Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama

Je, kuna tofauti za umri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za umri katika ngono/kufanya mapenzi? Ndio, kuna tofauti nyingi sana! Hiyo ndiyo sababu ni muhimu kuzungumza na mwenzi wako juu ya hilo kabla ya kuanza uhusiano wa kimapenzi.

Hapa kuna mambo mengi ya kuzingatia kuhusu tofauti za umri katika ngono/kufanya mapenzi:

  1. Hali ya afya- kwa ujumla, watu wazee hupatwa na matatizo ya kiafya kuliko watu vijana. Inaweza kuwa ni tatizo la nguvu za kiume au la kujamiana.

  2. Stamina- watu wazee hawana nguvu kama za watu vijana. Mtu mzee anaweza kuwa na uchovu haraka wakati wa kufanya mapenzi.

  3. Muda wa kufurahia- wanaume wazee wana uwezo wa kufanya mapenzi kwa muda mfupi tu kuliko wanaume vijana. Wanawake wazee wanaweza kuwa na shida ya kupata kilele.

  4. Ushauri wa kisaikolojia- wanaume wazee wana uwezekano mkubwa wa kuwa na matatizo ya kisaikolojia kuliko wanaume vijana. Matatizo kama haya yanaweza kusababisha tatizo la nguvu za kiume na shida nyingine za kufanya mapenzi.

  5. Uzoefu- watu wazee wana uzoefu zaidi wa kufanya mapenzi kuliko watu vijana. Wana uwezo wa kujua nini cha kufanya na jinsi ya kufanya kumfurahisha mwenzi wao.

  6. Mazoezi- watu wazee wanahitaji mazoezi ya kuongeza nguvu zao na stamina. Mazoezi haya yanaweza kuwasaidia kufurahia kufanya mapenzi zaidi.

  7. Mipango ya uzazi- wanawake wazee wanaweza kuwa na matatizo ya uzazi kuliko wanawake vijana. Ni muhimu kuzungumza na mwenzi wako juu ya mipango ya uzazi kabla ya kuanza uhusiano wa kimapenzi.

  8. Uthubutu- watu wazee wana uwezekano mkubwa wa kuwa na wasiwasi kuhusu kufanya mapenzi. Wanaweza kuwa na hofu ya kuhusiana na kuzidi kwa umri wao au kuhusu uwezo wao wa kufanya mapenzi.

  9. Kujielewa- watu wazee wana nafasi kubwa ya kujielewa zaidi kuliko watu vijana. Wanajua wanataka nini katika kipindi cha uhusiano wa kimapenzi.

  10. Upendo- Kufanya mapenzi kwa watu wazee ni kitu cha upendo. Ni muhimu kuonyesha upendo wako kwa mwenzi wako, na kuhakikisha unajua kile wanachotaka na wanachohisi.

Ili kumaliza, kuna tofauti nyingi za umri katika ngono/kufanya mapenzi. Ni muhimu kuzungumza na mwenzi wako juu ya hilo kabla ya kuanza uhusiano wa kimapenzi. Kwa njia hii, utaweza kupanga na kuwa tayari kwa tofauti hizo na kuhakikisha unapata uzoefu bora wa kimapenzi na mwenzi wako.

Hatua gani zichukuliwe dhidi ya wanaowakeketa au kuwachezea unyago Albino juani?

Swali hili linaonyesha mambo mawili ambayo ni mabaya. Jambo
la kwanza ni ukeketaji ambao ni kinyume dhidi ya haki ya afya
ya uzazi kwa mwanamke na ni uvunjaji sheria ya kukeketa mtoto
wa kike. Jambo la pili ni kuwacheza Albino unyago juani. Kitendo
hiki ni kuwaumiza Albino kwa sababu ya ulemavu walionao wa
ngozi watapata madhara wakikaa sana juani. Pia hii ni aina ya
unyanyapaa kwa nini weusi wachezeshwe ndani na Albino juani?

Hii ni imani potofu. Ushauri unaotolewa hapa ni kutoa taarifa
kwenye serikali na jamii husika ili wachukue hatua. Kwa sababu
ni vitendo labda vilivyokubalika na jamii kama mila, ni muhimu
kuhusishwa watu wenye umaarufu katika hiyo jamii ili waweze
kushawishi jamii kubadilika. Watu hawa ni kama viongozi wa
dini na wazee mashuhuri katika jamii.

Kupasuka kwa kondomu

Kupasuka kwa kondomu mara nyingi kunasababishwa na kondomu kutowekwa vizuri uumeni. Ni muhimu sana kutoa hewa ndani ya kondomu wakati wa kuvalisha uume. Kwa sababu ile hewa ndani ya kondomu inaweza ikasababisha kondomu kupasuka wakati wa kujamiiana.
Vilevile siyo vizuri kupaka mafuta kama vaselini juu ya kondomu ili kurahisisha kitendo cha kuingiliana. Mafuta kama vaseline yanadhoofisha uimara wa kondomu na yanarahisisha kondomu kupasuka. Mafuta haya yanayowekwa kwenye pakiti ya kondomu yanahifadhi uimara wa kondomu, na ni aina maalumu ya mafuta.
Ni muhimu kukumbuka kwamba mwanaume akivaa kondomu vizuri jinsi tulivyoeleza awali, uwezekano wa kondomu kupasuka ni mdogo sana.

Je, wasichana wana viungo gani vya uzazi na kazi zake ni zipi?

Viungo vya uzazi vya ndani vinaonekana katika michoro inayofuata:

Ukiangalia mchoro huu hapo juu, ambao unaonyesha via vya uzazi vya ndani, utaona uke, mfuko wa uzazi, kokwa za mayai na mirija ya kupitisha mayai. Uke ni mfereji ulio kati ya mfuko wa uzazi na sehemu ya nje ya via vya uzazi. Uke unatumiwa wakati wa kujamii ana, damu ya hedhi na mtoto hupita hapa. Urefu wa uke kwa wastani ni sentimita 7 hadi 8. Mfuko wa uzazi kwa kawaida huwa na ukubwa unaofikia embe ndogo. Yai moja lililorutubishwa hujishikilia kwenye kuta zake nazo huitunza mimba mpaka siku ya kuzaliwa mtoto. Wakati wa ujauzito mfuko wa uzazi hukua taratibu ukistahimili ukuaji wa mtoto. Kila upande wa mfuko wa uzazi i i ipo kokwa ya mayai, ambayo i ina ukubwa kama mbegu ya harage. Kila mwezi yai moja hukomaa kwa upande wa kulia au kwa upande wa kushoto na husafiri kwa kupitia katika mrija wa falopia. Kazi ya mirija ni kupitisha yai lililopevuka kila mwezi kutoka kwenye kokwa za mayai mpaka mfuko wa uzazi. Yai hutungishwa ndani ya mirija hii.

Ukiangalia mchoro huu unaoonyesha via vya uzazi vya nje, utaona midomo ya nje na midomo ya ndani, halafu kisimi, tundu la mkojo, sehemu ya haja kubwa na mlango wa uke. Midomo ya nje na ya ndani ni mii nuko ya ngozi na i iko hapo kuhifadhi sehemu za ndani za uke. Kisimi (au kinembe) ni sehemu ya juu kabisa ndani ya uke na ni sehemu ya uke ambayo humsaidia mwanamke awe na msisimko au asikie utamu wakati wa kujamii ana. Kama tulivyoona hapo juu, mlango wa uke ni tundu ambalo damu hutokea wakati wa hedhi. Pia ni sehemu unapoingia uume wakati wa kujamii ana na mtoto hutokea sehemu hii anapozaliwa. Tundu la mkojo ni juu ya mlango wa uke na ni tundu ambalo mkojo hutokea. Sehemu ya haja kubwa ni sehemu i inapopita haja kubwa (kinyesi).
Kama wewe ni msichana, unaweza kuamua kutumia kioo kujiangalia sehemu zako za via vya uzazi vya nje. Kwa njia hii unaweza kuyaelewa vizuri maumbile yako.

Ukweli kuhusu albino

  1. Je, ualbino unaambukiza? ……….. Hapana
  2. Ualbino ni ugonjwa? ………..Hapana
  3. Ualbino ni laana? ………..Hapana
  4. Ualbino ni kitu cha kawaida? ………..Hapana
  5. Ualbino unawapata tu watu weusi?……….. Hapana
  6. Watu wanaoishi na ualbino wana macho mekundu?……….. Hapana
  7. Albino ni watu wenye imani za ushirikina? ………..Hapana
  8. Albino wana nguvu za giza? ………..Hapana
  9. Je, Albino hawana akili? ………..Hapana
  10. Je, ni kosa la mwanamke anayezaa mtoto Albino? ………..Hapana
  11. Je, jamii ibadili mtazamo hasi iliyo nao kuhusu Albino?……….. NDIYO
Shopping Cart
41
    41
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About