Namna Mungu anavyojibu Sala au Maombi
Mungu ni mwenye Hekima, anajibu Sala zetu kwa kutupa kile tunachohitaji na chenye kutufaa na Sio kutupa kile tunachokitaka na kukitamani kwa kuwa anatupenda na kututakia mema.
Mungu ni mwenye Hekima, anajibu Sala zetu kwa kutupa kile tunachohitaji na chenye kutufaa na Sio kutupa kile tunachokitaka na kukitamani kwa kuwa anatupenda na kututakia mema.
Kama mtu anasali kila siku katika maisha yake hakuna kitu kitakachokuwa kigumu. Sala ni njia ya kujipatia neema za kuendesha maisha yetu. Usiache kusali kila siku hata kama upo katika hali gani.
Mungu daima ni Mwaminifu na mwenye Huruma. Kinachotakiwa ni kuamini kwamba kipo na kitakuwepo. Kusadiki kwamba kitafanyika na kitafanyika. Hii ndiyo Siri ya Imani.
Mungu haangalii matemdo ya mtu ya nje tuu, bali anaangalia ndani kabisa mawazo ya mtu na nia yake. Nia ya mtu ndiyo inayoonyesha mtu alivyo.
Sala ni kama chakula cha Roho, Bila sala roho inakufa. Tusali daima ili roho zetu ziwe hai siku zote.
Kwa kawaida kwenye maisha unapofikia Hatua unaona Mungu hayupo kabisa na wewe basi ujue huo ndio wakati ambao Mungu yupo karibu na wewe zaidi.
Mungu ni mwema sana tunapokua wadhambi anapotuadhibu haimaanishi kuwa anatuchukia. Inamaanisha kuwa anatuonya na hapendi turudie makosa.
Huwezi kusema unampenda Mungu usiyemuona kama huwapendi watu wale unaowaona. Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. Vile unavyotaka akutendee mtendee vivyo hivyo.
Mungu anasubiri sala zako kila siku. Anasubiri sala zako akujibu ili uone utukufu wake. Anasubiri sala zako ili akuze mahusiano yake na wewe. Sali daima kwani Mungu yupo milele kukusikiliza na kukuhudumia.
Uhuru Na Amani Ya Moyoni hupatikana kwa kusali wala sio kwa kusoma vitabu na kujua sana Mambo mengi.
Kila jambo lina Mkono wa Mungu juu yake hata kama limefanyika bila kupangwa au kukusudiwa. Mbele ya Mungu hakuna kitu kinachofanyika kwa Ajali au bahati mbaya.
Kutubu ndio njia pekee ya kumrudia Mungu. Toba ya kweli ndiyo iletayo maondoleo ya dhambi. Ukiondolewa dhambi unaimarishwa na kufanywa mya. Tubu usamehewe na kufanywa mpya.
Sala pasipo Imani thabiti, ya nia ya kweli, upendo wa kweli, unyenyekevu wa ndani na tumaini la kweli katika Amani ya rohoni; Haijakamilika na haifai kitu.
Mawazo ya Mungu ni makuu. Mungu anatuwazia mema daima. Hata unapopitia shida na matatizo katika maisha nia ya Mungu inabaki kuwa njema ya Kukuonyesha ukuu wake na kukuwezesha kumjua yeye. Pengine usingejua matendo ya Mungu bila kupitia shida na changamoto katika maisha. Mungu hapendi upate shida bali anaruhusu hayo ili upate faida ya kumjua na kujua uwezo wake. Hata Yesu ilibidi apitie mateso na kifo ili uwezo wa Mungu udhihirike baada ya kufufuliwa. Amini kuwa kuna mema mbele yako baada ya mateso haya ya sasa.
Wakati wazazi waliweza kuaamua kuzaa mtoto tuu, Mungu yeye alikuchagua wewe utungwe mimba na kukulinda ungali tumboni mwa mama yakoโฆ.Wakati wazazi wanasubiri kwa shauku kuona muonekano wako wewe, Mungu anawaweka wajukuu wa wazazi wako/ watoto wako ndani mwakoโฆ. Wakati wazazi wakitafuta chakula kwa ajili yako, Mungu yeye aliwawezesha kukipataโฆ. Wakati wazazi wakingoja kuona unavyoendelea kukua huku wakiwaza hatima ya maisha yako Mungu anakuendeleza na alishapanga maisha yako tangu alipokuchagua uwe mtu ukiwa tumboni mwa mama yakoโฆ. Wazazi wanaweza kukuombea kwa Mungu lakini Mungu ndiye anayeamua akufanyie nini maana Wewe ni wa kwakeโฆ.Wewe na wazazi wako ni watoto wa Baba mmoja ambaye ndiye Mungu.
Hakuna kitu cha Muhimu zaidi Duniani kama kumjua Mungu na kumuishi Mungu. Kila binadamu ameumbwa kwa ajili hii. Na Mungu anachotaka ndicho hichi, kumjua na kumuishi. Mengine yote ni maziada. Ukimuishi Mungu atakufanikisha katika yote.
Kama vile Baba anavyotamani mwanae akue katika maadili na aelekee katika njia nyoofu. Ndivyo na Mungu anavyotamani uachane na dhambi na kumfuata yeye.
Mungu ni mwenye Huruma na Upendo na Anataka watu wote waokolewe naye. Mungu hayupo kwa ajili ya kukuhukumu bali kwa ajili ya kukuhurumia na kukurehemu.
Kufanya Mambo mema ndipo kunaleta furaha ya kweli kwa Binadamu yeyote yule. Hakuna Binadamu anayefurahia kufanya maovu. Mema hayaambatani na majuto lakini uovu wowote unamajuto. Hata waovu wanafanyiana mema ili wapate furaha.
Kukosa hata mara moja inahesabika ni kukosea mbele ya Mungu. Kwa kuwa kwa Mungu hakuna kusema, ‘Kukosea mara moja sio kosa bali kurudia kosa ndio kosa’. Mbele ya Mungu kila kosa lina uzito wake haijalishi ni kosa la mara ya kwanza.
Recent Comments