguka zunguka na kuparua parua.

4. Wawekee calcium ya kutosha kwenye chakula chao ili mayai wanayotaga yawe na gamba gumu.

5. Wachunguze mara kwa mara
kama wana dalili za kuumwa, na endapo dalili zipo watibu mara moja.

6. Wapatie maji safi kila siku. Pia safisha vyombo vyao kwa sabuni kila siku.

7. Hakikisha banda lao ni safi muda wote ili kusiwe na wadudu kama viroboto, chawa na papasi. Wadudu hawa huwasumbua kuku na kuwafanya wapunguze kutaga.

8. Hakikisha kuku hawapati msongo/stress, mfano kusiwe na wanyama wa kuwatisha wanaopita au kuingia bandani kwao.

9. Chagua aina ya kuku wanaotaga mayai mengi.

10. Umri wa kuku. Kuku wenye umri wa miezi 6 – 18 wanataga sana. Wakiwa na miezi 19 – 24 wananyonyoka manyoya (Annual Molt), hivyo hupunguza kutaga, na wakianza kutaga tena, wanataga mayai makubwa na machache kuliko mwanzo.

11. Wasihamishwe hamishwe banda. Kuku hutaga vizuri zaidi wakiwa kwenye mazingira waliyoyazoea.

12. Walishe mboga za majani za kutosha.
Kumbuka: Kuku wenye furaha na afya ndio watakaotaga sana kwenye maisha yao.
Note: Wakati mwingine inadhaniwa kwamba Jogoo anaweza kumsaidia Tetea kutaga mayai mengi. Jogoo hawezi kuongeza utagwaji wa mayai, lakini anahitajika kuyarutubisha mayai (kuyafanya yawe na mbegu). Kama kuku wako anataga mayai machache, kuongeza Jogoo hakutamfanya Tetea atage mayai mengi.

Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Samaki Wa Pink Salmon

Vipimo

Mchele 3 vikombe

Mboga mchanganyiko 1 kikombe

Samaki wa Pink Salmon 5 -6 vipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Chumvi kiasi

Pilipili manga ya unga ½ kijiko cha chai

Pilipili nyekundu ya unga ½ kijiko cha chai

Ndimu zilokamuliwa 2

Parsley kavu (aina ya kotmiri) 2 vijiko vya supu

Bizari ya mchuzi 1 kijiko cha supu

Kidonge cha supu (stock) 2

Mafuta ¼ kikombe

Maji ½ kikombe

Namna ya Kutayarisha Na Kupika

Samaki:

Katika kibakuli kidogo, changanya; kitunguu thomu, tangawizi, chumvi, pilipili zote za unga, ndimu, parsely, bizari ya mchuzi na mafuta vijiko viwili vya supu.

Pakaza kwenye samaki.

Weka vipande vya samaki katika treya ya oveni kisha uchome (grill) huku ukigeuza hadi samaki awive. Epua weka kando.

Wali:

Osha mchele roweka kisha uchemshe uive nusu kiini

Mwaga maji uchuje mchele

Weka mafuta katika sufura, tia mboga mchanganyiko kakaanga kidogo

Weka vidonge vya supu, tia maji ½ kikombe, tia chumvi kiasi

Mimina mchele uchanganye vizuri, kisha funika hadi uive wali ukiwa tayari

Pakua katika sahani pamoja na samaki

Angalia huyu mwalimu alichokifanya

Mwalimu aliingia darasani akiwa amechoka kinoma
akawambia wanafunzi.

‘leo tutajifunza kipindi cha
dini ” wanafunzi wakiwa wanajiandaa ili kuendelea
na kipindi mwalimu akajiegesha kwenye kiti klichokua
karibuu yake baada ya dakika kadhaa mwalimu alipitiwa
na usingizi, ghafla alingia mkurugenzi na
kusimama pembeni mwa kile kiti alichokalia mwalimu
ghafla kmya kikatawala darasani kiasi cha kunfanya
mwalimu ashtuke usingizini aliamka huku akipiga
miayo alpotupa jicho pembeni alimuona mkurugenzi
kasimama pemben! akiwa anababaika alifungua
kinywa na kusema ‘ Hivi ndivyo walivyolala wanafunzi
wa YESU walipokua wakimsubli kule mlimani, je
kuna mwenye swal? mkurugeni pale alipokua
akapiga makofi na kumsifia mwalimu kwa kufundisha
kwa vitendo.

Je % Ngapi unampa mwalimu kwa
kusolve kibarua chake.????

Jinsi ya kutunza kucha kujiepusha na maradhi shambulizi ya Kucha

Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa msichana. Mikono hutumika kufanya shughuli nyingi za nyumbani, shuleni na sehemu mbalimbali katika maisha kuanzia kutandika kitanda, kupika, kufanya usafi, kuandika, kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi.

Mikono isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika, kupoteza mvuto wake wa asili na kuharibu afya ya kucha. Hitaji la urembo wakati mwingine humsukuma msichana katika matumizi ya vipodozi vya kupaka kwenye kucha zake ili kukamilisha urembo wake.

Urembo wa vidole na kucha sio lazima ufanyike katika saluni au kwa wataalamu wa kupamba kucha, msichana anaweza kushughulikia afya na urembo wa vidole na kucha zake kwa gharama nafuu na kwa muda ambao mwenyewe anaona unafaa kufanya hivyo hata akiwa nyumbani.

Hii pia itamsaidia Msichana kuchagua vipodozi salama kwa afya ya kucha zake na mwili kwa ujumla. Ni jambo la muhimu kufahamu kuwa baadhi ya vipodozi vinavyotumika katika urembo wa kucha, vina rangi na sumu zisizofaa kwa afya. Sumu kama vile ‘Formaldehyde na Toluene’ zinazopatikana katika baadhi ya rangi za kucha zina madhara kwa afya ya msichana.

Ni kweli kuwa kucha nzuri huongeza urembo, mvuto na furaha ya msichana lakini pia ni busara kukumbuka kuwa afya ni muhimu kuliko urembo na uzuri. Afya ya mwili na kucha za msichana kwa ujumla hutegemea chakula bora chenye protein, madini na vitamini na siyo rangi na vipodozi.

Upungufu wa vitamini A, B Complex, proteni, madini ya chuma na chokaa (kalishiamu) mwilini husababisha kucha zipoteze afya yake ya asili. Kucha ambazo hazina afya zinaweza kuoza, kukauka, kupinda, kupasuka au kuwa na umbo kama kijiko. Magonjwa ya kuvu (fungus), na baadhi ya dawa za kupunguza makali ya virusi pia huharibu afya ya kucha. Mojawapo ya athari za dawa za kupunguza makali ya VVU aina ya Zidovudine (ZDV) ni kucha kuwa na rangi nyeusi.

Kwa ajili ya afya bora ya kucha msichana anashauriwa kula mboga za majani, maharage, korosho, asali na matunda kwa wingi kila siku. Usafi wa kucha kila siku kwa kuziosha kwa maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono huimarisha afya ya kucha. Kucha pia zinaweza kusafishwa kwa maji ya mmea wa mshubiri (Aloevera), kitunguu saumu kilichopondwa pondwa au kitunguu maji kisha viganja na vidole vikaushwe vizuri na kupaka losheni.

Kucha za msichana zinatakiwa zisiwe ndefu ili kuepuka utunzaji wa vimelea vinavyosababisha magonjwa na kurahisisha utunzaji na usafi wa kucha. Kucha ndefu zinaweza kuwa chanzo cha hatari kwa afya ya msichana na familia yake hasa pale msichana anapohusika na uandaaji wa chakula cha familia. Katika familia nyingi, hasa familia za kiafrika wasichana ndio wanaobeba wajibu na majukumu ya kuandaa chakula cha familia.

Kwa afya nzuri ya kucha, msichana anashauriwa kukata kucha zake ili ziwe fupi kadri anavyotaka kwa kutumia ‘nail cutter’ au mkasi mdogo au wembe mpya ambao haujatumiwa na mtu mwingine. Kuchangia nyembe za kukatia kucha si salama kwani kunaweza kuwa njia mojawapo ya kusambaza vimelea vya magonjwa hatari ya kuambukiza kama vile virusi vinavyosababisha UKIMWI na ugonjwa wa homa ya ini.

Ni vizuri kulainisha ncha za kucha baada ya kuzikata kwa kutumia tupa ya kucha (nail file) na kuzisugua kuelekea upande mmoja ili kuepuka kucha zisivunjike au zisisababishe michubuko ya ngozi wakati wa kujikuna. Kusugua kucha kwa kwenda mbele na nyuma kunaweza kusababisha kucha zivunjike kwa urahisi na haraka.

Kwa afya njema ya kucha, msichana pia anashauriwa asifungue pini za barua au kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha. Kucha zisikatwe kwa kutumia meno na zisilowekwe kwenye maji kwa muda mrefu hasa pale maji hayo yanapokuwa na kemikali au sabuni.

Kwa ajili ya afya njema ya kucha za miguuni, ni muhimu kuhakikisha kuwa, viatu kabla ya kuvaliwa vinakuwa vikavu na safi kabisa. Viatu visipotumiwa pia vihifadhiwe sehemu kavu isiyo na vumbi, maji au unyevunyevu ili kuepusha visiwe makazi ya kuvu (fungus)

JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

Soma kidogo hapa.. Kuna watu wa aina NNE tunapoongelea pesa na muda.

1. WANA MUDA MWINGI ILA HAWANA PESA

Watu ambao hawana pesa ila wana muda wa bwerere. Hawajui thamani ya muda. Hawa ndo wale ambao hawajui cha kufanya. Anaamka mpaka analala usiku hana specific timetable. Unaweza kumkuta anaenda dukani ukamwambia nisindikize saluni na akakubali. Yupo yupo tu. Unaweza kuta ameingia Facebook hajui hata kwa mini. Basi tu kwa sababu ana bando. Akiperuzi akaona mahali wanaongelea mpira yumo. Akiscroll post za chini akakuta kuna mtu kapost kuhusu UKAWA yumo. Akikuta kuna mtu kapost mtu ana uvimbe mkuuubwa watu wameambiwa wacomment AMEN na yeye huyo anacomment AMEN. Akikuta watu wanaongelea TRUMP na yeye anaingia kucomment. Kundi hili ni kundi lenye watu wengi mno. Watu wa aina hii kufanikiwa ni bahati nasibu. Labda kwa bahati tu akutane na post nzuri kama hii na post zingine nzuri huenda ikamsaidia. Otherwise hawa ndo hawaelewi maisha yanaenda wapi maana hawana kitu fulani specific wanachofanya. Wakisikia tu kuna kitu kiko kama dili hivi wanaenda. Wakikuta kumbe kinahitaji bidii na kujituma wanaondoka. Wanataka maisha mazuri yaje tu yenyewe.

2. WANA PESA ILA HAWANA MUDA

Hili ni kundi la watu wenye shughuli fulani ya kiuchumi. Labda ameajiriwa au amejiajiri. Wako busy kweli kweli. Na ukweli pesa inaonekana. Hawa huwezi kumwambia njoo tuonane akaja hapo hapo. Huyu lazima apange kwanza ratiba zake. Maana yupo busy. Au lazima aombe ruhusa kazini maana hana uhuru na muda wake. Muda wake kamuuzia mtu (mwajiri). Au labda atoroke ndo anaweza kupata muda wa kufanya mambo yake binafsi. Au asubiri weekend ambapo kila ratiba itategemea siku hizo mbili, kama ni ibada, usafi, kutembelea wagonjwa au ndugu kwenda mahali kuona labda kiwanja kinauzwa au kuona ujenzi au mradi wake unaendeleaje nk. Mara nyingi watu wa kundi hili hushindwa kufanya vitu vingi vinavyohusu maendeleo yako binafsi mfano kujisomea, kuhudhuria semina zinazofundisha mambo yanayoweza kuwa na manufaa kwake nk. Sababu ana ratiba iliyobana. Ukiwa na sherehe ukamwomba mchango hashindwi kukuchangia angalau chochote kile lakini muda wa kuja kujumuika na wewe ni vigumu akaupata.
Hili ni kundi ambalo kuna watu wanaitwa MIDDLE CLASS people. Watu wa maisha ya kati. Mambo yako si mabaya sana lakini si kwamba ni mazuri. Wasomi wengi na watafutaji wengi wapo hapa. Afu ndo wanahisi wanajua kila kitu. Na wengi wao huishia kupata changamoto za kifedha na kiafya ukubwani au uzeeni kama stress na maradhi mbali mbali nk. Sababu ya kutokuwa na muda hata wa kuangalia wa kuinvest na kujifunza biashara au ujasiriamali mapema wala kujishughulisha na afya zao, mazoezi, kupumzika vizuri nk kwa kuwa walikuwa busy siku zote. Maisha ya watu hawa middle class mwishoni huja kuwa magumu kwa kuwa hata kuwa na muda na majirani tu ilikuwa ishu. Kwa kuwa wengi wana magari (mengi ni mkopo. Wengine gari la kazini) na kwa kuwa wanaweza kulipa kodi ya nyumba au hata kupata kakiwanja na kuanza kujenga huko Malamba Mawili basi wanaridhika. Hawawezi kuota kumiliki nyumba Masaki au kununua kiwanja Upanga. Kama upo kundi hili lazima uanze kutafuta mbinu mbali mbali za kuyakabili maisha vizuri siku za usoni. Waangalie wastaafu ambao walikuwa busy zamani. Saivi utasikia mgongo, miguu, macho nk vinasumbua. Hawa middle class people ndo ukimkuta social media wengi wao wako critical kwa kila kitu. Maana haoni kama ana shida yoyote.

3. HAWANA MUDA WALA HAWANA PESA

Ulishasikia mtu anaambiwa “busy for nothing”? Ni kitu kama hicho. Yani mtu unakuta labda ni kibarua tu mahali anatumwa kazi asubuhi mpaka jioni. Labda ameajiriwa kazi ya ulinzi, au gereji, au kwenye mradi wa ujenzi anabeba zege au kupaka rangi. Hashindi njaa ni kweli lakini ukweli hana hela. Wala hatamani kuendelea kuwa hivyo. Kuamka alfajiri kulala saa tano usiku. Hela anayopata inatosha kula kwa mama ntilie tu na nauli. Basi. Hawezi kuota hata gari. Hata ya mkopo. Maana hata hakopesheki. Huyu hata muda wa Facebook ni nadra akiingia ni kupitisha macho afu anatoka. Au hata simu ya Facebook hana.

4. WANA MUDA NA WANA PESA

Hapa ndo utakuta wale ambao hana tena shida ya pesa. Pesa iko. Hana tena shida ya muda. Akihitaji kwenda mahali haombi ruhusa wala kuaga mtu labda kumuaga mwenza wake tu. Anaweza kusikia kuna shamba linauzwa mahali na hahitaji kutafuta hela tena ili akalinunue bali anaanza michakato ya kisheria pale pale kununua kama amelipenda. Kuna siku nilienda Morocco Square hapo Kinondoni jirani na Airtel kuna Apartments zinajengwa nikaonana na watu wa NHC waliokuwa wanakagua ujenzi unaendeleaje. Nikawauliza hizo apartments zinauzwaje wakasema kuna za milioni 600 na za milioni 800. Na unatakiwa kulipa cash 10% (yaani aidha milioni 60 au 80 cash) halafu inayobakia unaweza kuimalizia ndani ya miezi 12. Na kuna watanzania kadhaa wamenunua tena kwa hela halali. Hawa wako kundi hili hapa. Hela ipo. Muda upo. Kuna watu walienda kutembea Marekani kibiashara walipokuwa njiani kurudi wakapita mahalinchi nyingine wakakuta kuna mnada wa nyumba kwenye nchi hiyo. Hawakujiuliza mara mbili wakanunua. Kuna wazee fulani wana mtoto wao alikuwa akisoma Canada. Alipograduate wakamuuliza unataka kuishi wapi akasema huku huku Canada wakamnunulia nyumba Canada. Ukisikia hivyo unaanza kuwaza ni mafisadi. Mawazo yako ninkuwa bila ufisadi watu hawanunui nyumba Canada. Kwa taarifa yako Hawa siyo waajiriwa serikalini wala popote ni wafanya biashara.. Kundi la watu kwenye pesa. Na muda. Wanaweza kuamua kesho wakaenda kutembea visiwa vya Comoros. Watu wanaoishi kundi hili wana discipline kubwa ya maisha. Na watu wengi wanatamani kufika kundi hili. Lakini HAWANA discipline ya kujifunza tabia zinazoweza kukufikisha huko.

Swali muhimu tu la kujiuliza tu ni kuwa je, wewe upo kundi lipi.

Una muda mwingi lakini huna hela? = FUKARA

Una hela nyingi lakini huna muda? = MIDDLE CLASS

Huna muda wala huna hela.. Vijisenti unavyopata vinaishia nauli kula kodi ya nyumba nk? = MASKINI

Au una muda mwingi na hela siyo shida tena? = TAJIRI

SMS nzuri ya mapenzi ya kutakia usiku mwema

Mungu akupe umri wa mnazi uishi mingi miaka.
Akupe thamani ya mnazi kila kitu chatumika.
Kuanzia kuti lake mpaka kwenye kidaka.
Kitale katikati yake ukila utaridhika.
Matamu na maji yake hukata kiu haraka.
Weupe watui lake lina ladha ukipika.
Kupaka mafuta yake mwili hulainika.
Na kwenye machicha yake kazi nying hufanyika.
Hata na upepo wake uvumapo utacheka.
Sikijui kitu chake kipi kisichotumika.usiku mwema

Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa

Jinsi ya kupika kisamvu bila nazi

Kisamvu ni aina ya mboga ya majani inayopatikana kwa wingi na kwa urahisi katika mikoa takriban yote nchini Tanzania.
Pia aina hii ya mboga hupikwa katika mapishi ya aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya mpishi.

Aina hii ya mboga kama zilivyo mboga zingine za majani ni nzuri na muhimu kwa afya ya binadamu. Aina hii ya mboga huleta virutubisho mbalimbali mwilini.
Hapa tunaenda kuona mapishi ya kisamvu kwa kutumia mafuta bila nazi kama ilivyozoeleka na wengi.

Mahitaji :

• Kisamvu kilichotwangwa na kuwa laini
• Kitunguu maji
• Kitunguu swaumu
• Kunde mbichi
• carrots
• Mafuta ya kula
• Chumvi kiasi

Maandalizi :

• Chemsha kisamvu ukiwa umechanganya na kunde mpaka uhakikishe vyote vimeiva. Baada ya kuiva weak pembeni.
• Chukua sufuria kavu, weak mafuta kasha weak katika jiko na yakipata moto weak kitunguu na koroga mpaka kibadilike rangi kasha weak kitunguu swaumu na endelea kukoroga kwa muda baada ya hapo weak carrots na kisha weka kisamvu chako ambacho kimechanganywana kunde.
• Endelea kukoroga kwa muda na kasha acha kichemke mpaka uhakikishe mboga yako imeiva vizuri.
• Mboga hii iko tayari kwa kulikwa na inaweza ikaliwa na wali au ugali.

Matumizi ya mbaazi kama dawa

Mbaazi ni zao la chakula ambalo linalimwa sehemu nyingi sana hapa nchini, zao hili pia linaweza kutumika kama dawa kwa kutumia majani, mizizi na maua

MAANDALIZI

Chukua majani, maua au mizizi kiasi cha nusu kilo (ni vizuri kama utachanganya vyote) pondaponda na uloweke kwenye maji safi kiasi cha lita 2 kwa muda wa masaa 24.

Chuja na uweke dawa hii mbali na jua/joto, ni vizuri kama ataweka kwenye friji, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa siku 3

TIBA

Dawa hii inaweza kutibu magonjwa yafuatayo

1-Inauwezo mkubwa wa kushusha homa

2-Husaidia kuponesha vidonda.

3-Husaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa wanawake.

4-Husaidia kupunguza uvimbe

5-Huponyesha kifua na kukohoa.

6-Husafisha kibofu/njia ya mkojo.

7- Huongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbali mbali

Maswali yanayoulizwa sana kuhusu Ibada ya Kanisa Katoliki

Masifu ni nini?

Masifu ni sala au wimbo unaomsifu na kumtambua Mungu kuwa Mungu


Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?

Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.


Kwa nini wakatoliki wanaweka sanamu Kanisani?

Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22)
Hata Waisraeli kwenye hekalu lao walikua na sanamu kama tunavyosoma hapa;
“18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :18-22.)
Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe aliagiza Sanamu za Malaika zichongwe na kusema atakua hapo na kuongea na watu wake. Je sio vyema zaidi kuwa na sanamu na Picha ya Mwanae wa Pekee Yesu Kristo na kuongea na Mungu mbele yake kama alitaka ya malaika ambao sio Mungu?
Mfano mwingine ni pale Mungu alivyomwabia Musa achonge Sanamu ya Nyoka wa shaba.
“BWANA akamwambia Mose, “Tengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti, ye yote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.’’ 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu ye yote alipoumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.” (Hesabu 21:8-9).
Kwa Mfano huu Je tunaweza kusema kuwa sanamu ya nyoka ina nguvu ya uponyaji kuliko ya Yesu aliye Mungu? Kumbuka hapa watu walioona sanamu hii ya nyoka hawakukoponywa na nguvu ya sanamu ya shaba bali kwa nguvu ya neema ya Mungu kupitia Imani kwa Mungu. Kwa hiyo unaposali mbele ya picha au sanamu hautegemei nguvu ya sanamu bali unategemea neema ya Mungu kwa njia ya Imani yako kwa Mungu.
Kama vile Sanamu hii ya nyoka aliyoagiza Mungu iwekwe ilivyowekwa kwa nia ya uponyaji kwa yule aitazamaye vivyo hivyo Sanamu na Picha za Kanisani zinawekwa kwa nia maalumu na kwa neema maalumu. Ndiyo maana hazifanani. Na zinabarikiwa kwa kuombewa Baraka Ili zizae neema kwa wanaozitumia.

Sanamu au picha sio haramu bali maana ya hiyo sanamu au picha ndio inaiharamisha.

Kuna tofauti kati ya kuabudu na kuheshimu. Wakatoliki wanaweka sanamu kwa heshima na sio kwa kuabudu, ndio maana unaposali mbele ya picha ya Yesu hausali ee sanamu nisaidie bali unasema ee Yesu nisaidie.
Je tuseme tunamwabudu Raisi kwa kuheshimu picha yake kwa kuiinamia? Je tunaabudu bendera kwa kuheshimu na kupigia saluti? Je taratibu zabunge za kutoa heshima na taratibu za mahakama ni kuabudu?. Je kuapa mbele ya picha ya Raisi ni kumuabudu Raisi? Je kuapa na Biblia ni kuabudu Biblia? Je tunapobusu Biblia na kuitunza kwa heshima tunaiabudu? Tofauti ya Biblia na sanamu ni nini? Je, kwenye Biblia kinachoheshimiwa ni karatasi au maana ya yale maneno kwenye karatasi. Pengine usingeheshimu kama hujajua kuyasoma.
Kuna tofauti gani kati ya biblia yenye Maandishi na msalaba wa kuchonga wenye kuonyesha kile kinachosemwa na biblia? kama unaweza kuheshimu biblia yenye karatasi tena pale unapoweza kuzisoma na pengine ungeizarau kama ni ya lugha tofauti na hujui kilichoandikwa? Je Msalaba uliobeba maana ya kile kilichoandikwa kwenye Biblia unaona si kitu? Kama Kinachoheshimiwa kwenye Biblia sio karatasi bali maana maneno yaliyoandikwa vivyo hivyo kinachoheshimiwa kwenye picha au sanamu sio chuma yake au mti ukiochongwa bali ni maana ya hiyo sanamu.
Hii ndio maana nasema kuna tofauti ya kuabudu na kuheshimu.
Kumbuka kuwa picha au sanamu yoyote ya Kikatoliki lazima ibarikiwe kwanza ndio uweze Kusali mbele yake. Inapobarikiwa inaombewa uwepo wa yule anayewakilishwa na picha/sanamu hiyo uwe pale sanamu ilipo na anayesali pale sala yake Ifike kwa mlengwa anayeonekana kwa ishara ya sanamu/picha. Kwa Mfano askofu au padri anapobariki sanamu ya Yesu anaomba kuwa “Yesu awepo pale kwenye sanamu na Neema zake”, kwa hiyo yeyote anayesali mbele ya sanamu hiyo anaamini kuwa Yesu yuko pale na anasali Mbele yake. Kwa hiyo kinachopewa heshima sio ile sanamu bali ni yule anayeonekana kwa ishara ya ile sanamu au picha.

Tofauti ya Sanamu za Kikatoliki na za kipagani ni Kwamba,

Sanamu za Kipagani: Sanamu hizi huchukuliwa kama Mungu na huabudiwa na kutolewa Sadaka kama Mungu Mwenyewe.

Sanamu za Kikatoliki: Sanamu hizi huchukuliwa kama ishara ya kile inachokiwakilisha, haiabudiwi kamwe bali inaheshimiwa tuu.

Daima Tumia Sanamu na Picha zilizobarikiwa kwani zimenuiwa uwepo wa yule inayemuwakilisha na utaongea naye hapo. Sisi tunaamini kwamba kwenye Sanamu ya Yesu kuna uwepo wa Yesu. Kama vile Mungu anavyowaambia Waisraeli katika (Kutoka 25 :22) baada ya kuwaagiza wachonge sanamu za Makerubi (Malaika) 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :22)Sanamu au picha ni ishara wazi ya uwepo wa kile kisichoonekana.

Jifunze kupitia Sanduku la Agano na Msalaba wa Yesu

Kwenye Agano la kale: Ndani ya hekalu la Waisraeli walikua na Sanduku la agano, sanduku hilo lilikua na vibao vya Amri za Mungu ambavyo ni Ishara ya Agano lao na Mungu na ndani ya sanduku kulikuwepo pia Mfano wa Kiti ambacho kimezugukwa na sanamu za viumbe kama malaika nyuso zao zikielekea kiti hicho Kutoka 25:10-22. Waisraeli walikua wanasali kuelekea sanduku la Agano wanapokuwa Hekaluni na hata wakiwa majumbani mwao walisali kuelekea upande lilipo Hekalu. Waisraeli walisali kuelekea Sanduku la Agano wakiamini kwamba Mungu yupo kati ya sanduku lile. Lakini sanduku lile halikuwa Mungu. Waisraeli waliona fahari juu ya Sanduku lile na walilithamini na kuliheshimu kwa kuwa lilionyesha uwepo wa Mungu na popote lilipokuwa waliamini Mungu yupo.
Kwenye Agano jipya: Wakristu wanasali Mbele ya Msalaba wa Yesu ambao unaonyesha kazi ya wokovu alioufanya Yesu kwa wanadamu ya Kuwakomboa watu kwa kifo chake Msalabani. Na Msalaba huo ni Ishara ya Ukombozi wa Agano jipya na la Milele. Kama ilivyokuwa kwa Sanduku la Agano, Wakristu wanaheshimu msalaba ambao ni ishara ya wokovu wao na wanaamini kuwa Mungu yupo kati ya Msalaba huo lakini Msalaba huo sio Mungu. Wakristu wanaona fahari juu ya msalaba wa Yesu kwa kuwa ndio ishara ya wokovu wao.
FUNZO:Kupitia Mfano wa Sanduku la Agano na Msalaba tunajifunza kuwa Vyote havikuwa Mungu ila vinaheshimiwa kwa Imani kuwa Mungu yupo pale. Vilevile, vyote ni ishara ya wazi ya Agano la Mungu na Wanadamu.

Kwa nini tunasali mbele ya Picha/Sanamu na Hasa kufanya Ishara ya msalaba?

Tunasali mbela ya sanamu kwa sababu tunaamini sanamu inaakisi uwepo wa mhusika aliyechorwa au kuchongwa kwenye hiyo sanamu/picha. Ndio maana wakatoliki wanasali kwenye picha au sanamu iliyobarikiwa tuu kwa sababu Sanamu inapobarikiwa inaombewa uwepo wayule anayewakilishwa pale.
Tunafanya ishara ya msalaba kwenye sanamu kama sala ya utangulizi ambayo inathibitisha kuwa hatuabudu kile kilichoko pale bali kile tunachokifanya tunakifanya huku tukikiri Umungu na Heshima ya Utatu Mtakatifu (Mungu; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.). Vile vile tunamtukuza Mungu katika Utatu Mtakatifu kwa sababu ya yule anayewakilishwa na picha au sanamu.

Kwa nini watu wanabusu picha na sanamu?

Hii ni ishara ya Upendo kwa yule anayewakilishwa kwenye picha au sanamu husika. Hata katika maisha ya kawaida watu hubusu picha za wazazi na wapendwa wao. Maana ni ile ile.


Tumuadhimishe nani?

Tumuadhimishe Mungu pekee siku zote za maisha yetu kwa tumaini la kumuadhimisha milele.
“Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, nitalihimidi jina lako milele na milele. Kila siku nitakuhimidi, nitalisifu jina lako milele na milele” (Zab 145:1-2).
“Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina” (Rom 11:36).


Je, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia?

Ndiyo, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia: Baba kama asili ya umungu na ya uhai wote, Mwana kama Neno wake aliyejifanya mtu atukomboe, tena Roho Mtakatifu kama Upendo wao ambao unawaunganisha na kututakasa.
Pamoja na viumbe vyote tuwaimbie usiku na mchana, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja!” (Ufu 4:8).
“Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli” (Yoh 4:24).


Tumuadhimishe Mungu kwa jinsi alivyo au kwa maajabu anayotutendea?

Tumuadhimishe Mungu kwa jinsi alivyo, halafu kwa maajabu anayotutendea tangu awali, ambayo anatujulisha kidogo jinsi alivyo.
“Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele” (Zab 136:1).


Tumuadhimishe Mungu hasa kwa maajabu gani?

Tumuadhimishe Mungu hasa kwa maajabu aliyoyatenda katika Yesu, lakini pia katika Maria na wengine ambao wamefanana naye na kutuonyesha uwezo wa neema yake kwetu.
“Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa” (Ef 1:5-6).
Yeye atakuja “ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki” (2Th 1:10).


Tumuadhimishe Mungu kwanza kwa njia gani?

Tumuadhimishe Mungu kwanza kwa kumsikiliza kwa makini na kumuitikia kwa imani.
“Masikio ya watu wote yalikisikiliza kitabu cha torati… watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati” (Ne 8:3,9).
Kunyamaza ni sehemu ya ibada yoyote: tunahitaji kimya ili tuelewe tunachoambiwa na tunachosema.
“Nisikieni nyote na kufahamu” (Mk 7:14).
“Hamjui mnaloliomba” (Mk 10:38).


Je, ibada zetu ziishie katika kusadiki?

Hapana, ibada zetu zisiishie katika kusadiki, kwa kuwa tangu Agano la Kale Mungu aliagiza matendo mbalimbali ya ibada yanayolisha imani.
“Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako: Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa… Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu” (Mwa 17:10,12).
“Mwanakondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja… Kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni… Ni Pasaka ya Bwana… Siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana” (Kut 12:5,6,11,14).
Kwetu sisi Wakristo ni yale tuliyoagizwa na Yesu ili yatuletee wokovu.
“Aaminiye na kubatizwa ataokoka” (Mk 16:16).


Kanisa linaitaje ibada hizo tulizoagizwa na Yesu?

Kanisa linaita ibada hizo tulizoagizwa na Yesu sakramenti, yaani mafumbo. Ziko saba: Ubatizo, Kipaimara, Ekaristi, Kitubio, Mpako wa Wagonjwa, Daraja na Ndoa. Ndiyo “mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono” (Eb 6:2) tuliyoyapata kupitia Mitume.
Tujihadhari na madhehebu yaliyopunguza sakramenti hizo saba tulizoachiwa na wema wa Yesu kwa kuwa alijua tunavyozihitaji.


Je, tuishie katika kusadiki na kuadhimisha mafumbo?

Hapana, tusiishie katika kusadiki na kuadhimisha mafumbo, kwa kuwa imani na sakramenti zinadai kutekelezwa maishani.
“Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?… Itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana” (Rom 6:2-3; 12:1).
“Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni” (Math 5:16).


Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake nini?

Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake mafumbo hayakuadhimishwa vizuri.
“Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa” (Yak 2:26).


Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa sababu gani?

Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa kuzingatia umbile letu, kwamba binadamu ni umoja wa roho na mwili, hivyo anahitaji mwili na hisi zake ili kuingiza chochote rohoni na kutokeza yaliyomo katika roho yake isiyoonekana.
Ndiyo sababu Yesu alipoletewa kiziwi mwenye utasi “akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, ‘Efatha’, maana yake, ‘Funguka!’” (Mk 7:33-34).
Hizo zote ni ishara wazi kwa milango yetu ya fahamu.


Je, hisi zetu zote zinaweza kutumika kuadhimishia mafumbo?

Ndiyo, hisi zetu zote zinaweza kutumika kuadhimishia mafumbo, kila moja kadiri ya uwezo wake: macho kwa kuona, pua kwa kunusa, kinywa kwa kuonja na kusema, mwili mzima kwa kugusa na kutenda, lakini hasa masikio kwa kupokea maneno yaletayo uzima wa Kimungu.
“Maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima” (Yoh 6:63).
“Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia… Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Rom 10:13-14,17).


Kwa nini maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo?

Maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo kwa sababu yanafafanua ishara nyingine na kuzitia nguvu ya kututakasa.
“Kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno” (Ef 5:25-26).
Pasipo maneno hapana sakramenti yoyote.


Ishara za mafumbo zimetokana na nini?

Ishara za mafumbo zimetokana na viumbe (maji, mafuta, mkate, divai n.k.) na maisha ya jamii (kuosha, kupaka, kula na kunywa pamoja n.k.) na historia ya wokovu (kunyunyiza na kuzamisha, kuwekea mikono, kula Pasaka, n.k.),
lakini ni kwa kuagizwa na Yesu kwamba zinabeba kazi yake ya kuokoa na kutakasa.
“Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu” (Lk 22:19).


Maneno na ishara kwenye ibada vinaweza kubadilishwa na nani?

Maneno na ishara vinaweza kubadilishwa na waandamizi wa Mitume, waliokabidhiwa na Yesu mamlaka ya kuendeleza kazi yake katika mazingira mbalimbali hata mwisho wa dunia.
“Amin, nawaambieni: Yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni, na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni” (Math 18:18).
Hao Maaskofu wanakiri hawawezi kamwe kuyabadilisha yale ambayo Yesu aliyaweka kuwa ya lazima kama yalivyo mafumbo yenyewe.
“Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi” (1Kor 11:23).
Mengine yote wanaweza kuyapanga na kuyarekebisha kadiri ya mazingira, kuanzia lugha, wakilenga daima wokovu wa watu.


Faida ya kupanga taratibu za ibada ni ipi?

Faida ya kupanga taratibu za ibada ni hasa kuhakikisha yote yafuate usahihi wa imani na maadili, yakidumisha umoja na upendo, badala ya kumuachia kiongozi au mwingine yeyote aseme na kufanya anavyotaka. Mitume wenyewe walianza kazi hiyo, wakidhibiti hata karama.
“Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga. Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri. Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu. Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue. Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze… Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana. Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga… Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu” (1Kor 14:26-30,37-38,40).
Polepole taratibu ziliongezeka na ibada zikapata mtiririko rasmi wa kueleweka: ndizo liturujia za mashariki na za magharibi ambazo zinaweza kuwa mbalimbali mradi zisipishane upande wa imani.


Mhusika mkuu wa mafumbo hayo ni nani?

Mhusika mkuu wa mafumbo hayo ni Mungu ambaye kwa njia hiyo anazidi kutufanyia maajabu alivyoyafanya Yesu alipokuwa duniani. Kama tunda la kutukomboa kwa kifo na ufufuko wake, Baba anatujaza humo Roho Mtakatifu kama advansi ya uzima wa milele.
“Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi yake aliye Mtakatifu. Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake” (Ef 1:13-14).


Sisi tunahusika na mafumbo hayo kama nani?

Sisi tunahusika na mafumbo hayo kama walengwa ambao tuyatumie vema ili yazae matunda yote yaliyokusudiwa na Mungu.
Ndiyo kiini cha ukuhani wetu ambao tunashiriki ule wa Kristo tangu tubatizwe.
“Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo” (1Pet 2:4-5).


Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa vipi?

Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa kwa kuwa ndivyo anavyotufanya “tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo… tupate kuwa sifa ya utukufu wake” (Ef 1:4,12).
Tukipokea neema hiyo tunampatia ibada, sifa na shukrani na tunazidi kumuomba atujaze Roho Mtakatifu kwa njia ya Mwanae.
“Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina” (Ef 3:20-21).


Je, mafumbo yote saba yanazaa matunda yaleyale?

Hapana, mafumbo yote saba hayazai matunda yaleyale, bali Yesu aliweka kila moja kwa lengo maalumu, litupatie Roho Mtakatifu kadiri ya nafasi na haja fulani ya maisha yetu.
Ubatizo, kipaimara na ekaristi vinatuingiza katika fumbo la Pasaka tuweze kuishi upya kama wana wa Mungu.
Kitubio na mpako wa wagonjwa vinatuponya roho na hata mwili. Daraja na ndoa zinatufanya wahudumu wa Kanisa na wa familia.
Ni muhimu tujue tunachohitaji na tukipate vipi.
“Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili. Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala. Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa” (1Kor 11:29-31).


Tushiriki mafumbo hayo mara ngapi?

Tushiriki mafumbo hayo kadiri ya umbile la kila mojawapo. Kuna “ubatizo mmoja” (Ef 4:5) kwa sababu ni kuzaliwa upya “kwa maji na kwa Roho” (Yoh 3:5), jambo lisiloweza kurudiwa.
Vilevile katika kipaimara na daraja, karama inayopatikana kwa kuwekewa mikono na mwandamizi wa Mitume haifutiki, inadai kuchochewa tu.
“Nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu” (1Tim 1:6).
Kumbe tunahitaji ekaristi mara nyingi, kwa sababu ni chakula cha roho.
“Bwana, sikuzote utupe chakula hiki” (Yoh 6:34).
“Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo” (1Kor 11:26).


Je, mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote?

Hapana, si mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote, bali mengine yanahitaji mhudumu wake awe amepewa daraja inayoshirikisha uwezo ambao Yesu aliwapa Mitume wake.
“Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume” (Lk 6:12-13).
“Yesu aliwaambia tena, ‘Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi’. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, ‘Pokeeni Roho Mtakatifu’” (Yoh 20:21-22).
Kwa kuwa Waprotestanti hawana sakramenti ya daraja, kati yao zinapatikana sakramenti zile mbili tu zisizohitaji padri, yaani ubatizo na ndoa.


Je, tunapoadhimisha mafumbo hayo tuko peke yetu?

Hapana, tunapoadhimisha mafumbo hayo hatuko peke yetu, bali tunashiriki ibada ambayo Yesu anamtolea Baba milele.
“Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao” (Math 18:20).
Kwa kuungana na Kristo Kichwa, tunaungana na viungo vyote vya Mwili wake, vya duniani, toharani na mbinguni.
“Ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu wa kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili” (Eb 12:22-24).


Je, kuna nyakati za kufaa zaidi kumuadhimishia Mungu?

Ndiyo, kuna nyakati za kufaa zaidi kumuadhimishia Mungu. Yesu aliyesema, “Sikuja kutangua, bali kutimiliza” (Math 5:17), alifuata kalenda ya dini ya Kiyahudi, halafu kwa kufa na kufufuka amekuwa kiini cha ibada zetu zote. Hivyo Mitume waliadhimisha siku aliyofufuka kama “siku ya Bwana” (Ufu 1:10) ambapo wakutane “ili kumega mkate” (Mdo 20:7) wa ekaristi.
Vilevile kwenye Pasaka hawakuadhimisha tu kazi ya Musa, bali ukumbusho wa Yesu.
“Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo” (1Kor 5:7).
Fumbo hilo ndio moyo wa mwaka wa liturujia, yaani wa mpangilio wa maadhimisho katika mzunguko wa mwaka.
“Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Kol 2:16).


Je, kuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu?

La! Hakuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu, kwa kuwa yeye hafungwi na mahali.
“Mungu je, atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga!” (1Fal 8:27).
“Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono” (Mdo 17:24).
Hata hivyo sisi watu tunahitaji mahali maalumu kwa matendo yetu mbalimbali, na kumwekea Mungu mahali patakatifu.
“Mwambieni mwenye nyumba, ‘Mwalimu asema: Ki wapi chumba changu cha wageni, niile Pasaka humo, pamoja na wanafunzi wangu?’ Naye mwenyewe atawaonyesha orofa kubwa, imeandikwa tayari; humo tuandalieni” (Mk 14:14-15).


Hekalu ndiyo nini?

Hekalu ndipo tunapomuendea Mungu kwa ibada. Vilevile sisi wenyewe ni Mahekalu.
Yesu aliheshimu na kutakasa hekalu pekee la taifa lake kama “nyumba ya Baba” yake (Yoh 2:16), lakini alitabiri kuwa litabomolewa moja kwa moja, na kuwa watu watapaswa kuabudu ndani yake aliye hekalu hai. “Wayahudi walisema, ‘Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?’ Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake” (Yoh 2:20-21).
“Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho” (Ef 2:22).
“Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi” (1Kor 3:16-17).


Je, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu?

Ndiyo, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu kwa sababu tunapaswa kutumia kwa utukufu wake vipawa alivyotujalia, kama vile vya kujenga, kupamba, kuchonga, kuchora na kucheza. Kwa njia hizo tutokeze na kukoleza imani yetu na ya wenzetu.
Mungu “amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi za kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yoyote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu. Basi, Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye Bwana amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote Bwana aliyoyaagiza” (Kut 35:35-36:1).
“Maskani zako zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi!” (Zab 84:1).


Kati ya sanaa kwenye ibada/kumuadhimisha Mungu, muhimu zaidi ni ipi?

Kati ya sanaa, muhimu zaidi ni uimbaji, kwa kuwa unahusiana zaidi na Neno la Mungu, ukilitia maanani kwa uzuri wa muziki. Katika Agano la Kale, kitabu cha Zaburi ni nyimbo tupu za kutumia katika ibada.
“Msifuni kwa mvumo wa baragumu; msifuni kwa kinanda na kinubi! Msifuni kwa matari na kucheza; msifuni kwa zeze na filimbi! Msifuni kwa matoazi yaliayo; msifuni kwa matoazi yavumayo sana!” (Zab 150:3-5).
Agano Jipya pia linatuletea nyimbo nyingi.
“Mjazwe Roho, mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu” (Ef 5:18-19).
Mbinguni washindi wana “vinubi vya Mungu. Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwanakondoo” (Ufu 15:2-3).


Kuimba wakati wa ibada ni kazi ya nani?

Kuimba ni kazi ya kusanyiko lote, yaani ya kila mwamini. Kwaya ziimbishe watu wamwadhimishe Mungu, zisiwaimbie tu na kuwanyima nafasi ya kuimba.
“Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote, mtumikieni Bwana kwa furaha, njoni mbele zake kwa kuimba” (Zab 100:1-2).
“Kila kiumbe kilichopo mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, ‘Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwanakondoo, hata milele na milele’” (Ufu 5:13).


Katika kutumia sanaa kwa ibada tuzingatie nini?

Katika kutumia sanaa kwa ibada tuzingatie utakatifu na ukweli, si uzuri tu. Zisiigeuze kamwe kuwa igizo wala tamasha, kwa kuwa lengo si kuchangamsha watu bali kumtukuza Mungu.
Ziinue mioyo kwake, zitokeze na kuchangia maisha safi, zilete ujumbe sahihi kadiri ya imani na maadili, kama ilivyo lazima kwa mahubiri na mafundisho.
“Watu hawa huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu” (Math 15:8-9).


Je, ni halali kuheshimu sanamu?

Ndiyo, ni halali kuheshimu sanamu kama viwakilishi vya Yesu, Mama yake na watakatifu wake, ambao zinaleta sura zao.
Kwa msingi huo walimsihi Yesu “waguse hata pindo la vazi lake tu. Na wote waliogusa wakaponywa kabisa” (Math 14:36).
“Mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote il msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo” (Gal 6:14).


Wakati wa ibada tuvae vipi?

Wakati wa ibada tuvae namna inayodhihirisha malengo ya moyo wetu, hasa usafi na heshima, unyenyekevu na udugu.
“Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki, kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote” (Math 23:27).
“Akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri, kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, ‘Keti wewe hapa mahali pazuri’, na kumwambia yule maskini, ‘Simama wewe pale’, au ‘Keti miguuni pangu’, je, hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?” (Yak 2:2-4).
“Wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani, bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu” (1Tim 2:9-10).
Kanisa si mahali pa mashindano: hatuendi kupendeza watu, ila Mungu.
“Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu?” (1Kor 11:22).


Mbali ya sakramenti, Kanisa linamuadhimisha Mungu vipi?

Mbali ya sakramenti, Kanisa linamuadhimisha Mungu hasa kwa Liturujia ya Vipindi, yaani kwa sala rasmi zinazotolewa mara kadhaa kwa siku, kufuatana na ratiba ya binadamu ya usiku na mchana. Hivyo linajitahidi kutimiza agizo la kusali daima.
“Imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa” (Lk 18:1).
“Kesheni ninyi kila wakati, mkiomba” (Lk 21:36).
“Ombeni bila kukoma, shukuruni kwa kila jambo” (1Thes 5:17).
“Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote” (Ef 6:18).
“Huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku” (1Tim 5:5).


Kanisa linamuadhimishaje Mungu tena?

Kanisa linamuadhimisha Mungu tena kwa visakramenti ambavyo kwa mamlaka ya Kristo linawatia watu neema zake katika nafasi yoyote ya maisha. Kati yake muhimu zaidi ni baraka na mazinguo, ambavyo vipo tangu zamani, hata nje ya taifa la Israeli.
Melkisedek alisema, “Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako” (Mwa 14:19-20).
Farao aliomba, “Mkanibariki mimi pia” (Kut 12:32).
Balaam alisifiwa, “Najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa” (Hes 22:6).
“Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha” (1Sam 16:23).
“Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je, wana wenu huwatoa kwa nani?” (Math 12:27).


Maana ya baraka ni ipi?

Maana ya baraka ni kumsifu Mungu kwa yale aliyokwishatujalia na kumuomba azidi kutujalia kadiri ya mahitaji ya wahusika. Mara nyingi inatolewa na mtu mwenye daraja au mamlaka fulani.
Yesu aliletewa “watoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombea” (Math 19:13).
Siku ya kupaa mbinguni “aliinua mikono yake akawabariki” (Lk 24:50).
“Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao” (Mdo 13:3).
Pengine vinabarikiwa vitu vinavyotumiwa na watu, au mahali wanapoishi.
“Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi wake ili wawaandikie mkutano” (Lk 9:16).


Mazinguo ndiyo nini?

Mazinguo ni sala za kupungia mashetani ili kuepusha watu na balaa au madhara, hasa kama wamepagawa nao.
“Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu” (Mk 5:8).
“Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena!” (Mk 9:25).
Yesu ameliachia Kanisa mamlaka yake juu yao.
“Aliwaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu” (Mk 6:7).
“Paulo alisikitika, akageuka akamwambia yule pepo, ‘Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu’. Akamtoka saa ileile” (Mdo 16:18).


Je, ni halali kwa Wakristo kujitungia ibada nyingine?

Ndiyo, ni halali kwa Wakristo kujitungia ibada nyingine, mradi wakubali zipimwe na Maaskofu kama zinalingana na imani, maadili na taratibu za Kanisa.
“Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure… Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu” (Kol 2:18,23).
“Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao” (2Tim 3:14).


Ni halali kujitungia ibada kwa sababu gani?

Ni halali kujitungia ibada kwa sababu sala ni hasa maongezi ya Mungu na mtu.
Adamu na Eva “walisikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga” (Mwa 3:8).
Yeye hachoki kumvuta kila mmojawetu kwake na kumtia hamu ya kumhimidi na kumuabudu, kumuomba kwa ajili yake na ya wengine, kumshukuru na kumsifu.
“Ee Bwana, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu, kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako” (Zab 143:1).
Hata tukisali pamoja, uhusiano wa kila mmojawetu na Mungu ni wa pekee. Tusiposali kwa moyo, ibada ni ya bure.
“Watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami” (Isa 29:13).


Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tufanye nini?

Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tumsikilize kwa makini na kutafakari alichosema ili tukifanyie kazi. Tukisema peke yetu si sala, kwa kuwa ukisema upande mmoja tu si maongezi.
“Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia” (1Sam 3:10).
“Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku” (Zab 63:6).
“Sheria yako naipenda mno ajabu, ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa” (Zab 119:97).
“Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu” (Yer 15:16).


Kielelezo cha sala yetu ni nani?

Kielelezo cha sala yetu ni Yesu Kristo.
“Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, ‘Bwana, tufundishe sisi kusali” (Lk 11:1).
Yeye kama binadamu alichota humo uaminifu kwa wito wake wa pekee.
“Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe” (Yoh 17:1).
“Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe” (Mk 14:36).


Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa nani?

Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa Mama yake na kwa mapokeo yote ya Israeli, yaliyojitokeza hasa katika Zaburi.
“Wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu” (Lk 2:41-42).
“Saa tisa Yesu alipaza sauti yake kwa nguvu, ‘Eloi, Eloi, lama sabakthani?’” (Mk 15:34).
“Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu” (Lk 23:46).
Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About