Vituko Vya Wazee

Majibu ya mkato ya kuchekesha Kutoka Kenya

Njeri:Β Roysambu ni ngapi?
Makanga:Β Roysambu ni moja tu. Pengine kama Chinese wamejenga ingine.

Odhis:Β Hii gari haina watu bana.
Makanga:Β Kwani hao wawili wenye wamekaa hapo ndani ni ng’ombe?

Man:Β Wekeni nyimbo za Yesu tafadhali.
Makanga:Β Yesu bado hajatoa album. Akitoa tutaeka.

Mwikali:Β Excuse me conda…gari za Mwingi zinapandiwa wapi?
Makanga:Β Ziliacha kupandwa juu hazimei.

Man:Β Kwani mwisho wa gari ni wapi?
Makanga:Β Mwisho ni hapo penye number plate iko.

Karis:Β Ruaka ni how much?
Makanga:Β Sijaskia Ruaka ikiuzwa. But nikiskia nitakwambia.

Passenger:Β Shukisha dere.
Makanga:Β Tukishukisha dere utaendesha gari?

Johnny:Β Maze, hii gari iko na joto sana.
Makanga:Β Basi shuka upande fridge

Huyu mke ni shida!

MUME: “Unajua mi unanishangaza sana, kila siku nakusikia mara useme TV yangu, gari yangu, chumbani kwangu, mara hoo watoto wangu. Sisi ni mke na mume, kila kitu ni chetu. Jirekebishe bwana”.πŸ‘΄πŸ˜ŽπŸ˜ŽπŸ˜’
MKE: Yuko kimya anaendelea na shughuli zake za kupekua kabatini kama hasikii, na hakumjibu kitu mumewe.πŸ‘΅πŸ˜·
MUME: Akamuuliza kwa hamaki,”Sasa hapo unatafuta nini?”.πŸ‘΄πŸ˜‘
MKE: “Sidiria yetu!!”πŸ‘™πŸ’
MUME: (kamfungia kabatini alafu kamwambia. “nipo chumbani , “)πŸ‘΄πŸ˜·πŸ˜·
πŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒ
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Huyu ndo mwanamke

Akikuta PESA wakati anafua atapiga kimya kimya, sasa ngoja akute umeacha CONDOM ndo utajua kama umeoa KIPAZA SAUTI πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

Ndio maana mimi nafungaga condom na hela kwa pamoja… akivikuta anachukua hela na kuishia kusonya tu.. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Huwa sipendagi ujinga Mimi

😑😑😑😑😑😑

Kilichotokea baada ya kichaa kumfumania mke wake na mwanamme mwingine

Jay akaruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na nyumbani kwake, akaulizwa unapakumbuka? akajibu ndio nyumba yangu ileee, mara wakatoka watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto wangu walee wanakwenda shule.. akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee, ghafla akatoka mwanaume Jay akasema na mimi yule naenda kazini. hivi Jay kweli kapona?

Kapresha kakiamua kuja kanakujaga tuu, cheki kilichompata huyu mme wa mtu mpenda michepuko

Kimchepuko chako kinakuandikia meseji kama hii…

…Samahani baby kama unavyojua nimeokoka ,nimetubu kanisani lakini nabii kaniambia niwaombe msamaha wote niliowakosea.

Nimemkosea sana mkeo kwa kumwibia mumewe na nimepanga kuja kumwomba msamaha kesho ntakuja na nabii na Mchumba wangu mpya nilie mpata kanisani.

Samahani kwa usumbufu uliojitokeza lakini hilo ni kwa ajili ya utukufu wa bwana!!!

Wako Manka wa MagorofaniπŸ˜…πŸ˜…

Eti wanadamu walikuja vipi duniani

Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa.
Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto
wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika
akamfuta mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na
manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi
kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa
manyani mwanzo?Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo
wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo waoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸšΆπŸΌπŸšΆπŸΌπŸšΆπŸΌ

Shopping Cart
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About