Katoliki: Biblia Takatifu

Mafundisho na mapokeo Katika Kanisa Katoliki yanapopatikana kwenye Biblia
2 Mak. 12:38-46
Hek. 3:1
Tob 4:17
2Fal 3:20-21
Hes. 21:8-9
Kut. 25:17-22
Kol. 1:20, 2:14
Yn. 12:32
Mt. 19:11-12
2 The 2:15
2 Kor. 10:10-11
Yn 21-25
2 Yoh. 1:12
3 Yoh. 1:13
Ufu 1:10
Mdo 20:7
Mt 28:1-8
Lk. 24:1-7
Lk. 24:13ff
1 Kor. 16:1-2
Yn. 20:1-22
Yn. 21:15-17
Mt 16:18-19
W 2:1-14
Mwa 17:4
Yer. 7:7
Hes. 12:14
Yn. 6:49
Mt 23:30
Lk. 1:73
Efe. 4:11-13
1Tim 5:17-25
1Tim 3:1-7,8-18
Isa 35:8, 52:1
Zek 13:1-2
1Kor 3:15
Lk 12:47-48, 58-59
Ufu 21:27
Ebr 12:22-23
Ayu 14:13-17
Kut 30:34-37
Hes 16:6-7
Law 16:12-13
Lk 1:10
Ufu 8:32
Lk 1:28
Lk 1:42
2Fal 2:19-22
Yn 5:1-18
Yn 7:37
Hes 19:1-22
Mit 15:8, 15:29
Ayu 42:8
Yak 5:16
Mt 16:19
2Fal 13:20-21
Mt 16:19,1-20
Yak 5:15-16
Mdo 16:15-33
Mdo 18:8
Mt 28:19
Mdo 10:47-48
Kut 28:4-43
Kut 27:9-29
Kut 25:31-40; 27:20-21
Hes 8:1-4
Kut 30:22-32
Yak 5:14-15
Swala la Mapadri kutooa limeandikwa wapi katika Biblia?
JE,SHERIA YA MAPADRE KUTOOA NA KUISHI USEJA IMEANDIKWA WAPI KATIKA BIBLIA AU IMETUNGWA TU NA PAPA?
“Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika,ni heri mwanaume asimguse mwanamke,8.Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane heri wakae kama mimi nilivyo”
“32Lakini nataka msiwe na masumbufu.Yeye asiyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya Bwana ampendezeje Bwana;33.bali yeye aliyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendeza mkewe.34-Tena iko tofauti kati ya mke na mwanamwali.Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana ili apate kuwa mtakatifu mwili na Roho.Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendezesha mumewe.,35.Nasema hayo niwafaidie ninyi,si kwamba niwategee tanzi,bali kwaajili ya vile vipendezavyo,tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine”
“Wanafunzi wake wakamwambia,kama mambo ya mme na mke yakiwa hivyo ni afadhali kutuooa kabisa.Lakini Yeye akawaambia ‘SI WOTE WAWEZAO KULIPOKEA NENO HILO,ILA TU WALE WALIOJALIWA,maana wako MATOWASHI waliozaliwa katika hali hiyo toka matumboni mwa mama zao;tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi,tena wako Matowashi WALIOJIFANYA WENYEWE KUWA MATOWASHI KWAAJILI YA UFALME WA MBINGUNI’,awezaye kulipokea neno hili na alipokee”
“Ndipo Petro akajibu akamwambia ‘Tazama sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe,tutapata nini basi?29.Amini nawaambia,kila mtu aliyeacha nyumba au ndugu wa kiume au wakike,au baba au mama au watoto au mashamba KWAAJILI YA JINA LANGU,atapokea mara mia zaidi na kuurithi uzima wa milele”
Maswali na Majibu kuhusu Mitume
Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume siku gani?
Roho Mtakatifu aliwafanyia nini Mitume?
Kanisa ni la Kitume maana yake ni nini?
Yesu amemweka nani kuwa mkubwa wa Kanisa?
Mapokeo ya Mitume ndiyo nini?
Je, tukipata mafundisho ya Kanisa tunapaswa kuyasadiki?
Kanisa kuwa la Mitume maana yake nini?
Je, Yesu amejenga Kanisa lake imara juu ya mwamba?
Maaskofu wote wamerithi mamlaka gani?
Pamoja na kuwekewa mikono na mwandamizi wa Mitume, mtu anapewa kipaimara vipi?
Je, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi?
Mwenye kuwaondolea watu dhambi ni nani?
Kabla ya Kupaa mbinguni Yesu aliwaahidi nini Mitume?
Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake
Je, Biblia ilipatikanaje? Nini chanzo na asili ya Biblia.
Je, Biblia ndicho kitabu pekee cha neno la Mungu?
Je nje ya Biblia hakuna Neno la Mungu au Maandiko matakatifu?
Je Biblia ndiyo mafundisho ya Mungu pekee?
Biblia inatuthibitishia yenyewe kuwa haijakamilika na Si mambo yote yameandikwa Kwenye Biblia
Biblia inatuambia hiviโฆ”Kuna mambo Mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo Kama yangeandikwa yote, moja baada ya jingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.”โฆKwa mstari huu Biblia inatuthibitishia kuwa haikuandikwa vitu vyote.
Je Biblia ni mwisho wa Maandiko ya Mungu?
Sababu ya Kanisa katoliki kutumia mapokeo na Maandiko ya Watakatifu
Yesu alituambia nini kuhusu Neno la Mungu na Mwendelezo wa kazi ya Mungu ya kusema na watu?
Nyaraka za Mitume katika Biblia ni zipi?
1. Waroma
2. 1 Wakorinto
3. 2 Wakorinto
4. Wagalatia
5. Waefeso
6. Wafilipi
7. Wakolosai
8. 1 Wathesalonike
10. 1 Timotheo
11. 2 Timotheo
12. Tito
13. Filemoni
14. Waebrania
15. Yakobo
16. 1 Petro
17. 2 Petro
18. 1 Yohane
19. 2 Yohane
20. 3 Yohane
21. Yuda
Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristu ni wapi?
1. Simoni/Petro
2. Yakobo
3. Yohane
4. Andrea
5. Filipo
7. Mathayo
8. Thomaso
9. Yakobo wa ALfayo
10. Thadayo (Yuda Thadey)
11. Simoni Mkanaani
13. Yuda Iskarioti – Aliyemsaliti
Baba Mtakatifu wa kwanza ni nani?
Nani ni Mitume wa Mataifa?
Uelewa wa namba katika Biblia
Biblia imeandikwa na Mungu kupitia waandishi wanadamu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hivyo Biblia ni Neno la Mungu. Hivyo mwandishi wa Biblia ni Mungu kupitia wanadamu (God is the primary author of the Bible while human authors are secondary authors). Mungu aliwavuvia (inspiration by the Holy Spirit) waandishi wanadamu ili waweze kuandika kile tu ambacho Yeye (Mungu) alitaka kiandikwe kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Kusema kuwa Biblia imeandikwa na Mungu kupitia wanadamu haina maana ya kuandikwa kwa njia ya imla (dictation), kana kwamba Mungu anataja sentensi au neno na wao wanaandika. Hapana, pamoja na kuwavuvia Roho Mtakatifu, waandishi wanadamu walikuwa huru kutumia vipawa mbalimbali vya uandishi na mazingira yao ili kufikisha ujumbe ambao Mungu amewavuvia. Hivyo walikuwa โactive writers of the Bible, and not passive writers.โ Walitumia akili (reason), utashi (will), ujengaji picha (imagination) na vipawa vingine. Lakini vipawa hivi vyote vilikuwa chini ya maongozi ya Roho Mtakatifu ili kuwawezesha waandishi wa Biblia kufikisha ujumbe kwa ufasaha bila makosa.
Hivyo kuelewa kifungu au ujumbe wa Biblia ni lazima kujua yafuatayo:
Maana aliyokusudia mwandishi (the meaning of the human author)
Kusudi/malengo ya Roho Mtakatifu
Na kwa kuwa kwa mara ya kwanza Biblia waliandikiwa Wayahudi na waandishi wengi walikuwa Wayahudi, hivyo tunapaswa kujua yafuatayo ili kufasiri Biblia vizuri:
Tamaduni za Wayahudi
Historia ya Wayahudi
Mambo ya Kijografia
Namna yao ya uandishi n.k
Jambo muhimu kuelewa
Namba, wanyama, rangi, vitu, watu, maeneo, shughuli mbalimbali n.k vilikuwa na maana sana kwa Wayahudi na kwa Wakristo wa kwanza. Hivyo si ajabu kuona vimetajwa au kutumika katika Biblia.
ISHARA NYINGINE TOFAUTI NA NAMBA
Kabla ya kuzungumzia namba tuzungumzie baadhi ya vitu, rangi, watu au mahali kama vinavyoongelewa kwenye kitabu cha Ufunuo na sehemu nyingine za Biblia:
Mwanamke:
kwenye Ufu.12:1+ anamaanisha taifa au mji, na siyo mwanamke kama tunavyojua
Pembe:
neno pembe kwenye Ufu. 5:6; 12:3 linamaanisha โmamlakaโ. Hata kwenye kiswahili mtu akiambiwa kuwa โameota pembeโ maana yake anajifanya kuwa ana mamlaka fulani na hivyo ana kiburi.
Mabawa:
kwenye Ufu. 4:8; 12:14 linamaanisha uwezo wa kufika mahali pote (mobility).
Upanga mkali:
kwenye Ufu. 1:16; 2:12,16) linamaanisha Neno la Mungu, ambalo lina hukumu na kuadhibu.
Matawi ya mtende:
kwenye Ufu. 7:9 ni ishara ya ushindi.
Taji:
kwenye Ufu. 2:10; 3:11 ni ishara ya utawala na ufalme.
Bahari:
kama lilivyotumika kwenye Ufu. 13:1; 21:1 linamaanisha sehemu ya uovu, chanzo cha machafuko na kifo.
Nyeupe:
rangi nyeupe inamaanisha furaha ya ushindi (Ufu. 1:14; 2:17)
Zambarau:
rangi ya zambarau huashiria anasa, utajiri na ufalme (Ufu. 17:4; 18:12,16). Kwenye Yohane 19:2,5; Mk. 15:17 vazi la zambarau huashiria โufalmeโ. Kwenye Lk. 16:19 vazi la zambarau la yule tajiri liliashiria โmaisha ya anasaโ.
Nyeusi:
rangi nyeusi iliashiria kifo (Ufu. 6:5,12).
NAMBA KATIKA BIBLIA
Namba zilikuwa na maana sana kwa Wayahudi kwa sababu za kimazingira, kiuandishi na kilugha. Kila namba ilikuwa na maana. Hebu tutazame baadhi tu ya namba hizo:
Namba 3 na7
Namba hizi kwa Wayahudi (kwenye Biblia) zinamaanisha ukamilifu au utimilifu wa jambo (perfection or completion). Kwa mfano katika Kiebrania (lugha ya Wayahudi) hakuna โsuperlativeโ (kulinganisha kwa kutumia sifa ya juu kabisa) mfano โthe tallest, the youngest, the holiestโ kama kwenye Kiingereza. Hivyo Myahudi kwa upande wake atatamka neno husika mara tatu kuonesha ukamilifu: God is holy, holy, holy (ambapo kwenye Kiingereza tungesema tu โGod is the holiestโ). Kwa hiyo akitaja neno mara tatu alimaanisha ukamilifu wa jambo(perfection). Anaposema Mungu ni Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ana maana kwamba Mungu ana ukamilifu wa utakatifu, yaani ni Mtakatifu kupita viumbe au vitu vyote. Mfano mwingine: Myahudi akisema kwamba nilipigwa viboko vitatu haina maana kuwa lazima vilikuwa vitatu tu. Hapa ina maana kwamba alipigwa katika ukamilifu wake yaani alipigwa barabara, sawia, alipigwa mno,
alipigwa mpaka basi. Hata kwenye Biblia ni vivyo hivyo. Yesu alimuuliza Petro mara tatu kama anampenda (Yohane 21:15-19). Hapa Yesu alitaka kujua kama Petro alimpenda katika ukamilifu wa upendo. Namba 7 imetumika mara 42 kwenye kitabu cha Daniel na Ufunuo: mfano โroho sabaโ ilimaanisha โukamilifu wa rohoโ yaani Roho Mtakatifu. Kwa hiyo namba 3 na7 ni namba za ukamilifu. Yesu anapomwambia Petro asamehe โsaba mara sabiniโ (Mt. 18:21-22) anamaanisha kuwa Petro asamehe โkwa ukamilifu, pasipo kukomaโ.
Namba 4
Namba 4 kwenye Biblia inamaanisha โulimwengu mzimaโ (universality of the visible world). Kwa hiyo aya isemayo โmalaika wanne waliokuwa wamesimama katika pembe nne za duniaโ (Ufu.7:1; 21:16; Rejea pia Is.11:12) ulimaanisha malaika walikuwa wameenea katika ulimwengu mzima. Pia aya hiyo hiyo inamaanisha kuwa jukumu lao lilikuwa ni kwa ulimwengu mzima.
Namba 6
Hii namba inasimama kumaanisha โmapungufu, isiyo kamilifuโ. Namba hii ilihusianishwa na maadui wa Mungu kwenye Biblia. Kitendo cha mtu kuwa adui wa Mungu kilimaanisha mtu huyo si mkamilifu na ana mapungufu (Rejea 1 Nyakati 20:6; Daniel 3:1; Ufu.13:18).
Namba 12, 24
Hizi mara nyingi kwenye Biblia zinawakilisha kabila kumi na mbili za Israeli. Wapo wataalam wa Maandiko wanaosema kuwa Mitume 12 waliwakilisha makabila 12 ya Israel, yaani kila mmoja alitoka miongoni mwa makabila 12 ya Israel. Pia namba 12 inawakilisha Kanisa zima. Lakini pia 12 ni namba ya ukamilifu. Kwa hiyo Mitume 12 walikamilisha taifa zima la Israeli.
Namba 40, 175
Namba hizi kwenye Biblia zinamaanisha โurefu wa jamboโ (longevity). Mfano wakisema fulani amekuwa mgonjwa kwa siku 40 ina maana amekuwa mgonjwa kwa kipindi kirefu, haina maana kuwa ni lazima zilikuwa 40 (huenda hata zilizidi). Kusema kuwa gharika ilidumu siku 40 mchana na usiku, ni kusema kuwa gharika ilidumu kwa kipindi kirefu; kusema kuwa Yesu alifunga siku 40 ni kumaanisha kuwa alifunga kwa muda au kipindi kirefu, yawezekana hata zaidi ya siku hizo 40. Kusema kuwa Waisraeli walikaa jangwani miaka 40 ni kusema kuwa walikaa jangwani kwa kipindi kirefu. Kusema kuwa Ibrahimu aliishi miaka 175 ina maana aliishi miaka mingi au kipindi kirefu, si lazima kwamba alifikisha miaka 175 lakini kwamba aliishi miaka ya kutosha, aliishi kipindi kirefu. Haya yote Wayahudi walielewa vizuri, hawakuhitaji kuuliza.
Kuanzia maelfu
Kwenye Biblia ikitajwa namba ya maelfu inamaanisha โumati mkubwaโ wa watu. Yohane anaposema โโฆna watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye..โ (Ufunuo 14: 1) anamaanisha kuwa aliona umati mkubwa wa watu wasio na idadi. Hivyo Ufunuo 14:1 haimaanishi watu 144,000 tu bali umati mkubwa wa watu wasio na idadi. Hata kwa Kiswahili kuna wakati tunasema โakihubutia maelfu ya watuโ tukiwa na maana kwamba alihutubia umati mkubwa wa watu.
N.B. Hapa nimeeleza baadhi ya namba tu. Zipo nyingine nyingi sana na zina maana yake. Hivyo tusitafsiri Biblia kwa maana sisisi tu (Literal interpretation), yaani kile kilichoandikwa tu. Twende zaidi ya hapo.
UFAFANUZI WA NAMBA 666 (Ufu.13:11-18)
Kuelewa maana ya namba hii ni lazima kuelewa mazingira na sababu za kuandikwa kitabu cha Ufunuo. Kitabu cha Ufunuo kiliandikwa karne ya kwanza (kati ya 90-96 AD) ambapo dini ya Ukristo ilianza kuenea kwa kasi. Hivyo tawala za Warumi na Wayahudi ziliona Ukristo kama dini mpya na tishio kwa imani, siasa na tamaduni zao. Ili kuifutilia mbali Warumi na hata Wayahudi waliendesha madhulumu (persecutions) dhidi ya Wakristo: kuwaua, kuwafunga, kuwatesa na kuwalazimisha wakane Ukristo. Yohane mwenyewe anaandika kitabu cha Ufunuo akiwa gerezani (uhamishoni) katika kisiwa cha Patmos kama matokeo ya madhulumu. Yohane anaandika kitabu cha Ufunuo kuwatia moyo Wakristo katika madhulumu wanayopata, wasikate tamaa, wasikane imani kwa kuwa baada ya madhulumu watapata utukufu katika Yerusalem mpya (mbinguni) na damu watakayomwaga katika madhulumu ndiyo itawatakasa (Ufu. 7:14).
Kwa kuwa madhulumu yalikuwepo ilikuwa ni vigumu Wakristo kuwasiliana kwa lugha ya wazi ili kuepuka kuuawa au kufungwa. Hivyo Wakristo walitumia lugha ya namba na mafumbo kufikishiana ujumbe kwa waandishi (they used coded language). Kumtaja mfalme wa dola ya Kirumi kwa jina ilikuwa ni dharau na hivyo sababu tosha ya kuuawa. Yohane anatumia lugha ya namba kumtaja mmoja wa wafalme wakatili wa dola ya Kirumi aitwaye NERO kwa kutumia namba 666. Wakristo na wataalamu wa Maandiko Matakatifu walijuaje kuwa 666 inamwakilisha mfalme NERO? Mpaka leo kwa Warumi na Wagiriki kila herufi imepewa thamani ya namba. Walipojumlisha herufi zinazounda jina โNEROโ walipata jumla ya 666. Kwa Warumi jina la NERO liliandikwa NERON (likiwa na โNโ mwishoni). Walijumlisha herufi za jina NERON na kupata 666 na hivyo kugundua kuwa mnyama aliyetajwa kwenye Ufu. 13:11-18 alikuwa NERO. Kwa nini amezungumziwa mnyama halafu sisi tunazungumzia mtu? Ni kwa sababu Yohane mwenyewe anasema: โHapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu [for it is man’s number]. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sitaโ (Ufu. 13:18).
Utaalamu wa kuzipa herufi thamani ya namba unaitwa โgematriaโ. Mfumo wa kuzipa herufi thamani ya namba unafanana na kutofautiana kwa kiasi fulani kwa Warumi na Wagiriki. Utaratibu wa kuthaminisha herufi na namba upo bado. Ndiyo maana tukiwa shule ya msingi tulifundishwa โNamba za Kirumiโ. Tunajuaje kuwa MM ni 2000 au MMIX ni 2009. Ni kwa sababu kwa Warumi kila herufi ina thamani ya namba: M ni 1000, hivyo M+M ni sawa na kusema 1000+1000, na hivyo 2000. Tuone sasa kwa jina NERO na thamani ya kila herufi.
Gematria kwa Kirumi: NERON
N = 50
E = 6
R = 500
O = 60
N = 50
neron (50 + 6 + 500 + 60 + 50) = 666
Gematria kwa Wayunani (Waebrania): KAISER NERON
Wayunani walitamka jina ya mfalme kwa kuanza na jina la heshima โtitleโ yaani Kaisari (Ceaser). Hivyo NERO aliitwa qsr nrwn (Kaiser Neron, kwa Kigiriki). Mwanzoni Kiebrania (Kiyunani) hakikuwa na irabu (vowels). Herufi zilizounda neno qsr nrwn (Kaiser Neron) zilipewa thamani ya namba kama ifuatavyo:
q = 60
s = 100
r = 200
n = 50
w = 6
Hivyo basi neno qsr nrwn (60 + 100 + 200 + 50 + 200 + 6 + 50) = 666.
Na Fr. Kelvin O. Mkama
Usiyumbishwe na kila upepo wa mafundisho
Siku moja, miaka kama 14 hivi iliyopita, nilimzingua mchungaji wa kikanisa fulani. Alinijia mbio na kuniambia, “Atiโฆ Kadinali wenu amesema kuwa pombe sio dhambi! Kwanini usihame huko? Angalia sasa, hata kiongozi wenu wa juu wa Kanisa amekosea kwa kusema pombe sio dhambi.”
Biblia inavyothibitisha kuwa Bikira Maria Mama wa Yesu ni Mama wa Wakristu Wote
Ufunuo 12:17
17Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke, likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo.
Kwa hiyo Bikira Maria ni Mama wa Wakritu wote yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo
Ukisoma kwa urefu inasomeka hivi
Ufunuo 12:1-18
Tunajifunza nini
Mwanamke ni Bikira Maria
Mwanamke aliyetukuzwa Uf 12:1
Anamzaa mtoto
Analindwa nyoka asimdhuru
Nyoka anapambana na wanawe
IShara ya joka kama Shetani
Mtoto Aliyezaliwa mwenye mamlaka
Kwa hiyo, Bikira Maria Aliwezeshwa kumshinda Shetani na ni Mama wa Wakristu wote
Maswali na Majibu kuhusu Biblia
Biblia inatuambia hiviโฆ”Kuna mambo Mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo Kama yangeandikwa yote, moja baada ya jingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.”โฆKwa mstari huu Biblia inatuthibitishia kuwa haikuandikwa vitu vyote.
2. Agano Jipya (A.J)
1. Vitabu vya Musa (5)
2. Vitabu vya Historia (16)
4. Vitabu vya Manabii (18)
1. Injili (4)
2. Kitabu cha Matendo ya Mitume
4. Kitabu cha Ufunuo
1. Mwanzo
2. Kutoka
4. Hesabu
5. Kumbukumbu la Torati
1. Mathayo
2. Marko
4. Yohane
2. Cha mwisho ni Kitabu cha Malaki
2. Kitabu cha mwisho ni Kitabu cha Ufunuo
1. Reubeni
2. Simeoni
3. Lawi
4.Yuda
5. Dani
7. Gadi
8. Asheri
9. Isakari
10. Zabuloni
11. Yosefu
12. Benjamini
1. Yoshua
2. Waamuzi
3. Ruthu
4. 1 Samweli
5. 2 Samweli
6. 1 Wafalme
8. 1 Mambo ya Nyakati
9. 2 Mambo ya Nyakati
10. Nehemia
11. Ezra
12. Tobiti
13. Yudith
14. Esta
15. 1 Wamakabayo
16. 2 Wamakabayo
1. Isaya
2. Yeremia
3. Maombolezo
4. Baruku
5. Eekieli
6. Danieli
8. Yoeli
9. Amosi
10. Obadia
11. Yona
12. Mika
13. Nahumu
14. Habakuki
15. Sefania
16. Hagai
17. Zekaria
18. Malaki
1. Yobu
2. Zaburi
3. Mithali
5. Wimbo ulio Bora
6. Hekima ya Solomoni
7. Yoshua Bin Sira
1. Waroma
2. 1 Wakorinto
3. 2 Wakorinto
4. Wagalatia
5. Waefeso
6. Wafilipi
7. Wakolosai
8. 1 Wathesalonike
10. 1 Timotheo
11. 2 Timotheo
12. Tito
13. Filemoni
14. Waebrania
15. Yakobo
16. 1 Petro
17. 2 Petro
18. 1 Yohane
19. 2 Yohane
20. 3 Yohane
21. Yuda
1. Simoni/Petro
2. Yakobo
3. Yohane
4. Andrea
5. Filipo
7. Mathayo
8. Thomaso
9. Yakobo wa ALfayo
10. Thadayo (Yuda Thadey)
11. Simoni Mkanaani
13. Yuda Iskarioti – Aliyemsaliti
2. Mateso, Kifo na Ufufuko wake
1. Baba uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya (Lk 23:34)
2. Nakuambia Hakika leo utakuwa pamojanami Mbinguni (Lk 23:43)
3. Mama huyu ndiye mwanao (Yoh 19:26)
5. Eloi, Eloi, lema Sabakthani (Mk. 15:34) Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?
6. Naona kiu (Yoh 19:28)
7. Yametimia (Yoh 19:30)
JE IMANI AU MAPOKEO YA KANISA KATOLIKI YANAPATIKANA KATIKA BIBLIA?
2 Mak. 12:38-46
Hek. 3:1
Tob 4:17
2Fal 3:20-21
Hes. 21:8-9
Kut. 25:17-22
Kol. 1:20, 2:14
Yn. 12:32
Mt. 19:11-12
2 The 2:15
2 Kor. 10:10-11
Yn 21-25
2 Yoh. 1:12
3 Yoh. 1:13
Ufu 1:10
Mdo 20:7
Mt 28:1-8
Lk. 24:1-7
Lk. 24:13ff
1 Kor. 16:1-2
Yn. 20:1-22
Yn. 21:15-17
Mt 16:18-19
W 2:1-14
Mwa 17:4
Yer. 7:7
Hes. 12:14
Yn. 6:49
Mt 23:30
Lk. 1:73
Efe. 4:11-13
1Tim 5:17-25
1Tim 3:1-7,8-18
Isa 35:8, 52:1
Zek 13:1-2
1Kor 3:15
Lk 12:47-48, 58-59
Ufu 21:27
Ebr 12:22-23
Ayu 14:13-17
Kut 30:34-37
Hes 16:6-7
Law 16:12-13
Lk 1:10
Ufu 8:32
Lk 1:28
Lk 1:42
2Fal 2:19-22
Yn 5:1-18
Yn 7:37
Hes 19:1-22
Mit 15:8, 15:29
Ayu 42:8
Yak 5:16
Mt 16:19
2Fal 13:20-21
Mt 16:19,1-20
Yak 5:15-16
Mdo 16:15-33
Mdo 18:8
Mt 28:19
Mdo 10:47-48
Kut 28:4-43
Kut 27:9-29
Kut 25:31-40; 27:20-21
Hes 8:1-4
Kut 30:22-32
Yak 5:14-15
Je Bikira Maria Alizaa Watoto Wengine?
Mt. Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa hata moja. Ndiyo maana kwenye
litania yake tunamuita mwenye usafi kamili. Yosefu likufa kabla Yesu hajaanza utume kwa kubatizwa kwenye mto
Yordani. Sisi tunasadiki Maria ni โBikira daimaโ.
Ndugu wa Yesu wanaosemwa katika Injili ni kina nani?
wa Bikira Maria wala Yosefu mtakatifu, bali ndugu wa kiukoo waliokuwa jirani sana na familia hiyo takatifu. Kama
Bikira Maria angekuwa na watoto wengine, je, Yesu Bwana wetu asingekuwa amefanya kosa la kiudugu
kuwanyangโanya Mama yao na kumfanya awe Mama wa mtume Yohane alipomkabidhi msalabani, โโMwana, tazama
Mama yakoโ. Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwakeโ (Yoh 19:27).
Katika Agano Jipya yupo Yakobo anayeitwa na mtume Paulo โndugu yake Bwanaโ (Gal 1:19): Yakobo huyo
alikuwa maarufu katika Kanisa la Yerusalemu (Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal 2:9). Yakobo huyo si mtume
Yakobo mwana wa Alfayo, wala mtume Yakobo kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni Yakobo ndugu yake Yose na
mama yao kwenye Injili anaitwa โMaria mwingineโ, si Maria Mama wa Yesu. โWalikuwepo pia wanawake
waliotazama kwa mbali. Miongoni mwao akiwa Maria Magdalena, Salome na Maria mama wa akina Yakobo mdogo
na Yoseโ (Mk 15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa wengi hivyo, tujue
kuwatofautisha kwenye Injili. Bikira Maria Injili zinamtaja kama โMama wa Yesuโ.
Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?
Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;
1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)
2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja
6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye
26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Maswali na Majibu kuhusu Mapokeo ndani ya Kanisa Katoliki
Mapokeo ya Mitume ndiyo nini?
Tunatambuaje Maandiko Matakatifu kati ya maandishi yote ya binadamu?
Sababu nyingine za Biblia kutojitosheleza ni zipi?
Je, inafaa tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi?
Tueleweje Maandiko Matakatifu?
Je, ufunuo wa Mungu unaweza kufafanuliwa rasmi na kila mtu?
Tupokeeje ufunuo wa Mungu?
Je, Mungu amegawanyika sehemu tatu?
Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake
Je, Biblia ilipatikanaje? Nini chanzo na asili ya Biblia.
Je, Biblia ndicho kitabu pekee cha neno la Mungu?
Je nje ya Biblia hakuna Neno la Mungu au Maandiko matakatifu?
Je Biblia ndiyo mafundisho ya Mungu pekee?
Biblia inatuthibitishia yenyewe kuwa haijakamilika na Si mambo yote yameandikwa Kwenye Biblia
Biblia inatuambia hiviโฆ”Kuna mambo Mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo Kama yangeandikwa yote, moja baada ya jingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.”โฆKwa mstari huu Biblia inatuthibitishia kuwa haikuandikwa vitu vyote.
Je Biblia ni mwisho wa Maandiko ya Mungu?
Sababu ya Kanisa katoliki kutumia mapokeo na Maandiko ya Watakatifu
Yesu alituambia nini kuhusu Neno la Mungu na Mwendelezo wa kazi ya Mungu ya kusema na watu?
Namna Biblia inavyomueleza Bikira Maria
Biblia inashuhudia kuwa watu wanatofautiana
Maandiko matakatifu yanawasifu watu mbalimbali kutokana na jinsi walivyomuamini Mungu na kutenda makuu kwa ajili ya taifa lake.Abrahamu alimuamini Mungu akawa tayari kumtolea sadaka mwanae Isaka, tukio lililomfanya apate baraka ya pekee ya kuwa baba wa waamini (Mwa 22:15-18).Yosefu, mwana mpenzi wa Yakobo, alikuwa mwaminifu hata akaliokoa taifa lisiangamie kwa njaa (Mwa 50:20).Musa ndiye mkombozi wa taifa la Mungu katika Agano la Kale: aliongoza Israeli kutoka [[utumwani Misri akalipatia sheria kutoka kwa Mungu katika mlima Sinai. Maandiko ya Agano la Kale yanakiri, โWala hajainuka kiongozi kama alivyokuwa Musaโ (Kumb 34:10-12).Waliofuata ni Yoshua, Debora, Gideoni, Ruthu, Samweli, wafalme Daudi na Solomoni, manabii Eliya, Isaya, Yeremia, Ezekieli na wengineo.Mwishoni Yesu Kristo akamsifu Yohane Mbatizaji akisema, โNi mkuu kati ya uzao wa wanawakeโ (Lk 7:24-28).Elizabeti, mama wa Yohane, alijiona hastahili kutembelewa na Bikira Maria, Mama wa Yesu, akamuita, โMama wa Bwana wanguโ (Lk 1:43).Bikira Maria si mtu wa ziada katika mpango wa Mungu bali ni mshiriki mkuu wa ukombozi wa binadamu. Maria amechangia wokovu kwa kukubali mpango wote wa Mungu aliyetaka amzae Mwanae, amlee na kumfuata kiaminifu hadi msalabani, aliposhiriki kumtoa kama sadaka ya kutuokoa. Msimamo wake ulikuwa mmoja tu: โTazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosemaโ (Lk 1:38).Tukichunguza nafasi yake katika fumbo hilo, tunaweza kukiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49), kwa kuwa, โMtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Munguโ (Yoh 3:27).Yale yote ambayo Wakristo wengi wanayasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia bali alijaliwa na Mwenyezi Mungu huku akiitikia kwa hiari fumbo la mpango wake.
Utabiri kuhusu Bikira Maria kwenye Biblia
Biblia inatupatia utabiri uliotolewa na Mungu mwanzoni mwa historia kuhusu mwanamke atakayemshinda nyoka wa kale (Shetani): โNitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke, kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa chakoโ (Mwa 3:15). Juu ya [[Eva wa kale, ambaye alidanganywa na kuangushwa na Shetani atende dhambi, imesemwa: โAdamu akamwita mkewe jina lake Hawa, kwa kuwa ndiye aliye Mama wa walio haiโ (Mwa 3:20). Hata hivyo Adamu na Eva wa kale wametuletea kifo (Rom 5:12). Mababu wa Kanisa wanamtazama Bikira Maria kama Eva mpya aliyemshinda Ibilisi na kuwa mama wa wote walio hai. Yesu, aliye Adamu mpya, alipokuwa anakamilisha sadaka ya ukombozi pale msalabani alimfanya Mama yake awe Mama wa waliokombolewa kwa kumkabidhi mwanafunzi, tena yule aliyempenda zaidi. โPenye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Kleopa, na Mariamu Magdalene. Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, โMama, tazama, mwanaoโ. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, โTazama, mama yakoโ. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake. (Yoh 19:26-27).Utabiri mwingine ulisema, โTazama Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamuita jina lake Emanueli, yaani Mungu pamoja nasiโ (Isa 7:14). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:34-35, โMariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu akakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Munguโ. โImba, ee binti Sion, piga kelele, ee Israeli, furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, ee binti Yerusalemu. Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana yu katikati yakoโ (Sef 3:14-15). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:28: โMalaika akaingia nyumbani mwake akamwambia, โFurahi Maria, umejaliwa neema kubwa, Bwana yu pamoja naweโโ. โUmebarikiwa wewe katika kila hema la Yuda na katika kila taifa, nao wanaposikia jina lako watafadhaika. Imani yako haitatoka mioyoni mwa watu wanaoukumbuka uweza wa Mungu mileleโ (Yudithi 14:7; 15:9). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:42, โAkapaza sauti kwa nguvu akasema, โUmebarikiwa wewe kuliko wanawake wote, na yeye utakayemzaa amebarikiwaโโ.Bikira Maria ni fumbo la ajabu alilolifanya Mungu katika mpango wa wokovu kwa ajili yake na kwa ajili yetu. Jamaa yake Elizabeti alimpongeza tena akiongozwa na Roho Mtakatifu, โHeri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale uliyoambiwa na Bwanaโ (Lk 1:45).Hivyo manabii mbalimbali kwa mwanga wa Roho Mtakatifu walimuagua Maria kwa heshima. Mambo yaliyotabiriwa katika Agano la Kale yalitimia katika Agano Jipya: ukombozi ulianza Bikira Maria alipokubali kwa imani fumbo la umwilisho wa Mwana wa Mungu. Bikira Maria hakuwa โchomboโ tu kilichotumika bila ya kuelewa, bali alikuwa mshiriki huru wa kazi ya ukombozi ya Mwanae, kwa kuwa alipopashwa habari na malaika alikubali kwa hiari mpango wa Mungu akisema, โMimi ni mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu kama ulivyonenaโ (Lk 1:38).
Bikira Maria katika maisha ya Yesu
Yesu, kama mtu yeyote mcha Mungu, aliwaheshimu na kuwatii wazee wake: โBasi, akarudi pamoja nao Nazareti, akawa anawatiiโ (Lk 2:51).Ishara ya kwanza kwenye maisha ya hadhara ya Yesu iliongozwa na Bikira Maria katika arusi ya Kana ya Galilaya, akisukumwa na huruma kwa wenye shida: kwa ombi lake Yesu aligeuza maji kuwa divai, na wanafunzi wake wakamwamini. Yohane alisimulia hivi, โSiku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, โHawana divaiโ. Yesu akamwambia, โMama tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadiaโ. Mamaye akawaambia watumishi, โLo lote atakalowaambia, fanyeniโ. Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yesu akawaambia, โJalizeni mabalasi majiโ. Nao wakayajaliza hata juu. Akawaambia, โSasa tekeni, mkampelekee mkuu wa mezaโ. Wakapelekea. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maj), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, akamwambia, โKila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasaโ. Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. (Yoh 2:1-12).Bikira Maria anasifiwa kwanza kwa imani yake kuu kabisa, kuliko kwa kumchukua Yesu tumboni tu. Yesu alitaka kuwainua wasikilizaji wake wafuate mambo ya roho kuliko ya mwili. โBasi, mtu mmoja akamwambia, โMama yako na ndugu zako wako nje, wataka kusema naweโ. Lakini Yesu akamjibu huyo mtu aliyemwambia hivyo, โMama yangu ni nani, na ndugu zangu ni akina nani?โ Kisha akanyosha mkono wake juu ya wanafunzi wake akasema, โHawa ndio Mama yangu na ndugu zangu, maana yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye kaka yangu na dada yangu na mama yanguโโ (Math 12:46-50). Vilevile, wakati wa utume wake, alimsikia โmwanamke mmoja katika lile kundi la watu akisema, โHongera kwa mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyeshaโ. Yesu akamjibu, โBarabara, lakini heri yake zaidi yule anayelisikia Neno la Mungu na kulishikaโโ (Mk 11:27-28).
Bikira Maria alivyoshiriki Mateso ya Yesu
Katika kumfuata Mwanae Bikira Maria alitabiriwa wazi na mzee Simeoni uchungu kama upanga utakaopenya moyo wake, โTazama huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe uchungu ulio kama upanga utauchoma moyo wakoโ (Lk 2:34-35).Bikira Maria alishiriki kwanza mateso ya ukimbizi huko Misri kwa lengo la kumficha Mwanae asiuawe na Herode Mkuu, โHivyo Yosefu aliamka akamchukua mtoto pamoja na Mama yake akaondoka usiku akaenda Misri akakaa huko mpaka Herode alipokufaโ (Math 2:14-15).Bikira Maria alishuhudia hatua kwa hatua kuteswa kwa Yesu; wanafunzi walipokimbia au kumtazama kwa mbali, yeye alikuwa karibu akaona vema kila teso lililompata Mwanae. Kutokana na fungamano la upendo wa ajabu lililokuwepo kati ya Yesu na Mamaye, alipoyashuhudia yote aliteseka sana katika moyo wake safi, kiasi kwamba Bernardo wa Klervoo akasema, โMsalaba wa Yesu uliwasulubisha wote wawili, Yesu mwilini na Mama yake moyoniโ. Uaguzi wa mzee Simeoni ulitimia hivyo.Kadiri ya mtume Paulo kuteseka ni kutimiliza yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya Kanisa, โNa sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu hapa duniani nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristoโ (Kol 1:24). โโฆ maana tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wakeโ (Rom 8:17b).Pale msalabani Bikira Maria, kwa njia ya mtume Yohane alifanywa Mama wa wote wanaompenda Mwanae; kisha kumzaa pasipo uchungu Bwana wa uzima, pale alituzaa sisi kwa uchungu wa kutisha uliotokana na kumuona Mwanae akifa msalabani. Hata hivyo Bikira Maria aliendelea kumuamini Mwanae aliyeonekana ameshindwa.
Bikira Maria baada ya kifo cha Yesu
Bikira Maria alikuwepo hapo mwanzo wa Kanisa, akilivutia zaidi Roho Mtakatifu kwa sala yake. โHao wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria Mama yake Yesu na ndugu zakeโ (Mdo 1:14).Yesu alisema, โNinayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili, lakini atakapokuja huyo Roho wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli woteโ (Yoh 16:12-13). Kwa msaada wa Roho Mtakatifu heshima kwa Bikira Maria ilienea katika Kanisa lote tangu zamani kabisa kadiri ya utabiri wake kuwa ataheshimiwa na vizazi vyote, โKwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mdogo, hivyo tangu sasa vizazi vyote wataniita mwenye heriโ (Lk 1:48).
Recent Comments