Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Je, mwanamke anaweza kufikia mshindo (kufika kileleni)?

Ndiyo, mwanamke anaweza kufikia mshindo wakati wa kujamiiana. Dalili ya mwanamke kufikia mshindo katika kujamiiana ni ile hali ya pekee ya kujisikia vizuri kimwili. Tofauti na mwanaume, anapofikia mshindo mwanamke hakojoi kitu chochote.

Kwa kawaida mwanaume anakojoa manii wakati wa kujamii ana anapofikia mshindo. Kwa sababu dalili hii ni rahisi kuona baadhi ya watu wanadhani kwamba ni wanaume tu wanaofikia mshindo wakati wa kujamii ana. Lakini hii siyo kweli. Mwanamke pia hufikia mshindo, ingawa siyo rahisi kuuona.

Madhara ya pombe kwa mwili na akili

Pombe huingia kwenye damu na kuzunguka mwili mzima pamoja
na kwenye ubongo wako. Ina madhara kwa viungo vya mwili
wako na ubongo wako na hivyo huathiri tabia na hisia zako.

Unywaji wa pombe kupita kiasi unaweza kuathiri viungo vingi
kwa mfano, ini ambalo ndilo huathirika zaidi. Ini hilo linafanya
kazi ya kufyonza kilevi katika mwili wako. Kama ukinywa zaidi
utaathiri ini kiasi kwamba halitaweza kufanya kazi kikamilifu au
litashindwa kabisa hatimaye utakufa. Kilevi kingi husababisha
kansa ya ini na tumbo.

Hatari kubwa siku hizi ni kupata na kusambaza virusi vya
UKIMWI. Mlevi mara nyingi huwa mzembe na husahau kinga
muhimu kama vile kutumia kondomu wakati wa kufanya mapenzi.
Anaweza pia kufanya mapenzi na watu ambao hafahamu afya
zao, kama ni wagonjwa au la. Zaidi ya hayo mlevi mara nyingi
huwa dhaifu, hivyo ni rahisi kushambuliwa na magonjwa
mbalimbali pamoja na VVU.

Pombe inaathiri pia uwezo wa kufanya tendo la ndoa. Huwa ni
vigumu kwa uume kusimama. Pia huathiri ubongo hasa sehemu
zile zinazomiliki ufahamu na mihemko.

Kwanza unaweza kujisikia mchangamfu na huru, lakini mara
tu unaanza kujisikia taabu na kushindwa kutembea vizuri.
Utakuwa na matatizo ya kutoona vizuri na matatizo ya kutoa
uamuzi sahihi. Watu huanza kuwa na vijitabia vya ajabu na
vipya baada ya kulewa. Kugombana na watu wengine na kufanya
mambo yasiyokubalika kama vile kujikojolea mbele za watu.
Kama utaendelea kunywa kuna uwezekano mkubwa wa kupata
madhara. Kila dhara huharibu mamilioni ya seli za ubongo wa
binadamu.

Kwanza hutakuwa na kumbukumbu ya nini kimetokea, lakini
unaweza pia kupoteza kabisa kumbukumbu zako. Kama ukinywa
pombe kupita kiasi kwa muda mrefu unaweza kupungukiwa
akili na mwisho kuharibu kabisa akili. Pombe pia ni dawa ya
kulevya kwani huweza kukutawala. Watu waliotawaliwa na
pombe, hutumia pesa nyingi na muda mwingi kwenye pombe,
hali ambayo inaweza kuwa ni mzigo mzito kwa familia na jamii,
na pindi mtu anapotawaliwa, ni vigumu kunywa kidogo au kuacha
kabisa. Kama mtu atajaribu kuacha, hupata matatizo kama
kutetemeka, mapigo ya moyo kuongezeka, kutokwa na jasho
jingi, na kukosa usingizi wakati wa usiku. Hali hiyo husababisha
maumivu na ni hatari kwa watu ambao wametawaliwa na pombe.

Nini kinatokea wakati Virusi vya UKIMWI (VVU) vinapoingia mwilini na vinakwenda wapi katika sehemu ya mwili?

Virusi hivi vinakaa katika chembechembe nyeupe zilizopo kwenye majimaji ya mwili i wa binadamu hasa kwenye damu, shahawa na maji maji ya ukeni na maziwa ya mama anayenyonyesha. Ndani ya chembechembe nyeupe ndiyo mahali virusi vinakaa na kuendelea kuzaliana. Vikiwa ndani ya chembechembe nyeupe hizi, virusi huendelea kuzaliana hadi kusababisha chembechembe nyeupe hizi kupasuka.

Virusi hivi hupata nafasi ya kuendelea kushambulia chembechembe nyingine nyeupe za damu. Kwa kadri chembechembe nyeupe zilizoshambuliwa zinavyoendelea kupasuka ni kwa kiwango hicho hicho chembechembe nyeupe zinaendelea kuharibiwa na kupungua. Matokeo yake ni kupungua kwa kinga mwilini na mtu kuendelea kudhoofika.

Je, kama mwanamke na mwanaume wanapata watoto wa jinsia moja tu, ni kosa la nani?

Hakuna mwenye kosa, kwa sababu jinsia ya mtoto i inategemea na bahati na hamna uwezekano wa kupanga kuzaa aina fulani ya mtoto. Tulivyoona juu ni mwanaume ndiye aliye na aina mbili za mbegu. Aina moja husababisha kutokea mtoto wa kike na aina nyingine mtoto wa kiume. Mwanaume hana uwezo wa kuhakikisha achangie aina ya mbegu gani. Kwa hiyo, hata kama ni mwanaume anayeyakinisha jinsia ya mtoto, hana kosa, kwa sababu hana uwezo wa kuamua achangie mbegu ya aina gani.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About