Mafundisho ya Msingi ya Kanisa Katoliki: Makala za Katoliki

Mambo manne ya mwisho katika maisha

Mambo manne ambayo ni ya mwisho katika maisha ni;
  1. Kifo
  2. Hukumu
  3. Mbinguni
  4. Motoni
Mambo haya yote yanaweza kutokea wakati wowote bila kujua wala kutarajia

Kifo

Kifo ni kitu ambacho kinaweza kumpata mtu yeyote wa umri wowote awe mtoto kijana au mzee na kwa wakati wowote.
Maranyingi watu hawapendi kuongelea kuhusu kifo kwakua ni kitu ambacho kinampata kila mtu na hakipingiki wala hakina mjadala.

Hukumu

Baada ya kifo, inafuata hukumu, kila mtu atahukumiwa kulingana na matendo yake kama ulitenda mema utaenda mbinguni, na kama umetenda mabaya utaenda motoni.

Mbingu

Kama mtu akifa akiwa katika hali usafi wa moyo anaelekea mbinguni. Haijalishi ni kwa kipindi gani aliishi hivyo. Ila ni kwa hali gani kifo kilimkuta. Kwa sababu hii kila mtu anatakiwa aishi katika hali ya usafi wa moyo kwani hajui ni wakati gani atakutwa na kifo.

Motoni

Kama mtu akifa katika hali ya dhambi anaenda motoni. Kwa hiyo inatupasa tutumie vyema msamaa na huruma ya Mungu katika maisha yetu ili mwishi wetu uwe mzuri wakati bado tukiwa na muda.
Kila unapoishi ni lazima ufikirie mambo haya ukizingatia hujui wakati yanaweza kukupata. Kwa hiyo, nilazima uishi ukiwa unatafakari haya
ili uwe na mwisho mzuri.

Je, Kanisa Katoliki linatetea na kufundisha maadili ya kijinsia na thamani ya ndoa kati ya mwanaume na mwanamke?

Katoliki ni dini inayoheshimu na kufundisha thamani ya maisha ya binadamu. Kanisa Katoliki linafundisha maadili ya kijinsia na thamani ya ndoa kati ya mwanaume na mwanamke. Katika maudhui haya, tunaweza kuelewa jinsi Kanisa Katoliki linavyolinda na kufundisha thamani ya kijinsia na ndoa.

Kanisa Katoliki linatetea maadili ya kijinsia kwa sababu binadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu na anastahili kuheshimiwa. Maadili ya kijinsia yanahusu uhusiano kati ya mwanaume na mwanamke. Kwa maana hiyo, Kanisa linafundisha kwamba ngono ni kitendo kitakatifu na kinapaswa kufanywa ndani ya ndoa tu.

Ndoa ni sakramenti na ina thamani kubwa katika Kanisa Katoliki. Inapasa ichukuliwe kama ndoa ya kiroho, kati ya mwanaume na mwanamke, na haihusishi mtu mwingine yoyote katika uhusiano huo. Kama ilivyoelezwa katika Kitabu cha Mwanzo, mwanaume na mwanamke waliunganishwa na Mungu wakati walipoumbwa. Ndoa inaunganisha mwanamume na mwanamke katika upendo wa Mungu.

Neno la Mungu linaelezea wazi na kwa undani jinsi Kanisa Katoliki linavyofundisha maadili ya kijinsia na thamani ya ndoa. Kwa mfano, katika Mathayo 19:5 inasema, "Kwa sababu hiyo, mwanamume ataacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja." Hii inaonyesha kwamba ndoa ni kati ya mwanaume na mwanamke na hawapaswi kutengana.

Kwa mujibu wa Catechism ya Kanisa Katoliki, ndoa inapaswa kuwa na upendo wa dhati kati ya wawili na inapaswa kuheshimiwa. Kwa mfano, ndoa inapaswa kutimiza mahitaji ya kiroho, kihisia na kijamii ya wanandoa. Ndoa inapaswa kuwa ya kitakatifu na inapaswa kutimiza matakwa ya Mungu.

Kwa ufupi, Kanisa Katoliki linatetea na kufundisha maadili ya kijinsia na thamani ya ndoa kati ya mwanaume na mwanamke. Ndoa inapaswa kuwa ya kitakatifu na kutimiza mahitaji ya kiroho, kihisia, na kijamii ya wanandoa. Ndoa ni sakramenti katika Kanisa Katoliki na linapaswa kuheshimiwa na kufanywa ndani ya ndoa, kulingana na neno la Mungu.

Kwa nini Bikira Maria hakuwa anaombwa akiwa hai? Watu na mitume hawakuwa wanasali kumuomba yeye

Kwa hiyo Mitume na wakristu wa mwanzoni hawakuwa kumuomba wakati akiwa hai. Ila Baada ya Kifo chake na kupalizwa kwake Mbinguni walianza ibada kwake.

Kumbuka, Kifo cha Bikira Maria hakijaandikwa kwenye biblia kwa kua wakati anakufa vitabu vya biblia vilikua vimekwishaandikwa

Ndio maana anaitwa Mama wa Wakristu. Mama mbarikiwa

Rejea Ufunuo 12:1-17

Ushauri wangu kwa leo, ni Heri kuchagua kunyamaza

MITHALI 11:12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.

MITHALI 17:28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.

Changamoto kubwa tuliyonayo ni kwamba tunataka kuongea kila wakati, tunataka kujibu kila tunachokisikia, kila tunachokiona tunataka kukisemea kitu.

Kuna wakati tunasikia na kukutana na mambo ambayo kiuhalisia moyo unagoma kabisa kunyamaza, unatamani ujibu, unatamani uwaambie watu yale umefanyiwa, unatamani uelezee vile umeumizwa lakini kumbe si kila jambo linatakiwa kuongelewa.

Si kila ukionacho unatakiwa kukisemea kitu. Si kila usikiacho/uambiwacho ni lazima ujibu.

Si kila ufanyiwacho ni lazima umwambie kila mtu.

MUHUBIRI 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;

Ipo nguvu katika kunyamaza

Yapo mambo ambayo tunapaswa kuongea, kusema, lakini yapo mambo ambayo tunapaswa kunyamaza kwa ajili ya usalama wa Roho zetu.

Ni kweli kuna wakati unasemwa sana vibaya, unasingiziwa, unatukanwa nk nk, lakini ni lazima ukumbuke kwamba kuna mazingira ambayo hupaswi kujibizana hata kama umeumia kiasi gani.

Unajua ni kwanini?

Ukisemwa vibaya, ukitukanwa, ukidharauliwa lazima moyo utaghafilika, moyo ukighafilika lazima utakuwa na hasira na ghadhabu.

Ukiwa na hasira katu usitegemee kuwa utajadiliana na mtu kwa hekima.

Ukiongea utaongea katika uwepo wa hasira, ukijibu utajibu kulingana na kiwango cha hasira ulichonacho.

Sasa jiulize majibu yanayotoka kutokana na msukumo wa hasira huwa yanakuwaje?

Mazuri? Ya upole? Ya hekima? Ya unyenyekevu? I am sure jibu ni hapana.

Kama jibu ni hapana that means utaongea vitu vibaya ambavyo ni chukizo kwa MUNGU kwa sababu amesema maneno yetu na yakolee munyu (chumvi).

Sasa badala ya kuongea upumbavu na ukamkosea MUNGU kwanini usichague kunyamaza?

AMOSI 5:3 Kwa ajili ya hayo mwenye busara atanyamaza kimya wakati kama huo; kwa kuwa ni wakati mbaya.

Nimekuwa inspired sana na mwanamke Abigaili, ni kweli mumewe alikuwa na makosa, ni kweli alikuwa mlevi, lakini mwanamke huyu alijua ni wakati gani, na mazingira gani alipaswa kuongea na mumewe na alijua aongee nini. Alipomkuta mumewe yupo katika hali ya ulevi, ALINYAMAZA, alijua kuwa huu sio wakati wa kusema jambo lolote.

1 SAMWELI 25:1

Ni vyema sisi pia tukajifunza kusoma mazingira na nyakati na hali za watu zilivyo ili tujue ni wakati gani tujibu, tuongee nini na ni wakati gani tunyamaze

Kilinde kinywa, hakikisha haukiachi kinene mabaya – ZABURI 50:19.

Usipoteze marafiki na kuharibu mahusiano kwa ajili ya kinywa kibovu – MITHALI 11:9.

Ni vyema tukajifunza kujua ni neno gani tukitamka kwa wakati/hali/mazingira gani litakubaliwa –MITHALI 10:32.

ZABURI 19:14 – Bwana na akafanye maneno yetu yakapate kibali mbele zake MUNGU na mbele za wanadamu pia.

1SAMWELI 25:36

Umeumizwa, umekwazwa, umetukanwa, umedharauliwa, KATIKA MAZINGIRA YA HASIRA NA GHADHABU JITAHIDI KUNYAMAZA.

Ni kweli moyo na akili na hisia vinakusukuma kujibu, kubisha nk nk, lakini elewa impact za kujibizana ukiwa na hasira na hizo ni bora ukae kimya.

*”AKUSHINDAE KUONGEA, MSHINDE KUNYAMAZA
“Uwe na siku njema!

Ni nini umuhimu wa Bikira Maria katika imani ya Kanisa Katoliki?

Ni nini umuhimu wa Bikira Maria katika imani ya Kanisa Katoliki?

Katika imani ya Kanisa Katoliki, Bikira Maria ni mfano wa kuigwa kwa waamini wote. Yeye ni Mama wa Yesu Kristo na pia Mama yetu wa kiroho. Ni kwa sababu ya upendo na uaminifu wake kwa Mungu, ndio maana amekuwa mfano wa utakatifu, ukarimu, na ujasiri kwa waamini wa Kanisa Katoliki.

Kwa mujibu wa Biblia, Bikira Maria alipata ujumbe kutoka kwa Malaika Gabriel kuwa atapata mimba ya Mwana wa Mungu. Hii imeelezwa katika kitabu cha Luka 1:26-38. Hapa Maria alitii kwa unyenyekevu na kusema "tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; iwe kwangu kama ulivyosema." Kwa njia hii, alijitolea kwa Mungu, akisema ndiyo kwa mpango wa Mungu kwa ajili ya wokovu wa binadamu.

Bikira Maria pia alikuwa karibu sana na Yesu Kristo, Mwana wake. Yeye alikuwa upande wake kwa maisha yote, hata wakati wa mateso yake na kifo msalabani. Hii imeelezwa katika kitabu cha Yohana 19:25-27. Yesu alimwambia Yohane, "Huyo ni mama yako," na akamwambia Maria, "Huyo ni mwanao." Kwa njia hii, Bikira Maria akawa Mama yetu wa kiroho, na sisi sote tukawa watoto wake.

Bikira Maria pia ni mfano wa utakatifu na unyenyekevu kwetu sisi. Yeye alijitolea kwa Mungu kwa unyenyekevu kamili, na kutuonyesha kwamba ni kupitia utumishi na upendo kwa wengine ndio tunaweza kumtumikia Mungu. Kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Luka 1:48, "kwa maana ameutazama unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana tazama, tangu sasa vizazi vyote wataniita mwenye heri."

Kwa mujibu wa Catechism ya Kanisa Katoliki, Bikira Maria ni mfano wa utakatifu, kwani alikuwa mtakatifu kabisa, hata kabla ya kuzaa Yesu Kristo. Yeye alikuwa tayari amejitolea kikamilifu kwa Mungu kabla ya kumpokea Mwana wa Mungu. Kwa njia hii, yeye ni mfano wa utakatifu kwetu sisi, na kutuonyesha kwamba tunaweza kufikia utakatifu kupitia imani na utumishi kwa Mungu.

Kwa ufupi, Bikira Maria ni mfano wa utakatifu, ukarimu, na ujasiri kwa waamini wa Kanisa Katoliki. Ni kwa sababu ya upendo na uaminifu wake kwa Mungu, ndio maana amekuwa mfano wa kuigwa kwa waamini wote. Kwa kufuata mfano wake, tunaweza kufikia utakatifu na kupata wokovu wa milele.

Jifunze kitu Kwenye mfano huu kuhusu Maombi na kuomba

Nabii mmoja aliumwa
na Jino, lilimtesa sana…
Akapiga magoti kumlilia
Mungu ili amponye..
Mungu akamuonesha mti
flani ili majani yake
Yapate kumtibu..
Akaenda kwenye mti ule,
Akachukua majani yake
akatumia na kweli
akapona…
Baada ya Muda Mrefu
Kupita, nabii yule aliumwa
na Jino tena…
Safari Hii alienda
moja kwa moja kwenye mti
Na kuchuma majani yake
na kuyatumia,Lakini
hakupona..
Akaja tena Kwa Mungu
na kumwambia…
“Mbona ule mti niliutumia
Haukuniponyesha kama
Wakati ule? “
Mungu akamjibu…
“Mara ya Mwanzo ulipona
Kwa kuwa
ulinitegemea mimi, mara ya
Pili hakupona kwa kuwa
Uliutegemea Mti”..

KILA WAKATI TUNAPASWA
KUMUOMBA NA
KUMTEGEMEA MUNGU,
HATA KAMA KWA JAMBO
AMBALO ALISHATUJIBU..
KWA KUTOKUFANYA HIVYO
NDIYO MAANA MARA
KADHAA
TUNAKOSA MAFANIKIO…

✔Tulipooomba mchumba
Tulipompata
Hatukuombea Ulinzi wa
ndoa zetu, matokeo yake
Ni vilio kwenye ndoa
Karibu zote..

✔ Tuliomba watoto,
Tulipowapata
muda mwingi tukatumia
Akili zetu kuwalea
Na kusahau kumshirikisha
Mungu katika malezi yao,
mwisho wa yote
Tunaishia kusema
Watoto wa siku hizi…

✔ Tuliomba kazi kwa Mungu ,
Tulipopata tukaanza
Kutumia akili zetu katika
Kazi hizo na kuanza
Kudharau wenzetu na
Kuzisaliti ndoa
na familia zetu..
▪ Familia zinalia…
▪ Watoto wanalia
Baraka zitatoka wapi?

▪ Kabla ya Kupata kazi
Tulikuwa Hatukosi
Kanisani,
Hakukosi kwenye
Maombi…
TUMEPATA KAZI
TUMEKUWA BIZE
HAKUNA MAOMBI
WALA KANISANI..
Baraka zitokee wapi?
Mafanikio yatoke wapi?
Mshahara mkubwa
Lakini madeni kila siku,
Tena tunakopeshwa na
Tuliowazidi mshahara…

Wapendwa tustuke..
Tumrudie Mungu…
Tusisingizie uchawi..
Tumejiroga wenyewe..

Tumuweke Mungu mbele..

Tafakari chukua hatua

Huruma ya Mungu: Faraja na Ufariji katika Majaribu

Huruma ya Mungu: Faraja na Ufariji katika Majaribu

Huruma ya Mungu ni zawadi kubwa kutoka kwake kwa sisi wanadamu. Mara nyingi tunapokuwa katika majaribu, tunahitaji faraja na ufariji. Kwa nini unahitaji kumtegemea Mungu katika kila hali? Tunajua kwamba kuna mambo mengi ambayo tunayaweza kwa uwezo wetu, lakini kuna wakati ambapo tunahitaji msaada wa Mungu.

  1. Mungu yuko karibu na sisi katika kila hali

Kama vile mtoto anavyohitaji upendo na msaada wa mzazi, hivyo ndivyo tunavyohitaji upendo na msaada wa Mungu katika hali zetu ngumu. Kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Zaburi 46:1, "Mungu ndiye kimbilio letu na nguvu yetu, msaada unaopatikana wakati wa dhiki."

  1. Huruma ya Mungu ni kubwa kuliko dhambi zetu

Mungu hutupenda sana hata kama tunafanya makosa na kukosea. Kama ilivyoelezwa katika Warumi 5:8, "Lakini Mungu huonyesha upendo wake kwetu kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi." Kwa hiyo, hatupaswi kuhisi hatia sana tunapofanya makosa, bali tunapaswa kumgeukia Mungu kwa toba na kumwomba msamaha.

  1. Tunapaswa kumtegemea Mungu katika kila hali

Mungu hupenda sana kuwa karibu nasi na kutusaidia katika kila hali. Kama ilivyoelezwa katika Wafilipi 4:6-7, "Msijisumbue kwa lolote; badala yake, katika kila hali, kwa kuomba na kuomba omba, pamoja na kutoa shukrani, maombi yenu yawasilishwe kwa Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawalinde mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu."

  1. Mungu hutusaidia kwa njia zake za ajabu

Mungu hufanya miujiza na hutusaidia kwa njia ambazo hatutarajii. Kama ilivyoelezwa katika Yeremia 32:27, "Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa kila mwili; je, mambo yoyote ni magumu sana kwangu?" Kwa hiyo, tunapaswa kuwa na imani kwamba Mungu atatusaidia katika njia ambazo hatutarajii.

  1. Tunahitaji kumtegemea Mungu kabla ya kila jambo

Mungu anataka tuwe na uhusiano mzuri naye na atusaidie katika kila jambo tunalofanya. Kama ilivyoelezwa katika Methali 3:5-6, "Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, naye ataelekeza mapito yako."

  1. Mungu hutuongoza katika njia sahihi

Mungu anataka tuwe na maisha bora na yenye furaha. Kama ilivyoelezwa katika Zaburi 16:11, "Umenijulisha njia ya uzima; furaha kamili iko mbele za uso wako; raha za milele ziko mkononi mwako." Kwa hiyo, tunapaswa kumfuata Mungu na kumwomba atuongoze katika njia sahihi.

  1. Mungu anatupenda hata katika dhiki

Mungu hutupenda hata katika wakati wa dhiki na majaribu. Kama ilivyoelezwa katika Warumi 8:35, "Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?" Kwa hiyo, tunapaswa kumtegemea Mungu hata katika wakati mgumu.

  1. Mungu hutuponya na kutuponyesha

Mungu ni mponyaji wetu na hutusaidia katika afya zetu. Kama ilivyoelezwa katika Zaburi 103:2-3, "Msifie Bwana, nafsi yangu, wala usisahau fadhili zake zote. Yeye ndiye anayesamehe maovu yako yote, naye ndiye anayeponya magonjwa yako yote." Kwa hiyo, tunapaswa kumwomba Mungu atusaidie katika afya zetu na kutuponya.

  1. Mungu anataka tuwe na amani katika mioyo yetu

Mungu anataka tuwe na amani katika mioyo yetu. Kama ilivyoelezwa katika Yohana 14:27, "Amani yangu nawapa; nawaachia amani yangu. Mimi sipi kama ulimwengu upeavyo. Msiwe na wasiwasi wala msifadhaike." Kwa hiyo, tunapaswa kumwomba Mungu atupe amani katika mioyo yetu na kutusaidia kuishi kwa amani na furaha.

  1. Mungu hutupenda sana

Mungu hutupenda sana na anataka tuwe karibu naye. Kama ilivyoelezwa katika Yohana 3:16, "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Kwa hiyo, tunapaswa kumwomba Mungu atusaidie kuwa karibu naye na kutusaidia katika kila jambo tunalofanya.

Kwa hiyo, tunapaswa kumtegemea Mungu katika kila hali na kumwomba atusaidie katika majaribu. Kwa kuwa Mungu hutupenda sana, tunaweza kuwa na uhakika kwamba atatusaidia na kutupa amani katika mioyo yetu. Tunapaswa pia kuwa na imani kwamba Mungu atatuponya na kutuponyesha. Kwa hiyo, tunapaswa kumwomba Mungu atutegemeze katika kila jambo tunalofanya. Je, unafikiri nini kuhusu huruma ya Mungu? Jisikie huru kutoa maoni yako.

Je, Kanisa Katoliki linamwomba Bikira Maria?

Je, Kanisa Katoliki linamwomba Bikira Maria?

Ndio, Kanisa Katoliki linamwomba Bikira Maria kwa sababu yeye ni Mama wa Mungu na Mama yetu pia. Tunaamini kuwa Bikira Maria ni mtakatifu na mwenye nguvu ya kuombea kwa ajili yetu kwa Mungu. Tunaomba Bikira Maria kwa sababu tunajua kuwa yeye anajua mahitaji yetu na anaweza kuwasilisha mahitaji yetu kwa Mungu.

Katika Injili ya Luka, tunasoma kuwa Malaika Gabrieli alimwambia Bikira Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Maria alisema "tazama, mimi ni mtumishi wa Bwana; iwe kwangu kama ulivyosema." (Luka 1:38). Bikira Maria alikuwa mtii kwa Mungu na aliitikia wito wa Mungu kwa unyenyekevu mkubwa. Hivyo, Bikira Maria anatupatia mfano wa kuigwa katika utii kwa Mungu na kujikabidhi kwa mapenzi ya Mungu.

Kanisa Katoliki linatambua kuwa Bikira Maria ni mpatanishi wetu kwa Mungu. Kwa hiyo, tunaweka matumaini yetu kwa Bikira Maria, tunawaomba awakumbuke watoto wake na kutuletea baraka za Mungu. Bikira Maria ni Mama yetu wa huruma ambaye daima yuko tayari kutusaidia. Kupitia sala zetu kwa Bikira Maria, tunaweza kuzidi kuimarisha uhusiano wetu na Mungu.

Kanisa Katoliki linatambua kuwa Bikira Maria ni mtakatifu na ndio sababu tunamwomba. Tunajua kuwa yeye anasikiliza maombi yetu na anatuombea kwa Mungu. Kama vile Yesu alivyomwambia mama yake msalabani "Mama yako" na kumkabidhi kwa wanafunzi wake kuwa mama yao, tunaona kuwa Bikira Maria ni Mama yetu pia (Yohana 19:27).

Kanisa Katoliki limejenga mafundisho ya kuwaomba watakatifu, na hii inajumuisha Bikira Maria. Katika Catechism of the Catholic Church, tunasoma kuwa "katika kumwomba Bikira Maria, tunajiongezea tunaomba kwa watakatifu wote" (CCC 2679). Kama vile tunamwomba Bikira Maria, tunawajibika kuomba kwa watakatifu wengine pia. Kuwaomba watakatifu kunatupa nafasi ya kujifunza kutoka kwao na kusali kwa ajili ya baraka zao.

Kwa hiyo, jibu ni ndio, Kanisa Katoliki linamwomba Bikira Maria. Tunamwomba kwa sababu yeye ni Mama yetu wa Mbinguni na mpatanishi wetu kwa Mungu. Tunajua kuwa yeye anatusikiliza na tunamwamini kuwa anaweza kutuletea baraka za Mungu. Tunamwomba Bikira Maria ili kutia moyo na kuimarisha uhusiano wetu na Mungu. Kwa hiyo, tunasali, "Salamu Maria, Mama wa Mungu na Mama yetu."

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu nguvu za shetani?

Katika imani ya Kanisa Katoliki, Shetani ni adui wa Mungu na mwanadamu. Kanisa linakiri kuwepo kwake kama roho mwovu, ambaye anatafuta kuharibu kazi ya Mungu na kuongoza watu mbali na Mungu. Shetani anajulikana kwa majina tofauti katika Biblia, kama vile Ibilisi, Mpinzani, na Mshindani. Katika makala hii, tutajadili imani ya Kanisa Katoliki kuhusu nguvu za shetani na jinsi ya kupinga majaribu yake.

Kwa mujibu wa Biblia, shetani ni kiumbe cha kiburi ambaye alitaka kuwa sawa na Mungu. Alipotupwa nje ya mbingu kwa sababu ya dhambi zake, aliamua kuwa adui wa Mungu na wanadamu. Shetani hutumia mbinu mbalimbali kumshawishi mwanadamu kufanya dhambi na hatimaye kumwongoza mbali na Mungu. Hii inafanyika kupitia majaribu ya dhambi, kuitumia nafsi za watu ili kufikia malengo yake.

Katika Kanisa Katoliki, tunajua kuwa shetani hana nguvu sawa na Mungu. Nguvu zake ni za kudumu kwa muda mfupi tu. Shetani hutumia majaribu ya dhambi kumshawishi mtu kufanya maamuzi yasiyo sahihi na kumwongoza mbali na Mungu. Hata hivyo, tunajua kuwa nguvu ya Mungu ni kubwa kuliko zote, na tunaweza kupinga majaribu ya shetani kwa kumtegemea Mungu.

Kanisa Katoliki linatupa njia mbalimbali za kupinga majaribu ya shetani. Kwanza, ni muhimu kujifunza Neno la Mungu na kumtegemea Mungu kwa sala. Tunapojifunza Neno la Mungu na kuzingatia mafundisho yake, tunakuwa na uwezo wa kupinga majaribu ya shetani. Pili, tunaweza kuchagua maisha ya utakatifu na kuishi kwa kuzingatia sheria za Mungu. Kwa kufanya hivyo, tunakuwa nguvu zaidi kuliko majaribu ya shetani.

Kuna mafundisho mengi katika Biblia yanayohusu shetani na majaribu yake. Kwa mfano, Yakobo 4:7 inasema, "Mpingeni shetani, naye atawakimbia." Neno la Mungu pia linatupa mfano wa jinsi Yesu alivyopambana na majaribu ya shetani jangwani, na jinsi alivyotumia Neno la Mungu kukabiliana na majaribu hayo.

Catechism ya Kanisa Katoliki pia inatupa mwanga kuhusu imani ya Kanisa kuhusu shetani. Kwa mfano, Catechism inasema, "Shetani anachukua nafasi yake katika ulimwengu wa wakazi wa dunia, kuwarubuni na kuwafanya waasi dhidi ya Mungu." (CCC 395). Catechism pia inatupa mafundisho juu ya jinsi ya kupinga majaribu ya shetani, kama vile kusali Rosary na kufunga.

Kwa hitimisho, imani ya Kanisa Katoliki kuhusu nguvu za shetani ni kwamba shetani ni adui wa Mungu na wanadamu, ambaye anajaribu kuwafanya watu waache njia za Mungu. Hata hivyo, tunajua kuwa nguvu ya Mungu ni kubwa kuliko zote, na tunaweza kupinga majaribu ya shetani kwa kumtegemea Mungu na kufuata Neno lake. Kama Wakatoliki, tunaweza kupambana na majaribu ya shetani kwa kusali, kufunga, na kuzingatia sheria za Mungu.

Je Bikira Maria Alizaa Watoto Wengine?

Mapokeo kuhusu Bikira Maria yanaonyesha alikuwa binti pekee wa wazee watakatifu Yohakimu na Ana. Vilevile
Mt. Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa hata moja. Ndiyo maana kwenye
litania yake tunamuita mwenye usafi kamili. Yosefu likufa kabla Yesu hajaanza utume kwa kubatizwa kwenye mto
Yordani. Sisi tunasadiki Maria ni “Bikira daima”.
Ndugu wa Yesu wanaosemwa katika Injili ni kina nani?
Wanaosemwa katika Injili “ndugu zake Yesu” si watoto
wa Bikira Maria wala Yosefu mtakatifu, bali ndugu wa kiukoo waliokuwa jirani sana na familia hiyo takatifu. Kama
Bikira Maria angekuwa na watoto wengine, je, Yesu Bwana wetu asingekuwa amefanya kosa la kiudugu
kuwanyang’anya Mama yao na kumfanya awe Mama wa mtume Yohane alipomkabidhi msalabani, “‘Mwana, tazama
Mama yako’. Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake” (Yoh 19:27).
Katika Agano Jipya yupo Yakobo anayeitwa na mtume Paulo “ndugu yake Bwana” (Gal 1:19): Yakobo huyo
alikuwa maarufu katika Kanisa la Yerusalemu (Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal 2:9). Yakobo huyo si mtume
Yakobo mwana wa Alfayo, wala mtume Yakobo kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni Yakobo ndugu yake Yose na
mama yao kwenye Injili anaitwa “Maria mwingine”, si Maria Mama wa Yesu. “Walikuwepo pia wanawake
waliotazama kwa mbali. Miongoni mwao akiwa Maria Magdalena, Salome na Maria mama wa akina Yakobo mdogo
na Yose” (Mk 15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa wengi hivyo, tujue
kuwatofautisha kwenye Injili. Bikira Maria Injili zinamtaja kama “Mama wa Yesu”.

Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?

Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.

Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;

1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu

Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)

2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi

19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.

3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12

Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.

4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu

Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno “Binamu” kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.

5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja

Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.

6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake

Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.

7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye

26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.

Majivuno na Kujikweza Mbele ya Mungu

Rejea Luka 14:7-24 na Luka 18 :9-18
Mungu anakawaida ya kumkweza yoyote ajishushaye na kumshusha yule ajikwezaye. Vile unavyojiona bora mbele ya Mungu na mbele ya watu ndivyo na Mungu anatakavyokuonyesha kuwa wewe sio bora au wewe sio zaidi ya wengine.

Madhara ya Kujikweza au majivuno

1. Sala zako hazitajibiwa kwa kuwa mara zote nia ya sala zako zitakua ni za kujitakia makuu.
2. Kusahau nafasi ya Mungu katika maisha yako na kuhisi unajitosheleza kwa yote.
3.Kusahau nafasi na umuhimu wa wengine kwa kuhisi kuwa hawana thamani kama wewe.

Dalili za Kujikweza au majivuno

1.Kutaka au kupenda kuwa na nafasi ya kwanza kwenye kila kitu.
2. Kukosa uvumilivu
3. Kuwa na hofu ya kushindwa na kufedheheshwa
4.Kukosa upendo na kujali kwa wengine
5. Kupungua imani kwa Mungu. Yani kuhisi kama Mungu anaweza kufanya au hawezi.
6. Kupungua ukaribu wako kwa Mungu.
7.Kutokupenda kusali /kuomba Mungu.

Dawa ya majivuno au jinsi ya kujishusha

1.Kujifunza unyenyekevu.
2.Kujifunza upendo wa kweli kwa Mungu na wengine.
3. Jifunze kuwaombea wengine. Hii itasaidia kujenga unyenyekevu.
4. Kujifunza kuridhika
5. Jifunze kufurahia mafanikio ya wengine.
6. Usiwe muongeaji sana na mchunguzi wa mambo ya watu sana.

Kuumbwa kwa mtu, Mungu alivyoumba binadamu

Mtu ni kiumbe pekee chenye mwili na roho kilichoumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Mungu alipotaka kumuumba mtu alisema “Tumfanye mtu kwa mfano wetu na sura yetu” (Mwa. 1:26-27)
Kuumbwa kwa sura na mfano wa Mungu maana yake tuna roho zenye akili na utashi yaani uwezo wa kutofaitisha mema na mabaya na zitakazoishi milele.
Watu wa kwanza walikua ni Adamu na Eva(Hawa), ambapo Adamu aliumbwa kwa udongo na kupuliziwa roho yenye uhai, na Eva aliumbwa kwa mfupa wa ubavu wa Adamu, akamtia roho (Mwa 2:7 na Mwa 2:21-24)
Baada ya kuumba watu Mungu aliwafundisha Dini, ambapo Dini ni mabo yatupasayo kutenda kwa Mungu Bwana wetu na Baba yetu
Mungu ametuumba ili tumjue, tumpende, tumtumikie tulipo wazima hapa duniani hata mwisho tukishakufa tuende kwake Mbinguni katika makao ya raha milele (Mwa. 2:7; Mt 19:17; Yoh 14:1-3 na Yoh 17:24).
Mungu aliwapa watu wa kwanza neema ya utakaso na neema nyingine nyingi na kukaa paradisi wenye heri bila kufa (Mwa 2:16-17), Lakini Adamu na Eva walitenda dhambi ya kutotii, wakataka kuwa kama Mungu lakini bila Mungu na pasipo kufuata maagizo ya Mungu.(Mwa 3:1-16)
Dhambi ya asili na kosa la Adamu na Eva
Adamu na Eva walitenda dhambi ya asili ambayo ni hali ya kukosa utakatifu na hali ya asili ya urafiki na Mungu ambayo kila binadamu anazaliwa nayo.
Baada ya kutenda dhambi yao ya kiburi na uasi walipewa adhabu zifuatazo;
  • Walipoteza neema ya utakaso
  • Walifukuzwa paradisini
  • Walipungukiwa na akili na kushikwa na tamaa ya kutenda dhambi
  • Walipata mahangaiko na tabu nyingi
  • Kupaswa kufa (Mwa 3:16-20; 5:5)
Baada ya kosa la Adamu Mungu aliahidi kuwaletea Mkombozi. (Mwa 3;15)

MAFUNDISHO KUHUSU NAFASI YA MAMA BIKIRA MARIA

Leo nimeamua kutoa makala kuhusu Bikira Maria Baada ya maswali mbalimbali kuibuka kuhusu nafasi yake kwetu sisi. Chanzo cha makala hii ni www.alfagems.com

MAFUNDISHO KUHUSU NAFASI YA MAMA B. MARIA

Sisi Wakatoliki nyakati hizi zilizojaa madhehebu mbalimbali ya Kikristo, yanayotumia Biblia na kuitafsiri kadiri ya
imani yao ama wenyewe wanavyojisikia kwa namna fulani, tunajikuta tukichanganyikiwa na pengine kuona aibu ya
kumheshimu Mama Bikira Maria. Tunapoanza kuchunguza nafasi yake katika fumbo la ukombozi wa mwanadamu,
tunakiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49). Halafu tunakiri kwa unyenyekevu
wote pamoja na Yohane Mbatizaji, “Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu” (Yoh 3:27). Hivyo yale yote
tunayoyasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia mwenyewe bali amejaliwa na Mwenyezi Mungu na kuitikia kwa
hiari fumbo la mpango wake.

MAANDIKO YANASHUHUDIA UMUHIMU WA WATU UNAOTOFAUTIANA

Maandiko matakatifu yanawasifu watu mbalimbali kutokana na walivyomuamini Mungu na kutenda makuu kwa
ajili ya taifa lake. Abrahamu alimuamini na kuwa tayari kumtolea sadaka mwanae Isaka, tukio lililomfanya apate
baraka ya pekee ya kuwa baba wa waamini (Mwa 22:15-18). Yosefu, kipenzi wa Yakobo, alikuwa mwaminifu hata
akaliokoa taifa lisiangamie kwa njaa (Mwa 50:20). Musa ndiye mkombozi wa taifa la Mungu katika Agano la Kale:
aliongoza Israeli kutoka utumwani Misri akalipatia sheria kutoka kwa Mungu katika mlima Sinai. Maandiko ya
Agano la Kale yanakiri, “Wala hajainuka kiongozi kama alivyokuwa Musa” (Kumb 34:10-12). Kwa kuwa watu hao ni
wengi mno tunaorodhesha wafuatao: Yoshua, Debora, Gideoni, Samsoni, Samweli, Ruthu, wafalme Daudi na
Solomoni, manabii Eliya, Yeremia na Ezekieli. Nabii Isaya ana sifa ya pekee katika kumchora Masiya. Mwishoni
Bwana Yesu mwenyewe anamsifu Yohane Mbatizaji akisema, “Ni mkuu kati ya uzao wa wanawake” (Lk 7:24-28).
Bikira Maria ana nafasi gani kati yao? Hao tuliowataja walitenda kweli mambo makuu kwa imani, lakini Bikira
Maria yuko juu sana kupita hao wote, tena kwa mbali: yeye ni malkia wa makundi yote ya mbinguni, sio ya watu
tu, bali hata ya malaika. Mapokeo ya mashariki humuita “daraja linalounganisha dunia na mbingu”, “mfano
aliouona Yakobo” (Mwa 28:12).

BIKIRA MARIA KATIKA BIBLIA

1. UTABIRI KUHUSU BIKIRA MARIA, EVA MPYA
Mapokeo yamtazama Bikira Maria kama Eva mpya atakayemshinda nyoka wa kale (Ibilisi). Kwa nini Eva mpya?
Kwa sababu Eva wa kale alidanganywa na kuangushwa na Shetani, hivyo alitenda dhambi. Kumbe Maandiko
matakatifu yanatupatia utabiri kuhusu Eva mpya atakayemshinda adui (Shetani) kwa kumponda kichwa: “Nitaweka
uadui kati yako na huyu mwanamke, kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa chako” (Mwa 3:15).
“Tazama Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamuita jina lake Emanueli, yaani Mungu
pamoja nasi” (Isa 7:14). Dondoo hilo lilinganishwe na Lk 1:34-35, “Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje
neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu akakujilia juu yako, na nguvu zake
Aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu”.
Utabiri mwingine wasema, “Litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa
matunda. Na Roho wa Bwana atakaa juu yake, Roho ya hekima na ufahamu, Roho wa shauri na uwezo, Roho wa
maarifa na ya kumcha Bwana” (Isa 11:1-2). Je, shina hilo si yeye Mama Bikira Maria, na tawi alilochipusha si
Mwanae Bwana wetu Yesu Kristo?
“Umebarikiwa wewe katika kila hema la Yuda na katika kila taifa, nao wanaposikia jina lako watafadhaika.
Imani yako haitatoka mioyoni mwa watu wanaoukumbuka uweza wa Mungu milele” (Yudithi 14:7; 15:9).
Linganisha dondoo hili na Lk 1:42, “Akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe kuliko wanawake wote,
na yeye utakayemzaa amebarikiwa”. Je, utasema Bikira Maria ni mtu wa ziada katika mpango wa Mungu?
Tena tunasoma, “Imba, ee binti Sion, piga kelele, ee Israeli, furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, ee binti
Yerusalemu. Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana yu katikati yako” (Sef 3:14-15). Linganisha dondoo hilo na
Injili: “Malaika akaingia nyumbani mwake akamwambia, Furahi Maria, umejaliwa neema kubwa, Bwana yu pamoja
nawe” (Lk 1:28).
2. BIKIRA MARIA KATIKA AGANO JIPYA
Mambo yaliyotabiriwa katika Agano la Kale yametimia katika Agano Jipya: ukombozi wetu ulianza pale Bikira
Maria alipokubali fumbo la umwilisho wa Mwana wa Mungu, akisema kwa hiari, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, na
iwe kwangu kama ulivyonena” (Lk 1:38).
Je, Bikira Maria ni bahasha? Siku hizi kuna baadhi ya waheshimiwa ambao wanadhani kujua Maandiko kuliko
watu wengine, tena wanadai wanaye Roho Mtakatifu; kumbe wanadiriki kumuita Mama huyo mtakatifu, eti ni
“bahasha” ambayo ikileta barua haina kazi! Jambo hili linasikitisha sana na sio tu kumkosea heshima Mama yetu
mpendwa wa mbinguni, bali inaweza pia kuwa kufuru kwa Mwenyezi Mungu aliyemuumba kama msaidizi wa
Mkombozi aliyejaa neema.
Manabii mbalimbali kwa mwanga wa Roho Mtakatifu walimuagua kwa heshima; Mama Elizabeti alijiona hastahili
kutembelewa naye akamuita, “Mama wa Bwana wangu”; mzee Simeoni alimuagulia mateso yenye uchungu kama
upanga yatakayopenya moyowe. Bwana Yesu aliyefurika Roho Mtakatifu tangu nukta ya kuchukuliwa mimba,
wakati alipokaribia kufa pale msalabani alimuita, “Mama”; jumuia ya Mitume na wafuasi wa kwanza walimtaja
kipekee ilivyo ishara ya heshima. Je, Roho Mtakatifu ndiye anayewaongoza hawa ndugu zetu wamuite bahasha? Je,
ni Roho yuleyule aliyewaongoza Mitume na manabii ama roho ya aina nyingine? “Wapenzi wangu, msisadiki kila
mtu asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa
Mungu au la, maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni” (1Yoh 4:1).
Bikira Maria sio “chombo” tu, bali mshiriki wa kazi ya ukombozi ya Mwanae. Kadiri ya mtume Paulo kuteseka ni
kutimiliza yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya Kanisa, “Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu,
maana kwa mateso yangu hapa duniani nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristo” (Kol
1:24). “… maana tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake” (Rom 8:17b). Katika hilo la
kumfuata Mwanae katika mateso Bikira Maria alitabiriwa wazi na mzee Simeoni, “Tazama huyu amewekwa kwa
kuanguka na kuinuka wengi katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe uchungu ulio kama
upanga utauchoma moyo wako” (Lk 2:34-35).
Bikira Maria alishiriki mateso ya ukimbizi huko Misri kwa lengo la kumficha Mwanae asiteswe na Herode, “Hivyo
Yosefu aliamka akamchukua mtoto pamoja na Mama yake akaondoka usiku akaenda Misri akakaa huko mpaka
Herode alipokufa” (Math 2:14-15).
3. BIKIRA MARIA MWOMBEZI KATIKA HARUSI YA KANA:
Mama Bikira Maria anaonekana mwenye kuonea
huruma wenye shida: kwa ombi lake huko Kana ya Galilaya Yesu aligeuza maji kuwa divai, na wanafunzi wake
wakamwamini (Yoh 2:1-12).
4. BIKIRA MARIA AFANYWA EVA MPYA:
Juu ya Eva wa zamani imesemwa ni Mama wa walio hai: “Adamu
akamwita mkewe jina lake Hawa, kwa kuwa ndiye aliye Mama wa walio hai” (Mwa 3:20). Hata hivyo Agano Jipya
linaonyesha Adamu na Eva wa zamani wametuletea kifo (Rom 5:12).
Yesu, aliye Adamu mpya, alipokuwa anakamilisha sadaka ya ukombozi pale msalabani alimfanya Bikira Maria
awe Eva mpya kwa kitendo cha kumkabidhi mwanafunzi, tena yule aliyempenda zaidi. “Basi Yesu aipomwona
Mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda amesiMama karibu akamwambia Mama yake, Mama, tazama
Mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama Mama yako” (Yoh 19:26-27). Zaburi yasema, “Lakini juu
ya Sion itasemwa, Sion ni Mama yao wote; Mungu mkuu ameuthibitisha. Mwenyezi Mungu ataorodhesha mataifa
na kuandika juu ya kila moja, Huyu chanzo chake ni Sion” (Zab 87:5-6).
Pale msalabani Bikira Maria:
• alifanywa Mama wa wote wanaompenda Mwanae;
• alifanywa malkia wa wafiadini;
• kisha kumzaa pasipo uchungu Bwana wa uzima, pale alituzaa sisi kwa uchungu wa kutisha uliotokana na
kumuona Mwanae akifa msalabani. Hata hivyo Bikira Maria aliendelea kumuamini Mwanae aliyeonekana
ameshindwa;
• katika kuteswa kwa Yesu Bikira Maria alishuhudia hatua kwa hatua; wanafunzi wa Yesu walipokimbia na
kumtazama kwa mbali, Bikira mtakatifu alikuwa karibu akaona vema kila teso lililompata. Tena
kutokana na fungamano la upendo wa ajabu lililokuwepo kati ya Yesu na Mamaye, aliposhuhudia mateso
ya Mwanae aliteseka sana katika moyo wake safi usio na doa, kiasi kwamba baadhi ya watakatifu
wanasema, Msalaba wa Yesu uliwasulubisha wote, Yesu mwilini na Mama yake moyoni. Uaguzi wa mzee
Simeoni ulitimia hivyo.

JE, BIKIRA MARIA ALIZAA WATOTO WENGINE?

Mapokeo kuhusu Bikira Maria yanaonyesha alikuwa binti pekee wa wazee watakatifu Yohakimu na Ana. Vilevile
Mt. Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa hata moja. Ndiyo maana kwenye
litania yake tunamuita mwenye usafi kamili. Alikufa kabla Yesu hajaanza utume kwa kubatizwa kwenye mto
Yordani. Sisi tunasadiki Maria ni “Bikira daima”.
Ndugu wa Yesu wanaosemwa katika Injili ni kina nani? Wanaosemwa katika Injili “ndugu zake Yesu” si watoto
wa Bikira Maria wala Yosefu mtakatifu, bali ndugu wa kiukoo waliokuwa jirani sana na familia hiyo takatifu. Kama
Bikira Maria angekuwa na watoto wengine, je, Yesu Bwana wetu asingekuwa amefanya kosa la kiudugu
kuwanyang’anya Mama yao na kumfanya awe Mama wa mtume Yohane alipomkabidhi msalabani, “‘Mwana, tazama
Mama yako’. Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake” (Yoh 19:27).
Katika Agano Jipya yupo Yakobo anayeitwa na mtume Paulo “ndugu yake Bwana” (Gal 1:19): Yakobo huyo
alikuwa maarufu katika Kanisa la Yerusalemu (Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal 2:9). Yakobo huyo si mtume
Yakobo mwana wa Alfayo, wala mtume Yakobo kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni Yakobo ndugu yake Yose na
mama yao kwenye Injili anaitwa “Maria mwingine”, si Maria Mama wa Yesu. “Walikuwepo pia wanawake
waliotazama kwa mbali. Miongoni mwao akiwa Maria Magdalena, Salome na Maria mama wa akina Yakobo mdogo
na Yose” (Mk 15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa wengi hivyo, tujue
kuwatofautisha kwenye Injili. Bikira Maria Injili zinamtaja kama “Mama wa Yesu”.

JE, WAKATI WA KUFANYA UTUME YESU ALIMDHARAU MAMA YAKE?

Wengine husoma Maandiko matakatifu wakiishia ujuu bila ya kufikiria wala kulinganisha na mistari mingine.
Hivyo hukwazwa na semi kadhaa za Bwana Yesu ambazo kimsingi hazimpingi Mama yake, bali zinampongeza.
“Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika lile kundi la watu akasema, ‘Hongera kwa mwanamke
aliyekuzaa na kukunyonyesha’. Yesu akamjibu, ‘Barabara, lakini heri yake zaidi yule anayelisikia Neno la Mungu na
kulishika’” (Mk 11:27-28).
Tena lingine lasema, “Basi, mtu mmoja akamwambia, ‘Mama yako na ndugu zako wako nje, wataka kusema
nawe’. Lakini Yesu akamjibu huyo mtu aliyemwambia hivyo, ‘Mama yangu ni nani, na ndugu zangu ni akina nani?’
Kisha akanyosha mkono wake juu y aweanafunzi wake akasema, ‘Hawa ndio Mama yangu na ndugu zangu, maana
yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye kaka yangu na dada yangu na Mama
yangu’” (Math 12:46-50).
Je, sehemu hizi za Maandiko zinampinga kweli Bikira Maria au zinampongeza? Sababu:
• Jamaa yake Elizabeti alimpongeza, tena akiongozwa na Roho Mtakatifu, “Heri yako wewe uliyesadiki
kwamba yatatimia yale uliyoambiwa na Bwana” (Lk 1:45).
• Bikira mtakatifu alipopashwa habari na malaika hakukataa mpango wa Mungu, bali kwa hiari yake
alikubali fumbo la mpango wake. “Maria akasema, ‘Mimi ni mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu kama
ulivyonena’. Kisha malaika yule akaenda zake” (Lk 1:38).
• Bwana Yesu alitaka kuwainua wasikilizaji wake wafuate mambo ya Kiroho kuliko ya mwilini. Hivyo ni
kweli, Bikira Maria anasifiwa kwanza kwa imani yake, iliyokuwa ya juu zaidi kushinda hata ile ya
Abrahamu, kuliko kwa kumchukua Yesu tumboni tu. Hata hivyo tusisahau kuwa Yesu, kama mtu yeyote
mcha Mungu, aliwaheshimu wazazi wake, tena tunasikia aliwatii. “Basi, akarudi pamoja nao Nazareti,
akawa anawatii” (Lk 2:51).
Naomba, kabla hujahukumu neno moja, angalia ujumla wake.
Yesu alizaliwa na Bikira mtakatifu, ndiye aliyemlea na kuhangaika naye huko na huko hata Misri ili kumuepusha
na kifo. Ishara ya kwanza kwenye maisha ya hadhara iliyongozwa na Bikira Maria huko Kana. Maria alikuwepo hata
wakati wa Yesu kuteswa, akiteseka pamoja naye. Pale msalabani alikabidhiwa Kanisa kwa njia ya Yohane mtume.
Bikira Maria alikuwepo hapo mwanzo wa Kanisa, na ndiye aliyelivutia zaidi Roho Mtakatifu kwa njia ya sala yake.
“Hao wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria Mama yake Yesu na
ndugu zake” (Mdo 1:14).

DOGMA ZA KANISA KUHUSU BIKIRA MARIA

Kuna mafundisho makuu manne kumhusu Bikira Maria ambayo ni lazima kila Mkatoliki ayasadiki kutokana na
ufunuo wa Mungu:
1. B. Maria mkingiwa dhambi ya asili
2. B. Maria Mama wa Mungu
3. B. Maria Bikira daima
4. B. Maria kupalizwa mbinguni mwili na roho

MKINGIWA DHAMBI YA ASILI

Tunasadiki Bikira Maria tangu atungwe mimba Mungu alimkinga na kila doa la dhambi kwa kutazamia stahili za
Yesu Kristo aliye Mkombozi wa binadamu wote. Ndiye mwanakanisa aliyekombolewa kwa namna bora kushinda
viungo vyote vya Kanisa. Maisha yake yote hakutenda dhambi hata moja. Mapokeo ya mashariki yanamuita A
Panagia = Mtakatifu tu. Dogma hiyo ilitangazwa na papa Pius IX mwaka 1854, hata mwaka 1858 Bikira Maria
alijitambulisha huko Lurdi (Ufaransa) kwa Mt. Bernadetta Soubirous kama Mkingiwa. Tena pale Fatima (Ureno)
tumefunuliwa moyo wake safi usio na doa.

MAMA WA MUNGU

Injili ya Yohane inaanza kwa kishindo, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,
naye Neno alikuwa Mungu” (Yoh 1:1). Huyo Mungu Mwana ndiye aliyetwaa ubinadamu katika Bikira Maria
akazaliwa mtoto, jina lake Yesu, maana yake Mungu Mwokozi. Huyo ni binadamu kama sisi isipokuwa hana
dhambi. Ubinadamu wa Yesu unategemea Nafsi yake ya Kimungu, hivyo akisema, ‘Mimi’, anamaanisha Nafsi yake
ya Kimungu. Ndiyo maana aliwaambia Wayahudi, “Kweli nawaambia, kabla Abrahamu hajazaliwa, nalikuwepo”
(Yoh 8:50). “Kama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhai” (Yoh 5:26).
Je, Bikira Maria ni Mama wa Mungu tangu lini? Mtume Paulo anaeleza, “Wakati maalumu ulipotimia Mungu
alimtuma Mwanae aliyezaliwa na mwanamke” (Gal 4:4). Ni kwanzia wakati huo: sasa imepita miaka 2006 tangu
Bikira Maria ajiliwe na sifa hiyo ya kumchukua mimba, kumzaa, kumnyonyesha na kumlea mtu ambaye kwa asili ni
Mungu. Cheo hicho kimemuinua juu kuliko hata malaika, akawa malkia wao. “Malaika alimwambia, ‘Hicho
kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu, Mwana wa Mungu’” (Lk 1:35). Dogma ilitolewa mwaka 431 kwenye Mtaguso wa
Efeso uliomuita “Mzazi wa Mungu”.

BIKIRA NA MAMA

Fumbo la Bikira Maria hapa linagongana na akili ya kibinadamu. Wote wanakiri ya kuwa Yesu alimwilishwa bila
ya mchango wa mwanamume, kumbe la ajabu zaidi ni kwamba hata uzazi wenyewe haukuondoa ubikira wake, bali
uliutakasa. Ingawa akili yetu inakataa, sisi tunakiri na malaika, “Hakuna lisilowezekana kwa Mungu” (Lk 1:38).
Ndiyo maana tunamkiri ni Bikira daima.

KUPALIZWA MBINGUNI MWII NA ROHO

Baada ya maisha haya ya duniani Bikira Maria mwenye heri alipalizwa mbinguni mwili na roho, ishara ya
mwanamke mshindi. “Ishara kubwa ikaonekana mbinguni, ambapo mwanamke aliyevikwa jua, pia na mwezi chini
ya miguu yake, na taji la nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake” (Ufu 12:1).

HESHIMA ZA LITURUJIA KWA MARIA

Kuna ibada za Mama Bikira Maria zinazoadhimishwa katika liturujia. Hapa tunazipanga kulingana na heshima
zinavyozidiana:

SHEREHE

8 Desemba – Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili
1 Januari – Bikira Maria Mama wa Mungu
25 Machi – Bikira Maria Kupashwa Habari
15 Agosti – Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni

SIKUKUU

31 Mei – Maamkio ya Bikira Maria
8 Septemba – Kuzaliwa kwa Bikira Maria

KUMBUKUMBU

Juni – Moyo Safi wa Maria
15 Septemba – Mama Yetu wa Huzuni
22 Agosti – Bikira Maria Malkia
7 Oktoba – Bikira Maria wa Rozari
21 Novemba – Bikira Maria Kutolewa Hekaluni
KUMBUKUMBU YA HIARI
11 Februari – Mama Yetu wa Lurdi
16 Julai – Mama Yetu wa Mlima Karmeli
5 Agosti – Kutabaruku wa Kanisa la B. Maria
Tena kila Jumamosi isiyo na adhimisho maalumu, Kanisa huadhimisha kumbukumbu ya Mama wa Mungu.
Pia zipo heshima za binafsi kwa Bikira Maria mwenye heri: mashariki tenzi na nyimbo (k.mf. Akatistos, tenzi za
mt. Efrem shemasi, na nyingine); magharibi (Roma) tunamheshimu binafsi na hata kijumuia kwa kusali rozari
takatifu. Ndiyo ibada ya binafsi inayompendeza sana baada ya zile za liturujia hata akatokea sehemu mbalimbali
duniani akihimiza tusali rozari ili tupate amani binafsi, kitaifa na kimataifa. Mwezi wa tano ni mwezi wa Maria.
Mwezi wa kumi ni mwezi wa Rozari. Mtu aliyeonja matunda ya kumheshimu Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,
anajua uwezo wa maombezi yake. Kanisa linakiri neema zote za Mungu zaja kwetu kwa njia ya Maria.
Je, tunamuabudu Bikira Maria? Hapana, Bikira Maria hatumuabudu hata kidogo, bali tunamtolea heshima ya juu
kuliko watakatifu wengine. Mungu tu tunampa heshima ya ‘latria’ (kuabudu), watakatifu tunawaheshimu (dulia) na
Bikira Maria tunampa heshima sana (yuper-dulia).
Kweli Mama Bikira Maria ni “kina kisichochunguzika kwa macho ya malaika” (Akatistos). Ni fumbo la ajabu
alilolifanya Mungu katika mpango wa wokovu kwa ajili yake na kwa ajili yetu. Katika Injili ya Yohane Bwana Yesu
alisema, “Ninayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili, lakini atakapokuja huyo Roho
wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yoh 16:12-13). Kwa msaada wa Roho Mtakatifu heshima kwa Bikira
Maria ilienea katika Kanisa lote tangu zamani kabisa. Tena katika Injili ya Luka kuna utabiri wa kumheshimu Bikira
Maria vizazi vyote, “Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mdogo, hivyo tangu sasa vizazi vyote
wataniita mwenye heri” (Lk 1:48).

Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?

Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.

Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;

1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu

Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)

2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi

19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.

3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12

Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.

4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu

Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno “Binamu” kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.

5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja

Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.

6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake

Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.

7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye

26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.

Huruma ya Mungu: Karama ya Upatanisho na Ukarabati

Karibu kwenye makala hii inayoeleza kuhusu huruma ya Mungu na jinsi karama hii inavyohusiana na upatanisho na ukarabati. Kama Mkristo, unajua kwamba Mungu ni mwingi wa huruma na upendo. Kwa hivyo, jukumu letu kama wafuasi wake ni kuigiza huruma yake kwa wenzetu.

  1. Huruma ya Mungu ni zawadi kubwa kwetu sisi binadamu. Inatupa fursa ya kufanya upatanisho na Mungu wetu na hivyo kuwa karibu naye. Kama ilivyoelezwa katika Kitabu cha Isaya 55:7 "Mwenye dhambi na aache njia yake mbaya, Na mtenda maovu aache mawazo yake; Naye arudi kwa Bwana, Naye atamrehemu, Na kwa Mungu wetu, Maana atasamehe kwa wingi."

  2. Upatanisho ni mojawapo ya matunda ya huruma ya Mungu. Yeye hupatanisha na kutulinda kama ilivyoelezwa katika Warumi 5:10 "Kwa maana kama tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana sasa, tulipokuwa tayari tumepatanishwa, tutahifadhiwa na kifo chake cha uzima."

  3. Upatanisho ni jukumu letu kama Wakristo. Kupatanisha na wenzetu na Mungu ni sehemu muhimu ya huduma yetu ya kiroho. Kama ilivyoelezwa katika 1 Wakorintho 5:18 "Lakini haya yote yanatoka kwa Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, na kutupa huduma ya upatanisho."

  4. Kukubali upatanisho kutoka kwa Mungu kunahitaji kuungama na kutubu dhambi zetu. Kama ilivyoelezwa katika 1 Yohana 1:9 "Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."

  5. Ukubali wa upatanisho kutoka kwa Mungu unakuja na neema ya kujikomboa kutoka kwa dhambi. Kama ilivyoelezwa katika Warumi 6:14 "Kwa sababu dhambi haitatawala juu yenu, kwa maana hamko chini ya torati, bali chini ya neema."

  6. Huruma ya Mungu pia inahusiana na ukarabati wetu. Yeye hutuponya kutoka kwa majeraha ya dhambi zetu. Kama ilivyoelezwa katika Zaburi 147:3 "Anaponya waliopondeka moyo, Na kuwaunganisha katika maumivu yao."

  7. Ni muhimu kujua kwamba Huruma ya Mungu inapatikana kwa wote, sio kwa watu wachache. Kama ilivyoelezwa katika Warumi 10:12-13 "Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani; kwa maana yeye yule ni Bwana wa wote; naye ni mwingi wa rehema kwa kila mtu amwitaye; kwa kuwa, Kila mtu atakayeliitia jina la Bwana ataokoka."

  8. Kupitia huruma ya Mungu, tunaweza kushinda dhambi na kukua kiroho. Kama ilivyoelezwa katika Tito 2:11-12 "Kwa maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa, na kufundisha sisi, tukataa ubaya na tamaa za kidunia, tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa."

  9. Huruma ya Mungu inatulea kuwa na unyenyekevu kwa wenzetu. Tunatakiwa kuwa na roho ya kusamehe na kusaidia wengine. Kama ilivyoelezwa katika Wagalatia 6:2 "Bear ye one another’s burdens, and so fulfil the law of Christ."

  10. Hatimaye, Huruma ya Mungu inatupatia fursa ya kumjua Mungu wetu vizuri zaidi na kuishi kwa kufuata mafundisho yake. Kama ilivyoelezwa katika Yohana 17:3 "Na uzima wa milele ndio huu, wapate kukujua wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma."

Katika Catechism ya Kanisa Katoliki, tunajifunza kwamba huruma ya Mungu inahusiana na neema, ukombozi, na upatanisho. Pia tunajifunza kwamba karama hii inatufundisha kuwa na huruma kwa wengine. Katika Kitabu cha Diary of Saint Maria Faustina Kowalska, tunasoma juu ya huruma ya Mungu na jinsi tunaweza kuinyenyekea kwa wengine.

Kuwa Mkristo ni kujifunza kujitoea kwa Mungu na kwa wenzetu. Kupitia huruma ya Mungu, tunaweza kupatanisha na kuwa karibu na Mungu wetu, kujikomboa kutoka kwa dhambi, na kujenga mioyo yetu kwa kumjua Mungu vizuri zaidi.

Je! Wewe ni mfuasi wa Kristo? Je! Unatambua huruma ya Mungu katika maisha yako? Je! Unajitahidi kumtumikia Mungu na kujitoea kwa wenzako? Jibu maswali haya na utusaidie kujifunza zaidi juu ya karama hii ya upatanisho na ukarabati kupitia huruma ya Mungu.

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu maisha ya watoto wachanga?

Katika Kanisa Katoliki, watoto wachanga ni baraka kubwa kutoka kwa Mungu. Imani yetu inaamini kuwa kila mtoto anapewa uhai na Mwenyezi Mungu, na hivyo wanastahili heshima na upendo. Watoto wachanga ni zawadi kubwa kwa familia zao, na wanapaswa kuheshimiwa na kulindwa kwa kila hali.

Kanisa limeelezea kwa undani jinsi maisha ya mtoto wachanga yanapaswa kulindwa. Kwa mfano, kwa mujibu wa Catechism of the Catholic Church, "Maisha yote ni takatifu, tangu kuanzia mimba, mpaka kifo cha asili kinapotokea" (2258). Hii ina maana kwamba mtoto anayekua kwenye tumbo la uzazi anastahili heshima na kulindwa kama mtu mzima.

Kwa hiyo, Kanisa linapinga vitendo vyote vinavyoleta madhara kwa mtoto wachanga. Hii ni pamoja na utoaji mimba, ambao unaharibu uhai wa mtoto kabla hata hajazaliwa. Kanisa pia linapinga utoaji mimba kwa sababu yoyote ile, hata kama ni kwa ajili ya afya ya mama. Kanisa linatetea haki ya mtoto wa kuishi, na kuheshimu maisha yake kutoka mwanzo hadi mwisho.

Kanisa pia linawahimiza wazazi kuwa waangalifu katika jinsi wanavyokabiliana na watoto wachanga. Wazazi wanapaswa kuwa na upendo, uvumilivu, na subira katika kuwalea watoto wao. Kama ilivyoelezwa katika Catechism, "Wazazi wanapaswa kuwa mfano bora kwa watoto wao, na kuwafundisha jinsi ya kuishi kwa kumtegemea Mungu na kuwapenda wengine" (2225). Kwa hiyo, wazazi wanapaswa kuwa waangalifu katika kuchagua maneno yao na vitendo vyao wanapokuwa karibu na watoto wao.

Kanisa pia linawahimiza wazazi kuwabatiza watoto wao mara wanapozaliwa. Kupitia ubatizo, mtoto anapokea Roho Mtakatifu na anakuwa sehemu ya familia ya Kanisa. Ubatizo pia unafuta dhambi ya asili ya mtoto na kumweka katika njia ya kumfuata Kristo. Kwa hiyo, ubatizo ni muhimu sana katika maisha ya mtoto wachanga.

Kwa ufupi, maisha ya watoto wachanga ni muhimu sana katika imani ya Kanisa Katoliki. Watoto wachanga wanapaswa kulindwa kwa kila hali, na kutambuliwa kama zawadi kutoka kwa Mungu. Wazazi wanapaswa kuwa waangalifu katika jinsi wanavyowalea watoto wao, na kuhakikisha kuwa wanawafundisha jinsi ya kuishi kwa kumtegemea Mungu. Kupitia ubatizo, mtoto anakuwa sehemu ya familia ya Kanisa, na anapokea Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, watoto wachanga ni baraka kubwa katika Kanisa, na wanapaswa kutunzwa kwa kila hali.

Namna Biblia inavyomueleza Bikira Maria

Biblia inashuhudia kuwa watu wanatofautiana

Maandiko matakatifu yanawasifu watu mbalimbali kutokana na jinsi walivyomuamini Mungu na kutenda makuu kwa ajili ya taifa lake.
Abrahamu alimuamini Mungu akawa tayari kumtolea sadaka mwanae Isaka, tukio lililomfanya apate baraka ya pekee ya kuwa baba wa waamini (Mwa 22:15-18).
Yosefu, mwana mpenzi wa Yakobo, alikuwa mwaminifu hata akaliokoa taifa lisiangamie kwa njaa (Mwa 50:20).
Musa ndiye mkombozi wa taifa la Mungu katika Agano la Kale: aliongoza Israeli kutoka [[utumwani Misri akalipatia sheria kutoka kwa Mungu katika mlima Sinai. Maandiko ya Agano la Kale yanakiri, “Wala hajainuka kiongozi kama alivyokuwa Musa” (Kumb 34:10-12).
Waliofuata ni Yoshua, Debora, Gideoni, Ruthu, Samweli, wafalme Daudi na Solomoni, manabii Eliya, Isaya, Yeremia, Ezekieli na wengineo.
Mwishoni Yesu Kristo akamsifu Yohane Mbatizaji akisema, “Ni mkuu kati ya uzao wa wanawake” (Lk 7:24-28).
Elizabeti, mama wa Yohane, alijiona hastahili kutembelewa na Bikira Maria, Mama wa Yesu, akamuita, “Mama wa Bwana wangu” (Lk 1:43).
Bikira Maria si mtu wa ziada katika mpango wa Mungu bali ni mshiriki mkuu wa ukombozi wa binadamu. Maria amechangia wokovu kwa kukubali mpango wote wa Mungu aliyetaka amzae Mwanae, amlee na kumfuata kiaminifu hadi msalabani, aliposhiriki kumtoa kama sadaka ya kutuokoa. Msimamo wake ulikuwa mmoja tu: “Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema” (Lk 1:38).
Tukichunguza nafasi yake katika fumbo hilo, tunaweza kukiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49), kwa kuwa, “Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu” (Yoh 3:27).
Yale yote ambayo Wakristo wengi wanayasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia bali alijaliwa na Mwenyezi Mungu huku akiitikia kwa hiari fumbo la mpango wake.

Utabiri kuhusu Bikira Maria kwenye Biblia

Biblia inatupatia utabiri uliotolewa na Mungu mwanzoni mwa historia kuhusu mwanamke atakayemshinda nyoka wa kale (Shetani): “Nitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke, kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa chako” (Mwa 3:15). Juu ya [[Eva wa kale, ambaye alidanganywa na kuangushwa na Shetani atende dhambi, imesemwa: “Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa, kwa kuwa ndiye aliye Mama wa walio hai” (Mwa 3:20). Hata hivyo Adamu na Eva wa kale wametuletea kifo (Rom 5:12). Mababu wa Kanisa wanamtazama Bikira Maria kama Eva mpya aliyemshinda Ibilisi na kuwa mama wa wote walio hai. Yesu, aliye Adamu mpya, alipokuwa anakamilisha sadaka ya ukombozi pale msalabani alimfanya Mama yake awe Mama wa waliokombolewa kwa kumkabidhi mwanafunzi, tena yule aliyempenda zaidi. “Penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Kleopa, na Mariamu Magdalene. Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, “Mama, tazama, mwanao”. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, “Tazama, mama yako”. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake. (Yoh 19:26-27).
Utabiri mwingine ulisema, “Tazama Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamuita jina lake Emanueli, yaani Mungu pamoja nasi” (Isa 7:14). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:34-35, “Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu akakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu”. “Imba, ee binti Sion, piga kelele, ee Israeli, furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, ee binti Yerusalemu. Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana yu katikati yako” (Sef 3:14-15). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:28: “Malaika akaingia nyumbani mwake akamwambia, ‘Furahi Maria, umejaliwa neema kubwa, Bwana yu pamoja nawe’”. “Umebarikiwa wewe katika kila hema la Yuda na katika kila taifa, nao wanaposikia jina lako watafadhaika. Imani yako haitatoka mioyoni mwa watu wanaoukumbuka uweza wa Mungu milele” (Yudithi 14:7; 15:9). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:42, “Akapaza sauti kwa nguvu akasema, ‘Umebarikiwa wewe kuliko wanawake wote, na yeye utakayemzaa amebarikiwa’”.
Bikira Maria ni fumbo la ajabu alilolifanya Mungu katika mpango wa wokovu kwa ajili yake na kwa ajili yetu. Jamaa yake Elizabeti alimpongeza tena akiongozwa na Roho Mtakatifu, “Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale uliyoambiwa na Bwana” (Lk 1:45).
Hivyo manabii mbalimbali kwa mwanga wa Roho Mtakatifu walimuagua Maria kwa heshima. Mambo yaliyotabiriwa katika Agano la Kale yalitimia katika Agano Jipya: ukombozi ulianza Bikira Maria alipokubali kwa imani fumbo la umwilisho wa Mwana wa Mungu. Bikira Maria hakuwa “chombo” tu kilichotumika bila ya kuelewa, bali alikuwa mshiriki huru wa kazi ya ukombozi ya Mwanae, kwa kuwa alipopashwa habari na malaika alikubali kwa hiari mpango wa Mungu akisema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu kama ulivyonena” (Lk 1:38).

Bikira Maria katika maisha ya Yesu

Yesu, kama mtu yeyote mcha Mungu, aliwaheshimu na kuwatii wazee wake: “Basi, akarudi pamoja nao Nazareti, akawa anawatii” (Lk 2:51).
Ishara ya kwanza kwenye maisha ya hadhara ya Yesu iliongozwa na Bikira Maria katika arusi ya Kana ya Galilaya, akisukumwa na huruma kwa wenye shida: kwa ombi lake Yesu aligeuza maji kuwa divai, na wanafunzi wake wakamwamini. Yohane alisimulia hivi, “Siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, ‘Hawana divai’. Yesu akamwambia, ‘Mama tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia’. Mamaye akawaambia watumishi, ‘Lo lote atakalowaambia, fanyeni’. Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yesu akawaambia, ‘Jalizeni mabalasi maji’. Nao wakayajaliza hata juu. Akawaambia, ‘Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza’. Wakapelekea. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maj), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, akamwambia, ‘Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa’. Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. (Yoh 2:1-12).
Bikira Maria anasifiwa kwanza kwa imani yake kuu kabisa, kuliko kwa kumchukua Yesu tumboni tu. Yesu alitaka kuwainua wasikilizaji wake wafuate mambo ya roho kuliko ya mwili. “Basi, mtu mmoja akamwambia, ‘Mama yako na ndugu zako wako nje, wataka kusema nawe’. Lakini Yesu akamjibu huyo mtu aliyemwambia hivyo, ‘Mama yangu ni nani, na ndugu zangu ni akina nani?’ Kisha akanyosha mkono wake juu ya wanafunzi wake akasema, ‘Hawa ndio Mama yangu na ndugu zangu, maana yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye kaka yangu na dada yangu na mama yangu’” (Math 12:46-50). Vilevile, wakati wa utume wake, alimsikia “mwanamke mmoja katika lile kundi la watu akisema, ‘Hongera kwa mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha’. Yesu akamjibu, ‘Barabara, lakini heri yake zaidi yule anayelisikia Neno la Mungu na kulishika’” (Mk 11:27-28).

Bikira Maria alivyoshiriki Mateso ya Yesu

Katika kumfuata Mwanae Bikira Maria alitabiriwa wazi na mzee Simeoni uchungu kama upanga utakaopenya moyo wake, “Tazama huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe uchungu ulio kama upanga utauchoma moyo wako” (Lk 2:34-35).
Bikira Maria alishiriki kwanza mateso ya ukimbizi huko Misri kwa lengo la kumficha Mwanae asiuawe na Herode Mkuu, “Hivyo Yosefu aliamka akamchukua mtoto pamoja na Mama yake akaondoka usiku akaenda Misri akakaa huko mpaka Herode alipokufa” (Math 2:14-15).
Bikira Maria alishuhudia hatua kwa hatua kuteswa kwa Yesu; wanafunzi walipokimbia au kumtazama kwa mbali, yeye alikuwa karibu akaona vema kila teso lililompata Mwanae. Kutokana na fungamano la upendo wa ajabu lililokuwepo kati ya Yesu na Mamaye, alipoyashuhudia yote aliteseka sana katika moyo wake safi, kiasi kwamba Bernardo wa Klervoo akasema, “Msalaba wa Yesu uliwasulubisha wote wawili, Yesu mwilini na Mama yake moyoni”. Uaguzi wa mzee Simeoni ulitimia hivyo.
Kadiri ya mtume Paulo kuteseka ni kutimiliza yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya Kanisa, “Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu hapa duniani nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristo” (Kol 1:24). “… maana tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake” (Rom 8:17b).
Pale msalabani Bikira Maria, kwa njia ya mtume Yohane alifanywa Mama wa wote wanaompenda Mwanae; kisha kumzaa pasipo uchungu Bwana wa uzima, pale alituzaa sisi kwa uchungu wa kutisha uliotokana na kumuona Mwanae akifa msalabani. Hata hivyo Bikira Maria aliendelea kumuamini Mwanae aliyeonekana ameshindwa.

Bikira Maria baada ya kifo cha Yesu

Bikira Maria alikuwepo hapo mwanzo wa Kanisa, akilivutia zaidi Roho Mtakatifu kwa sala yake. “Hao wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria Mama yake Yesu na ndugu zake” (Mdo 1:14).
Yesu alisema, “Ninayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili, lakini atakapokuja huyo Roho wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yoh 16:12-13). Kwa msaada wa Roho Mtakatifu heshima kwa Bikira Maria ilienea katika Kanisa lote tangu zamani kabisa kadiri ya utabiri wake kuwa ataheshimiwa na vizazi vyote, “Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mdogo, hivyo tangu sasa vizazi vyote wataniita mwenye heri” (Lk 1:48).

Utaratibu wa Mkristo Mkatoliki Kanisani

Ninapoingia kanisani nachovya maji ya baraka na kusema;
“Unitakase Ee Bwana mimi na uovu wangu wote, ili nipate kustahili kushiriki ibada takatifu’ Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” Amina!
Ninapiga goti huku nikisema
“Mungu wangu na Bwana wangu”
🙋🏽Nikiinuka nasema
“Nitakusifu na kukuabudu katika Ekaristi takatifu”
🙋🏽Naenda mpaka kwenye bench, napiga magoti au nakaa nikiwa mimeinamisha kichwa (kama mabenchi yameisha nabaki nimejisimamia) huku nikitoa nia yangu ya kusali misa siku hiyo, mfano
“Ee Mungu, ninaungana nawe na jeshi lote la mbinguni, pamoja na Mama Bikira Maria, nikiwa na nia ya kumwombea mama yangu ambaye ni mgonjwa, jirani yangu ambaye mpaka sasa hatuelewani na pia familia yetu ambayo haina amani, Mungu kupitia misa hii rejesha hali ya mama yangu, rejesha uelewano na jirani yangu, na pia rejesha amani ya familia yetu pamoja na familia zote ambazo hazina amani”
🙋🏽Ninaendelea na misa na Kushiriki litrujia kikamilifu
🙋🏽Wakati wa komunyo nikikumbuka kuwa nina dhambi kubwa huwa nakominika kwa sala ya tamaa wala siendi mbele, huwa najikalia tu kwenye bench naangalia wenye moyo safi wanaenda mbele kumpokea Yesu (Kweli huwa najisikia wivu sana, itanibidi katikati ya wiki nifanye kitubio ili nisikae tena)”
🙋🏽Mwisho wakati wa kuondoka nachovya maji ya baraka nikisema
“Unilinde Ee Mwenyezi Mungu, nikapate kuwa mfano katika jamii yangu, na nikushuhudie katika matendo yangu”
(Hapo nachovya maji ya baraka na kufanya ishara ya msalaba) “Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, amina”
Usiku mwema wapendwa. Malaika awalinde

Maana halisi ya kuolewa au ya kuwa mke

NDOA sio kichaka cha kujificha kukimbia matatizo. NDOA sio mahali pa kutolea mkosi. Wala sio mahali pa kupunguzia shida. Ndoa sio mbadala wa elimu na michakato ya kimaisha. Huolewi ili kupunguza adha za maisha. NDOA ni jukumu zito kuliko hata kusoma masters degree ya Neuro-surgeon. Wengi hamjaweza kumudu maisha yenu binafsi na bado mnalilia Mungu kuwaongezea jukumu la kumeneji maisha ya mtu mwingine.

Kama huwezi hata kujitafutia hela ya kusuka nywele zako utawezaje kuendesha maisha ya familia. Maana unaweza kuolewa na mwanaume mwenye pesa lakini akapitia mithihani pesa zikatoweka utafanyaje kama huna akili ya kujiongeza? Ndio maana wengi mnawakataa watu wenye Ndoto lakini hawanapesa kwa sasa kwa sababu ya akili ya utegemezi. Unataka mwanaume mwenye kila kitu, sababu kubwa ni uvivu na uzembe. Hutaki kujitafutia vya kwako.
Ukisoma MITHALI 31 inaeleza habari za MKE MWEMA.

Hapo ndio pa kujipima je unakidhi hivyo viwango? Mke mwema sio tegemezi ila ni mwanamke mwenye uhuru wa kifedha (Financial Freedom). JIULIZE TU KAMA IKITOKEA HUJAOLEWA MIAKA MITANO IJAYO UTAKUWAJE? MAISHA YAKO YATAKUWAJE? UTAKUWA NA HALI GANI? Maswali kama haya yatakusaidia kujiongeza. Tafuta kitu cha kufanya hata kama Ndoa isipotokea leo isiwe mwisho wa maisha, Ndoto na maono yako. Siku hizi wanaume hawaulizi ukoo wanauliza UNAFANYA NINI?

Mtu anapiga hesabu akikuoa mkaunganisha nguvu mtafanya nini kwenye maisha. Sasa wewe kalia kubandika kope na kuchora kucha kutwa nzima huna shughuli ya kufanya huku ukingoja kuombewa upate Mume. Watu hawaoi mapambo wanataka Wake watakao tengeneza nao hatma zao. Pambo ni kwaajili ya Starehe lakini MKE ni kwaajili ya maisha. Sikupondi wala sio nia yangu kukuvunja moyo, nataka utoke hapo ulipo ujiongeze ili hata ukiingia kwenye Ndoa isijae visa na kuonewa. Pesa itakupa heshima, pesa inakupa sauti, hata Wakwe zako hawawezi kukunyanyasa ukiwa na pesa kwani wanajua watakosa vitenge.

Nataka nikwambie kweli, ukiwa na hela utachagua mwanaume wa kukuoa kwani wapo wengi ila kama umefulia, tegemezi kweli utaona wanaume ni wachache. Pata kitu cha kufanya, tengeneza milango ya kipato. Badala ya kukesha unaomba Mungu akupe Mume anza kuomba Mungu akupe uhuru wa kifedha, kama itakubidi kurudi shule rudi tu. Jiongeze usibaki hapo ulipo. Ni Yesu peke yake asiyebadilika (Hebrania 13) Lakini wanadamu wote lazima tubadilike kila kukicha tukihama hatua moja kwenda nyingine.

Mungu akufungue macho kuona kiini cha ujumbe huu na lengoF lake na wala usichukuliwe na upepo wa adui upindishao maana katika jumbe zenye kubadilisha maisha kama hii.

Kuolewa sio mwisho wa maisha, Mungu kwanza achukue nafasi kwenye maisha yako na akupe utoshelevu katika moyo wako kiasi kwamba uone hata bila Mume unaweza kuishi.

JE, WAKATOLIKI WANABUDU SANAMU?

Mpenzi msomaji, kumekuwa na tuhuma nyingi dhidi ya wakatoliki kwamba wanaabudu sanamu. Je, tuhuma hizo zina ukweli gani? Hilo ndilo swali tunalotaka kujibu leo.
Amri ya kukataza ibada kwa sanamu imewekwa wazi katika Biblia Takatifu, Kutoka 20:4-5, “Usijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au kinyago chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia. Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu.”
Sheria hiyo inapatikana pia katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 5:8-9: “Usijifanyie sanamu za miungu za kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Isivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu.”
Ni kutokana na vifungu hivyo vya Maandiko Matakatifu, Waamini wa Kikatoliki wamekuwa wakituhumiwa, kushtakiwa na kushambuliwa na baadhi ya waamini wa madhehebu mengine kwamba wanapingana na maagizo ya Mwenyezi Mungu, yanayokataza ibada kwa sanamu. Tuhuma hizo zinakuwa nzito zaidi, hasa zinapohusishwa na Ibada inayofanywa na Waamini Wakatoliki siku ya Ijumaa Kuu kila mwaka.

KUNA TOFAUTI KATI YA KUABUDU NA KUHESHIMU

Mpenzi msomaji, kuna tofauti kubwa kati ya kuabudu na kuheshimu. Kamusi ya Kiswahili ya Maana na Matumizi, ya mwaka 1993, iliyoandikwa na SALIM K. BAKHRESSA, na kuchapishwa na OXFORD UNIVERSITY PRESS, DAR ES SALAAM, inaeleza kuwa neno “kuabudu” maana yake ni “kuomba au kufanya ibada”; na neno “kuheshimu” maana yake ni “kutukuza, kustahi au kuogopa.”
Katika maana yake ya ndani, anayeabudiwa na mwenye haki ya kuabudiwa ni Mungu peke yake. Hakuna mtu, kiumbe wala kitu chochote kinachopaswa kuabuduiwa na chenye haki ya kuabudiwa. Mtu, kiumbe au kitu hupewa heshima tu, tena ya kiwango maalum. Kwa mfano, Bikira Maria, kwa sababu ya nafasi yake katika kazi ya ukombozi, anapewa heshima ya juu kuliko watakatifu wengine. Watakatifu hao wengine hupewa heshima ya kadiri tu, chini ya heshima ile anayopewa Bikira Maria.

KWA NINI MUNGU PEKE YAKE ANASTAHILI KUABUDIWA?

Tumesema ni Mungu pekee yake, ndiye anayestahili kuabudiwa, kwa sababu ndiye MUUMBA wa vitu vyote, vinavyoonekana na visivyoonekana; ndiye anayevitawala na kuviongoza vitu vyote; ndiye mwenye uwezo juu yetu sisi wanadamu na viumbe vingine vyote; ndiye anayejua yote; ndiye aliye pote kwa ajili yetu; ndiye mwanzo na mwisho wa kila kitu; ndiye mkuu na Bwana wa wote.
Aidha, tunapomwabudu Mungu, tunakiri kwamba ndiye aliyetuumba na “ndani yake yeye sisi tunaishi, tunajimudu na tuko!” (Mdo.17:28). Kwa kufahamu hilo, Wakatoliki hawawezi kumwabudu mtu, kiumbe au kitu chochote, isipokuwa Mungu tu.

MAMBO MAKUU NA MUHIMU KATIKA IBADA YA SANAMU

Ili kufahamu vema kinachofanywa na Wakatoliki ni vema kufuatilia na kutafakari yale wanayoyafundisha na kuyasadiki wao wenyewe, badala ya kuwahukumu kadiri watu wengine wanavyofikiri na kusema. Ukweli ni kwamba hakuna Ibada yoyote ya sanamu katika Kanisa Katoliki. Hilo ni dhahiri kwa sababu ili ibada ya sanamu iwe kweli kuabudu sanamu lazima yawepo mambo makuu na muhimu mawili: Kwanza, NIA KAMILI YA KUABUDU SANAMU INAYOHUSIKA;
Pili, KUWEPO NA IBADA YA DHATI YA KUABUDU SANAMU. Ikitazamwa kwa makini, hayo mambo mawili yanakosekana katika Kanisa Katoliki linapokuja suala la picha na sanamu. Kwa hiyo, Wakatoliki hawaabudu sanamu wala picha. Kama ni hivyo, wakatoliki wanafanya nini na hizo sanamu au picha? Wanaziheshimu tu! Tukumbuke kuwa anayemwabudu mtu, kiumbe au kitu, ni sharti akihesabu na kukisadiki kuwa ndicho kinachomwezesha kuishi, kujimudu na kuwa na uhai wake (Rej. Mdo.17:28).

JE, BINADAMU TUNAHITAJI SANAMU AU PICHA?

NDIYO. Binadamu tunahitaji sananmu au picha, tena ni jadi yetu! Kwa sababu gani tunahitaji picha maishani mwetu? Kwa sababu katika udhaifu wetu, mara nyingi tunaweza kufikiri vema kwa kutumia vielelezo au vichokoo vyenye kuonekana na kugusika. Kwa njia ya vielelezo hivyo, binadamu tunaweza kuyafikia kwa urahisi mambo magumu na mafumbo yaliyo juu ya fikra zetu za kawaida. Ndiyo maana tukiona picha au sanamu ya Yesu au Mama Maria au Watakatifu wengine, akili zetu zinaweza kutafakari mambo matakatifu na kupata picha ya kina cha msamaha wa dhambi na mapendo ya Mungu kwetu wanadamu.

KWA NINI WAKATOLIKI HAWAABUDU SANAMU AU PICHA?

Wakatolikihawaabudu sanamu kwa sababu wanajua kwamba Mungu pekee ndiye anayepaswa kuabudiwa. Kwa hiyo, hawaziabudu sanamu au picha kwa sababu wanajua kwamba hivyo siyo Mungu. Zaidi hayo, wanajua kwamba Mungu mwenyewe amekataza kuziabudu sanamu na picha kwani hazina daraja la Muumba. Mungu amepiga marufuku kuzigeukia na kuzisujudia (Law.19:4). Aidha, wameaswa kuziepuka sanamu na Ibada kwa sanamu – “Watoto wangu, epukaneni na sanamu za miungu!” (1Yoh.5:21). Pia wakatoliki wanajua kuwa sanamu na picha hazina uwezo wowote wa kimungu. “Mungu wetu yuko mbinguni, hufanya yote anayotaka. Miungu yao ni fedha na dhahabu; imetengenezwa na mikono ya wanadamu. Ina vinywa lakini haisemi. Ina macho lakini haioni. Ina masikio lakini haisikii. Ina pua lakini hainusi. … Wote wanaoitengeneza wanafanana nayo, kadhalika na wote wanaoitumainia. Enyi wa nyumba ya Israeli mtumainieni Mwenyezi Mungu, yeye ndiye msaada wenu na ngao yenu” (Zab.115:3-9). Pia kuziabudu sanamu ni jambo la kidunia, ambalo haliwezi kumpeleka mtu peponi (Rej. Isa.45:16; Isa.45:20; Gal.5:20). Kwa hiyo, Wakatoliki wanajua kuwa kuabudu sananmu na picha ni jambo haramu kabisa mbele ya Mungu, Mwumba wao (1Pet.4:3-4).

IBADA YA KWELI YA SANAMU INAKUWAJE?

Ibada ya kweli ya sanamu siyo rahisi hivyo, kama baadhi ya watu wanavyodhani! Ibada ya kweli ya sanamu siyo kitu cha mchezomchezo, kama baadhi ya watu wanavyofikiri na kusema. Ibada ya Sanamu ni suala la kuabudu, na kuabudu siyo suala la kuwa na kitu au kikiheshimu tu, bali ni kwenda mbali zaidi ya hapo! Hivyo kumiliki sanamu au picha, mathalani majumbani au kanisani, hakusemi lolote juu ya uwepo wa ibada ya sanamu kwa wale wanaohusika nazo. Kwa hiyo, ikiwa watu hawazipi sanamu au picha hizo mahali pa Mungu wa kweli, basi hawana hatia yoyote.
Jambo muhimu hapa ni kwamba wamiliki wa sanamu au picha hizo wanaziheshimu tu huku wakijua kuwa wenyewe wanaowakilishwa na sanamu au picha hizo hawapo pale kwa hali halisi. Katika maana hiyo, inakuwa sahihi kabisa kuziheshimu picha za marais, ndugu na marafiki wetu tunaowapenda, ambao hawapo karibu nasi. Picha zao hatuzikejeli wala hatuzibwagi chini na kuzikanyaga au kuzitia vumbi. Hatufanyi hivyo, siyo kwa sababu tunawaabudu watu hao au vitu hivyo, bali kwa sababu tunawapenda na kuwathamini wenyewe katika hali zao halisi.
Kwa mfano ikiwa tuna kitabu cha picha (Album) chumbani, chenye picha 100 za ndugu, rafiki na jamaa zetu, hatusemi tuna miungu 100 tunaowaabudu nyumbani mwetu! Vinginevyo, mambo yangetisha sana majumbani mwetu! Wenye picha hizo hatuwaabudu kamwe, ila tunawapa heshima tu kwa sababu tunawajali na kuwapenda. Kwa nini tusiwape heshima hiyo, ambayo ni kitu cha bure! Ukweli huo pia unahusu Bendera ya Taifa, Wimbo wa Taifa, nk.

JE, MUNGU ANACHUKIA KILA SANAMU NA PICHA?

Mungu hachukii kila sanamu au picha. Hapa inafaa ieleweke vema kwamba Mungu alipopiga marufuku sanamu katika Kitabu cha Kut. 20:3-5 na Kumb. 5:7-10, hakupiga marufuku kila sanamu. Yeye mwenyewe anaonesha kwamba anazichukia sanamu zinazotengenezwa kusudi zichukue nafasi yake tu. Kama sanamu au picha hazihatarishi nafasi yake, hana maneno nazo! Ndiyo maana, basi, baada ya kumwagiza MUSA awaambie watu wasizitengeneze sanamu na kuziabudu kama miungu (Kut.20:4-5), alimwagiza MUSA huyo huyo azitengeneze sanamu zisizokuwa hatari, ambazo hazikupewa daraja la Mungu. Mungu alimwagiza MUSA kutengeneza sanamu katika nafasi mbili:
(i) Musa anaagizwa atengeneze sanamu mbili za Makerubi azibandike kwenye Sanduku la Agano wakifunike kiti chake cha rehema. “Utatengeneza pia mfano wa viumbe hai viwili kwa kufua dhahabu, uwaweke kwenye miisho miwili ya kiti hicho; kiumbe kimoja mwisho mmoja na kiumbe mwingine mwisho mwingine. Waweke viumbe hao kwenye miisho ya hicho kiti, lakini wawe kitu kimoja na hicho kiti. Viumbe hao wataelekeana, mabawa yao yamekunjuka kukifunika kiti cha rehema, nyuso zao zitakielekea kiti hicho” (Kut.25:18-20; Rejea pia Ebr.9:5).
(ii) Mungu alimwagiza pia Musa atengeneze Nyoka wa Shaba kama dawa kwa wale ambao waling’atwa na nyoka wa moto kule Jangwani. Musa alielezwa wazi kwamba wale ambao wangemtazama huyo nyoka wa shaba kwa imani kwa Mungu wa Israeli wangepona. “Ndipo naye Mwenyezi Mungu akamwambia Musa: Tengeneza Nyoka wa shaba, umtundike juu ya mlingoti. Mtu yeyote atakayeumwa na nyoka, akimtazama nyoka huyo wa shaba, atapona. Basi, Musa akatengeneza nyoka wa shaba, akamtundika juu ya mlingoti. Kila mtu aliyeumwa na nyoka alipomtazama huyo nyoka wa shaba, alipona” (Hes. 21:8-9; Rejea pia Yoh.3:14-15).
Basi, Musa alitekeleza maagizo hayo ya Mwenyezi Mungu, naye alifurahia. Kwa maagizo hayo mawili ni dhahiri kwamba Mungu hachukii kila sanamu au picha. Mungu anachukizwa na sanamu zile ambazo zimekusudiwa kuchukua daraja la umungu wake, maana ni yeye tu ndiye anayestahili kuabudiwa. Yule nyoka wa shaba alikuwa dawa kwa wale walioumwa na nyoka wa moto. Watu hao hawakumwabudu nyoka wa shaba, lakini walipona, siyo kwa sababu ya nguvu zake, ila kwa nguvu za mwokozi zilizokuwa nyuma yake. “Kama mtu akiitazama alama hiyo aliponywa, lakini kilichomponya siyo hicho kitu alichokiona, bali wewe uliye Mwokozi wa watu wote” (Hek.16:7).
Hapa ni vifungu vingine vya Maandiko Matakarifu, vinavyoonesha kuwa Mungu hachukii kila sanamu au picha.
1Fal. 7:29 “kulikuwa na sanamu za simba, mafahali na viumbe vyenye mabawa. Sanamu hizo za simba na mafahali zilikuwa, zimefunikwa na kutandikwa mapambo yaliyosokotwa vizuri”.
2Nyak.3:10 “Alitengeneza sanamu mbili za viumbe wenye mabawa kwa mbao, akazifunika kwa dhahabu na kuziweka mahali patakatifu sana”
Ezek.41:17-18 “… kwenye ukumbi palikuwepo na michoro iliyofanana na mitende na picha za viumbe vyenye mabawa. Kila baada ya mtende kulichorwa picha ya kiumbe chenye mabawa kukizunguka chumba chote”.
Yoh. 3:14-15 “Kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka wa shaba kule Jangwani, naye Mwana wa mtu atainuiliwa juu vivyo hivyo, ili kila anayemwamini awe na uhai wa milele.”
Ebr.9:5 “Juu ya hilo sanduku kulikuwa na viumbe wenye mabawa, na mabawa yao yalitanda juu ya mahali ambapo dhambi huondolewa”

UBAYA WA SANAMU AU PICHA UKO WAPI?

Ubaya wa sanamu au picha upo katika kuzipa sanamu au picha daraja la Mungu. Hatari na ubaya wa sanamu au picha vimo katika kitendo cha binadamu kuzipa sanamu au picha hizo daraja la Mwenyezi Mungu. Kama sanamu au picha hazipewi daraja la Mungu, haziwi hatari na wala hazina ubaya wowote mbele ya Mungu. Kwa sababu hiyo, basi, mtu anaweza kuwa na sanamu au picha ndani ya nyumba yake au kanisani, lakini bila kumkasirisha Mungu.
Zaidi ya hayo, Mungu mwenyewe anajua fika kuwa sanamu au picha fulani imepewa daraja lake au siyo. Kwa nini Mungu akasirike pale ambapo sanamu au picha haziingilii daraja na ukuu wake? Mungu mjinga wa aina hiyo hayupo! Mungu wa kweli hawezi kukasirikia picha na sanamu ambazo zinaheshimiwa tu, na wala haziabudiwi. Aidha, Mungu mwenye haki hawezi kumwadhibu na kumtupa Jehanamu mtu ambaye anamiliki picha au sanamu duniani lakini bila kuziabudu, yaani pasipo kuzipa daraja la Mungu.

BIBLIA INAWEZA KUTUSAIDIA KUIELEWA IBADA YA SANAMU?

Jibu ni ndiyo! Biblia inatoa maelezo ya kina na ufafanuzi mzuri juu ya ibada ya sanamu. Tumesema hapo juu kuwa ibada ya sanamu siyo jambo la mzaha au mchezo wa kitoto! Ni suala la kuabudu, na kuabudu siyo tu jambo la kuwa na sanamu au picha na kuiheshimu tu. Ni zaidi ya hapo! Kuna mambo muhimu ambayo lazima sanamu zitendewe, ndipo ihesabike kuwa ni ibada ya sanamu.
a) Tukitaka kujua kama kitendo fulani mbele ya sanamu ni kuabudu au sivyo, kwanza lazima iwepo nia thabiti ya mtu anayehusika katika kitendo hicho kinachofanyika. Ibada inakuwa ya kuabudu sanamu ikiwa mtu anayefanya kitendo hicho anaamini moyoni mwake kwamba hiyo sanamu au picha inayofanyiwa kitendo hicho inachukua daraja na nafasi ya Mwenyezi Mungu. Katika kitendo hicho, mtu anaamini kuwa sanamu au picha hiyo ndiyo inayomwezesha kwenda, kuishi, kujimudu na kuwa na uhai wake hapa duniani.
b) Jambo la pili ni kuangalia kama kitendo hicho kinachofanyika katika ibada hiyo ni Liturujia ya kueleweka/maalum. Baada ya kubaini nia thabiti ya mtendaji, tunaweza kuitambua ibada ya sanamu kwa kuangalia yale yanayofanyika mbele ya sanamu au picha kwa kufuatilia mambo ambayo waabudu sanamu huyafanya. Mambo hayo, ambayo waabudu sanamu wanayafanya tunaweza kuyakusanya kutoka katika Biblia yetu. Agano la Kale linaonesha kuwa Ibada ya Kuabudu Sanamu inajumuisha mambo makuu yafuatayo:
i. Kuzitolea sadaka: za kuteketezwa: Rej. Hos.4:13; nafaka na vyakula 2Fal.5:17.
ii. Kuzitolea ubani kwa heshima kamili: Rej. 1Fal.11:8; Isa. 57:6; Yer.7:18.
iii. Kuzimwagia matambiko: Rejea Isa. 57:6
iv. Kuzitolea zaka ya sehemu ya kumi ya mapato ya mwaka ya mazao ya mashambani: Rejea Hosea 2:8
v. Kuziandika meza mbele yao: Rejea Isa. 65:11
vi. Kuzibusu sanamu kwa kuzisujudia kama viumbe vyenye enzi.
Rejea 1Fal. 19:18; Hos.13:2; Ayu. 31:2.
vii. Kuziinulia sanamu mikono katika kuzisujudia: Rejea Isa.44:20
viii. Kuziangukia sanamu kifudifudi ama kuzipigia magoti kwa kuziabudu: Rejea 1Fal.18:26,28.
ix. Kuzichezea ngoma na wakati mwingine kujikatakata kwa visu kama kitendo cha ibada kwa sanamu: Rejea 1Fal.18:26,28.
Hayo yote yakichunguzwa kwa makini, tutaona wazi kuwa hakuna Ibada ya kuabudu sanamu katika Kanisa Katoliki. Kwa hiyo, shutuma kwamba Wakatoliki wanaabudu sanamu siyo za kweli, hazina msingi, na ni uchochezi wa bure wenye lengo la kuleta mafarakano na magomvi. Jambo hilo ni dhahiri kwa sababu Wakatoliki hawana nia thabiti ya kuabudu sanamu wanapotoa heshima kwa sanamu au picha mbalimbali. Pili, matendo ya kiliturujia yanayofanywa na wakatoliki katika kuheshimu sanamu hayalingani na matendo ya kiliturujia yanayofanywa na waabudu sanamu, kama ilivyoelezwa katika Biblia Takatifu, hususan Agano la Kale. Kifupi, wakatoliki hawana nia thabiti moyoni ya kuziabudu sanamu au picha, tena hawazifanyii liturujia yoyote sanamu au picha walizo nazo majumbani au makanisani.
Ni wapi ambapo Kanisa Katoliki linafanya au kuwafundisha rasmi na kuwahimiza wafuasi wake wafanye matendo hayo tisa ya kiliturujia kwa ajili ya kuabudu sanamu? Hakuna! Kwa hiyo, Wakatoliki hawana hatia yoyote ya kuabudu sanamu mbele ya Mungu. Kama mtu mmoja akifanya hivyo, hilo ni shauri lake binafsi, siyo shauri au utaratibu wa Kanisa lote. Aidha, afanyaye hivyo amepotoka peke yake, kwa sababu hajafundishwa na Kanisa Katoliki afanye hivyo. Hilo ni kweli kwa sababu mambo binafsi, siyo mambo rasmi ya Kanisa lote!
Kwa hiyo, tunaona wazi kwamba Wakatoliki hawaabudu sanamu kamwe, kama inavyodaiwa na baadhi ya waamini wa madhehebu mengine ya kikristo. Wanaotoa shutuma hizo inafaa wajiangalie kwanza wao wenyewe, maana imeandikwa: “… mtu akidhani kwamba kitu fulani ni najisi, basi, kwake huwa najisi” (Rom.14:14).

JE, IJUMAA KUU WAKATOLIKI WANAABUDU NINI?

Je, ni kweli kwamba Siku ya IJUMAA KUU Wakatoliki wanaabudu Sanamu au Mti wa Msalaba? HAPANA! WANAMWABUDU WOKOVU-YESU! Kiini cha utata hapa ni “NINI MAANA YA IBADA YA KUABUDU MSALABA” inayoendeshwa siku ya Ijumaa Kuu? Madhehebu hayo yanayofanywa na Wakatoliki Siku ya IJUMAA KUU siyo Ibada ya Kuabudu Sanamu. Labda hapa ni tatizo la lugha au maneno yanayotumika, ndiyo yanayowachanganya watu! Hilo ni kweli kwa sababu jina la madhehebu yenyewe halisemi wazi kitu gani hasa kinanuiwa kufanywa katika ibada hiyo.
Wengi hawajui nini hasa kinanuiwa kufanyika siku ya Ijumaa Kuu katika “Ibada ya Kuabudu Msalaba” – jina ambalo nimesema halitoi picha halisi ya jambo linalokusudiwa kufanyika. Mtu mwenye akili timamu akijua kitu halisi kinachofanyika siku ya Ijumaa Kuu, hawezi kusema madhehebu hayo ni Ibada ya Sanamu au kuabudu mti. Tatizo hapo ni lugha tu inayotumika katika kuieleza ibada hiyo. Labda jina hilo lichunguzwe upya na wataalamu wetu katika Kanisa na ikiwezekana kulirekebisha ili kuondoa utata kwa baadhi ya watu wenye uelewa mdogo, wenye wanaokwazwa nalo!

NINI HASA KINAFANYIKA SIKU YA IJUMAA KUU?

Wanachofanya Wakatoliki Siku ya Ijumaa Kuu ni KUUHESHIMU MTI WA MSALABA na KUMWABUDU WOKOVU. WOKOVU ni nani? WOKOVU NI YESU KRSITO BWANA WETU. Basi, kinachofanyika siku ya Ijumaa Kuu ni kumwabudu WOKOVU yaani YESU KRISTO, ambaye alitundikwa msalabani. Hivyo ndivyo anavyotangaza Kiongozi wa Ibada hiyo ya Ijumaa Kuu, pale anapotoa mwaliko kwa waamini mara tatu, ili kila muumini ausikie na kuelewa vema: “HUU NDIO MTI WA MSALABA, AMBAO WOKOVU WA DUNIA UMETUNDIKWA JUU YAKE, NJOONI TUUABUDU.” Waamini wanaalikwa kiimani kuuabudu WOKOVU, na hilo ndilo linalofanyika, yaani kuuabudu WOKOVU – YESU KRISTO. Waamini wote wanaalikwa kujongea mbele kwa imani kwenda kumwabudu YESU. Watu wanamwabudu YESU kwa sababu WOKOVU maana yake ni YESU.
Jina YESU ambalo linatokana na Kiebrabia “YESHUA”, maana yake “WOKOVU” (Rej. Mt.1:21;1:25; Lk.1:31). Ikiwa wokovu ni YESU, basi Ijumaa Kuu Wakatoliki hawaabudu sanamu au mti, bali wanamwabudu YESU KRISTO. Kwa sababu hiyo, yote yanayofanyika Siku ya Ijumaa Kuu, yanafanyika kihalali na kwa haki kwa sababu YESU KRISTO, ambaye ni WOKOVU ni MUNGU, na MUNGU peke yake ndiye mwenye haki na anayepaswa kuabudiwa. Ikiwa mkristo hataki kumwabudu YESU KRISTO, aliye Mwana wa Mungu na Mungu kamili, na ambaye ameeleta wokovu, anafanya makosa makubwa!
Basi, nasisitiza kuwa Siku ya Ijumaa Kuu, Wakatoliki hawaabudu sanamu wala mti. Wanamwabudu WOKOVU, yaani YESU KRISTO, Nafsi ya Pili ya MUNGU. Kutomwabudu YESU KRISTO ni sawa na kumkana Mungu, kukana wokovu ulioletwa naye. Basi, tujiepushe na ukanaji Mungu wa aina hiyo. Nawaalika wote Siku ya Ijumaa Kuu tufungue mioyo yetu kwa imani kubwa ili tumwone WOKOVU aliyetundikwa msalabani, apate kuukomboa ulimwengu. Kwa imani, wote tumsujudie YESU ili apate kutukumbuka katika Ufalme wake wa milele.
Hatimaye, niseme kwamba ingawa Mungu ametoa amri ya kukataza sanamu na picha (Kut. 20:4-5; Kumb. 5:6-10), lakini hachukizwi na kila sanamu au picha. Sanamu na picha ambazo hazipewi daraja la Mungu, Yeye hazichukii, kwa sababu hazichukui nafasi yake kama Muumba. Basi, Wakatoliki hawaendi kinyume na Biblia kwa kuziheshimu sanamu na picha zilizoko kwenye majumba yao na makanisani.

JE,SHERIA YA MAPADRE KUTOOA NA KUISHI USEJA IMEANDIKWA WAPI KATIKA BIBLIA AU IMETUNGWA TU NA PAPA?

Pengine umewahi kuulizwa swali hili wakati fulani.Na jibu lake ni kama ifuayavyo:
Mtu anapouliza kila kitu kimeandikwa wapi katika Biblia ni kudhihirisha kutokuijua au kuielewa vizuri Biblia Takatifu na historia yake.Mtu anapong’ang’ania “nionyeshe kitu fulani kimeandikwa wapi kwenye Biblia”ni kutaka kujiona ya kwamba yeye anaielewa sana Biblia na ameisoma yote kwa hiyo kila kitu kilichopo kwenye Biblia anakifahamu kumbe haijui Biblia bali anakariri Biblia!
Na hili suala la kushupalia swala la kuoa linadhihirisha jinsi gani tulivyo kizazi cha zinaa,ni kama tunadhani kuwa UZIMA upo katika kujamiiana!La hasha.
Paulo anasema “Kwasababu ya zinaa ni bora kuoa na kuolewa”(1Wakorintho 7:2.9) haya sio maneno ya kufurahia na kuchekelea tu maana “YANAWALENGA WALE WALIOSHINDIKANA KATIKA YALE YAPENDEZAYO”(1Wakorintho 7:1.8)sasa ni lazima tujiulize je tumeshindikana kiasi hicho?,hiyo sio sifa!
1Wakorintho 7:1.8
“Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika,ni heri mwanaume asimguse mwanamke,8.Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane heri wakae kama mimi nilivyo”
Na Paulo Mtume anasema “Ni bora kuoa au kuolewa” lakini hakusema “Ni LAZIMA kuoa au kuolewa”
Suala la kutooa kwa mapadre kadiri ya historia lilianza tangu zamani kabisa mwanzoni mwa milenia ya pili katika mtagusi wa pili wa Laterani mwaka wa 1139 ili waweze kumtumikia Mungu kwa uhuru na bila mawaa wala pasipo vikwazo(1wakorintho 7:32-35)
1wakorintho 7:32-35
“32Lakini nataka msiwe na masumbufu.Yeye asiyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya Bwana ampendezeje Bwana;33.bali yeye aliyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendeza mkewe.34-Tena iko tofauti kati ya mke na mwanamwali.Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana ili apate kuwa mtakatifu mwili na Roho.Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendezesha mumewe.,35.Nasema hayo niwafaidie ninyi,si kwamba niwategee tanzi,bali kwaajili ya vile vipendezavyo,tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine”
Maandiko hayo hapo juu yanajieleza wala sidhani kama yanahitaji kufafanuliwa zaidi ya yanavyojifafanua yenyewe.
Watu wengine wanafikiri kwamba kutooa ni dhambi,kama ni hivyo basi hata Yesu mwenyewe alikosa maana hata yeye mwenyewe hakuoa.
Yesu mwenyewe anafundisha kuhusu ubikira(Mathayo 19:10-12)
Mathayo 19:10-12,
“Wanafunzi wake wakamwambia,kama mambo ya mme na mke yakiwa hivyo ni afadhali kutuooa kabisa.Lakini Yeye akawaambia ‘SI WOTE WAWEZAO KULIPOKEA NENO HILO,ILA TU WALE WALIOJALIWA,maana wako MATOWASHI waliozaliwa katika hali hiyo toka matumboni mwa mama zao;tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi,tena wako Matowashi WALIOJIFANYA WENYEWE KUWA MATOWASHI KWAAJILI YA UFALME WA MBINGUNI’,awezaye kulipokea neno hili na alipokee”
Yesu mwenyewe analifafanua jambo hili kwa mapana,katika orodha ya matowashi Yesu aliowataja,Mapadre ni Matowashi waliojifanya hivyo kwaajili ya huduma ya kanisa na ufalme wa Mungu.
Tena Yesu anatuambia waziwazi kwamba”sio wote wawezao kulipokea neno hilo”yaani sasa sio wote wawezao kuwa Matowashi(Mapadre)bali ni wale tu waliojaliwa na Mungu neema hiyo.wale wasioweza kuishi upadre huoa na kuwa na familia.Tena Yesu anamalizia kwa kusema “Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee”,kwa maana nyingine ni kusema “Fundisho au Utowashi huu sio wa lazima”anayeweza kuishi maisha hayo basi na ayapokee na yule asiyeweza basi aache!
Vilevile Mitume ili kumfuata Yesu kikamilifu waliyaacha yote waliokuwa nayo ikiwepo familia zao ili wamtumikie Bwana(Mathayo 19:27.29)
Mathayo 19:27.29:
“Ndipo Petro akajibu akamwambia ‘Tazama sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe,tutapata nini basi?29.Amini nawaambia,kila mtu aliyeacha nyumba au ndugu wa kiume au wakike,au baba au mama au watoto au mashamba KWAAJILI YA JINA LANGU,atapokea mara mia zaidi na kuurithi uzima wa milele”
katika injili hiyo,Yesu anadhihirisha kwamba aliyeacha hayo yaliotajwa si kwasababu hawezi kuyapata la hasha,bali ameyaacha hayo yote KWAAJILI YA JINA LA YESU atapokea mengi hapa duniani halafu tena ataurithi ufalme wa mbinguni.
Mapadre wameyaacha hayo yote,wameacha nyumba,familia zao na kila kitu SIO KWASABABU HAWANA UWEZO AU HAWAWEZI KUPATA MAMBO HAYO bali WAMEACHA KWASABABU YA KUMTUMIKIA MUNGU KWA KADIRI YA MAANDIKO MATAKATIFU na kwakutaka kwao kuyaishi kimamilifu MASHAURI YA INJILI ikiwepo USEJA.
Maneno ya Paulo na yale ya Yesu mwenyewe kuhusu kumtumikia Mungu bila kuoa sio ya bahati mbaya bali ndiyo njia bora na inayofaa sana na kukubalika mbele ya Mungu.
Kwahiyo unapowaona mapadre hawaoi ujue sababu yake ni hiyo kwamba “Wamejitoa kwaajili ya kulihudumia kanisa”
(Na pia huwa nawashangaa mno watu wanaowapiga vita Mapadre kwamba kwanini hawaoi,najiuliza je,hao Mapadre wamewakataza wao kwamba wasioe?.)..na kama jibu ni hapana,sasa Je,”Pilipili ya shamba usiyoila inakuwashia nini?”
TUMSIFU YESU KRISTO!
Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About