Siri ya Imani kwa Mungu
Mungu daima ni Mwaminifu na mwenye Huruma. Kinachotakiwa ni kuamini kwamba kipo na kitakuwepo. Kusadiki kwamba kitafanyika na kitafanyika. Hii ndiyo Siri ya Imani.
Mungu daima ni Mwaminifu na mwenye Huruma. Kinachotakiwa ni kuamini kwamba kipo na kitakuwepo. Kusadiki kwamba kitafanyika na kitafanyika. Hii ndiyo Siri ya Imani.
Njia pekee ya Kumrudia Mungu tunapoanguka dhambini ni Njia ya Toba ya kweli ikiambatana na kukiri makosa na kusamehewa. Mara nyingi tunapotubu tunasahau dhambi za mawazo na kukumbuka za matendo tuu. Dhambi ya Mawazo pia ni dhambi yapaswa toba na maondoleo.
Mungu anaporuhusu ukaingia katika majaribu na mateso hana nia ya kukutesa bali anataka kukuimarisha. Mungu ni mwema kila wakati.
Sala ni ufunguo wa kufungulia mema na kufungia Mabaya. Tusali ili tufungue mema katika maisha yetu na tufunge mabaya katika maisha yetu.
Hakuna kitu cha Muhimu zaidi Duniani kama kumjua Mungu na kumuishi Mungu. Kila binadamu ameumbwa kwa ajili hii. Na Mungu anachotaka ndicho hichi, kumjua na kumuishi. Mengine yote ni maziada. Ukimuishi Mungu atakufanikisha katika yote.
Hakuna Binadamu anayemchukia Mungu kama hajichukii yeye mwenyewe na wale wanaomzunguka. Huwezi kusema humtaki Mungu kama hujichukii mwenyewe na wale waliokuzunguka vivyo hivyo huwezi kusema Unampenda Mungu kama hupendi wengine waliokuzunguka.
Upendo wa Mungu hauna kikomo. Mama anaweza kumchoka na kumtelekeza mwanae lakini Mungu kamwe hamchoki mtu.
Kutubu ndio njia pekee ya kumrudia Mungu. Toba ya kweli ndiyo iletayo maondoleo ya dhambi. Ukiondolewa dhambi unaimarishwa na kufanywa mya. Tubu usamehewe na kufanywa mpya.
Usiogope wala usisite kutubu na kuomba msamaha kwa Mungu. Uwe na Amani na Matumaini katika Huruma ya Mungu itokayo katika Upendo wake wa Mfano wa baba awapendavyo wanawe. Mungu anasubiri kukupokea kwenye mikono yake Ili akutunze kama mtoto wake kama utatubu na kumrudia yeye. Amua kumwendea leo! Anakungoja ni wewe tuuโฆ
Kufanya Mambo mema ndipo kunaleta furaha ya kweli kwa Binadamu yeyote yule. Hakuna Binadamu anayefurahia kufanya maovu. Mema hayaambatani na majuto lakini uovu wowote unamajuto. Hata waovu wanafanyiana mema ili wapate furaha.
Mungu ni mwema sana tunapokua wadhambi anapotuadhibu haimaanishi kuwa anatuchukia. Inamaanisha kuwa anatuonya na hapendi turudie makosa.
Uzuri wa Mungu ni kwamba anasamehe na kisha anasahau. Unapotubu dhambi zako na kutaka huruma zake yeye anakufutia uovu wote na kukufanya mpya.
Kukosa hata mara moja inahesabika ni kukosea mbele ya Mungu. Kwa kuwa kwa Mungu hakuna kusema, ‘Kukosea mara moja sio kosa bali kurudia kosa ndio kosa’. Mbele ya Mungu kila kosa lina uzito wake haijalishi ni kosa la mara ya kwanza.
Kwa njia ya sala Binadamu anampa Mungu Utukufu, Mungu anampa Binadamu Wokovu na Neema.
Uwe na maono au ndoto ya mambo unayotaka kufanya maishani naye Mungu atakubariki na kujidhihirisha katika ndoto zako.
Upendo wa Mungu hauna mwisho. Mtu anaweza akaacha kukupenda na kukusahau kabisa lakini kamwe Mungu haachi kumpenda Mtu wala hamsahau Mtu.
Jifunze na jijengea tabia ya kumsikiliza Mungu rohoni mwako unaposali. Sala ni mazungumzo ya Mungu na mwanadamu. Mazungumzo yanahusisha kuongea na kusikiliza.
Sala yoyote ili iwe SALA lazima itolewe kwa Imani, Upendo, Unyenyekevu na kwa Matumaini. Sala kama hii ndiyo ipendezayo mbele ya Mungu.
Sala za kila siku katika maisha ndiyo hazina kubwa na msaada hasa wakati wa kufa. Adumuye katika sala Mungu hatomwacha saa ya mwisho. Tusali, tusali, tusali daimaโฆ
Ukitaka kupata amani, tumaini katika Ahadi za Mungu. Ahadi ya Mungu ni hii “Hatoacha kutusaidia wala kututupa”.
Recent Comments