Vituko Vya Xmass

Askari na yeye kumbe muoga, cheki anachomjibu afande

Askari wametumwa nyumba iliyokuwa kuna ugomvi wakafika wakatakiwa kuripoti kwa njia ya simu juu ya walichokikuta
ASKARI: Mkuu tumekuta mama mwenye nyumba kampiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza vibaya sanaa

AFANDE: Kha! kisa mkasa mpk akafanya hivyo
ASKARI: Mama mwenye nyumba alikua anapiga deki mumewe akaingia ndani viatu kabla sakafu haijakauka
AFANDE: Sasa mmesha mkamata huyo mwanamke
ASKARI: Bado mkuu
AFANDE: Kha! sasa mnangoja nini
ASKARI: Si tunangoja sakafu ikauke

Angalia huyu msichana alichonifanyia

Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa.
Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba.
Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- “Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3.”
SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGINE

Namna wazazi wanavyoongea na mabinti katika umri tofauti

Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya.
Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena!
Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako?
Miaka 26: Wenzio wanaolewa.
Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha
kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia!
Miaka 33: Kuna mtu wa Mungu yupo kule
anaombea unaweza kupata mchumba
Miaka 36: At least pata mtoto mmoja.
Miaka 39: We will take care of all the wedding
bills…yeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu .
Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?

😂😂😂 changamkia fulsa umri ukifika

Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili

MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday

MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?😂😂😂😂😂

Wachaga kweli kiboko: Mcheki huyu mchaga na mbuzi!!!

Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.

Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. 😄😄

Amri za chuo

Ndio hizi sasa

1.Hicho ndicho chuo chako usiwe na chuo kingine ila hicho.
2.Usilitaje bure jna la chuo chako mana utawaumiza wengine.
3.Ikumbuke cku uliyochaguliwa na kuiheshimu.
4.Waheshimu tcu, bodi ya mkopo na uongoz wa chuo ili upate kuendelea kuwepo chuon.
5.Usisapu
6.Usidisko
7.Usitumie mkopo ovyo.
8.Usitaman chuo cha mwenzio
9.Usitamani fakat ya mwenzio
10. Usitaman bumu lake wala chochote alichonacho. hahaha chezea chuo weye!

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About