Vituko Vya Wazee

Majibu ya mkato ya kuchekesha Kutoka Kenya

Njeri: Roysambu ni ngapi?
Makanga: Roysambu ni moja tu. Pengine kama Chinese wamejenga ingine.

Odhis: Hii gari haina watu bana.
Makanga: Kwani hao wawili wenye wamekaa hapo ndani ni ng’ombe?

Man: Wekeni nyimbo za Yesu tafadhali.
Makanga: Yesu bado hajatoa album. Akitoa tutaeka.

Mwikali: Excuse me conda…gari za Mwingi zinapandiwa wapi?
Makanga: Ziliacha kupandwa juu hazimei.

Man: Kwani mwisho wa gari ni wapi?
Makanga: Mwisho ni hapo penye number plate iko.

Karis: Ruaka ni how much?
Makanga: Sijaskia Ruaka ikiuzwa. But nikiskia nitakwambia.

Passenger: Shukisha dere.
Makanga: Tukishukisha dere utaendesha gari?

Johnny: Maze, hii gari iko na joto sana.
Makanga: Basi shuka upande fridge

Kilichompata huyu jamaa mroho wa nyama, Hata kaa arudie tena

Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake Levi, kule sehemu za kwetu, akakaribishwa bonge ya ugali na nyama nyingi tu, wakati anakula akagundua kuwa shemeji yake, mke wa rafiki yake hali nyama;

JAMAA: Aise hili ni bonge ya lanchi hii, lakini Levi mbona sisi tu tunakula nyama shemeji Gulo hagusi kabisa anaishia mchicha tu? Tabia gani hii?
LEVI: Hapana sijamkataza, ila shemeji yako Mngoni halagi nyama ya FISI kama sisi

Kali za leo: Misemo ya kuchekesha na kuvunja mbavu

1. Ati wee ni m-black mpaka ukiingia kwa dinga(gari), dirisha zinakuwa tinted!

2. Kwenu kuchafu mpaka mende zinatema mate.

3. Vile wewe mfupi, ukipiga picha ya passport inatokea full.

4. Ati(house) yenu ina gate lakini hakuna fence.

5. Baba alienda ku buy ngombe akaona ikikojoa akasema sitaki hiyo imetoboka.

6.Wee mblack mpaka ukikutana na mzungu afternoon anakusalimia: Good evening.

7. Mko wengi kwa house mpaka kuna rush hours na kukinyesha kunakuwa na jam.

8. Paka yenu noma mpaka ikishika panya inaomba chumvi, fork na pilipili.

9. We ni mrefu mpaka ukikunywa maziwa inafika kwa tumbo ikiwa mgando.

10.Wewe ni mweusi ukikanyanga makaa unawacha footprint nyeusi.

11. Kwenyu mkikunywa maji mnaitisha toothpick

12. We ni mbishi hadi ulikataa kuzaliwa uchi

13. Kwenu kuna insecurity ikifika usiku hadi geti mnaingiza ndani

14. Kwenu ni wengi sana hadi mmeweka round about ndani.

15. Wewe ni mlafi hadi maji uliyochemshia mayai unayafanya supu.

16. We ni mjinga sana hadi blood test ulifeli.

17. Una chogo refu hadi ukigeuka haraka unaweza kuliona.

18. Una kichwa kikubwa hadi ukiingia kwenye daladala konda anakwambia “abiria usiingie na mizigo, tunaweka juu kwenye carrier

Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki

Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana.”
Padri, “Endelea…”

“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuua….. Yesu atanisamehe?”

Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye pia… Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”

Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”

“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.

Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe na hilo?”

Kimyaa….
“Padri yesu atanisamehe?”
kimya….

Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.

Jamaa, “Sasa baba mbona umekimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetu…….”

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About