Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Msichana ambaye hajawahi kujamiiana anaitwa bikira, je mvulana huitwaje?

Neno “bikira” ni mtu yeyote ambaye hajawahi kujamii ana maishani mwake, awe mwanamke au mwanaume.
Zamani, watu walimtambua msichana bikira kwa njia ya kuhakikisha kwamba kile kiwambo chembamba ndani ya uke kipo. Lakini kwa sababu ngozi hii huweza kuchanika kwa njia nyingine zaidi ya kujamii ana, siyo kipimo kizuri cha kumtambua msichana ambaye hajajamii ana kabisa (yaani bikira).
Katika jamii nyingi ni kawaida kuwaita `bikira` wanawake ambao hawajawahi kujamii ana. Pia, jamii nyingi wanasisitiza umuhimu wa mwanamke kuwa bikira mpaka siku ya kuolewa. Hata hivyo, neno “bikira” hutumiwa kwa wanawake na wanaume.

Nini kinatokea wakati Virusi vya UKIMWI (VVU) vinapoingia mwilini na vinakwenda wapi katika sehemu ya mwili?

Virusi hivi vinakaa katika chembechembe nyeupe zilizopo kwenye majimaji ya mwili i wa binadamu hasa kwenye damu, shahawa na maji maji ya ukeni na maziwa ya mama anayenyonyesha. Ndani ya chembechembe nyeupe ndiyo mahali virusi vinakaa na kuendelea kuzaliana. Vikiwa ndani ya chembechembe nyeupe hizi, virusi huendelea kuzaliana hadi kusababisha chembechembe nyeupe hizi kupasuka.

Virusi hivi hupata nafasi ya kuendelea kushambulia chembechembe nyingine nyeupe za damu. Kwa kadri chembechembe nyeupe zilizoshambuliwa zinavyoendelea kupasuka ni kwa kiwango hicho hicho chembechembe nyeupe zinaendelea kuharibiwa na kupungua. Matokeo yake ni kupungua kwa kinga mwilini na mtu kuendelea kudhoofika.

Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?

Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa sababu huyo ndiye atakayekuwa mwenzi wake wa maisha. Katika kuchagua mchumba kila mtu ana mawazo yake kuhusiana na kilicho muhimu kuzingatiwa. Mara nyingi mhemuko una nguvu zaidi kuliko uamuzi wa kimantiki

Hata hivyo, vifuatavyo ni kati ya vigezo ambavyo vinaweza kuangaliwa:

• Chagua mtu anayekuheshimu wewe na wengine; Chagua mtu unayemwamini;
• Chagua mtu ambaye unaweza kuongea, kujadiliana, na kuhojiana naye kwa uwazi bila kugombana;
• Chagua mtu mwenye umri unaokaribiana na wa kwako;
• Chagua mtu anayependelea vile unavyopendelea;
• Chagua mtu ambaye ataelewa matatizo yako na yuko tayari kukusaidia kuyatatua; na
• Chagua mtu mwenye afya nzuri.

Hii inamaanisha pia kumpata mtu ambaye kabla ya kuanza kujaamiana naye, atakuwa tayari kwenda kupima kwa hiari kujua hali yake ya VVU na pia kuwa tayari kutumia kinga kwa maana ya kondomu hadi hapo mtakapojua hali zenu.

Wafahamishe wazazi wako mtu uliyemchagua kama mchumba na mtambulishe kwao i ili wamfahamu na yeye awafahamu wazazi wako. Wakati huohuo na wewe jaribu kuwafahamu wazazi wake. Usifanye uchumba wa haraka. Pata muda wa kutosha kumwelewa rafiki yako.

Kwa nini vijana wengine Albino wanaanza kujamiiana katika umri mdogo?

Kuna sababu nyingi ambazo zinamfanya kijana kuanza kujamiiana
katika umri mdogo. Baadhi ya sababu hizi ni kama vile:
• Ushindani kati ya vijana wa kuwa na vitu vya anasa kama
vile simu ya mkononi, saa na vitu vya kuchezea. Ama kutaka
mahitaji ya pesa kwa ajili ya kulipa ada ya shule.
• Shinikizo kutoka kwa rika wa kumfanya mtu ajiingize kwenye
kujamiiana. Shinikizo rika unakuwa na nguvu zaidi kwa
kijana Albino kwani yeye tayari anajiona ametengwa na
hivyo kushawishika zaidi katika mambo wanayofanya wengine
ili akubalike na wanarika hao.
• Kwa kuamini kwamba njia halisi ya kuonyesha mapenzi ni kujamiiana
na pia kulazimika kujamiiana hata kama ni kinyume
na matakwa yake kwa mtazamo kuwa haya ndio mapenzi ya
kweli.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About